Posted in Hadithi

UKUTA WA GIZA 1

NA Patrick J Massawe Utangulizi Alijulikana kwa jina la Marko Kitenge mtoto wa mjini anayetafuta maisha ndani ya jiji la Dar es Salaam . Anakutana na StellaMkwizu dada mzuri pia mwenye uwezo wa kifedha. Anaendesha gari la kifahari ana ya Ford Munstang Sports  anamilki  nyumba  huko Mbezi Beach ufukweni mwa Bahari ya Hindi  na ndiko anampeleka  kijana Makrko. Mrembo huyo mwenye wingi wa uzuri mali na mapenzilakini vilevile anafanya biashara hatari ya dawa za kulevya  kwa siri.Hilo ndilo Marko alitaka kujuana kujutia baadaye  baada ya kuingizwa katika hekeheka nzito  inayomwacha mdomo wzi. Hebu fuatilia hadithi hi  nzito nay a kusisimua…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

Biashara haramu

Na Ackley Ludovick Diana yuko ndani ya ofisi yake nadhifu sana akipitia taarifa mbalimbali za kikazi.  Ghafla simu yake ikaita na alipoipokea akafahamishwa kuwa kuna mgeni muhimu anataka kumwona. Mgeni mwenyewe alipomuona  kuanzia hapo wakawa pamoja kama chanda na pete.  Je, ni nani huyo? Endelea. Ilikuwa ni ofisi kubwa yenye meza moja kubwa, viti vikubwa viwili kwa ajili ya wageni wawapo ofisini hapo. Meza ilijaa mafaili yaliyokuwa na nyaraka muhimu za kampuni ya THE GREAT DIANA. Ilikuwa ni kampuni iliyojihusisha na uagizaji na  usambazaji wa samani. Nyuma ya meza alikaa mwanamama aliyekuwa na mvuto sana. Aliitwa Diana Mavune Mutozya. Kampuni…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

Kasheshe la Fedha Bandia

Na Dennis Njalambaya Ilikuwa ni mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha ambalo liliwapiga kikumbo matajiri na mabepari waliokuwa na mali nyingi kupita kiasi. Azimio lilipotangazwa msambaratiko wa mabepari kuikimbia Serikali ya Nyerere ulikuwa mkubwa. Wapo waliokimbilia Ulaya na Asia na wengine walivuka mpaka kwenda nchi jirani ya Kenya. Kati ya matajiri wote hao, mmoja wao alikuwa Benson Papi, Mtanzania pekee aliyekuwa anakula sambamba na matajiri wa Kizungu waliokuwa sumu kali kwa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere katika kuleta uwiano sawa kati ya matajiri na maskini. Katika kukimbiza mali zao zisihodhiwe na Serikali, Benson Papi alihamia…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

Wosia kwa wajukuu

 Na Jacob Qorro (SEHEMU YA KWANZA) Mara baada ya kupata uhuru Mwalimu  Nyerere aliiweka Tanzania katika reli ya kuwa taifa lenye uhuru wa kweli baada ya kutawaliwa na wakoloni kwa miaka arobaini. Kwa maana nyingine alitaka Tanzania iwe nchi inayojitegemea kama wakoloni walivyoikuta kwani wakoloni hawakuwakuta akina Mkwawa na Isike wala Mirambo  ombaomba na alitaka  tuishi katika utamaduni wa kiafrika wa ujamaa kwani taifa au kabila lisilothamini utamaduni na mila zake kwa maneno ya Nyerere ni Taifa au kabila mfu yaani iliyokufa ingawa watu wake wanaweza kuwa hai. Baada ya Mwalimu  kustaafu waliomfuata badala ya kuiwekea reli hiyo aliyoisanifu Nyerere…

Soma zaidi..
Posted in Hadithi

Muuaji asakwe

MUUAJI ASAKWE Patrick J. Massawe 0715676249 Utangulizi Mwanamke mrembo anauawa ndani ya bafu, nyumbani kwake, eneo la Tabata, Jijini Dar es Salaam. Kwanza kabisa, muuaji huyo katili alimtumia ujumbe wa vitisho muda mfupi tu kabla ya kutekeleza mauaji hayo. Pia, muuaji huyo alimbaka mrembo huyo kabla ya kumuua. Upelelezi wa Jeshi la Polisi, unafanyika mara moja. Msako mkali dhidi ya muuaji huyo unafanyika, na inagundulika siri nzito iliyojificha nyuma ya mapazia kuhusiana na kifo hicho chenye utata. Kama kawaida, mtunzi wako mahiri,  PATRICK J. MASSAWE anatiririka na hadithi hii ya kusisimua.     Fuatilia mpaka mwisho wake… MCHANA  wa saa sita hivi,…

Soma zaidi..