Posted in Hadithi

Mzimu Katabi

Hapo zamani za kale katika kijiji cha inyonga mkoa wa Katavi palikuwa na familia moja iliyokuwa na baba na mama walioishi kwa mda mrefu bila kupata mtoto. Na ilipotokea mama akabeba mimba basi iliharibika kabla ya wakati wake. Waliteseka sana na tatizo hilo bila kupata msaada wowote. Ndipo alipotokea mzee mmoja anayejulikana kwa jina la Magoye aliyewaeleza kuwa kama wanahitaji msaada waende kwa mzimu Katabi anayepatikana milimani mbali kidogo na kijiji chao kilipo. Baada ya wazazi kupata habari ile kwao ilikuwa habari njema zaidi kesho yake wakaanza safari kuelekea inapopatikana milima hiyo wakiongozana na wazee wa kimila. Safari ilikuwa ndefu…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

Msemo wa leo

Mungu akikupa kilema hakunyimi mwendo Msemo huu una maana ya kuwa mwanadamu anapopatwa na changamoto au tatizo lolote huwa kuna njia mbadala ya utatuzi wa jambo lake Mungu anakuwa amemuandalia. Kwa kawaida kilema ni mtu anakuwa na kasoro katika mwili wake inaweza kuwa ya kiungo, lakini kuna njia ambayo mtu huitumia kutimiza haja zake na kupata mahitaji yake.

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

msemo wa leo

Mwili haujengwi kwa matofali Msemo huu una maana ya kuwa ili binadamu aweze kuwa na mwili imara na wenye afya anatakiwa ale chakula vizuri. Na chakula kiwe cha kutosha kinachoweza kuufanya mwili kukua na kuimarika. Watu wengi huwa wanautumia msemo huu pale wanapokutana na watu wakiwasema wanakula sana hivyo hudai mwili unajengwa kwa chakula na si matofali.

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

PANYA ROAD-2

Na Sosteness Isengwa 0657 241821 Damu nyingi zikiruka mithili ya bomba na mlinzi huyo akaanza kupaparika kwa kihoro, alijaribu kupiga kelele ili kuomba msaada lakini sauti haikutoka na kuishia kukoroma tu kwa maumivu makali aliyoyapata na kuikamatia shingo yake iliyokuwa na majeraha makubwa ya visu. Kwa hofu ya kuonwa na wapita njia wakamburuta hadi ndani na kufunga geti. Kitendo hicho kilionekana kumshtua mno Beka, hakutarajia kabisa kama hali hiyo ingejitokeza mapema kiasi hicho, alianza kuona dalili ya mambo kwenda tofauti na mipango yake. Aliduwaa kwa sekunde kadhaa akimshangaa yule mlinzi alivyokuwa anatapatapa pale chini  kabla ya kutulia tuli na kuashiria…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

PANYA ROAD- 1

Na Sosteness Isengwa    UTANGULIZI Bakari Mfaume (Beka) ni kijana mwenye umri wa miaka kumi na tisa aliyekuwa miongoni mwa vijana kadhaa waliokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kati (Central Police) jijini Dar es salaam, akihusishwa na mtandao maarufu wa uhalifu uliotikisa jiji hilo kwa muda mrefu uliofahamika kwa jina la Panya Road. Mtandao huo uliohusisha vijana wengi wenye umri mdogo, ulishamiri kwa kasi na kushiriki matukio mengi ya unyang’anyi ambapo wafuasi wake walivamia kwa staili ya makundi makubwa mithili ya mbwa mwitu mawindoni wakipora mali na kujeruhi watu. Vijana hao nunda walioshindikana na familia zao na jamii…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

MFALME IZANA – SEHEMU YA 2

JINA LA MTUNZI: Shung Thong Xhi Mawasiliano: 0623410370, 0693548469 INSTAGRAM: @Shungthong UTANGULIZI: Wiki iliyopita tulianza sehemu ya kwanza ya hadithi tamu ya Mfalme Izana, sasa endelea…….  “Nimekuja kuonana na kiongozi mkuu wa mila…!?” Wale vijana walio kuwa nje pale waliinamisha nyuso zao wakati Mizana anaongea kuonyesha heshima!. “Karibu mtukufu Mizana!…” “Asante……!” “Hivi unavyo tuona tayari tumesha jiandaa kujongea kwenda huko kwenye mlima wa miungu yetu kwenda kuomba shauri! Hivyo nakuomba wala usijali mtukufu Mizana kila jambo lita kwenda sawa!” Aliongea hivyo ili kumtuliza Mizana kisha akainama kuonyesha heshima kabla hajaondoka mbele ya uoni wa Mizana pamoja na msafara wake.Mizana aliwageukia…

Soma zaidi..