Posted in Makala

msamiati wa leo

Kifumanzi, aina ya shanga zinazovaliwa aghalabu na mcheza ngoma miguuni, mikononi au shingoni au na mtoto mdogo anayejifunza kutambaa au kutembea zinazotoa mlio zinapotikiswa.

Soma zaidi..
Posted in Makala

Congo kuingia EAC kutaongeza matumizi ya Kiswahili duniani

Gadi Solomon Unakumbuka ile dhana Kiswahili  asili yake ni Kikongo? Hivi karibuni wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameidhinisha kuingizwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika umoja huo. Kwa sasa Kiingereza na Kiswahili ndizo lugha rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ingawa kumekuwa na mazungumzo kuhusu kuanzisha Kifaransa, ambacho kinazungumzwa nchini Rwanda na Burundi. Lugha rasmi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni Kiswahili, Kifaransa, Kilingala, Kituba (Kikongo) na Tshiluba. Wataalamu wanasema asili ya lugha nyingi katika eneo hili inapaswa kuangaliwa kama fursa na sio kizuizi. Wasanii wengi wa Congo tumeona wakiishi Ufaransa au nchi zinazozungumza…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mbinu hizi zitasaidia kuzifikia ajira za Kiswahili duniani

Na Gadi Solomon Wahitimu wa Kiswahili wamekuwa wakiongezeka kila mwaka kutoka kwenye vyuo vikuu na kati hapa nchini, huku wigo mafunzo  kwa ngazi mbalimbali kuanzia kozi za muda mfupi, kozi ngazi ya cheti na shahada ya awali na uzamivu ukiwa umeongezeka. Tanzania ikiwa ni wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  tumepata viongozi wenye utashi wa kutambua thamani ya lugha ya Kiswahili  karibu awamu zote, jambo ambalo limeifanya Taifa letu kuwa ndio kinara wa kubeba ajenda mbalimbali za Kiswahili kimataifa. Ni viongozi hao wa serikali kwa kushirikiana na mabaraza ya Kiswahili, Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) na Baraza la…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Chama cha Kiswahili kuhimiza wanafunzi kukipenda Kiswahili

Na CHRIS ADUNGO CHAMA cha Kiswahili cha Triple ‘S’ ni chombo kinachotumiwa na wanafunzi wa Shule ya Upili ya Satima katika Kaunti ya Nyandarua kuboresha matokeo ya KCSE Kiswahili. Chama hiki ambacho kimeinua ari ya kuthaminiwa kwa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, kiliasisiwa na mwalimu Mwai wa Nguyo kwa kushirikiana na Bw R.M. Kariuki (Makamu Mwalimu Mkuu) mnamo 2018. Ingawa wakati huo Triple S ilikuwa na wanachama 15 pekee, idadi hiyo iliongezeka zaidi maradufu kwa kipindi kifupi na chama kwa sasa kinajivunia wanachama 60. Mbali na kuweka wazi umuhimu wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi, madhumuni mengine makuu ya Triple S ni…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mikakati ya kukuza matumizi ya Kiswahili ibuniwe Kenya

NA BITUGI MATUNDURA WIKI ya Lugha za Kiafrika kwa mwaka 2022 inatoa fursa muhimu ya kutafakari masuala mengi kuhusu lugha zetu za kiasili, umuhimu na mustakabali wazo katika siku zijazo. Huku ikiwa na jumla ya mataifa 53, Afrika ndilo bara lenye nchi nyingi zaidi ikilinganishwa na mabara mengine. Mataifa kadhaa ya Afrika yana mamia ya lugha mbalimbali, lakini zinazozungumzwa na watu wachache. Hali hii inaibua taswira ya ‘watu wachache, lugha nyingi’. Kwa mfano, Cameroon ina takriban watu milioni 26, lakini ina zaidi ya lugha 250. Je, wingi-lugha katika bara la Afrika ni balaa au neema? Kutokana na ukweli kwamba mataifa…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mbinu za kukabili mitazamo hasi kuhusu lugha ya Kiswahili shuleni

Na CHRIS ADUNGO CHAMA cha Kiswahili katika Shule ya Msingi ya Minhaj Academy (CHAKIMA) kilianzishwa kwa lengo la kubadilisha mtazamo hasi wa wanafunzi kuhusu somo la Kiswahili na kukuza talanta zao katika sanaa mbalimbali. Ikiongozwa na Bw David Chombo, kamati ya walimu wa Kiswahili shuleni humo iliteua jopo la wanafunzi ambao walitwikwa jukumu la kuwa vinara wa chama baada ya kubaini utashi wao katika Kiswahili. Kupitia CHAKIMA, wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Minhaj Academy katika mtaa wa Eastleigh Nairobi, walifunguliwa milango ya kuanza kukithamini Kiswahili, kumudu sarufi na kuandika insha za kusisimua. Tangu kiasisiwe, chama hiki kimekuwa chombo maridhawa…

Soma zaidi..