Posted in Matukio ya Kiswahili

Mabaraza ya Kiswahili yahimiza wataalamu kujiandikisha kanzidata za Taifa

Gadi Solomon na Amani Njoka, Swahili Hub Zanzibar. Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili (Bakita), Dk Selemani Sewangi amewahimiza wataalamu wa Kiswahili kujiandikisha kwenye kanzidata ya Taifa. Dk Sewangi alisema huutilia mashaka uandikishaji huo wa wataalamu huku wengine wakidhani ni mradi wa Bakita kuwa ni mbinu ya kupiga hela. Hivyo anawatoa wasiwasi kuwa lengo ni kutambua wakalimani hao walipo.  Bakita kujipatia kipato, dhana hiyo inapaswa kuachwa. “Bakita tumeshaanza uandikishaji wa wataalamu wa Kiswahili kwenye kanzidata. Hadi sasa wamefikia zaidi ya 1,000 na Baraza la Kiswahili la Zanzibar tayari nao wameanza,” alisema Dk Sewangi. Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mwenyekiti wa  Baraza…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Dk Shein alipongeza Bakiza

Gadi Solomon na Amani Njoka, Swahili Hub Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohemed Shein amelipongeza Baraza la Kiswahili la Zanzibar kuandaa kongamano la kimataifa la tatu la Kiswahili linalowakutanisha wataalamu mbalimbali wa Kiswahili duniani. Salamu hizo za pongezi ziliwasilishwa na Makamu wa  Pili wa  Rais  wa  Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais Shein. Amesema kongamano hilo ni muhimu kuendelezwa kwa sababu linatoa fursa ya wataalamu wachanga kuchangamana na wenzao wakongwe. “Kongamano hilo litumike kama darasa kuongeza maarifa kwa wanataaluma wa Kiswahili na kwamba kumekuwa na mafanikio katika Kiswahili kutokana na kuongezeka…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Serikali ya Zanzibar imeanza mchakato wa kuandaa Sera ya lugha ya Kiswahili

Gadi Solomon, Swahili Hub Kifupi: Ni habari njema kwa wataalamu na wapenzi wa Kiswahili Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Serikali ya Zanzibar inaanda sera ya lugha ambayo itaipa hadhi zaidi lugha. Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji, Dk Mwanahija Omary leo Alhamisi Desemba 19 wakati wa  uzinduzi wa  Kongamano la  Tatu la  Kimataifa la  Zanzibar linalofanyika kwenye kwenye Ukumbi wa  Dk Sheikh Idris Abdul Wakil Mnazi Mmoja Zanzibar. Alisema tayari Bakiza imeanza kufanya kazi kwa ushirikiano na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa mabaraza haya. Kongamano hilo kimehudhuriwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Kongamano la Kiswahili kuanza leo Zanzibar

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Kongamano hilo litawakutanisha wataalam, watafiti, wakufunzi, wanafunzi, wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari za Kiswahili. Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar na masuala mbalimbali yahusuyo Kiswahili yatajadiliwa. Unguja. Leo ndiyo siku ambayo Kongamano la Kiswahili litaanza rasmi mjini Unguja. Kongamano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili kujadili mambo muhimu kwa ajili ya ustawi wa lugha hiyo. Dhima kuu ya Kongamano hilo ni juu ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa, kubadilishana uzoefu katika utafutaji wa soko la Kiswahili kama bidhaa na Kujadili mchango wa watalamu na wadau mbalimbali wa lugha na fasihi katika…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Mabati-Cornell waandaa tuzo za fasihi ya Kiswahili

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Kila mwaka Chuo cha cornell kwa kushirikiana na Mabati wamekuwa wakitoa tuzo kwa wanafasihi, wataalam na wadau wengine wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za kukiuza na kukiendeleza Kiswahili. Nairobi. Mabati-Cornell imeandaa tuzo maalum za fasihi ya Kiswahili za mwaka 2019. Tuzo hizo zitakazohusisha vipengele vya riwaya na ushairi zitakuwa zinakamilisha mara ya 5 ya uandaaji wa tuzo wa taasisi hiyo ambayo ilianza kufanya hivyo mwaka 2014. Mmoja wa wasimamizi wa tuzo hizo, Dk Mukoma wa Thiong’o ambaye ni Profesa mshiriki katika Chuo cha Cornell anasema kuwa tuzo hizi zimeandaliwa kwa kusudi la kutambua uandishi wa kazi…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Mfanyakazi wa Taifa Leo ashinda tuzo ya kimataifa, akipaisha Kiswahili

Na WANDERI KAMAU MMOJA wa wasimamizi wakuu wa gazeti la Taifa Leo, Nuhu Bakari ameibuka mshindi kwenye tuzo za kimataifa kuhusu tafsiri. Bakari, almaarufu kama Al Ustadh Pasua aliibuka bora barani Afrika katika shindano lililoandaliwa na Shirika la Proz.Com, lenye makao yake jijini New York nchini Amerika. Kauli mbiu ya shindano hilo ilikuwa “The 21st Century Translation Contest: The Tides of Tech” (Shindano la Tafsiri katika Karne ya 21: Mawimbi ya Teknolojia). Kwa mujibu wa Bakari, mchakato wa kuwateua washindi ulikuwa wenye ushindani mkali kwani zaidi ya watu 100 walishiriki. Shindano hilo lilichukua muda wa miezi minne. “Katika awamu ya…

Soma zaidi..