Posted in Matukio ya Kiswahili

Uganda kuanza kufundisha Kiswahili shule za Msingi

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Kiswahili ni lugha rasmi ya pili nchini Uganda baada ya Kiingereza. Pia ni lugha kuu ya mawasiliano nchini Kenya, Tanzania, Kongo, Somalia, Sudani Kusini. Kampala. Kiswahili sasa kitaanza kufundishwa rasmi katika shule za msingi nchini Uganda ifikapo 2020. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, 3 Desemba 2019, utaratibu huo utaanzia darasa la nne na kuendelea. Hayo yalisemwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, Mh Janet Museven alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari na kuongeza kuwa hatua hiyo inapaswa kufurahiwa na kupokelewa vyema. “Kwanza, Kiswahili ni lugha ya pili rasmi nchini Uganda baada ya…

Soma zaidi..
Posted in Jifunze Kiswahili Notisi

MISINGI YA TAFSIRI NA UKALIMANI

Amani Njoka, Swahili Hub MISINGI YA TAFSIRI NA UKALIMANITafsiri ni nini? Katika kuifasili istilahi hii, tunaweza kupata maana mbili kutokana na miktadha miwili ambauo ni: Tafsiri kama Taaluma (somo) na Tafsiri kama zao, (kile kinachopatikana baada ya kutafsiriwa/matokeo ya tafsiri)Newmark (1982) Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe uleule ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine. Mwansoko na wenzake (2006) Tafsiri ni zoezi la uhauwilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja hadi lugha nyingine. Nida na Taber (1969) wanaona kuwa tafsiri hujumuisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutumia visawe asilia vya lugha lengwa vinavyokaribiana zaidi na lugha chanzi, kwanza…

Soma zaidi..
Posted in Vitendawili

Vitendawili vya Kiswahili

Amani Njoka, Swahili Hub Hunioni lakini nakupikia-Gesi Ingawa sina mbawa naruka kama ndege-Tiara Jiwe la mviringo, maji umeyatoa wapi?-Jicho Kaa hapa, nikae hapa tumfinye mchawi-Kula ugali Namkata mwanangu huku nalia-Kitunguu Ana mabaka kama chui-Chapati Imamu wangu hana msikiti-Jogoo Nilienda naye, narudi peke yangu-Kujisaidia msalani Popoo mbili zavuka mto-Macho Nimekaa mbali na wenzangu wala sina mwenzi-Dole gumba Rafiki yangu anatembelea tumbo-Nyoka Natembea na nyumba yangu-Kobe Sichoki kuubeba mzigo wangu-Konokono Sahani letu dogo linatusaidia-Mwezi Mbwa wangu hung’ata kwa nyuma-Nyigu Natoka juu nateremka chini-Majani ya miti Liwali amekonda lakini hana mganga-Sindano Mama hana miguu lakini mtoto anayo-Yai na kifaranga Nyoka wa chuma-Garimoshi Nyumba…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya mtindo, sajili na masharti ya matumizi ya lugha katika Kiswahili

Na MARY WANGARI KULINGANA na mtazamo huu, dhana ya mtindo inafafanuliwa kama utunzi wa fasihi ya hali ya juu kabisa. Ufafanuzi au maelezo haya hata hivyo yanatatiza kimaana kwa kuwa hayazingatii kikamilifu mahusiko ya dhana ya mtindo wenyewe. Yamkini mtazamo huu unalenga ama umbuji au ubunifu wa kurejelea mbinu za kujieleza kama vile matumizi ya tamathali za semi. Hata hivyo, jinsi tunavyofahamu, mtindo ni zaidi ya mbinu hizi. Mtindo haurejelei tu jinsi waandishi wanavyoandika bali pia njia mbalimbali zinazotumiwa na watu ama kuongea au kuandika katika hali za kawaida za kila siku. Mtindo hivyo basi ni jumla ya namna lugha…

Soma zaidi..
Posted in Uchambuzi

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi dhana zilivyotumiwa katika methali za Kiswahili

Na ENOCK NYARIKI KATIKA kuunda methali za Kiswahili, dhana ziliteuliwa kwa makini ili kutilia mkazo ujumbe fulani uliokusudiwa. Katika makala haya nitaziangazia dhana mtambuko katika methali za Kiswahili na zile ambazo zilitumiwa kwa njia finyu. Nimelitumia neno ‘mtambuko’ hapa kwa maana ya dhana ambazo hazikuchipuza wala kujikita katika mazingira fulani maalumu. Hapa tena nimeitumia kauli ‘mazingira maalumu’ kusudi kwa sababu kila methali imechipuza katika mazingira ya aina fulani ila kuna zile dhana ambazo zilipotumiwa katika baadhi ya methali, kila jamii iliweza kujinasibisha nazo. Aidha, kunazo dhana ambazo jamii fulani bali si nyingine ndizo ziliweza kujinasibisha nazo. Sababu ni kwamba, dhana…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Uchanganuzi wa datakanzi katika teknolojia ya lugha

KATIKA mchakato wa lugha na utafiti kidijitali changamoto kuu mojawapo inayohitaji kuangaziwa ni Usanifishaji. Ujanibishaji Hii ni nyanja ingine muhimu ambayo imechangia mno katika kukuza na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika lugha. Ujanibishaji unahusisha mambo kadha ya mchakato wa datakanzi ikiwemo: ujenzi wa programu za kikompyuta kama Kilinux (Kiswahili katika mfumo wa Linux) kuwa na kitengo cha programu-huria ya Kiswahili almaarufu Open Office pamoja na tafsiri ya MS Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili. Microsoft East Africa – Huu ni mradi muhimu unaosheheni Kiolesura Fungasha cha Windows. Kwa mujibu wa Mabeya (2009) Kiolesura Fungasha ni daraja la kuruhusu mtumiaji…

Soma zaidi..