Posted in Uchambuzi

UCHAMBUZI: Kitabu cha ‘My Life, My Purpose’ kikitafsiriwa kwa Kiswahili kitagusa wengi

Gadi Solomon, Swahili Hub Rais John Magufuli amegusa mioyo ya Watanzania wengi, huku akikata kiu ya wapenzi, wadau na wanataaluma wa Kiswahili ambao walikuwa wakitamani kuona Kitabu cha ‘My Life, My Purpose’ kikitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Kiongozi huyu wa nchi wa Awamu ya Tano, Rais Magufuli ni dhahiri amekipa nguvu mpya Kiswahili katika bara la Afrika kutoka na kutaka kitumike kwa vitendo kila mahali. Ni miaka mingi kumekuwa na nguvu nyingi za kutaka Kiswahili kipewe nafasi katika nyanja mbalimbali za elimu, kiuchumi, diplomasia lakini hakukuwa na nguvu kubwa ya kufanya hayo kwa vitendo. Awali, huenda watu wengi hawakumuelewa Rais…

Soma zaidi..
Posted in Nahau

Nahau za Kiswahili na Maana zake

Amani Njoka, Swahili Hub Nahau Maana Kumpa mtu ukweli wake                               Kumwambia mtu wazi Sina hali                                                             Sijiwezi/nipo hoiKupiga uvivu                                                     Kukaa tu bila kazi Kupiga kubwa                 …

Soma zaidi..
Posted in Makala

UCHAMBUZI: Kiswahili kinaweza kuwa Lingua Franka ya Dunia

Amani Njoka, Swahili Historia inaonesha kuwa biashara, dini, elimu, siasa na vyombo mbalimbli vilichangia sana kukieneza Kiswahili sehemu nyingi za Tanzania, Afrika Mashariki. Hata hivyo mambo hayo yameendelea kukieneza Kiswahili duniani na kukifanya kizidi kukubalika katika mataifa mengi kwa siku za hivi karibuni. Baada ya Kiswahili kuenea na kuendelea kuenea, hivi sasa lugha hiyo inatumiwa karibu kila sehemu duniani ingawa kwa uchache kwa baadhi ya sehemu. Nchi kadha wa kadha kama vile Sudan Kusini na Afrika Kusini zimeonesha nia ya dhati ya kutaka kujifunza Kiswahili ikiwemo kutaka kifundishwe mashuleni. Sababu kubwa ya serikali ya Afrika Kusini kufikia maamuzi hayo ni…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

World Academy waja na kongamano lingine la Kiswahili na Utamaduni Dubai

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi:Ni kongamano ambalo wasomi na watafiti watawasilisha mada, midahalo, tafiti na matokeo ya tafiti zao kwa mapana na marefu kuhusu lugha ya Kiswahili, utamaduni wake na uhusiano wake na lugha nyingine. Paris. Taasisi inayojihusisha na uchapishaji na uendeshaji wa makongamano mbalimbali ulimwenguni kuhusu siasa, uchumi, sayansi na teknolojia, utamaduni na masuala mengine iitwayo World Academy imeandaa kongamano kuhusu Kiswahili na Utamaduni wake. Tovuti ya Taasisi hiyo yenye makao makuu yake mjini Paris, Ufaransa  inaeleza kuwa kongamano hilo litafanyika tarehe 17-18 Desemba, 2020 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu. Kongamano hilo litakuwa na mada mbalimbali ambazo…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Vitabu vya Watanzania, kwa Watanzania viandikwe kwa Kiswahili kwanza

Nianze kwa kupongeza kazi nzuri za uandishi wa vitabu kadhaa ambavyo vimeandikwa na waandishi mbalimbali kuelezea maisha yao binafsi na ya kijamii jambo ambalo linatoa hamasa kwa watu wengi pale ambapo vitabu hivyo vitasomwa hasa ukizingatia umashuhuri, umaarufu na ushawishi wa watu hao kwa jamii. Kwa kweli ni jambo la kupongeza sana. Uandishi huu ni muhimu kwani wasomaji hupata maarifa na kufahamu mbinu mbalimbali, changamoto na mafanikio ya waliyoyapa watu hao. Waandishi hawa wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao kutoa kile walichonacho kwa kutumia lugha iliyokuwa rahisi kwao. Ni ukweli usiopingika kwamba lugha ni mhimili mkubwa kwa jamii yoyote. Ni…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Magufuli apendekeza Kitabu cha ‘My Life, My Purpose’ kitafsiriwe Kiswahili

KWA UFUPI: Rais John Magufuli amezindua kitabu cha My Life, My Purpose ambacho kimeandikwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kuwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kusoma vitabu. Gadi Solomon, Swahili Hub Dar es Salaam. Dar es Salaam. Rais John Magufuli amezitaka mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kutafsiri kitabu cha My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudio Langu) kwa lugha ya Kiswahili ambacho kimezinduliwa leo Jumanne Novemba 12, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandikwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye pia…

Soma zaidi..