Category: Nahau
Nahau
na Pelagia Daniel 1.Mate ya fisi = Tamaa kupita kiasi2.Kata tamaa = Vunjika moyo kutokuwa na hamu ya jambo fulani.3. Mbiu ya mgambo = Tangazo4.Mungu amemnyooshea kidole = Mungu amemuadhibu5.Mkubwa jalala = Kila lawama hutupwa kwa mkubwa6.Mkaa jikoni= Mvivu wa kutembea7.Mungu si Athumani= Mungu hapendelei8.Paka mafuta kwa mgongo wa chupa = Danganya9.Usiwe kabaila = Usichume tokana na jasho la mwingine10.Usiwe kupe = Fanya kazi
Nahau
1.Maneno ya uwani = Maneno yasiyo na maana au porojo2.Mate ya fisi = Tamaa kupita kiasi3.Kata tamaa = Vunjika moyo kutokuwa na hamu ya jambo fulani.4. Mbiu ya mgambo = Tangazo5.Mungu amemnyooshea kidole = Mungu amemuadhibu6.Mkubwa jalala = Kila lawama hutupwa kwa mkubwa7.Mkaa jikoni= Mvivu wa kutembea8.Mungu si Athumani= Mungu hapendelei9.Paka mafuta kwa mgongo wa chupa = Danganya10.Usiwe kabaila = Usichume tokana na jasho la mwingine11.Usiwe kupe = Fanya kazi
Nahau
na Pelagia Daniel 1.Usiwe bwanyenye = Usichume kwa vitega uchumi vyake.2. Usiwe na mirija = Usinyonye wenzako3.Utawala msonga= Utawala wa wachache4.Usiwe nyang’au = Nchi moja kuifanyia nyingine ubaya na udhulumati.5.Usiwe kikaragosi = Nchi kuwa kibaraka wa nchi kubwa.6.Usiwe chui katika ngozi ya kondoo=Kujifanya rafiki kumbe ni adui7.Kutoa ya mwaka =Kufanya jambo zuri na la pekee8.Kumpa mtu ukweli wake = Kumwambia mtu wazi ubaya wake.9.Pua kukaribiana kushikana na uso =Kukunja uso kwa hasira10.Kusema kutoka moyono=Kunena kilicho kweli
Nahau
na Pelagia Daniel 1.Kwa udi na uvumba= Tekeleza jambo kwa namna yoyote ile iwezekanavyo 2.Piga jeki= Toa msaada kwa mtu hasa pale anapokuwa amekwama (kibiashara au kifedha). 13.Tumbo moto= Hofu, wasiwasi 14.Tupa karata = bahatisha, 15.Piga kitabu= soma sana, soma kwa bidi 16.Vua macho= Tazama kwa makini, sehemu/mahali 17. Vunja mbavu= Chekesha sana 18. Vuta pumzi= Pata mapumziko 19. Weka uzibe= Zuia jambo nyima mtu 20. Zunguka mbuyu= Toa rushwa/pita mlango wa nyuma.
Nahau
na Pelagia Daniel 1.Kujipalia mkaa = Ujitia matatani2.Kumeza au kumezea mate = Kutamani3.Kumuuma mtu sikio = Kumnong’oneza mtu jambo la siri4.Kumpa nyama ya ulimi = Kumdanganya mtu kwa maneno matamu5.Kumchimba mtu = Kumpeleleza mtu siri yake6.Kutia chumvi katika mazungumzo = Uongea habari za uwongo7.Vunjika moyo = Kata tamaa8.Kata maini = Kutia uchungu9. Kujikosoa = Kujisahihisha10.Kutia utambi = Kuchochea ugomvi
Jifunze nahau za lugha ya Kiswahili na mwalimu wa Swahilihub
Fyata mkia – Nyamaza Fimbo zimemwota mgongoni – Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni Hamadi kibindoni – Akiba iliyopo kibindoni Hawapikiki chungu kimoja – Hawapatani kamwe Kupika majungu – Kufanya mkutano wa siri Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka – Kumsifu mtu kwa unafiki Kula mlungula – Kula rushwa Kupelekwa miyo – Kutiwa [kupelekwa] jandoni Amekuwa mwalimu – msemaji sana Amemwaga unga – Amefukuzwa kazi……Itaendelea kesho
Maoni Mapya