Posted in Makala

Siakago kueneza Kiswahili

CHAMA cha Kiswahili katika shule ya upili ya St Albert The Great Siakago Boys kinadhamiria kuboresha matumizi ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na kupiga jeki shughuli za Idara ya Kiswahili. Aidha, kinakusudia kuwapa wanafunzi majukwaa maridhawa ya kusoma magazeti na kukuza vipaji vyao katika sanaa na fani zinazofungamana na Kiswahili kama vile uigizaji, uanahabari, ulumbi, uandishi wa hadithi na utunzi wa mashairi. Chama hiki ni kiungo muhimu cha Idara ya Kiswahili inayoongozwa kwa sasa na John Macharia Karori ambaye pia ni mlezi wa chama. Wanachama hukutana kila Jumanne jioni kuzamia mada zinazowatatiza katika Kiswahili na kuratibu midahalo na mijadala mbalimbali…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Usanifishaji wa Istilahi

Na Nabil Mahamudu Istilahi ni neno au maneno (msamiati) yanayotumika katika uga fulani maalumu, unaweza ukawa uga wa kimichezo, kitabibu, kisanaa na kiutawala. Idara ya Istilahi na Kamusi katika Baraza la Kiswahili la Taifa ndio yenye kazi ya kukusanya maneno kutoka nyanja mbalimbali ambayo yana uhitaji katika jamii kimatumizi kwa mujibu wa Wema. Msigwa (Mchunguzi wa lugha, Bakita) anabaisha kwamba “kinachofanyika tunakusanya istilahi kutoka lugha mbalimbali huwa mara nyingi tunakusanya istilahi kutoka lugha ya Kiingereza na kuzitafutia visawe, visawe ni yale maneno yanakuwa na maana sawa na msamiati wa lugha ya kiingereza.” alisema Msigwa ambaye pia ni Mkuu wa Idara…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Zijue fursa ndani ya Mpango Mkakati wa Taifa wa kubidhaisha Kiswahili

Nabil Mahamudu na Loveness John Serikali ya Tanzania kupitia wizara zenye dhamana ya utamaduni, imeandaa Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili katika kutekeleza mambo mbalimbali ya ukuzaji na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa mambo yaliyobainishwa ni pamoja na kuwasajili wataalamu wa Kiswahili katika kanzidata na kuwatumia kikamilifu, kutoa mafunzo ya kunoa stadi kwa wataalamu wa nyanja mbalimbali katika Kiswahili (mfano, wakalimani wa lugha ya kawaida na lugha ya alama, wafasiri, walimu wa kufundisha Kiswahili kwa wageni, wahariri). Pia kuandaa vitendeakazi vya kuwezesha ubidhaishaji wa Kiswahili kwa maana ya kuandika vitabu vya kufundishia na kujifunzia wageni, kuwezesha matumizi ya Teknolojia…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mwanasiasa Louis Rwagasore alivyofanikiwa kuwaunganisha Warundi kupitia lugha zao

Na Antonio Onorati Sote tumepoteza fursa nyingi za kujua historia za mashujaa au viogozi hodari kwa sababu tunasoma sehemu moja ya historia tukisahau umuhimu wa michango ya watu wa nchi mbalimbali.  Mfano mkubwa ni ule wa Louis Rwagasore kutoka Burundi, mtu ambaye anaweza kutufundisha mambo mengi kwa kupitia maisha yake. Watu wachache wanajua historia ya mwanasiasa huyo ambaye aliishi wakati wa ukoloni na alithubutu kukabili utawala wa kikoloni kwa ajili ya uhuru wa nchi yake. Louis Rwagasore alizaliwa mwaka 1932 mjini Gitega, alikuwa mtoto wa Mfalme wa Burundi, Mwambutsa Mbangiricenge, kutoka ukoo wa “Baganwa”, hawa walikuwa watu muhimu wa makao…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Kiswahili kilianza kama lugha mama sasa ni ya kimataifa

Na Benard Semen Neno Kiswahili linatokana ni neno la kiarabu Sawahil lenye maana ya upwa au Pwani. Hivyo, Kiswahili ni lugha ambayo ilizungumzwa na watu wa Pwani ya Afrika Mashariki. Lugha ya Kiswahili ilianza kuzungumzwa tangu mwaka 700 AD, hasa katika Kisiwa cha Lamu na ukanda wa Mto Tana. Ilienea zaidi baada ya mwaka 975 AD wakati Sultan Ali Ibn al-Hassan Shirazi alipoitawala Kilwa, ilienea hadi Kusini mwa mji wa Sofala (kwa sasa Msumbiji) na kuvuka ng’ambo ya mto Zambezi kwani ilitumia katika shughuli za kibiashara.Lugha ya Kiswahili ilikuwa na lahaja nyingi, baadhi ya lahaja hizo ni Chimiini, Kitikiu, Kisiu,…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mambo ya msingi kuzingatia unapotaka kuandika kitabu chako

Na Ismail Himu Uandishi wa fashihi hasa tamthiliya na riwaya umekuwa ni sehemu ya maisha yangu kwa zaidi ya miaka kumi sasa na ninajivunia kwa hilo. Miongoni mwa vitabu nilivyoandika ni tamthiliya ya CHANZO NI WEWE, USASA USASAMBU, NJIA IMEPATIKANA, WAKILIA TUTACHEKA na riwaya ya DIWANI HAYAWANI. Pia nina kitabu cha ushairi kiitwacho TUMAINI AFRIKA nilichoshirikiana na BERYA M. JASPER Kwenye majukwaa mbalimbali ya waandishi ninayopita nakutana na makundi makubwa ya vijana wanaotamani kuandika au hata waliowahi kuandika vitabu lakini wakiwa na changamoto mbalimbali. Wapo wanaohoji, “Himu mbona mimi nimeandika lakini sioni manufaa ya kuandika kitabu?” Wengine wakiamini maisha niliyonayo…

Soma zaidi..