Category: Matukio ya Kiswahili
Bakita yapongeza Ubalozi wa Marekani kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani
Summary: Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) lilitangaza Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili Duniani, mwaka huu ni mara ya pili maadhimisho hayo kufanyika duniani kote. Gadi Solomon, Mwananchi gsolomon@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limeupongeza ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa juhudi kuhamasisha matumizi ya Kiswahili duniani, huku wakifanya maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kwa mara ya pili mwaka huu katika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya Kiswahili yaliyofanyika leo Juni 27, 2023, Katibu Mtendaji wa BAKITA, Consolata…
Ubalozi wa Marekani kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani Dar
Gadi Solomon, Mwananchi Kwa ufupi: Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) lilitangaza Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili Duniani, mwaka huu ni mara ya pili maadhimisho hayo kufanyika duniani kote. Dar es Salaam. Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unatarajia kufanya maadhimisho ya Kiswahili katika ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2023. Mgeni maalumu katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Consolata Mushi. Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo, maadhimisho hayo yatayayofanyika kwenye ofisi za ubalozi yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa 9 alasiri hadi…
Chaukidu kufanya Kongamano la Kiswahili Arusha
Gadi Solomon, SwahiliHub Dar es Salaam. Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (Chaukidu) kinatarajia kufanya kongamano la Kiswahili Desemba mwaka huu ambalo litafanyika katika Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MSTCDC), Arusha. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 14-16 Desemba 2023 likitarajiwa kuwakutanisha wadau na wapenzi wa Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali. Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti mwenza wa Kamati ya maandalizi hivi karibuni Said Omary, ilisisitiza wapenzi na wana familia ya Kiswahili kuhakikisha wanawasilisha ikisiri zao mapema, ambapo mwisho wa kutuma ikisirikwa ajili ya kongamano hilo ilikuwa Juni 15, 2023. Chaukidu ambayo makao makuu yake yapo nchini Marekani kimekuwa na mashiko…
Maadhimisho ya Kiswahili 2023 kunongeshwa na Swahili Marathon Arusha
Gadi Solomon, Swahili Hub Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili la Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) wameandaa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo mwaka huu kitaifa yatafanyika Zanzibar.Taarifa iliyotolewa na mabaraza hayo imeeleza kwamba maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na mbio za Swahili Marathon ambazo zitafanyika jijini Arusha Julai Mosi mwaka huu.Maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa taaarifa hiyo imeeleza kwamba tarehe 4 Julai imetengwa kwa ajili ya Siku ya Wanafunzi wa Sekondari na Shule za Msingi.Vilevile wadau na wapenzi wa Kiswahili watapata nafasi ya kushiriki mdahalo wa wazi utakaofanyika Julai 5.Maadhimisho ya…
Washindi wa Tuzo ya Taifa Mwalimu Nyerere wazoa mamilioni
Juma Issihaka, Mwananchi Dar es Salaam. Washindi mbalimbali wamezawadiwa tuzo ya Taifa za Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu zilizoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), huku mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias akiibukia nafasi ya nne kwa upande wa mashairi akipata zawadi ya cheti. Katika kundi hilo, aliyeshinda ni Amri Abdalla na kupata zawadi ya fedha Sh10 milioni, huku Shaaban Athuman Maulid akiwa nafasi ya pili akipata Sh7 milioni na wa tatu ni Suphian Almas aliyepata Sh5 milioni. Kwa upande wa riwaya aliyeshinda ni Hamis Kitare (Sh10 milioni), nafasi ya pili ni Nickson Damas (Sh7 milioni), wa…
Waandishi waitwa kushiriki Tuzo ya Fasihi ya Afrika 2023
Mwandishi Wetu, SwahiliHub Dar es Salaam. Waandaaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika wametangaza wito kwa watu mbalimbali kuwasilisha miswada kwa ajili ya shindano la nane la tuzo hiyo, ambayo hapo awali iliitwa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika. Kuanzia mwaka jana, jina hilo lilibadilishwa ili kuakisi jina la kampuni mama, ambayo ndiyo mdhamini mkuu, Safal Group Limited, kupitia kampuni zake tanzu za Mabati Rolling Mills (MRM) ya Kenya, na ALAF Limited ya Tanzania. Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika ilianzishwa mwaka 2014 na Dk Lizzy Attree na Dk Mukoma…
Maoni Mapya