Posted in Mashairi

Lugha yetu

Bismilah ninaanza, Kukuomba Rahmani, Mwenye wingi wa majaza, Asubuhi na jioni, Utujalie kukuza, Lugha yetu ya thamani, Kiswahili tukithamini, Kipate yake heshima.

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Uke wenza

Uke wenza Litege lako sikio, nipate kusimulia, Yalonisibu mwenzio, katika hii dunia, Moyo wanienda mbio, sijui pa kuanzia, Kumpenda nampenda, uke wenza sitaweza. Hadithi yangu ya kweli, leo nakuhadithia, Yanichanganya akili, kila nikifikiria, Lengo kukwambia hili, uweze nisaidia, Kumpenda nampenda, uke wenza sitaweza. Kuna bwana mvulana, jina nitakutajia, Siku aliponiona, moyoni akaingia, Akaniambia bayana, moyo umekuridhia, Kumpenda nampenda, uke wenza sitaweza. Siku zikazidi kwenda, nikaja mtamkia’ Kwamba nami nakupenda, jibu ninakupatia, Uendako nitakwenda, wala sitakuachia, Kumpenda nampenda, uke wenza sitaweza. Hapo hakuficha kitu, wazi akaniambia, Mimi ni mume wa mtu, hivyo nina familia, Nina watoto watatu, mke amenizalia, Kumpenda nampenda,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

MALENGA NAYANGU NANE, NAONGEZA YAWE KUMI

1.Nimekuja ninayangu, imefurika dayari, Sisemi siri za watu, niko kwenye msitari, Hapa takumbusha vitu, wala sisemi na kiti, Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi. 2.Kwani huku sio kwetu, mbona kama utumwani, Waliobeba mitutu, wanalilia sikonzi, Jamaa wa bakurutu, amenitoa machozi, Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi. 3.Ni ya ule mwaka tuu, yasojirudia rudi, Tutakumbuka mabutu, na ile ya mawe keki, Ninalikataa gundu, naeleza umakini, Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi. 4.Hapa roho yangu kwatu, nikiyatoa machozi, Bora kulilia buku, kuliko shilingi sitini, Nimeyaona nadubu, yenye sura staili, Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi. 5.Sasa tano toka matatu, ninasubiria chenji, Nakwambia…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

MAISHA NA UMAUTI

MAISHA NA UMAUTI1. Mwanadamu ni maua, mwanadamu ni majani,Akiwa anapumua, furaha ulimwenguni,Asubuhi huchanua, na kunyauka jioni,Maisha na Umauti, Tuwe Mali Yake Mungu. 2. Siku alipozaliwa, watu walifurahia,Mungu alishukuriwa, pia tulishangilia,Sasa leo katwaliwa, tusione ni kadhia,Maisha na Umauti, Tuwe Mali Yake Mungu. 3. Kila kinachoingia, kutoka pia lazima,Hakuna wakukimbia, wala wa kushika tama,Siku ikishawadia, haiwezi rudi nyuma,Maisha na Umauti, Tuwe Mali Yake Mungu. 4. Mwenzetu ameshatoka, sote tumehuzunika,Mwili wake twauzika, upate kupumzika,Mwenzetu aliokoka, anakwenda farijika,Maisha na Umauti, Tuwe Mali Yake Mungu. 5. Mwenzetu katangulia, leo twamsindikiza,Japo kuwa tunalia, mwendo ameumaliza,Nasi tutafuatia, ni vema kujiuliza,Maisha na Umauti, Tuwe Mali Yake Mungu. 6….

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Kidani chaniunguza

Ulikuwa mwezi Machi, wa tatu kwa Kingereza, Nilipofungua pochi, japo za kudunduliza, Pesa zangu mwananchi, sikuhofu kupoteza, Kidani chaniunguza, naomba yenu maoni. Mitaa ya katikati, siku nilipokatiza, Kwa uzuri wa bahati, nakuta wakitembeza, Kidani chema fedhati, moyo kilinipendeza, Kidani chaniunguza, naomba yenu maoni. Ni wakati wa baridi, kipupwe kinafukiza, Sikuwaza ya zaidi, muda ukapitiliza, Kulipia ilibidi, kuvaa sikukawiza, Kidani chaniunguza, naomba yenu maoni. Nilitamba pande zote, kila nilipokatiza, Sifa ngoja zinifate, kwa kweli chakupendeza, Kichwa kikabaki bwete, nabaki kukidekeza, Kidani chaniunguza, naomba yenu maoni. Hivi sasa Septemba, sita nimeshatimiza, Mwezi wa jua sambamba, sasa linahanikiza, Linaunguza mashamba, wakulima lawaliza, Kidani…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Pumzika kwa amani, Muhammed Seif Khatib

Pumzika kwa amani, Muhammed Seif KhatibMsiba huu mzito, Hassani niseme nini,Nalia kama mtoto, yanikatika maini,Bingwa kaitika wito, amerudi kwa Manani,Pumzika kwa amani, M. S wa Khatib. Kwenye lugha ulitamba, asiyejuwa ni nani,Ukatajika ni mwamba, lughani huna kifani,Simanzi imetukumba, tulio bara na pwani,Pumzika kwa amani, M. S wa Khatib. Kitabu WASAKATONGE, ni chako twakibaini,Kimefichua mazonge, na maovu si utani,Umezima kama mwenge, Muhamedi muhisani,Pumzika kwa amani, M. S wa Khatib. Na FUNGATE YA UHURU, kimezitwaa medani,Kitabu chema na huru, chenye mashairi ndani,Hae! Imezima nuru, Waswahili tu gizani,Pumzika kwa amani, M. S wa Khatib. TAARAB ZANZIBARI, ni kitabucho makini,Kimetupasha habari, na mapisi ya…

Soma zaidi..