Chaukidu kufanya Kongamano la Kiswahili Arusha

Gadi Solomon, SwahiliHub


Dar es Salaam. Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (Chaukidu) kinatarajia kufanya kongamano la Kiswahili Desemba mwaka huu ambalo litafanyika katika Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MSTCDC), Arusha.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 14-16 Desemba 2023 likitarajiwa kuwakutanisha wadau na wapenzi wa Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti mwenza wa Kamati ya maandalizi hivi karibuni Said Omary, ilisisitiza wapenzi na wana familia ya Kiswahili kuhakikisha wanawasilisha ikisiri zao mapema, ambapo mwisho wa kutuma ikisirikwa ajili ya kongamano hilo ilikuwa Juni 15, 2023.

Chaukidu ambayo makao makuu yake yapo nchini Marekani kimekuwa na mashiko miongoni mwa vyama vya Kiswahili duniani ambapo huwakutanisha wanataaluma, wanafunzi na wapenzi wa Kiswahili.

Author: Gadi Solomon