Posted in Makala

KAULI YA MATUNDURA: Athari ya lugha za kigeni kwa Kiswahili na jinsi zilivyochangia kupanua leksikoni

Na BITUGI MATUNDURA MOJAWAPO ya vipengee muhimu ambavyo mwalimu na mwanafunzi wa isimujamii anahitajika kujua ni historia ya Kiswahili. Katika kuangazia historia ya lugha hii muhimu ya Afrika Mashariki na Kati, mwalimu na mwanafunzi wake hawawezi kukwepa suala la jinsi Kiswahili kimeathiri na kuathiriwa na lugha nyingine. Katika makala haya, ninaangazia jinsi wageni kutoka nje ya bara Afrika walivyochangia katika kuathiri Kiswahili. Athari ambazo hujitokeza wazi kwenye mada kama hii angalau huwa ni ya kileksikoni au msamiati. Miongoni mwa wageni wa awali kabisa kuwasili katika pwani ya Afrika Mashariki walikuwa ni pamoja na Waajemi, Wafarsi, Wamisri,Wachina na Waarabu. Utafiti wa…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Kuenea kwa Kiswahili: Ipo haja ya lugha kufundishwa katika kambi za wakimbizi

Amani Njoka, Swahili Hub Mkimbizi ni mtu aliyeondoka kwake nyumbani, nchi yake na mahali anapoishi kwa sababu ya kulazimishwa, kufukuzwa au kwa hofu ya kuteswa. Baada ya watu hawa kukimbia makazi yao hatimaye hukutana kambini wakitoka mataifa mbalimbali. Wamekimbia vita na majanga kadha wa kadha yanayotokea katika nchi zao na hatimaye kujikuta kwenye mataifa ya watu na hivyo wanakuwa ugenini aua wakati mwingine ndani ya nchi yao wenyewe. Tanzania inapokea wakimbizi kutoka nchi kama Burundi, Kongo, Rwanda na nchi nyingine nyingi zilizo nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakimbizi hawa baada ya kufika katika kambi mbalimbali kama Nyarugusu na kwingineko wanakuwa…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Fafanuzi na nadharia za fasihi

Na ALEX NGURE WANANADHARIA wengi wamelielezea neno hili fasihi. Kwa hakika fafanuzi na nadharia juu yake ni nyingi. Neno fasihi kama linavyoelezewa na wananadharia wote,laonyesha kiwango fulani cha makubaliano kwao kwamba fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia matendo na lugha inayotamkika na kuandikika ili kufikisha ujumbe wake kwa jamii iliyokusudiwa.Zifuatazo ni baadhi ya sifa za fasihi: Fasihi ni sanaa: Maana yake ni kuwa fasihi ni matokeo ya kiufundi. Kitu chochote kilichoundwa kwa ufundi hupendeza: huvutia na kuamsha hisia ndani ya mhusika. Hisia hizo zaweza kuwa michomo mbalimbali ambayo yaweza kutufanya tuchukie, tulie, tuhuzunike, tufurahi,tushangae n.k.Ili kazi yoyote ihitimu kupewa jina…

Soma zaidi..
Posted in Makala

KINA CHA FIKIRA: Twaweza kukimakinikia Kiswahili na kukisarifu ipasavyo madhali nia ipo

Na KEN WALIBORA BAADHI ya wasemaji wa Kiswahili hawana habari kuhusu tofauti iliyopo kati ya tunda la limao na ndimu. Ukienda sokoni kununua ndimu aghalabu utapewa limao Ajabu ni kwamba tatizo hilo halipo tu kwa wanunuzi bali hata kwa wauzaji wa matunda haya sokoni. Unaweza kukumbana na tatizo hilo, si hoja upo soko la Kongowea, Mombasa au Soko Mjinga kwenye eneo la Fly Over. Vile ninavyoelewa mimi katika Kiswahili changu duni, tunda linaloitwa kwa Kiingereza “lemon” ndilo kwa Kiswahili tunaliita limao. Kwa upande mwingine tunda lile linaloitwa “lime” katika Kiingereza ndilo katika Kiswahili tunaliita ndimu. Mchanyanyiko huu wa mambo kilugha…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya utafiti kidijitali katika ukuaji, maendeleo ya Kiswahili

Na MARY WANGARI KATIKA siku za hivi karibuni, wadau kadha wa Kiswahili wamejitokeza kulipigia debe suala la Kiswahili kuwa lugha rasmi si tu Kenya, bali pia Afrika Mashariki kwa jumla. Juhudi hizi zinapaswa kupongezwa na pia zinapaswa kuwa mwamko mpya kwa wadau wa Kiswahili kutilia maanani teknolojia ili kuimarisha nafasi ya lugha hii katika kizazi cha sasa. Kwa mintarafu hiyo, ni muhali kupuuza nafasi ya teknolojia katika ukuzaji na maendeleo ya Kiswahili ili kuweza kukidhi mahitaji ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika karne hii. Utafiti wa kidijitali pamoja na lugha mitandaoni ni baadhi ya masuala mapya ambayo yana nafasi muhimu…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Tathmini ya kina kuhusu matamshi katika Kiswahili

Na WANDERI KAMAU MATAMSHI yanayopaswa kufundishwa shuleni nchini Kenya ni yale ya Kiswahili sanifu. Je, tunapozungumzia matamshi ya Kiswahili sanifu, huwa hasa tunazungumzia matamshi ya aina gani? Je, yapo matamshi yanayoweza kuhusishwa na Kiswahili sanifu hapa nchini Kenya. Ikiwa yapo, tunaweza kuyatambua vipi? Matamshi ya Kiswahili sanifu hapa nchini Kenya yanaweza kuhusishwa na taasisi tofauti tofauti zinazotumia lugha ya Kiswahili. Shule, kwa mfano, ni miongoni mwa asasi hizo. Ingawa walimu tofautitofauti hutofautiana kwa jinsi wanavyotamka kwa sauti za Kiswahili, inafikiriwa kwamba walimu wengi wa lugha ya Kiswahili wanaweza kubainisha matamshi yaliyo sanifu kutokana na yale mengine. Si walimu peke yao…

Soma zaidi..