Posted in Makala

KINA CHA FIKIRA: Twaweza kukimakinikia Kiswahili na kukisarifu ipasavyo madhali nia ipo

Na KEN WALIBORA BAADHI ya wasemaji wa Kiswahili hawana habari kuhusu tofauti iliyopo kati ya tunda la limao na ndimu. Ukienda sokoni kununua ndimu aghalabu utapewa limao Ajabu ni kwamba tatizo hilo halipo tu kwa wanunuzi bali hata kwa wauzaji wa matunda haya sokoni. Unaweza kukumbana na tatizo hilo, si hoja upo soko la Kongowea, Mombasa au Soko Mjinga kwenye eneo la Fly Over. Vile ninavyoelewa mimi katika Kiswahili changu duni, tunda linaloitwa kwa Kiingereza “lemon” ndilo kwa Kiswahili tunaliita limao. Kwa upande mwingine tunda lile linaloitwa “lime” katika Kiingereza ndilo katika Kiswahili tunaliita ndimu. Mchanyanyiko huu wa mambo kilugha…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya utafiti kidijitali katika ukuaji, maendeleo ya Kiswahili

Na MARY WANGARI KATIKA siku za hivi karibuni, wadau kadha wa Kiswahili wamejitokeza kulipigia debe suala la Kiswahili kuwa lugha rasmi si tu Kenya, bali pia Afrika Mashariki kwa jumla. Juhudi hizi zinapaswa kupongezwa na pia zinapaswa kuwa mwamko mpya kwa wadau wa Kiswahili kutilia maanani teknolojia ili kuimarisha nafasi ya lugha hii katika kizazi cha sasa. Kwa mintarafu hiyo, ni muhali kupuuza nafasi ya teknolojia katika ukuzaji na maendeleo ya Kiswahili ili kuweza kukidhi mahitaji ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika karne hii. Utafiti wa kidijitali pamoja na lugha mitandaoni ni baadhi ya masuala mapya ambayo yana nafasi muhimu…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Tathmini ya kina kuhusu matamshi katika Kiswahili

Na WANDERI KAMAU MATAMSHI yanayopaswa kufundishwa shuleni nchini Kenya ni yale ya Kiswahili sanifu. Je, tunapozungumzia matamshi ya Kiswahili sanifu, huwa hasa tunazungumzia matamshi ya aina gani? Je, yapo matamshi yanayoweza kuhusishwa na Kiswahili sanifu hapa nchini Kenya. Ikiwa yapo, tunaweza kuyatambua vipi? Matamshi ya Kiswahili sanifu hapa nchini Kenya yanaweza kuhusishwa na taasisi tofauti tofauti zinazotumia lugha ya Kiswahili. Shule, kwa mfano, ni miongoni mwa asasi hizo. Ingawa walimu tofautitofauti hutofautiana kwa jinsi wanavyotamka kwa sauti za Kiswahili, inafikiriwa kwamba walimu wengi wa lugha ya Kiswahili wanaweza kubainisha matamshi yaliyo sanifu kutokana na yale mengine. Si walimu peke yao…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UCHAMBUZI: Kiswahili kinaweza kuwa Lingua Franka ya Dunia

Amani Njoka, Swahili Historia inaonesha kuwa biashara, dini, elimu, siasa na vyombo mbalimbli vilichangia sana kukieneza Kiswahili sehemu nyingi za Tanzania, Afrika Mashariki. Hata hivyo mambo hayo yameendelea kukieneza Kiswahili duniani na kukifanya kizidi kukubalika katika mataifa mengi kwa siku za hivi karibuni. Baada ya Kiswahili kuenea na kuendelea kuenea, hivi sasa lugha hiyo inatumiwa karibu kila sehemu duniani ingawa kwa uchache kwa baadhi ya sehemu. Nchi kadha wa kadha kama vile Sudan Kusini na Afrika Kusini zimeonesha nia ya dhati ya kutaka kujifunza Kiswahili ikiwemo kutaka kifundishwe mashuleni. Sababu kubwa ya serikali ya Afrika Kusini kufikia maamuzi hayo ni…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Vitabu vya Watanzania, kwa Watanzania viandikwe kwa Kiswahili kwanza

Nianze kwa kupongeza kazi nzuri za uandishi wa vitabu kadhaa ambavyo vimeandikwa na waandishi mbalimbali kuelezea maisha yao binafsi na ya kijamii jambo ambalo linatoa hamasa kwa watu wengi pale ambapo vitabu hivyo vitasomwa hasa ukizingatia umashuhuri, umaarufu na ushawishi wa watu hao kwa jamii. Kwa kweli ni jambo la kupongeza sana. Uandishi huu ni muhimu kwani wasomaji hupata maarifa na kufahamu mbinu mbalimbali, changamoto na mafanikio ya waliyoyapa watu hao. Waandishi hawa wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao kutoa kile walichonacho kwa kutumia lugha iliyokuwa rahisi kwao. Ni ukweli usiopingika kwamba lugha ni mhimili mkubwa kwa jamii yoyote. Ni…

Soma zaidi..
Posted in Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya Kiswahili kama lugha rasmi na ya taifa

Na ALEX NGURE LUGHA ya taifa ni lugha inayotumika katika taifa fulani kwa shughuli za kitaifa kama vile mikutano ya kisiasa. Kimsingi, ni lugha inayoleta mshikamano wa kitaifa. Aghalabu hutumiwa kwa utambulisho wa taifa mbali na kazi ya msingi ya mawasiliano. Kwa mujibu wa Prof J Habwe na wenzake (2010), Lugha ya taifa ni lugha inayotumiwa kuwaleta pamoja watu wenye historia na asili moja, au makundi ya watu wamoja waliofungamana na kuwa na tabia na nyendo ambazo zina manufaa kwa wote. Katika Kenya na Tanzania, Kiswahili ni lugha ya taifa na rasmi vilevile. Chiraghdin (1977), Fishman (1968), Eastman(2001) na Greenfeld…

Soma zaidi..