
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) limewapongeza wanafunzi bora wa shahada ya awali ya Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es Salaam (Tudarco) na kuwapatia zawadi.
Wanafunzi hao ambao ni wahitimu wa mwaka 2022/2023, wamepatiwa fedha taslimu, Kamusi Kuu ya Kiswahili toleo la tatu na Kitabu cha Furahia Kiswahili zikiwa ni nyenzo za kufundishia Kiswahili kwa wageni.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Bakita, mwishoni mwa wiki iliyopita Ijumaa Novemba 10,2023, Mussa Kaoneka amesema baraza hilo lipo katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili wa miaka 10 unaoanzia 2022-2032,
Hivyo limetoa fursa kwa wanafunzi hao kuhudhuria bure Mafunzo ya Kuimarisha Stadi za Kufundisha Kiswahili kwa wageni yanayotolewa na BAKITA ili wakawe mabalozi wa utekelezaji wa mkakati huo.
Maoni Mapya