Posted in Makala

KINA CHA FIKIRA: Taaluma ya Kiswahili yahitaji asasi madhubuti kuboresha utumizi wake

Na KEN WALIBORA PROF Kimani Njogu amewasha kiberiti cha moto ambao ulitishia kuteketeza msitu mkubwa alipouliza hivi karibuni kwa nini istilahi “literary stylistics” imetafsiriwa elimumtindo na baadhi ya wanataaluma. Unapojaribisha kitu ili kuona matokeo yake yatakuwaje au yatakuwa nini, tunaweza kusema “unatingisha kiberiti ili kuona kama ndani mna njiti” katika Kiswahili cha kisanii. Prof Njogu hakuwa anatingisha tu njiti, ameuliza swali la kuchochea mjadala mpevu kuhusu usahihi wa baadhi ya istilahi zinazotumika katika taaluma za Kiswahili. Kama hatuwezi kuanza kusaili baadhi ya istilahi na mikondo na mikabala tutakuwa tunazihini taaluma fursa ya kwenda mbele. Kiswahili mbele hakiendi pasi na kuuliza…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Mwingiliano wa Kiswahili, Kibantu

Na Wanderi Kamau KATIKA jumla ya masuala yanayohusu lugha ya Kiswahili, hasa uhusiano wake na lugha zingine, uhusiano uliopo baina yake na lugha za Kibantu ndilo limewahi kujadiliwa na wanaisimu mbalimbali kwa marefu na mapana. Hata hivyo, kuna haja ya kutathmini kwa kina mwoano wa Kiswahili na lugha za Kibantu. Je, undani wa mwoano huu ni upi? Ulifikia wapi? Katika taaluma ya isimu ya lugha za Kiafrika, na hasa lugha za Kibantu, msomi wa kwanza na anayejulikana sana kutokana na utafiti wake wa miaka mingi katika lugha hizo alikuwa Wilhelm H.I. Bleek. Katika uainishaji wake wa makundi ya lugha za…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Uigaji hauzuiliki katika ubunifu hasa wa kazi za fasihi

Na Enock Nyariki KATIKA ubunifu wa kazi za fasihi – novela, riwaya, tamthilia au hadithi fupi – mwandishi hujikuta amemuiga mwandishi au waandishi wa kazi fulani. Jambo hilo hutokea hivyo kusudi au hata bila kukusudiwa. Hata hivyo, haitakuwa sahihi kusema kuwa yupo mwandishi mmoja ambaye hakuathiriwa na kazi za mtunzi au watunzi wengine. Vivyo hivyo, hayupo mwandishi aliyefanikiwa katika uandishi wake bila kuzisoma kazi za wengine. Uandishi mzuri hutokana na usomaji mpana wa kazi za watunzi wengine. Usomaji huo haukamiliki pasi na kuathiriwa na kazi hizo. Waandishi huathiriwa na wengine kwa njia mbalimbali. Huathiriwa katika matumizi ya msamiati. Baadhi ya…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Mdau wa Kiswahili Kenya: Rais atuonyeshe mfano bora katika kuthamini Kiswahili

NA HENRY INDINDI  TUNAPOKARIBIA kuufunga mwaka huu, ninatamani kutangaza matumaini yangu katika mwaka ujao. Ninatamani sana kuwa na matumaini kwamba mwaka huo ujao, tutaweza kuwa na Baraza la Kiswahili nchini. Ninatumai pia kumwona Rais akijitokeza kama mfano bora kwenye usiku wa kuamkia mpya atakapoitoa hotuba yake. Yaani akiitoa hotuba yake katika Kiswahili na atuahidi kwamba hotuba zake za tangu hapo katika hafla za kitaifa atazitoa katika Kiswahili basi nami pamoja na walezi wenzangu wa Kiswahili tutafurahi sana. Lakini hayo ni matamanio na matumaini tu. Watekelezaji ni tofauti na sisi na huenda hawaishi katika ulimwengu wetu wakayaona mambo kwa jinsi tunavyoyaona…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Utamaduni na lugha ya Kiswahili

MARY WANGARI KWA mujibu wa msomi Mbaabu (1985), utamaduni unahusu mila, asili, jadi, na desturi za mavazi, vyakula, imani, tabia, na maisha ya jamii kwa jumla. Anasisitiza vilevile kuwa utamaduni ndiyo msingi wa fasihi. Katika makala hii, tutajikita katika uchambuzi na upambanuzi wa utamaduni wa Kiswahili ambao bila shaka, ndio kiini cha fasihi ya Kiswahili. Ni bayana kuwa hatuwezi kutathmini dhana ya utamaduni wa Kiswahili, pasipo kuwaangazia Waswahili nchini Kenya pamoja na kudadisi vipengele kadha muhimu kama vifuatavyo: Vipengele Muhimu katika Utamaduni wa Kiswahili 1. Uislamu ambao una nafasi ya kipekee katika imani na dini ya Waswahili wengi 2. Malezi…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Tunakivuruga Kiswahili kwa sababu hatukifahamu au makusudi?

Amani Njoka, Swahili Hub Mawasiliano ni mhimili wa kila kitu kinachofanyika katika maisha ya binadamu awaye yote, katika jamii na katika nyanja zote duniani. Zipo mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kufikisha ujumbe, taarifa au habari upande wa pili ikiwemo ishara, alama, picha na sauti zisizo na mpangilio kama miluzi na sauti zinazotumiwa na viumbe mathalani wanyama na ndege. Ili kukidhi haja ya mawasiliano kwa binadamu, kiliibuka kitu kinachoitwa lugha. Walimu wangu wa lugha ngazi zote nilizopitia walinijuza kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu (kubahatisha) zilizobuniwa na kukubaliwa miongoni mwa wanadamu katika jamii walizopo kama nyenzo ya mawasiliano miongoni mwao….

Soma zaidi..