Posted in Makala

Tunakivuruga Kiswahili kwa sababu hatukifahamu au makusudi?

Amani Njoka, Swahili Hub Mawasiliano ni mhimili wa kila kitu kinachofanyika katika maisha ya binadamu awaye yote, katika jamii na katika nyanja zote duniani. Zipo mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kufikisha ujumbe, taarifa au habari upande wa pili ikiwemo ishara, alama, picha na sauti zisizo na mpangilio kama miluzi na sauti zinazotumiwa na viumbe mathalani wanyama na ndege. Ili kukidhi haja ya mawasiliano kwa binadamu, kiliibuka kitu kinachoitwa lugha. Walimu wangu wa lugha ngazi zote nilizopitia walinijuza kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu (kubahatisha) zilizobuniwa na kukubaliwa miongoni mwa wanadamu katika jamii walizopo kama nyenzo ya mawasiliano miongoni mwao….

Soma zaidi.. Tunakivuruga Kiswahili kwa sababu hatukifahamu au makusudi?
Posted in Makala

Bakita ifanye kazi kwa ukaribu zaidi na taasisi zinazofundisha Kiswahili na wataalam

Amani Njoka, Swahili Hub  Baraza la Kiswahili la Taifa (Basata) ni baraza lililoundwa chini ya kifungu cha 3 cha sheria namba 27 ya mwaka 1967. Baraza hili ndilo chombo rasmi cha kisheria chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za ukuzaji, uendelezaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili duniani. Mojawapo ya majukumu ya baraza hili hili miongoni mwa mengi ni pamoja na kusanifu istilahi za Kiswahili katika nyanja mbalimbali kwa dhamira ya kukikuza, kukieneza na kukifanya Kiswahili kuwa lugha yenye nguvu zaidi duniani katika siku za usoni kwa kushirikiana na wataalamu kutoka mamlaka na taasisi nyingine. Kwa ujumla majukumu ya Bakita…

Soma zaidi.. Bakita ifanye kazi kwa ukaribu zaidi na taasisi zinazofundisha Kiswahili na wataalam
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya mtindo, sajili na masharti ya matumizi ya lugha katika Kiswahili

Na MARY WANGARI KULINGANA na mtazamo huu, dhana ya mtindo inafafanuliwa kama utunzi wa fasihi ya hali ya juu kabisa. Ufafanuzi au maelezo haya hata hivyo yanatatiza kimaana kwa kuwa hayazingatii kikamilifu mahusiko ya dhana ya mtindo wenyewe. Yamkini mtazamo huu unalenga ama umbuji au ubunifu wa kurejelea mbinu za kujieleza kama vile matumizi ya tamathali za semi. Hata hivyo, jinsi tunavyofahamu, mtindo ni zaidi ya mbinu hizi. Mtindo haurejelei tu jinsi waandishi wanavyoandika bali pia njia mbalimbali zinazotumiwa na watu ama kuongea au kuandika katika hali za kawaida za kila siku. Mtindo hivyo basi ni jumla ya namna lugha…

Soma zaidi.. UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya mtindo, sajili na masharti ya matumizi ya lugha katika Kiswahili
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Uchanganuzi wa datakanzi katika teknolojia ya lugha

KATIKA mchakato wa lugha na utafiti kidijitali changamoto kuu mojawapo inayohitaji kuangaziwa ni Usanifishaji. Ujanibishaji Hii ni nyanja ingine muhimu ambayo imechangia mno katika kukuza na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika lugha. Ujanibishaji unahusisha mambo kadha ya mchakato wa datakanzi ikiwemo: ujenzi wa programu za kikompyuta kama Kilinux (Kiswahili katika mfumo wa Linux) kuwa na kitengo cha programu-huria ya Kiswahili almaarufu Open Office pamoja na tafsiri ya MS Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili. Microsoft East Africa – Huu ni mradi muhimu unaosheheni Kiolesura Fungasha cha Windows. Kwa mujibu wa Mabeya (2009) Kiolesura Fungasha ni daraja la kuruhusu mtumiaji…

Soma zaidi.. UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Uchanganuzi wa datakanzi katika teknolojia ya lugha
Posted in Makala

KAULI YA MATUNDURA: Athari ya lugha za kigeni kwa Kiswahili na jinsi zilivyochangia kupanua leksikoni

Na BITUGI MATUNDURA MOJAWAPO ya vipengee muhimu ambavyo mwalimu na mwanafunzi wa isimujamii anahitajika kujua ni historia ya Kiswahili. Katika kuangazia historia ya lugha hii muhimu ya Afrika Mashariki na Kati, mwalimu na mwanafunzi wake hawawezi kukwepa suala la jinsi Kiswahili kimeathiri na kuathiriwa na lugha nyingine. Katika makala haya, ninaangazia jinsi wageni kutoka nje ya bara Afrika walivyochangia katika kuathiri Kiswahili. Athari ambazo hujitokeza wazi kwenye mada kama hii angalau huwa ni ya kileksikoni au msamiati. Miongoni mwa wageni wa awali kabisa kuwasili katika pwani ya Afrika Mashariki walikuwa ni pamoja na Waajemi, Wafarsi, Wamisri,Wachina na Waarabu. Utafiti wa…

Soma zaidi.. KAULI YA MATUNDURA: Athari ya lugha za kigeni kwa Kiswahili na jinsi zilivyochangia kupanua leksikoni
Posted in Makala

Kuenea kwa Kiswahili: Ipo haja ya lugha kufundishwa katika kambi za wakimbizi

Amani Njoka, Swahili Hub Mkimbizi ni mtu aliyeondoka kwake nyumbani, nchi yake na mahali anapoishi kwa sababu ya kulazimishwa, kufukuzwa au kwa hofu ya kuteswa. Baada ya watu hawa kukimbia makazi yao hatimaye hukutana kambini wakitoka mataifa mbalimbali. Wamekimbia vita na majanga kadha wa kadha yanayotokea katika nchi zao na hatimaye kujikuta kwenye mataifa ya watu na hivyo wanakuwa ugenini aua wakati mwingine ndani ya nchi yao wenyewe. Tanzania inapokea wakimbizi kutoka nchi kama Burundi, Kongo, Rwanda na nchi nyingine nyingi zilizo nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakimbizi hawa baada ya kufika katika kambi mbalimbali kama Nyarugusu na kwingineko…

Soma zaidi.. Kuenea kwa Kiswahili: Ipo haja ya lugha kufundishwa katika kambi za wakimbizi