Posted in Nahau

usiwe kabaila

Nanahu hii ina maana ya kutokuchuma mali kutokana na jasho la mtu.

Soma zaidi.. usiwe kabaila
Posted in Nahau

usiwe Nyang’au

Nahau hii ina maana ya kuwa usidhulumu kwa kutumia madaraka uliyonayo.

Soma zaidi.. usiwe Nyang’au
Posted in Nahau

Duniani ni msiba na furaha, kuna ugonjwa na siha

Nahau hii ina maana katika ulimwengu kuna vipindi mbalimbali ambavyo mwanadamu hupitia katika maisha, kuna wakati wa furaha, huzuni, magojwa na afya. Hivyo kila nyakati inayokuja katika kipindi fulani hutakiwa kuendana nayo.

Soma zaidi.. Duniani ni msiba na furaha, kuna ugonjwa na siha
Posted in Nahau

Aliyepata fedha hutaka kuiliza

Nahau hii ina maana mtu anapata fedha nyingi ambazo huzitumia vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na ulazima, hivyo kuleta dhana ya kuiliza pesa.

Soma zaidi.. Aliyepata fedha hutaka kuiliza
Posted in Nahau

umaskini si kilema

Nahau hii ina maana ya mtu ukiwa maskini haimaanishi kuwa huna uwezo wa kutafuta hela kwa sababu viungo vyote unavyo vinavyokuwezesha kutafuta njia za kujikwamua na maisha.

Soma zaidi.. umaskini si kilema
Posted in Nahau

Nahau

Adhabu ya kaburi aijua maiti Nahau ina maana ya kuwa mtu anayepitia matatizo yeye ndo anayejua uchungu, uzito wake tofauti na mtu asiyehusika na tatizo hilo.

Soma zaidi.. Nahau