Posted in Matukio ya Kiswahili

World Academy waja na kongamano lingine la Kiswahili na Utamaduni Dubai

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi:Ni kongamano ambalo wasomi na watafiti watawasilisha mada, midahalo, tafiti na matokeo ya tafiti zao kwa mapana na marefu kuhusu lugha ya Kiswahili, utamaduni wake na uhusiano wake na lugha nyingine. Paris. Taasisi inayojihusisha na uchapishaji na uendeshaji wa makongamano mbalimbali ulimwenguni kuhusu siasa, uchumi, sayansi na teknolojia, utamaduni na masuala mengine iitwayo World Academy imeandaa kongamano kuhusu Kiswahili na Utamaduni wake. Tovuti ya Taasisi hiyo yenye makao makuu yake mjini Paris, Ufaransa  inaeleza kuwa kongamano hilo litafanyika tarehe 17-18 Desemba, 2020 mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu. Kongamano hilo litakuwa na mada mbalimbali ambazo…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Rais Magufuli apendekeza Kitabu cha ‘My Life, My Purpose’ kitafsiriwe Kiswahili

KWA UFUPI: Rais John Magufuli amezindua kitabu cha My Life, My Purpose ambacho kimeandikwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kuwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kusoma vitabu. Gadi Solomon, Swahili Hub Dar es Salaam. Dar es Salaam. Rais John Magufuli amezitaka mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kutafsiri kitabu cha My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudio Langu) kwa lugha ya Kiswahili ambacho kimezinduliwa leo Jumanne Novemba 12, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandikwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye pia…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Chuo cha Indiana kutoa kozi fupi ya Kiswahili mwakani

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Warsha hiyo ya muda mfupi itawaandaa wanafunzi wanajitayarisha kuchukua masomo mbalimbali ya lugha katika idara ya Taaluma ya Lugha za Kiafrika katika Chuo hicho. Vilvile itakuwa ni kujinoa kwa wale ambao tayari wamepitia ngazi ya awali. Indiana. Katika kuadhimisha miaka 200 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Indiana, Idara ya Lugha katika chuo hicho imeandaa warsha ya mwezi mmoja kwa watu wote wanajiandaa na masomo ya lugha katika Idara ya Lugha za Kiafrika chuoni hapo. Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 8 Juni mpaka 31 Julai mwaka 2020. Taarifa ya mtandao wa chuo hicho inasema programu hiyo…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Wanataaluma wa Kiswahili wamwandikia kitabu Profesa Madumula

Amani Njoka na Gadi Solomon, Swahili Hub Kwa ufupi: Makala mbalimbali zinazohusu lugha na fasihi ya Kiswahili zinapatikana ndani ya kitabu hicho kiitwacho ‘Koja la Taaluma za Insia’. Zimeandikwa na wanazuoni kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla. Dar es Salaam. Wataalamu mbalimbali wa Kiswahili kutoka ndani nan je ya Tanzania wameandika makala za kitabu cha heshima kinachoitwa Koja la Taaluma za Insia kwa ajili ya kumtunuku Profesa Joshua Madumula. Koja la Taaluma za Insia kimeandikwa kwa heshima ya Profesa Madumula. Kitabu hicho chenye mkusanyiko wa makala mbalimbali za Kiswahili na Fasihi ya Kiswahili kimechapishwa kwa ajili ya kusomwa…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Waserbia wapigana msasa wa Kiswahili kwao

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Taasisi hiyo imesema warsha hiyo ni maalum kwa ajili ya raia w3a Serbia pekee wanaojifunza lugha ya Kiswahili na warsha hiyo itahusu vipengele vyote vya lugha ambavyo ni kuongea, kusikiliza, kuandika na kusoma. Belgrade. Makumbusho ya Sanaa za Afrika ya mjini Belgrade nchini Serbia imeandaa warsha maalum kwa ajili ya raia wake wanaojifunza kuzungumza na wanaozungumza Kiswahili kwa kiwango cha awali ili kuwapiga msasa. Warsha hiyo itawahusisha watu wenye umri wa miaka 16 na kuendelea. Warsha hiyo itaongozwa na Dk Marija Panic na Benjamin Towett Chemarum. Mtandao wa makumbusho hayo unaeleza kuwa warsha hiyo ilianza…

Soma zaidi..
Posted in Matukio ya Kiswahili

Italia waja na kongamano la Kiswahili na utamaduni

Amani Njoka, Swahili Hub Kifupi: Kongamano hilo litakawakutanisha watafiti, wadau na wanasayansi wa lugha na tamaduni mbalimbali kujadili kuhusu mustakabali wa lugha ya Kiswahili. Mada mbalimbali kuhusu lugha ya Kiswahili ikiwemo fasihi ya Kiswahili, Semantiki ya Kiswahili, ukuzaji wa mtaala wa Kiswahili, mbinu za ufundishaji Kiswahili na nyingine nyingi zitajadiliwa na washiriki. Roma. Chuo cha Sayansi, Uhandisi na Teknolojia cha Mjini Roma, Italia kimeandaa Kongamano la Lugha ya Kiswahili na Utamaduni litakalofanyika kwa siku mbili tarehe 13-14 Desemba, 2021. Kongamano hilo litahudhuriwa na wasomi na watafiti mbalimbali wa lugha kutoka vyuo vikuu kadhaa ulimwenguni kutoka Marekani, Kanada, Japani, Australia, Nigeria,…

Soma zaidi..