Posted in Hadithi

Ushetani wa Alphonce

MTUNZI NA MWANDISHI Egidius Jack Matungwa   Ndege ya papa, ilizunguka mara tatu, juu ya anga la uwanja wa ndege, wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Dar. Hiyo ilikuwa ni ishala ya salamu kwa maelfu ya watu waliojumuika uwanjani hapo, wakimgoja mgeni adhimu, kiongozi wa juu kabisa ulimwenguni, wa dini ya Romani Katoliki, baba mtakatifu papa Carol Peter wa 16.      Ulinzi uliimalishwa. Maofisa wa vyombo vya ulinzi, na wananjeshi wa ngazi tofauti, walisambazwa kila kona ya uwanja, ili kuhakikisha hali ya usalama ni ya kulidhisha.     Viongozi mbalimbali wa dini na serikali, walijumuika kumpokea papa. Watu ambao hawakuweza kufika…

Soma zaidi..
Posted in Uncategorized

MAAFISA WAFANYA MSAKO MKALI AFRICAN SPIRIT DISTILLERS THIKA

THIKA, KenyaMAAFISA wa kitengo cha jinai cha Flying Squad, na wale wa KRA Alhamisi jioni walivamia kampuni moja ya mvinyo na kuwatia nguvuni mameneja watatukwa kukwepa ulipaji wa ushuru. Kikundi hicho kilichoongozwa na afisa mkuu wa kitengo cha Flying Squad Bw Musa Yego, na naibu kamishna wa KRA Bi Anne Nyaguthie Irungu, kilipata fununu kutoka kwa wananchi ndipo wakavamia eneo hilo. Makachero kadha kutoka jijini Nairobi walifanya upelelezi wao ambapo walifuata lori lililobeba bidhaa gushi ambapo lilikamilisha safari yake katika kampuni ya African Spirit mjini Thika. “Tulipofanya uchunguzi kamili tulipata ya kwamba lori hilo lilitoka nchini Tanzania likiwa limebeba bidhaa gushi. Lakini…

Soma zaidi..
Posted in taifaleo habari

USAJILI MPYA WA WATU KUANZA NCHINI KENYA

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Dkt Karanja Kibicho alisema Alhamisi shughuli hiyo itaanza katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Januari 2019 hasa baada ya shambulizi la kigaidi katika hoteli ya Dusit jijini Nairobi lililosababisha vifo vya watu 21 wasio na hatia, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuwa lazima maelezo ya kila raia nchini yasajiliwe kwa mtambo wa kisasa wa Nimis. Rais alisema mpango huu utasaidia serikali kukabiliana na visa vya uhalifu na kigaidi, ambapo idara ya usalama itaweza kufuatilia hali ya kila mwananchi mkasa unapotukia. Pia alisema shughuli hii itafanikisha mipango ya serikali katika utekelezaji wa maendeleo. Dkt Kibicho…

Soma zaidi..
Posted in Tahariri

Wanawake wanaweza, wasisubiri kwezeshwa

Tahariri tarehe 8th Machi, 2019 -MwananchiLeo ni siku ya Wanawake duniani. Ni siku ambayo wanawake nchini wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha siku hii iliyoanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1975. Historia ya siku hii ilianza karne ya 20 nchini Marekani, kabla ya wazo hilo kupokwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na hivyo kuadhimishwa na nchi wanachama wa umoja huo. Siku ya Wanawake Duniani ni fursa muhimu inayowakutanisha wanawake na wadau wengine kutafakari na kuweka mikakati ya masuala yanaowahusu kama sehemu muhimu ya jamii. Ni siku ambayo moja ya malengo yake ni kuhanikiza kuwepo kwa fursa sawa kwa watu wa makundi…

Soma zaidi..
Posted in Tahariri

Kila mmoja achukue tahadhari ugonjwa wa kimeta

Tahariri tarehe 1st Machi, 2019 -MwananchiK Ugonjwa wa kimeta umelipuka katika baadhi ya maeneo nchini. Mpaka sasa takriban watu sita wameripotiwa kufariki dunia kwa kula nyama ya ng’ombe walioathirika na ugonjwa huo. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kimeta ni ugonjwa wa mlipuko utokanao na vimelea vya bakteria vinavyojulikana kitaalamu kwa jina la ‘bacillus anthracis’. Ni ugonjwa unaowakumba wanyama na unaweza kuwaambukiza binadamu ama kwa kula na kunywa nyama na maziwa ya mnyama aliyeathirika au hata kumgusa. Wanasema majimaji yanayotoka kwenye mzoga wa mnyama aliyeugua kimeta yanaweza kuhifadhi vimelea vya ugonjwa huo kwa miaka mingi. Kama hautotibiwa mapema, ugonjwa huo…

Soma zaidi..
Posted in Tahariri

Hili la kondomu lisiturudishe tulikotoka

Tahariri tarehe 3rd Machi, 2019 -MwananchiWiki iliyopita kulikuwa na taarifa ya upungufu wa mipira ya kujikinga na magonjwa ya zinaa, hasa Ukimwi na hali hiyo ilijitokeza zaidi mkoani Njombe, moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo hatari. Taarifa hiyo ilisema mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa ikipatikana bure au kwa bei rahisi kutokana na programu mbalimbali za Serikali za kudhibiti Ukimwi. Sasa imeadimika na iliyo katika maduka binafsi inauzwa kwa bei kubwa ambayo si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuimudu. Hizi si taarifa nzuri kwa nchi ambayo ilishapiga hatua kubwa kudhibiti ugonjwa huo hatari unaoambukiza kwa njia ya damu,…

Soma zaidi..