Posted in Mashairi

Uyatima sikuita

1. Salamu kwenu natuma, wenza wangu viokote, Niweleze wimawima, nifute machozi yote, Ini laniumauma, yao sumu ni ya mate, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 2.Nilijipata kilema, tano ya kwangu miaka, Sikuyaelewa jama, kiguu kujafanyika, Kumbe! Amu nayatema, likata sije rithika, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 3.Mali ya baba na mama, kwa ulafi ‘lichukua, Nami kuniandama, cha kwangu kukitegua, Kitwana kachwa waama, pasi haki zingatia, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 4.Ukongo wewe natema, weye nakulaumu, Saratani siko wima, wazazi sasa hatamu, Nalia ila hatima, ni kuitika ya sumu, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya?

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Ushairi haujafa

Na Msimbe Chamdula (Answar –Badr) 1. Sheikh Mataka kipenzi, ninakupa taarifa, Wanaokufa watunzi, ushairi haujafa, Ushairi ni kiunzi, katika letu taifa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 2.Ushairi ungezikwa, yangetangazwa maafa,  Matanga yangetandikwa, siku tatu takrifa, Mshairi humbukwa, wakati anapokufa. Ushairi haujafa, waliokufa watunzi. 3.Tupo tulobaki tupo, tupo bado kutwita Raufa, YOB Mitimingi yupo, Side mwana falsafa, Mazengo katika jopo, bado akalia sofa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 4.Kitu huwa cha msingi, kinapojengewa sifa, Utapoweka vigingi utashindwa ziba ufa, Tanajua siku nyingi, mnatunyoa sharafa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 5.Dharau zikiwa nyingi, huondoa maarifa, Mpenda mema hapingi, ndio nzuri harifa, Kisha mbuyu hakaangi, hawezi…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Kiswahili ni asili

Lugha iliyonawiri, leo inadidimia, Potofu zilizojiri, lugha kutuharibia, Ilizidi kushamiri, zama ilipotokea, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Chanzo kilipoanzia, ubovu kupindukia, Mitandao asilia, wengi tumetumia, Lugha wanajifungia, kisha inaendelea, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Kama kawa naileta, wapi ilipoanzia, Kamusi sijaikuta, kila nilipopitia, Acheni wenu utata, lugha kutuchafulia, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Bamaji hatamwagika, nabaki kuangalia, Mnazidi kupinduka, asili mnakimbia, Isije ikatoweka, kibovu kikaenea, Kiswahili ni asili, acha kukiharibia, Wengi wanakitamani, nyinyi mnakifukia, Lugha hii ya thamani, wengine hamjajua, Basata mpo makini, mzidi kutuenzia, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Nizidi kujifunza, Kiswahili kutumia, Nisije nikajiponza, lugha kujiharibia, Wazee waliitunza,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

SIKIO LA KUFA

Usipouziba ufa, utaujenga ukuta, Usipokwepa maafa, dhahama itakupata, Biashara ni taarifa, kabla hasara kupata, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Ukafunzwa na wazazi, kabla ya ulimwengu, Tena wakaweka wazi, yasikupate machungu, Kuinama sio kazi, ukitaka cha uvungu, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Mama aliuza uji, ili uende shule, Baba ni fundi gereji, uvae vizuri ule, Kukidhi lako hitaji, usiku vema ulale, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Ukasoma hadi chuo, kisha kapata ajira, Mepata maendeleo, tajiri mwenye ngawira, Kazini mepanda cheo, bosi kampuni bora, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Sasa umebadilika, mekuwa mmarekani, Mjini umejiweka, hutaki rudi nyumbani,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

1.Idd iwe na Amani (Ombi)

Na Yahya O. Barshid Naanza Bismillah, kwa nguvu zake Wadodi, Ni sikukuu Wallahi, inayokuja na Idd Kwa Amani tufurahi, Amani iwe juhudi Idd iwe na Amani. Mwezi huu mtukufu, waramadhani swaumu, Mwezi hu maarufu una wake umuhimu, Hivyo tuwe wakunjufu, Kumshukuru Kkaumu, Idd iwe na Amani. Idd iwe na Amani, ninaomba utulivu, Tufate ya Qurani, ni kitabu chenye nguvu, Tusalihusende motoni, tusigeuke majivu, Idd iwe na Amani Siku hizi thelathini, zakaribia kuisha, Twendeni msikitini, mafupi yetu maisha, Idd iwe na Amani. Sinunie Kiswahili Na Bryan Rop Kimutal (Nakuru, Kenya). Maisha haya kwa hatua, soma anga hujatua, Kabula kusukutua hepuka kujishaua,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

HUWEZI KUTIBU MAITI

Assalam allaykum, naisalim jamia, Nasalim binadam, viongozi wa dunia, Salam ya Isilam, salama iliyo dua, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Maneno ya aghalabu, na akili za kitume, Sineni yalo ghadhabu, vibaya msiniseme, Kinywa cha kistaarabu, mekuja kutoa shime, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Mwana mwenda mwele, pitia huku chukule, Mwana wewe mvimbele, kaulilo waambile, Hayafi yalo yalele, ukufi utuzingatile, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Vipi tuchimbe kaburi, maiti tuzifukue? Na tena watanabahari, eti tiba upatie, Maiti haiwi nzuri, ukweli tuupokee, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Kufa wamekufa wengi, tena wakafa kibudu, Jambo liliso msingi, hawakuwa waabudu,…

Soma zaidi..