Posted in Methali

Vyanda vya miguu havivishwi pete

Na Pelagia Daniel Yajapo yapokee, makusudio ya neno ‘yajapo’ (yanapokuja). Yaani unapojiwa na mambo, hasa mabaya au mazito, yapokee. Usibabaike, usilalame wala usipite ukishtakia watu. Pambana nayo wewe mwenyewe kiume. Methali hii inatufunza kuwa na ustahamilivu na moyo wa kuweza kupambana na matatizo, tuwe tayari saa zote kwa litakalotokea. Visima vya kale havifukiwi, si vizuri kuvifukia visima vya zamani, huenda siku moja vikafaa. Methali hii hutumiliwa wazee-kwamba wasiachwe au wasitupwe ovyo ovyo bila ya kutazamwa kwa sababu ni wazee. Maarifa waliyonayo ni mengi, kwa hivyo wakati wowote wanaweza kutufaa. Vyanda vya miguu havivishwi pete, ‘Vyanda’ maana yake ni vidole. Vidole…

Soma zaidi..
Posted in Methali

Ulimi hauna mfupa

Na Pelagia Daniel 1.Ukiujua huu, huu huujui. Ukiujia upande mmoja, upande mwingine huujui. Methali hii hutumiwa kuonyesha kuwa hakuna mtu anayejua kila kitu. Ikawa analijua jambo moja kushinda wenziwe, bila shakaliko lingine ambalo wenziwe wanalijua kuliko yeye. 2. Ulimi hauna mfupa, mtu anaweza kuupeta ulimi wake anavyotaka bila ya kuuvunja au kuukata, kwa sababu hauna mfupa. Methali hii hutumiwa kwa mtu anayependa kujisifusifu sana, hasa kama sifa zenyewe hanazo. 3. Subira yavuta kheri, methali hii hutumiwa kufunza watu kuwa na subira. wawe wastahimilivu, wasibabaike kwa shida, mashaka, au misukosuko inayowapata.

Soma zaidi..
Posted in Methali

Vita vya panzi neema ya Kunguru

Na Pelagia Daniel Vita vya panzi neema ya Kunguru, Panzi ni aina ya wadudu, na Kunguru ni aina ya ndege ambao hula hao panzi. Panzi wanapigana na kuuana, kunguru hupata chakula cha bure na kwa urahisi. Methali hii hutumiwa kuonyesha kuwa watu wawili wanapogombana (au makundi mawili), anayepata faida ni mtu wa tatu. Wao hupata hasara tu. Kwa hivyo wajitahidi wasigombane. Usioweza kuukata, ubusu mkono usioweza kuukata ubusu. kama mtu humwezi, usigombane naye, bora utafute njia ya kusikilizana naye ili asikudhuru. Ukubwa ni jaa, Jaa ni jalala mahali ambapo watu hutupa taka taka zao. Kwa hiyo mtu mkubwa ni kama…

Soma zaidi..
Posted in Methali

Zobe na msuwele ni wamoja

Na Pelagia Daniel Zobe na msuwele ni aina ya samaki (vinyama vya baharini) ambao wana michacha (miguu) na migando (mikono) kama vile kaa. Wana magamba kama vile kobe. Kwa hivyo wao si kama samaki ingawa wanaishi baharini . wao ni tofauti. Methali hii ina maana ya sawa na hutumiwa kama ile isemayo ng’ombe na mbuzi ni wamoja. Zindiko la mwoga ni kemi ‘Zindiko’ maana yake ni hifadhi au kinga, na ‘kemi’ ni kelele au ukelele. Mtu mwoga huhifadhiwa na ukelele wake kwa kuwa yeye mwenyewe hawezi kupigana, akipiga ukelele watu wengine watakuja na waamue. Kwa hivyo atasalimika. Methali hii inatufunza…

Soma zaidi..
Posted in Methali

Usiyavuke maji usiyoweza kuyaogelea

Na Pelagia Daniel Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali. Methali hii ina maana ya nyuki hutengeneza asali kutokana na kufyonza maua na sehemu mbalimbali. Kuna baadhi ya sehemu huwa ni chafu hivyo, ikitokea ukajua sehemu ambapo nyuki hutua unaweza usionje asali. Ushikwapo shikamana. Methali hii ina maana ya pale unapopata msaada ni muhimu na wewe kutoa ushirikiano mzuri.  Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga. 

Soma zaidi..
Posted in Methali

Methali

Na Pelagia Daniel Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili. Methali hii ina maana ya mtu anaye mtangaza mtu kwa wema na uzuri lakini kwa upande wake humchafua hata katika mambo ambayo hata mhusika hajayafanya. Ng’ombe avunjikapo guu hurejea zizini. Methali hii ina maana ya mtu anapopata matatizo akiwa mahali tofauti na kwake hivyo hurejea nyumbani kwake. Pabaya pako Si pema pa mwenzako. Methali hii ina maana ya pale unapopaona ni pabaya hutakiwi kumshawishi mtu mwingine apaone pabaya.

Soma zaidi..