Posted in Vitendawili

Vitendawili vyetu

Amani Njoka-Swahili Hub Hauna adabu-Utelezi Ana mishale isiyo na idadi-Nungunungu/Karunguyeye Hauonekani-Upepo Kila nifanyacho anaiga- Kivuli Babu amelala ndani ndevu kaacha nje-Mhindi Anaoga kila saa lakini hatakati-Chura Kila nikienda nasikia wifi wifi-Choroko/Mbaazi Kila Mtu ana yake- Akili Triii! mpaka Maka-Utelezi Popoo mbili zavuka mto-Macho Chumba changu kidogo lakini nalala pekee yangu-Kaburi Hawa wanaingia, hawa wanatoka- Nyuki Koti la Babu halikosi chawa-Anga na nyota Hayahesabiki-Maji Hausimami, hausimiki- Mkufu Jani la mgomba laniambia habari zinazotokea Ulimwenguni kote-Gazeti Juu majani, chini majani, katikati nyama-Nanasi Wavu wangu hauvui samaki-Utamdo wa Buibui Kamba yangu haifungi kuni-Barabara Mlango wa Chuma ukiufungua hauna huruma-bunduki REJELEO Salla H. D….

Soma zaidi..
Posted in Vitendawili

VITENDAWILI

Huu ni usemi unaotolewa kwa njia ya fumbo unaoumbwa na pande mbili. Upande mmoja ukiuliza swali na upande wa pili ukijibu swali. Kwa mfano”: ”Popoo mbili zavuka mto= macho. Kitendawili hakipigwi wala hakisimuliwi bali hutegwa. Vitendawili hutegwa hivi: Kutega kitendawili Mtega kitendawili huanza kwa kusema; Kitendawili— Naye msikilizaji huitika Tega— Kisha mtegaji kitendawili hukisema kitendawili chenyewe. 1. Abeba mishale kila aendako= Nungunungu. 2. Aenda mbio ingawa hana miguu =nyoka 3. Afahamu sana kuchora lakini hajui  achoracho         = konokono 4.Amezalia hali, amekufa hali na amerudi hali=Nywele 5. Anaota moto kwa mgongo=Chungu kiwapo jikoni. NB: Sehemu ya Vitendawili hivi vimenukuliwa kutoka kwenye…

Soma zaidi..