Posted in Matukio ya Kiswahili

Madaktari, maprofesa nguli wa Kiswahili kuwasilisha mada Maadhimisho ya Kiswahili ya Kitaifa Arusha

Gadi Solomon Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha MS TCDC wameandaa maadhimisho ya Kitaifa ya Kiswahili na Utamaduni ya siku tatu yatakayofanyika jijini Arusha mwezi Septemba. Katika taarifa ya Bakita Iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Seleman Sewangi ilieleza kwamba maadhimisho hayo yatafanyika tare 12, 13 na 14 ya mwezi Septemba. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Maadhimisho hayo makubwa ambayo yanafanyika mwaka huu yamelenga kukiukienzi Kiswahili na Utamaduni kama nyenzo za maendeleo. Lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kutoa fursa…

Soma zaidi.. Madaktari, maprofesa nguli wa Kiswahili kuwasilisha mada Maadhimisho ya Kiswahili ya Kitaifa Arusha
Posted in Matukio ya Kiswahili

Msemaji wa Serikali: Wataalamu wa Kiswahili 708 wamejiandikisha kanzi data ya Taifa

Gadi Solomon Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema mfumo utakaotumika kuwathibitisha wataalamu wa Kiswahili ni kupitia kanzi data ya taifa ya wataalamu wa Kiswahili, ambayo ipo chini ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). Dk Abbas amesema hayo, Alhamisi tarehe 30.05.2019 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alisema kama nchi tunapaswa kujiandaa kupata wataalamu watakaokwenda kufundisha huko. Alisema hadi sasa kuna Watanzania 708 wameshajisajili na kutambulika kuwa wataalamu wa Lugha ya Kiswahili. Hivyo ikitokea fursa hao ndio watakaokuwa wa tayari kupata. Pia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKIZA), limeanza zoezi la kuwatambua wataalamu wa Kiswahili visiwani humo…

Soma zaidi.. Msemaji wa Serikali: Wataalamu wa Kiswahili 708 wamejiandikisha kanzi data ya Taifa
Posted in Matukio ya Kiswahili

Washindi wa fasihi wafunguka

By Kalunde Jamal, Mwananchi [email protected] Dar es Salaam. Washindi wa tuzo ya Kiswahili ya Mabati- Cornell Dotto Rangimoto na Ali Hilal wameeleza kilichowavuta kuandika kabla ya kushiriki tuzo hizo mwaka 2017. Wakizungumza kwenye hafla ya utoaji tuzo ya Kiswahili ya mabati- Cornell ya fasihi ya Afrika zinazotolewa leo Februari 15, 2019. Dotto ambaye alishinda kwenye kitengo cha ushairi kwa mswada wake ‘ Mwanangu Rudi Nyumbani’ amesema kuwa alianza kuandika baada ya kufiwa na mama yake mzazi. Amesema alipofiwa na mama yake alipata maumivu makali na kuanza kuandika namna mama yake alivyoteseka na maradhi. Amefafanua kuwa alikwenda mbali zaidi na kuandika…

Soma zaidi.. Washindi wa fasihi wafunguka
wanafunzi Zanzibar
Posted in Matukio ya Kiswahili

Wanafunzi wamtuhumu mwalimu wao

Unguja. Wanafunzi wa Sekondari ya Kombeni wilaya ya Magharibi B Unguja wamelalamikia adhabu waliyopewa na mwalimu mmoja ya kuwataka wafue taulo za kike chooni. Kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walilaani kitendo hicho na kwamba, Wizara ya Elimu inatakiwa kutoa tamko. Kwa masharti ya kutotajwa mmoja wa wanafunzi hao alisema licha ya kukataa kutekeleza adhabu hiyo, mwalimu huyo (anamtaja) alimlazimisha. Mwanafunzi mwingine alisema mwalimu huyo amekuwa kero na kwamba kwa kitendo hicho hataweza kumsahau maishani mwake. Hata hivyo, jitihada za gazeti hili kuupata uongozi wa shule hiyo ili kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa. Mmoja wa wazazi Shaame Ngwali alisema walimu walipaswa kutenda…

Soma zaidi.. Wanafunzi wamtuhumu mwalimu wao
Posted in Matukio ya Kiswahili

Kiswahili chambeba Kindoki

Kindoki alisema hata kiungo mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban alipofika katika timu hiyo alimsaidia haraka kuweza kuongea kiswahili zaidi na sasa anajua kuongea vyema. ASIKWAMBIE mtu, Klaus Kindoki amekuwa mtamu kule Jangwani kiasi cha kuwashangaza wengi, lakini mwenyewe amefichua kilichombadilisha kutoka kuonekana bomu hadi kuwa shujaa na kuwataja watu watano walimsaidia kumnogesha kwa sasa. Akizungumza na Mwanaspoti, Kindoki alisema tatizo kubwa kwake lilikuwa ni kujua Lugha ya Kiswahili ambalo sasa ameshaliondoa kwa kujua kuzungumza lugha hiyo. “Tatizo langu kubwa lilikuwa ni mawasiliano. Sikuwa najua jinsi ya kuzungumza na wenzangu sasa najua kuongea kiswahili, naweza kuwaambia kitu mabeki na mchezaji mwingine akaelewa,”…

Soma zaidi.. Kiswahili chambeba Kindoki