Posted in Matukio ya Kiswahili

Waziri Mwakyembe: Mabaraza ya Kiswahili yafanye kazi kwa ushirikiano

Gadi Solomon, Swahili Hub Summary: Maadhimisho ya Kiswahili yalifanyika kwa siku tatu jijini Arusha yakiwakutanisha wanahabari, wanafunzi wa ndani na wageni wanaosoma kozi za Kiswahili, wahadhili pamoja na wapenzi wa Kiwahili kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Arusha. Serikali imelitaka Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) na Baraza la Kiswahili la Zanzibar (Bakiza) kufanya kazi kwa pamoja ili wasiwachanganye watu wanaojifunza Kiswahili duniani. Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizindua Maadhimisho ya Kitaifa ya Kiswahili na Utamaduni kwenye Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS TCDC) Septemba 12 jijini…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Baraza la Mawaziri lapitisha Kiswahili lugha ya Taifa Uganda

Gadi Solomon Baraza la Mawaziri nchini Uganda limekamilisha mpango wa  Kiswahili kiwe lugha ya Taifa nchini humo na kutangaza kitumike kwenye usafiri Shirika la Ndege la Uganda. Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo, leo Alhamisi Septemba 5, Waziri wa Jinsia, Peace Mutuuzo alisema kwamba Bunge la nchi hiyo litajadili suala hilo. Lengo ni kuhakikisha kwamba wanaendana na makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano kwenye ukanda huo. “Tupo kwenye hatua za mwisho kuanzisha Baraza la Kiswahili. Jumatatu wiki ijayo tutawasilisha muswada kwa ajili ya kupitishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Waziri Mutuuzo. Alisema…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Miss Tanzania 2019 aahidi kutumia Kiswahili ‘Miss World’

Nasra Abdallah, Mwananchi Dar es Salaam. Siku chache baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kumtaka Miss Tanzania 2019, Sylvia Sebastian akazungumze Kiswahili atakapokwenda kushiriki Miss World mwenyewe ameahidi kufanya hivyo huku akisema ni muhimu kuwepo mkalmani. Shindano la Miss World 2019  linatarajiwa kufanyika jijini London, nchini Uingereza Desemba 2019 huku warembo zaidi ya 100 wakitazamiwa kupanda jukwaani kuchuana. Akizungumza leo Alhamisi Agosti 29, 2019 alipofanya ziara katika ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Tabata Relini, jijini Dar es Salaam Sylvia amesema amepokea ushauri huo wa Waziri Mwakyembe huku akitaja sababu itakayomfanya kutumia Kiswahili…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Magufuli atangaza Kiswahili kuwa lugha rasmi Sadc

By Kelvin Matandiko, kmatandiko@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (Sadc) ambaye pia ni Rais wa Tanzania, John Magufuli ametangaza Kiswahili kuwa lugha ya nne itakayotumika katika nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo. Siku nne zilizopita baraza la mawaziri la jumuiya hiyo lilipitisha pendekezo kuwa Kiswahili kianze kutumika kama lugha ya nne pamoja na kuwasilisha hoja nyingine 107 ili kujadiliwa. Akizungumza Jumapili Agosti 18, 2019 katika kilele cha  mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi, Rais Magufuli amesema katika kikao kilichofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakuu hao kwa pamoja wamekubaliana lugha hiyo ianze…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Dk Shein alivyopigia chapuo Kiswahili kutumika SADC

By Kelvin Matandiko Dar es Salaam. ‘Chako kipende mpaka cha jirani ukisahau’ ndiyo msemo aliotumia Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katikati ya hotuba yake aliyokuwa akipigia chapuo matumizi ya lugha ya Kiswahili. Dk Shein amesema muda umefika wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) kuitambua na kuanza kutumia lugha ya Kiswahili rasmi katika majukwaa mbalimbali za jumuiya hiyo. “mtasema rais anapiga debe, sawa napiga debe.” Dk Shein alitoa kauli hiyo akiungana na Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyetumia lugha hiyo katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa katika wiki ya viwanda kwa Nchi 16…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Viongozi Tanzania walivyokibeba Kiswahili SADC

Dar es Salaam. Titi la mama ni litamu, hata likiwa la mbwa. Kiswahili naazimu, sifayo inayofumbwa. Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa. Titi la mama litamu, jingine halishi hamu. Ni sehemu ya maudhui katika shairi la Pambo la lugha, lililoandaliwa miaka kadhaa iliyopita na nguli wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania, Shaaban Robert. Mwenyekiti mtarajiwa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye ni Rais wa , John Magufuli anaitumia lugha hiyo katika uzinduzi wa maonyesho ya bidhaa katika wiki ya viwanda kwa nchi 16 za SADC, uliofanyika Jumatatu wiki hii, Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, kabla ya…

Soma zaidi..