Posted in Mashairi

TENZI:Bismillah kadimu

Kwa upande wa tenzi, Ghora Haji ameandika nyingi na anakiri kuwa idadi ya tenzi alizowahi kuandika ni 50 au zaidi. Kwa hakika anakiri kuwa alichelewa kuingia katika rubaa ya tenzi na utenzi wake wa mwazo ulikuwa ni ule wa Visa vya Nabii Suleiman bin Daud (SAW) kuhusu maisha yake. Ghora alijaribu kufuata nyayo za watunzi waliomtangulia kama Bin Faqih aliyeandika utenzi wa Rasil Ghul na Kadara Bakathir aliyeadika Utenzi wa Inkishaf. Moja ya sifa ya mtunzi wa utenzi ni kufanikiwa kuzipanga vyema beti zake za ufunguzi ambazo hujumuisha maamkizi kama ada lakini pia kuelezea dhamiri ya tungo zake na kuonesha…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

MASHAIRI NA TENZI ZA GHORA

MASHAIRI NA TENZI ZA GHORA Ghora Haji amekuwa akitunga mashairi na tenzi mbalimbali kuhusu matukio. Mojawapo ya shairi alilolikumbuka ni lile la maradhi ya kipindupindu na kusomwa katika Redio ya Sauti ya Tanzania Zanzibar lililosema: Mungu twaomba kwako, wewe ndie uombwaye, Utufu moja wa kwako, kherizo zitushikiye Maradhi yenye vituko, hima tuhamishiye Kitoke kipindupindu, kifukuze kikimbie, Maradhi hayo matundu, kwetu yatuondokee, Yabanduwe bandu bandu, kwa kote yasibakie, Makubwa hayo maafa, illahi tubanduliye, Hatunayo maafa, twakutegemeya weye, Tuondolee kalifa, ili isitufyagiye. Kitoke hima kitoke, kitowe kitokomeye, Uzima utubandike, firaha zituingie, Waume kwa wanawake, nyoyo zetu zituliye. Vifo vimetiya fora, Manani tuhurumiye,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Kweli ni mchapa kazi

Na Rehema M Chadoe Nasimama uwanjani, nitoe yangu maoni, Hana hata majinuni, awapo kwake kazini, Amjalie Manani, nguvu sisizo kifani, Kwali mchapakazi, katwambia si utani. Ni mpole kwa usoni, mchappa kazi mmakini, Akitoka ofisini tembea tabu haoni, Ukipima kwa mzani ni vit havilingani, Kweli mchapakazi katwambia si utani. Hapa kazi tu semeni na kzi hazifanani, Hakuongea kwa undani katangaza hadharani, waume kawambieni, pamoja na wanandani, Kweli mchapakazi katwambia si utani Mkono tumuungeni, ni baba mwenye imani, Wote shirikianeni taifa tulijengeni, Mikanda tujifungeni, tuchape kazi jamani, Kweli mchapa kazikatwambia si utani. Sio kutwa mitaani, bangi ipo mifukoni, Lawama serikalini maslahi hatuoni,…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

HONGERA IDDI MBARAKA

Nawapa wote hongera, wa pwani hadi wa bara, Waumini wa Tabora, hadi mji wa Mtwara, Hongera na Ifakara, na ndugu wote Kagera, Iddi Mbaraka hongera, amani iwe imara. Hongera wa Morogoro, na kule Kilimanjaro, Hongera wa Mvomero, Kidodi na Kilombero, Pasiwepo na kasoro, hongera na wa Comoro, Iddi Mbaraka hongera, amani iwe imara. Hongera ndugu Dodoma, pamoja na Mzizima, Sikusahau Musoma, na waumini Kigoma, Waume na kina mama, nawatakia uzima, Iddi Mbaraka hongera, amani iwe imara. Hongera ndugu Iringa, na waumini wa Tanga, Sikusahau Shinyanga, msiseme ninaringa, Na Mungu Atawakinga, muepuke kila janga, Iddi Mbaraka hongera, amani iwe imara. Hongera…

Soma zaidi..
Posted in Mashairi

Sukari ama chumvi?

Na Mohamed Abdallah Kidevu (Likoni) Nakuomba editori, utangaze vitu hivi, Naandika ushairi, kwa furaha si ugomvi, Asili ya kusubiri, ni utowe utauvi, Ama sukari na chumvi, chumvi ni kitu muhimu. Sababu kuwa muhimu, takupa mfano wake, Mchuzi hauna tamu mpaka chunvi uweke, Kweli sukari tamu, bali chumvi peke yake, Ama sukari na chuvi, chumvi ni kitu muhimu. Iwapo iko sukari, chumvi hamna nyumbani, Wali hauwi mzuri, hata ukafanya nini, Hula huku wafikiri, ukaombe majirani, Ama sukari au chumvi, chumvi ni kitu muhimu. Na sukari hutumiwa, kwa vitu vya ufahari, Nayo chai huchukiwa kama haina sukari, Na kirimu ya maziwa, ikosapo…

Soma zaidi..