Posted in Matukio ya Kiswahili

Maktaba ya Kiswahili kuanzishwa Zanzibar

Gadi Solomon na Amani Njoka, Swahili Hub Zanzibar. Serikali ya Zanzibar imekiagiza Chuo Kikuu cha Zanzibar (Suza) kuanzisha skuli ya utafiti na ukalimani ili kuweza kukidhi mahitaji ya wataalamu wa tafsiri na ukalimani kwenye mikutano ya kimataifa na kutoa wito kwa wataalamu kuanza kupelekea tasnifu zao kwa ajili ya makataba ya Kiswahili inayotarajiwa kujengwa Zanzibar. Akizungumzungumza kwenye Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kiswahili, Mgeni rasmi, Balozi Seif Ali Idd kwa niamba ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema kutokana na Suza kuwa kitovu cha kufundisha Kiswahili kwa wageni na sasa kituo hicho kimekuwa Skuli ya Kiswahili na…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Chawakita-MUM wamkumbuka Shaaban Robert

Na Dk Ahmad Sovu Kifupi: Chuo Kikuu cha Kiislamu cha mkoani Morogoro (MUM), Jumatano (1/1/2020) kiliandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kumuenzi mwanafasihi mashuhuri Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, Shaaban Robert. Katika kongamano hilo, washiriki walihimizwa kukitumia Kiswahili ipasavyo kama sehemu ya kumuenzi nguli huyo wa mashairi pamoja na kupata fursa mbalimbali. Morogoro. Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu vya Tanzania (CHAWAKITA) Tawi la MUM wameadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa Fasihi ya Kiswahili Shaaban Robert huko Morogoro Tanzania Siku ya Mwaka mpya 2020. Mgeni Kiongozi katika hafla hiyo alikuwa Karii na mshairi maarufu Ustadh Mzee Sudi…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Ufaulu Kiswahili wapanda Kenya

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Matokeo ya mitihani kwa somo la Kiswahili yamekuwa si mazuri kwa kipindi cha hivi karibuni. Hata hivi katika matokeo ya mwaka huu wanafunzi wameonekana kufanya vizuri zaidi kulinganisha na matokeo yaliyopita. Nairobi. Wiki iliyopita Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC) lilitangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya sekondari (Kidato cha nne). Akizutangaza matokeo hayo, Katibu wa Baraza la Elimu Profesa George Magoha alisema kwamba, matokeo ya mwaka huu yamekuwa mazuri kulinganisha na yaliyopita. “Matokeo ya mwaka 2019 yanaonekana kupanda katika ufaulu wake hasa kwa masomo ya Kiingereza, Kiswahili, Fizikia, Kemia, Biolojia na…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Afrika Kusini kuanza na shule 90 kufundisha Kiswahili

Amani Njoka, Swahili Hub Johannesburg. Kuanzia mwaka 2020 Afrika Kusini itaanza kufundisha rasmi lugha ya Kiswahili kama lugha mbadala katika shule mbalimbali nchini humo kwa kuanza na shule 90. Kiswahili itakuwa ni lugha ya kwanza kutoka nje ya Afrika Kusini kufundishwa katika shule za nchi hiyo ambayo tayari inakitumia kama Kifaransa, Kijerumani na Kimandarini zinafundishwa kama lugha za kigeni. Miezi michache iliyopita Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imeridhia Kiswahili kuwa lugha yake ya 4, miongoni mwa lugha nyingine zinazotumiwa na jumuiya hiyo. Kiswahili kinatumiwa na SADC baada ya Kiingereza, Kireno na Kifaransa. Kiswahili ndiyo lugha…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ahimiza kutumia fursa za Kiswahili duniani

Gadi Solomon, Swahili Hub Ufupisho: Kongamano la Tatu la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar limefungwa leo Ijumaa Desemba 19. Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa “Fursa za Soko la Kiswahili Duniani Katika Maendeleo ya Fasihi na Isimu.” Kongamano hili limehitinishwa kwa washiriki kufanya utalii wa kifasihi kwa kutembelea maeneo yaliyotajwa kwenye kitabu cha Kuli kilichoandikwa na Mwandishi Shafi Adam Shafi. Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya kugha ya Kiswahili. Akuzungumza wakati wa  kufunga Kongamano la  Tatu la  Kiswahili la  Kimataifa, Waziri wa  Ofisi ya Makamu wa  Pili wa Rais, Mohamed Abood…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Chuo Kikuu Huria chang’ara Kongamano la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar

Na Dkt. Mohamed Omary Maguo Zanzibar. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimepata heshima kubwa katika Kongamano la Kimataifa la Kiswahili linalofanyika hapa Zanzibar kuanzia leo 19-20/12/2019 na kuhusisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani. Chuo kimepata heshima baada ya kukabidhi tasinifu zaidi ya 60 za wahitimu wa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kwa Mgeni rasmi Mhe. Balozi Seif Ali Idi Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar. Wahitimu hawa ni kutoka Pemba tu. Tasinifu hizi zilizokabidhiwa kwa mgeni rasmi ni sehemu tu ya wahitimu wa shahada ya Uzamili ya Kiswahili zaidi ya 150 waliohitimu tangu Programu…

Soma zaidi..