Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Samia apongeza Bunge la Kenya kutumia lugha ya Kiswahili

Gadi Solomon, Mwananchi Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelipongeza Bunge la Kenya kwa kuazimia kutumia Kiswahili ndani ya Bunge. Rais Samia ameyasema hayo Jumatano Mei 5, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Kenya kwenye ziara ya kikazi siku mbili nchini humo. “Tulifurahishwa zaidi na uamuzi wenu wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili ndani ya Bunge. Na ndicho kinachonifanya mimi nisikilize Bunge la Kenya. Nainjoy kile Kiswahili kile. Kiswahili chenu kinavionjo vingi kuna vionjo vyake ambavyo peke yake ni burudani tosha kusikiliza,” alisema Rais Samia. Amesema anapenda kusikiliza Bunge la Kenya kwa sababu yanayojadiliwa mle pia nasi…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Waandishi watangaziwa fursa Tuzo za Mabati Cornell ya Fasihi 2021

 Gadi Solomon, Mwananchi Waandaaji wa mashindano ya Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika yatakayofanyika kwa mara ya sita mwaka huu wamewataka waandishi mbalimbali wa vitabu kutuma miswada yao.  Tuzo hii, iliyoanzishwa mwaka wa 2014 na Dk Lizzy Attree (Short Story Day Afrika) na Dk Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani), ina madhumuni ya kuhimiza uandishi kwa lugha za Kiafrika, na kuhimiza sanaa ya tafsiri kutoka lugha za Kiafrika, baina ya lugha za Kiafrika, na kwa lugha za Kiafrika. Baada ya kusimamisha Tuzo ya Mabati-Cornell mwaka 2020 kwa sababu ya janga la Covid-19, miswada iliyopelekwa mwaka…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Sheria 450 kuwa kwa Kiswahili Desemba mwaka huu

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanza kuzitafsiri sheria kuu 450 zilizotungwa kwa lugha ya Kiingereza ili ziwe kwa lugha ya Kiswahili kuanzia mwishoni mwa mwaka huu. Mwandishi Mkuu wa Sheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro katika Mkutano wa  Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo. Alisema kuanzia sasa sheria zitakazotungwa bungeni zitakuwa kwa lugha ya Kiswahili. Njole alisema mchakato wa kuzitafsiri sheria zilizopo zilizotungwa kwa Kiingereza unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu. Alisema baada ya kukamilika kwa sheria hizo kuu, kazi itakayofuata ni kuzitafsiri sheria ndogo 30,000 zilizotungwa na taasisi,…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Mkalimani hotuba za viongozi Dodoma awaomba radhi Watanzania

Gadi Solomon, Mwananchi Dar es Salaam. Mkalimani  Matungwa Lwamwasha amekiri kupotosha fasili ya kile ambacho kilikuwa kinazungumzwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa siku ya kuaga mwili wa Hayati John Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Lwamasha amesema hata hivyo baada ya kutokea kwa dosari hiyo alitoa taarifa haraka kutokana na  tafsiri potofu aliyoitoa. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena kinachorusha na kituo cha Redio Clouds, Lwamasha amesema chanzo cha tatizo ni kutokana na kutokuwepo vifaa vya kusikilizia pia kukosekana spika karibu yake, hivyo kulazimika kusikiliza sauti iliyokuwapo uwanjani hapo na wakati mwingine ilikuwa inakatakata.  Alisema baada ya…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Magufuli afariki dunia

Na Mwandishi Wetu Ni huzuni kwa Watanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amefariki dunia. Akitangaza taarifa ya msiba huo, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu alisema Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam. Alisema alilazwa Machi 06, 2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa Machi 7 na kuendelea na majukumu yake. “Machi 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta, nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti,” Makamu wa Rais Mama…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Milango ya Kiswahili yafunguliwa rasmi SADC

Kelvin Matandiko, Mwananchikmatandiko@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Milango ya fursa kwa wasomi wa lugha ya Kiswahili imeendelea kufunguka zaidi baada ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ulioanza kuanza majadiliano ya kuwezesha lugha hiyo ianze kutumika katika nyaraka na shughuli zote za kisekta. Katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi SADC Agosti mwaka jana, lugha ya Kiswahili ilipitishwa rasmi kutumika ngazi ya vikao vya wakuu wa nchi na baraza la mawaziri, sawa na lugha ya Kireno, Kifaransa na Kiingereza. “Sasa imeamuliwa rasmi itumike ngazi ya kisekta na katika nyaraka…

Soma zaidi..