Posted in Matukio ya Kiswahili

Waziri Mkuu Majaliwa aagiza bidhaa kuwekwa maelezo kwa Kiswahili

Gadi Solomon, Mwananchi gsolomon@mwananchi.co.tz Dar es Salaam. Serikali imeagiza kampuni zote zinazozalisha bidhaa hapa nchini kuhakikisha vifungashio vyake vinakuwa na maelezo kwa lugha ya Kiswahili pamoja na bidhaa zote zinazoingia nchini. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Safal- Cornell ya Fasihi ya Kiafrika, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kampuni zote zinazozalisha bidhaa kuhakikisha wanaweka maelezo kwa lugha ya Kiswahili. Amesema kuwa mbali na hayo pia mamlaka husika zihakikishe mabango mbalimbali ya matangazo barabarani yawe kwa Kiswahili. Aidha, Waziri Mkuuu Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Alaf kutokana na mchango wake kwa kutumia sehemu ya faida kuwekeza kwenye lugha ya Kiswahili….

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Tuzo ya Kiswahili Safal-Cornell Fasihi ya Afrika kutolewa Dar es Salaam

Gadi Solomon, Mwananchi gsolomon@mwananchipapers.co.tz Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika kutoka Kampuni ya Mabati ya Alaf ambayo ni tawi la Kampuni ya Safari Investments Mauritius Limited kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Corenll Marekani. Tuzo za mwaka huu jumla ya Watanzania watano wameingia kwenye kinyang’anyoro katika vipengele vya riwaya na ushairi wakiwania jumla ya zawadi ambazo ni takribani Sh34,800,000. Shughuli ya utoaji tuzo hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Mlimani City keshokutwa Jumatano Janurai 25, 2023 kuanzia saa 3 asubuhi. Tuzo hiyo inayofadhiliwa na Safal Group,…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Uhuru uendane na malengo ya Watanzania

Leo ni Desemba 9, siku ambayo Watanzania tunaadhimisha Uhuru wa Tanganyika, nchi ambayo ilipoungana na Zanzibar ikaundwa Tanzania. Imetimia miaka 61 tangu Taifa letu adhimu lilipoondokana na makucha ya mabeberu wa Kiingereza. Ndio siku ambayo Watanzania tunaikumbuka kila mwaka kama siku kielelezo kwa Watanzania kufurahi kurudi kwa utu na uhuru wao kama Waafrika na binadamu. Hata hivyo, mwaka huu kwa mujibu wa Serikali, maadhimisho hayo hayatakuwa yale ya shamrashamra, zikiwamo za gwaride maalumu la vikosi vya ulinzi na usalama, bali Serikali imeagiza bajeti ya Sh960 milioni iliyotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo, ipelekwe katika ujenzi wa mabweni ya shule za…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Somo la Kiswahili lang’ara darasa la saba

Na Aurea Simtowe Wakati Baraza la Mitihani la taifa (Necta) likitangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 leo, Kiingereza ndiyo somo lililoonekana kuwa somo gumu kwa wanafunzi wengi tofauti na somo la Kiswahili ambalo limeng’ara kwa ufaulu. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa leo Desemba Mosi na Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Almasi yanaonyesha kuwa asilimia 67.71 ya watahiniwa wote katika mtihani huo walipata daraja D katika somo la kiingereza. Matokeo hayo ya kumaliza elimu ya msingi yametangwa leo jijini hapa ikiwa ni baada ya watahiniwa 1,384,186 kukaa katika chumba cha mtihani Oktoba 5 na 6 mwaka huu….

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Samia atunukiwa shahada ya Uzamivu

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa udaktari wa heshima (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkuu huyo wa nchi ametunukiwa udaktari huo Jumatano Novemba 30, 2022 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jakaya Kikwete katika mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. “Kwa mamlaka niliyokabidhiwa, ninakutunuku digree ya heshima ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hongera sana” amesema Kikwete akimtunuku Rais Samia udaktari huo wa heshima. Baada ya kutunukiwa udaktari huo, Rais Samia ameshukuru huku akibainisha kuwa alijaribu kuitafuta shahada hiyo…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Bakita yampa tuzo mwanafunzi bora Kiswahili Chuo Kikuu Tumaini

Na Nasra Abdallah Dar es Salaam. Baraza la Kiswahili Taifa (Bakita), limeanza utaratibu wa kuwatunuku tuzo wanafunzi wanaofanya vizuri somo la Kiswahili katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kiswahili wa Bakita, Vida Mutasa alipokuwa akikabidhi tuzo hiyo kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika somo hilo Chuo Kikuu cha Tumaini, Mary Daudi. Vida amesema awali walikuwa wakitoa tuzo hizo kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne na cha sita, lakini sasa wameona watoe na kwa vyuo vikuu kama moja ya njia ya kuwahimiza kupenda kusoma lugha hiyo kwa kuwa sasa imekuwa bidhaa ambayo wanaweza kuitumia kujiajiri mara…

Soma zaidi..