Posted in Mashairi

Washairi Tanzania

Na Nyembo Atwai Nyembo Hadi hodi gazetini, kwenu naja kurasani, Niweke japo pembeni, nisomeke hadharani. Niyatowe ya moyoni, kwa washairi nchini, Washairi Tanzania, tengenezeni umoja. Ni kweli yasopingika, kutengeneza kikundi, Washairi kuunganika na kutoweka kilindi, Mwisho tutanufaika, kwa kupitia kikundi, Washairi Tanzania, tengenezeni umoja. Mbetumbetu tuwe moja, shime na tubebe dhima, Nguvu yetu kuwa moja, tujenge yaliyo mema, Kikundi ni nguvu moja, kwa kauli ya Karima, Washairi Tanzania, tengenezeni umoja. Wa bara na visiwani, wote tuwe kundi moja, Tukitoka hadharani, na tulonge lugha moja, Jahazi litoke chini, kwa nguvu jasho kuvuja, Washairi Tanzania, tengenezeni umoja. Watunzi wale watangu, na hawa…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

SIKIO LA KUFA

Usipouziba ufa, utaujenga ukuta, Usipokwepa maafa, dhahama itakupata, Biashara ni taarifa, kabla hasara kupata, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Ukafunzwa na wazazi, kabla ya ulimwengu, Tena wakaweka wazi, yasikupate machungu, Kuinama sio kazi, ukitaka cha uvungu, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Mama aliuza uji, ili uende shule, Baba ni fundi gereji, uvae vizuri ule, Kukidhi lako hitaji, usiku vema ulale, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Ukasoma hadi chuo, kisha kapata ajira, Mepata maendeleo, tajiri mwenye ngawira, Kazini mepanda cheo, bosi kampuni bora, Sikio lako la kufa, halitosikia dawa. Sasa umebadilika, mekuwa mmarekani, Mjini umejiweka, hutaki rudi nyumbani,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

HUWEZI KUTIBU MAITI

Assalam allaykum, naisalimu jamia, Nasalimu binadam, viongozi wa dunia, Salamu ya Isilam, salama iliyo dua, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Maneno ya aghalabu, na akili za kitume, Sineni yalo ghadhabu, vibaya msiniseme, Kinywa cha kistaarabu, mekuja kutoa shime, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Mwana mwenda mwele, pitia huku chukule, Mwana wewe mvimbele, kaulilo waambile, Hayafi yalo yalele, ukufi utuzingatile, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Vipi tuchimbe kaburi, maiti tuzifukue? Na tena watanabahari, eti tiba upatie, Maiti haiwi nzuri, ukweli tuupokee, Kutibu tibu mgonjwa, huwezi tibu maiti. Kufa wamekufa wengi, tena wakafa kibudu, Jambo liliso msingi, hawakuwa waabudu,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Kijogoo wachekesha

MASHAIRI YA MALUMBANO Na Gora Haji Shairi la Malumbano limetungwa na gwiji wa mashairi kutoka Kisiwani Tumbatu huko Zanzibar kwa jina la Haji Ghora. Alizaliwa Mtaa wa Kokoni, Kisiwa cha Tumbatu mwaka 1933. Haji Gora anaamimi kuwa mashairi ya malumbano ni mtindo wenye faida nyingi. Kwanza ni kwa ajili ya kuwa na mafumbo ili kufumbuliwa. Hatua hii inasaidia uelewa na kukuza kiwango cha uchambuzi. Pili husaidia kujenga kiwango cha kujenga hoja. Tatu huweza kuchota elimu ya uchangiaji na usambaza kwa umma. Kwa utamaduni wa Waswahili, mashairi ya malumbano yapo sehemu nyingi. Kwanza kwenye ngoma za asili, ambapo wale manju hurushiana…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Wachawi saidieni

Sifa zenu naamini, zimeenea mjini, Kadhalika vijijini, pia kote duniani, Kwa kweli twawaamini, ila bado kuwathamini, Wachawi saidieni, tupate maendeleo. Mtunzi nimebaini, mna mengi kwa yakini, Mwaweza fanya nchini, uchumi usiwe duni, mkaongeza thamani, dunia kututhamini, Wachawi saidieni, tupate maendeleo. Tunataka televisheni, zenye bei afueni, Mwazitengeza nyumbani, hamuuzi madukani, Tunachotaka maishani, hizo ziwe mitaani, Wachawi saidieni, tupate maendeleo. Mwazungumza hewani, ila simu hatuoni, Nalo hili twaamni, ni biashara auni, Zije simu za mkononi, tuwe nasi washindani, Wachawi saidieni, tupate maendeleo. Finland na Marekani, kwa Nokia ni makini, Matorola nayo ndani, ya kwetu iwe akilini, Tuuite jina gani, pengine la majinuni,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Shati limenitenda

Na Magdalena Maregesi Shati langu nilipenda, nilipata kwa amana, Nalivaa kwa kupenda, kwa marefu na mapana, Moyoni shati napendawa ungwana nimenena Ghafla limetoweka, Amani moyoni sina. Hadhi ya shati kupanda, kulipa yangu hazina, Upendo nikaupanda, mwilini kushikamana, Thamaniye sijaponda nivaapo naiona, Ghafla limetoweka, Amani moyoni sina. Rangiye niliipenda, yavutia na vimwana, Kosa kumbe nilitenda, kulipa yangu dhamana, Laazimwa na kiranda, Ilala hadi Banana. Ghafla limetoweka, moyoni Amani sina. Kwa nini limenitenda mwilini sijalikana, Umeniweka kidonda, naumia sana sana, Hasira zimenipanda, kutoweka yangu dhana, Ghafla limetoweka, moyoni Amani sina. Hakika sijampenda, mtu alonipokonya, Dukani nipokwenda, mimi pekee bila wana, Nikanunua kwa…

Soma zaidi..