Posted in Mashairi

Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar:Kuingia kwa ukoloni wa Kiarabu

Na Muhammed S. Khatib (2) Wa kwanza mtangulizi Alojipa uongozi Kuanzisha ujambazi Kwa jina nawatajiya Huyo Seyyid Said Babaye Ahmedi Aliyetoka baidi Kuja kututawaliya Huku kavutiwa na mengi Ya faraja na msingi Hakuyagundua kwingi Ndipo akatufikiya Kwanza lililomvuta Si nchi yenye matata Tena haipendi vita Ila yapenda umiya La pili maji matamu Yasomwisha mtu hamu Na ladha yake timamu Meupe ya kuvutiya La tatu yake bahari Imetuliya shuwari Vyombo na zake ayari La nne ni biashara Kwetu imetiya fora Muhali kula hasara Bidhaa kuzifanyiya La tano ni atashiba Kwa ardhi ya rutuba Itampa matilaba Vipando vitaeneya Saidi bin Sultani Akabaki…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Maelezo ya utangulizi kuhusu Mashairi

Lugha ya Kiswahili ina tanzu zake za Kifasihi hususan katika usimulizi. Utanzu mkongwe kuliko zingine ni ushairi. Ushairi ulikuwapo  karne nyingi kabla ya ujio wa wageni kuja pwani ya Afrika Mashariki. Kwa mfano tungo za Fumo Luyongo ni miongoni mwa ushauri wa zamani katika upwa wa Afrika Mashariki kabla ya kuja kwa Waarabu. Waswahili walijulikana  kwa majina ya jamii zao za asili za kibantu kama vile Walamu, Wapate, Wapemba, Wadigo, Wavumba, Waunguja, Wangazija, Watumbatu nk. Kihistoria tungo za fasihi ya Kiswahili hususan ushairi zilihifadhiwa katika hati ya Kiarabu.  Utanzu wa ushairi una historia ndefu miongoni mwa tanzu zote za kifasihi….

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

SOKOMOKO: Wasichana wala hela

1. WASICHANA ni wazuri, ukikuwa nazo pesa, Shababi muwe tayari, kwepuka hii mikasa, Mnatupandisha mori, hamuoni ni makosa, Tumechoka nazo simu, kila wakati ni hela. 2. Wasichana mumezidi, wanaume walalama, Mwavunja hata ahadi, wanabaki kuwasema, Haja yenu si akidi, moyoni mnatuchoma, Tumechoka nazo simu, kila wakati ni hela. 3. Wasichana fikiria, wavulana wajipanga, Fulusi mwaangalia, mwafikiri ndio mwanga, Akina dada tulia, maisha ni kujipanga, Tumechoka nazo simu, kila wakati ni hela. 4. Wasichana fahamuni, tabia ni ya maana, Msianguke shimoni, hela ni kama laana, Mkiweka fikirani, mtajipata mwasona, Tumechoka nazo simu, kila wakati ni hela. LIONEL ASENA ‘Malenga Kitongojini’ Seeds…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Uyatima sikuita

1. Salamu kwenu natuma, wenza wangu viokote, Niweleze wimawima, nifute machozi yote, Ini laniumauma, yao sumu ni ya mate, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 2.Nilijipata kilema, tano ya kwangu miaka, Sikuyaelewa jama, kiguu kujafanyika, Kumbe! Amu nayatema, likata sije rithika, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 3.Mali ya baba na mama, kwa ulafi ‘lichukua, Nami kuniandama, cha kwangu kukitegua, Kitwana kachwa waama, pasi haki zingatia, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya? 4.Ukongo wewe natema, weye nakulaumu, Saratani siko wima, wazazi sasa hatamu, Nalia ila hatima, ni kuitika ya sumu, Uyatima sikuita, mbona yanipate haya?

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Ushairi haujafa

Na Msimbe Chamdula (Answar –Badr) 1. Sheikh Mataka kipenzi, ninakupa taarifa, Wanaokufa watunzi, ushairi haujafa, Ushairi ni kiunzi, katika letu taifa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 2.Ushairi ungezikwa, yangetangazwa maafa,  Matanga yangetandikwa, siku tatu takrifa, Mshairi humbukwa, wakati anapokufa. Ushairi haujafa, waliokufa watunzi. 3.Tupo tulobaki tupo, tupo bado kutwita Raufa, YOB Mitimingi yupo, Side mwana falsafa, Mazengo katika jopo, bado akalia sofa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 4.Kitu huwa cha msingi, kinapojengewa sifa, Utapoweka vigingi utashindwa ziba ufa, Tanajua siku nyingi, mnatunyoa sharafa, Ushairi haujafa, wanaokufa watunzi. 5.Dharau zikiwa nyingi, huondoa maarifa, Mpenda mema hapingi, ndio nzuri harifa, Kisha mbuyu hakaangi, hawezi…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Kiswahili ni asili

Lugha iliyonawiri, leo inadidimia, Potofu zilizojiri, lugha kutuharibia, Ilizidi kushamiri, zama ilipotokea, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Chanzo kilipoanzia, ubovu kupindukia, Mitandao asilia, wengi tumetumia, Lugha wanajifungia, kisha inaendelea, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Kama kawa naileta, wapi ilipoanzia, Kamusi sijaikuta, kila nilipopitia, Acheni wenu utata, lugha kutuchafulia, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Bamaji hatamwagika, nabaki kuangalia, Mnazidi kupinduka, asili mnakimbia, Isije ikatoweka, kibovu kikaenea, Kiswahili ni asili, acha kukiharibia, Wengi wanakitamani, nyinyi mnakifukia, Lugha hii ya thamani, wengine hamjajua, Basata mpo makini, mzidi kutuenzia, Kiswahili ni asili, acha kutuharibia. Nizidi kujifunza, Kiswahili kutumia, Nisije nikajiponza, lugha kujiharibia, Wazee waliitunza,…

Soma zaidi..