Posted in Hadithi

msemo wa leo

Mwili haujengwi kwa matofali Msemo huu una maana ya kuwa ili binadamu aweze kuwa na mwili imara na wenye afya anatakiwa ale chakula vizuri. Na chakula kiwe cha kutosha kinachoweza kuufanya mwili kukua na kuimarika. Watu wengi huwa wanautumia msemo huu pale wanapokutana na watu wakiwasema wanakula sana hivyo hudai mwili unajengwa kwa chakula na si matofali.

Soma zaidi.. msemo wa leo
Posted in Hadithi

PANYA ROAD-2

Na Sosteness Isengwa 0657 241821 Damu nyingi zikiruka mithili ya bomba na mlinzi huyo akaanza kupaparika kwa kihoro, alijaribu kupiga kelele ili kuomba msaada lakini sauti haikutoka na kuishia kukoroma tu kwa maumivu makali aliyoyapata na kuikamatia shingo yake iliyokuwa na majeraha makubwa ya visu. Kwa hofu ya kuonwa na wapita njia wakamburuta hadi ndani na kufunga geti. Kitendo hicho kilionekana kumshtua mno Beka, hakutarajia kabisa kama hali hiyo ingejitokeza mapema kiasi hicho, alianza kuona dalili ya mambo kwenda tofauti na mipango yake. Aliduwaa kwa sekunde kadhaa akimshangaa yule mlinzi alivyokuwa anatapatapa pale chini  kabla ya kutulia tuli na kuashiria…

Soma zaidi.. PANYA ROAD-2
Posted in Hadithi

PANYA ROAD- 1

Na Sosteness Isengwa    UTANGULIZI Bakari Mfaume (Beka) ni kijana mwenye umri wa miaka kumi na tisa aliyekuwa miongoni mwa vijana kadhaa waliokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kati (Central Police) jijini Dar es salaam, akihusishwa na mtandao maarufu wa uhalifu uliotikisa jiji hilo kwa muda mrefu uliofahamika kwa jina la Panya Road. Mtandao huo uliohusisha vijana wengi wenye umri mdogo, ulishamiri kwa kasi na kushiriki matukio mengi ya unyang’anyi ambapo wafuasi wake walivamia kwa staili ya makundi makubwa mithili ya mbwa mwitu mawindoni wakipora mali na kujeruhi watu. Vijana hao nunda walioshindikana na familia zao na jamii…

Soma zaidi.. PANYA ROAD- 1
Posted in Hadithi

MFALME IZANA – SEHEMU YA 2

JINA LA MTUNZI: Shung Thong Xhi Mawasiliano: 0623410370, 0693548469 INSTAGRAM: @Shungthong UTANGULIZI: Wiki iliyopita tulianza sehemu ya kwanza ya hadithi tamu ya Mfalme Izana, sasa endelea…….  “Nimekuja kuonana na kiongozi mkuu wa mila…!?” Wale vijana walio kuwa nje pale waliinamisha nyuso zao wakati Mizana anaongea kuonyesha heshima!. “Karibu mtukufu Mizana!…” “Asante……!” “Hivi unavyo tuona tayari tumesha jiandaa kujongea kwenda huko kwenye mlima wa miungu yetu kwenda kuomba shauri! Hivyo nakuomba wala usijali mtukufu Mizana kila jambo lita kwenda sawa!” Aliongea hivyo ili kumtuliza Mizana kisha akainama kuonyesha heshima kabla hajaondoka mbele ya uoni wa Mizana pamoja na msafara wake.Mizana aliwageukia…

Soma zaidi.. MFALME IZANA – SEHEMU YA 2
Posted in Hadithi

MFALME IZANA- SEHEMU YA 1

JINA LA MTUNZI: Shung Thong Xhi Mawasiliano: 0623410370, 0693548469 INSTAGRAM: @Shungthong UTANGULIZI “IZANA” ni stori yenye visa vya kusisimua! Ikielezea mausiano na taratibu za jamii za kiafrika  ikihusisha migogoro ya kusisimua,visa vya mahusiano ya kimapenzi pamoja na nguvu za ajabu!.Ikiwa inaongelea jamii ya kiutawala wa kifalme iliyokuwa inaitwa mizi,ambayo ilikuwa kaskazini huko.Ilikuwa ni kipindi ambacho Wajerumani walikuwa wanajaribu kutanua utawala wao na kusababisha vita ambayo inapelekea jamii ya mizi kupoteza kiongozi wao waliyekuwa wana muita “Miziya” wakiwa na maana ya mtukufu mfalme! Jambo hilo linawashitua wengi! Na kuwaacha na maswali mengi yasiyo na majibu ya haraka ama majibu ya kufaa…

Soma zaidi.. MFALME IZANA- SEHEMU YA 1
Posted in Hadithi

Mawimbi

Patrick J. Massawe 0715 676249 Utangulizi. Fred Samson kijana mtanashati anakutana ndani ya basi la daladala na mwanadada mrembo, Mariana, wakati huo mvua kubwa inayesha upande wa nje. Lakini wanapofika mwisho wa safari yao, Mariana anamsitiri kumfunika kwa mwavuli wake ili asilowane. Hatimaye wanaongozana wote huku wakitambulishana, na safari yao inaishia kujenga uhusiano mzito wa kimapenzi ambao baadaye unaleta misukosuko mingi na karaha na kuhatarisha penzi lao! Endelea na hadithi hii ya kusisimua mpaka mwisho wake…. MVUA za masika zilikuwa zinaendelea kunyesha mfululizo ndani ya jiji la Dar es Salaam, na kulifanya liwe katika utulivu wa hali ya juu.  Ni…

Soma zaidi.. Mawimbi