Posted in Methali

METHALI ZA KISWAHILI

1. Aanguaye huanguliwa. 2. Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu. 3. Abebwaye hujikaza. 4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti. 5. Adui aangukapo, mnyanyue. 6. Adui mpende. 7. Adui wa mtu ni mtu. 8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna. 9. Ahadi ni deni. 10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 11. Akiba haiozi. 12. Akili ni mali. 13. Akili ni nywele kila mtu ana zake. 14. Akili nyingi huondowa maarifa. 15. Akutukanae hakuchagulii tusi. 16. Akipenda chongo huita kengeza. 17. Akufaaye kwa dhiki, ndiye rafiki. 18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema. 19. Akupaye kisogo si mwenzio. 20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.

Soma zaidi..
Posted in Methali

Methali za Kiswahili na maana zake

Amani Njoka, Swahili Hub Aliye juu mngoje chini: Inatukumbusha kuwa na subira na kukubali pale ambapo mwenzio amekuzidi nafasi fulani basi hauna budi kumheshimu. Kamba hukatikia pembamba: Kamba ni kitu chochote kinachotumika kufungia vitu mathalani kuni n.k. Ili uweze kulitatua jambo fulani ni vyema ukaangalia penye udhaifu ili usitumie nguvu kubwa. Jungu kuu halikosi ukoko: Ni kawaida kuona chakula kikipikiwa kwenye vyungu vikubwa na masalia ya chakula hasa ukoko kubaki. Watu wenye hekima na wazee hawakosi neno la kutia kwenye mazungumzo. Watu wanapaswa kuomba ushauri kwa watu wazima wakati wowote ili wapate msaada wa mawazo kwa watu wazima au viongozi…

Soma zaidi..
Posted in Methali

Methali za Kiswahili na maana zake

Amani Njoka-Swahili Hub Asiyesikia la mkuu, huvunjka guu: methali hii ina lengo la kuwatahadharisha watoto au vijana wadogo kuheshimu yale wanayoambiwa na wakubwa zao. Sababu kuu ya kufanya hivyo ni kwa sababu watu wazima wanatajiriba ya maisha na hivyo maelekezo yao huwa ni msaada kwa vijana wadogo na endapo wakiipuuza wanaweza kujikuta katika matatizo. Abebwaye hujikaza: huwakumbusha watu wajibu wa kufanya juhudi za kujisaidia wenyewe pale wanapopewa msaada wa awali. Ikiwa utasaidiwa basi abgalau onesha juhudi za kujiweza pindi msaada utakapofika mwisho Akili ni nywele kila mtu ana zake: hutukumbusha kuwa kila binadamu ana mawazo na mtazamo wake wa kufanya…

Soma zaidi..
Posted in Methali

Methali

1. Aanguaye huanguliwa. 2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu. 3. Abebwaye hujikaza. 4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti. 5. Adui aangukapo, mnyanyue. 6. Adui mpende. 7. Adui wa mtu ni mtu. 8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni. 9. Ahadi ni deni. 10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 11. Akiba haiozi. 12. Akili ni mali. 13. Akili ni nywele kila mtu ana zake. 14. Akili nyingi huondowa maarifa. 15. Akutukanae hakuchagulii tusi. 16. Akipenda chongo huita kengeza. 17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki. 18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema. 19. Akupaye kisogo si mwenzio. 20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.

Soma zaidi..