Posted in Matukio ya Kiswahili

Waziri Mwakyembe azindua mpango wa kuwatathmini wakalimani BAKITA

Kwa ufupi: Vigezo muhimu vinavyomfanya mtu kuwa mkalimani bora ni; umahili wa lugha, usahihi wa ujumbe, kasi ya muwasilishaji, kujiamini pamoja na uelewa wa mada husika. Gadi Solomon, Mwananchi gsolomon@tz.nationmedia.com Dar es Salaam. Serikali imesema ni matarajio yake kuwepo na wakalimani zaidi ya 200 ambao watasaidia hitaji la wataalamu hao hapa nchini. Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameyasema hayo jana Jumatatu Oktoba 21, kwenye uzinduzi wa Mpango wa Kuwatathmini Wakalimani katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). “Ni aibu katika nchi ya watu zaidi ya milioni 45 kuwa na wakalimani 10…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Klabu ya AS Roma yazindua rasmi akaunti ya Kiswahili Twitter

Ufupisho: Ushindi wa mwanariadha Eliud Kipchoge umechochea klabu ya AS Roma kuamua kufungua akaunti ya Kiswahili Twitter. Hii ni baada ya AS Roma kutoa pongezi kwa mwanariadha mashuhuri Eliud Kipchoge kwa kutumia kiingereza, huku mashabiki wakiuomba uongozi wa klabu kuwafikia wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutoka Kenya, Tanzania na Uganda. Gadi Solomon, Swahili Hub Klabu ya As Roma ya Italia imekuwa klabu ya kwanza barani Ulaya kutumia lugha ya Kiswahili katika mtandao wa Twitter ili kuwasiliana na mashabiki hususani kutoka ukanda wa Afrika ¬†Afrika Mashariki. Hatua hiyo itawawezesha Roma kuwasiliana na mamilioni ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii ulimwenguni kote…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Gavana Hogan apigia chapuo Tamasha la Kiswahili Maryland Marekani

Gadi Solomon, Swahili Hub Gavana wa Jimbo la Maryland nchini Marekani, Larry Hogan amewaalika watu mbalimbali kujumuika kwenye Tamasha la mwaka la Swahili Society litakalofanyika Novemba 2 mwaka huu. Barua iliyotolewa na ofisi ya gavana huyo, ilieleza kuwa hivi sasa Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 140 duniani kote ikiwamo nchi za Tanzania, Congo, Rwanda, Kenya, Afrika Kusindi na Burundi. Pia, nchi zingine zinazongumza lugha ya Kiswahili ni pamoja na Uganda, Sudan Kusini, Comoro, Zambia. Aidha, juhudi za viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimeipa lugha hiyo nguvu ya kupenya kwenye nchi za ukanda huo. Gavana…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Diamond Platnumz atunukiwa Tuzo ya Kiswahili Canada

Gadi Solomon, Swahili Hub Dar es Salaam. Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametunukiwa tuzo ya Kiswahili na Taasisi ya Swahili Vision International Association (SVIA) ya nchini Canada. Diamond amepata tuzo hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita Oktoba 12, kutokana na mchango wake katika kukitangaza Kiswahili duniani kupitia nyimbo zake anazotumbuiza kwa lugha ya Kiswahili. Mmoja wa mameneja wa msanii huyo, Babu Tale aliweka tuzo hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, huku akimpongeza msanii wake Diamond kwa juhudi zake za kukitangaza Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania. SVIA ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inaziunganisha jamii za Waswahili nchini…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

ACALAN-AU yaanza rasmi kutumia Kiswahili katika nyaraka zake

Gadi Solomon, Swahili Hub UFUPISHO: ACALAN ni taasisi ya Umoja wa Afrika (AU) inayosimamia lugha za Kiafrika na maendeleo yake. Lugha rasmi zinazotumika AU ndizo lugha rasmi zinazotumika kwenye taasisi hiyo, huku Kiswahili kikipewa nafasi zaidi ya kuwa lugha ya mawasiliano mapana na kuwaunganisha Waafrika. Taasisi ya African Academy of Languages (ACALAN) imeanza kutumia lugha ya Kiswahili katika nyaraka zake na machapisho ikiwa ni kutekeleza mapendekezo na maazimio ya mkutano uliofanyika mwezi Julai mwaka huu jijini Dar es Salaam. Andiko la ACALAN ambalo limetolewa leo Jumatano likionesha umuhimu wa kuzienzi lugha za Kiafrika, linasomeka kwa Kiswahili; “Lugha za Waafrika huongoza…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

NMB yaboresha mfumo kuunga mkono juhudi za kukuza Kiswahili nchini

Kwa kifupi;Benki ya NMB imeziweka huduma zake katika lugha ya Kiswahili kwa njia ya digitali, sasa huduma zote kupatikana kwenye simu ya mkononi kupitia NMB Mkononi Mwandishi Wetu, MwananchiDar es Salaam. Benki ya NMB imebadilisha mfumo wa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi uliokuwa unatumia lugha ya Kiingereza kwenda katika Kiswahili kwa lengo la kuwahudumia Watanzania wengi zaidi ambao wanaielewa vyema lugha yao. Hivyo, katika kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia Watanzania wengi bila kujali kiwango chao cha elimu Benki ya NMB imeziweka huduma zake katika lugha ya Kiswahili.Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni mpya ya benki hiyo…

Soma zaidi..