Posted in Makala

Serikali ichukue ombi shule chache za mfano kufundisha kwa Kiswahili

Gadi Solomon, gsolomon@tz.nationmedia.com HIVI karibuni Serikali imesema wanafunzi katika shule 16 nchini watafanya mtihani wa taifa kidato cha nne wa Lugha ya Kichina. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Avemaria Semakafu wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya Kichina Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro, alisema kwamba kutokana ushirikiano wa China na Tanzania, Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeona umuhimu wa lugha hiyo kufundishwa shuleni na vyuoni. Hiyo ni hatua kubwa kwa nchi yetu kuweza kufungua milango kufanyia mtihani wa Taifa lugha za mataifa mengine. Pia ni fursa kwa sababu China kwa kuwa imeendelea  kupanua wigo…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Tukipeleke Kiswahili Afrika Kusini, tujifunze namna ya kuandaa makongamano

NA CAESAR JJINGO Huku nchi ya Afrika Kusini ikiazimia kuanza kufundisha Kiswahili kwenye shule za nchi hiyo, wadau wa Kiswahili kutoka nje na ndani Afrika Mashariki,  wanepania kufanya msururu wa makongamano ya Kiswahili. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimekwisha kusambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, makongamano hayo yataandaliwa katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki;  Kenya, Uganda na Tanzania. Makongamano hayo ni pamoja na kongamano la nne la Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA), katika Chuo Kikuu cha St. Augustine, Mbeya (Tanzania-Bara). Mkutano huo wa siku mbili kati ya Agosti 2-3 mwaka huu. Kongamano la pili ni…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Nafasi ya ushairi kudumisha Kiswahili

Na Chris Adungo Ushairi wa Kiswahili una historia ndefu na unaendelea kustawishwa kifani, kiumbuji na kimaudhui (Masinde 2003) katika kitabu chake “Mielekeo ya Ushairi”. Hali hii imetokana na dhima ya utanzu huu katika jamii za Afrika Mashariki zinazotumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kwa mapana na kitaifa. Kwa mfano, hapo awali, ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa kimasimulizi na baadaye ukaanza kutungwa kimaandishi miongoni mwa jamii za Waswahili zilizoishi katika upwa wa Afrika Mashariki. Kiswahili kilipoenea na kuwa maarufu katika mataifa ya Afrika Mashariki, ushairi wa Kiswahili ulitungwa kwa kuzingatia utamaduni na jamii pana. Haya ni kwa mujibu wa Gesero katika…

Soma zaidi..
Posted in Makala Uchambuzi

Mambo matano wataalamu wa Kiswahili wafanye kulishika soko la ajira duniani

Gadi Solomon Hivi karibuni tumesikia jinsi fursa za ajira na kiuchumi kwenye Kiswahili zinavyozidi kufunguliwa nje ya mipaka ya Tanzania. Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (KAKAMA) pia hivi karibuni, imefungua wigo kwa wataalamu wa Kiswahili kupata fursa ya kubadilisha uzoefu wa kitaaluma. Lengo la fursa hiyo ni kuleta utangamano kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kamisheni hiyo imelenga kusimamia na kuratibu maendeleo ya Kiswahili katika taasisi mbalimbali, asasi na mashirika binafsi ili kuhakikisha Kiswahili kinaleta mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kijamii. Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kipekee amehakikisha anakitangaza Kiswahili katika nchi…

Soma zaidi..
Posted in Makala

Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari na elimu ya juu.

Kwa muda mrefu, kumekuwapo na mjadala mrefu kuhusu kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kutokana na mijadala hii mwaka 1976 Baraza la Kiswahili la Taifa liliamua kufanya utafiti kuhusu hali halisi ya ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari. Maeneo muhimu yaliyozingatiwa ni nafasi ya Kiswahili katika uchumi, sayansi na teknolojia, afya , elimu, habari na mawasiliano na sheria. Kiswahili katika shule za msingi: Kiswahili ni lugha ya kufundishia katika shule za msingi na Kiingereza somo la kawaida linalofundishwa kuanzia darasa la 111. Kiswahili katika shule…

Soma zaidi..