Dunia yaadhimisha Siku ya Kiswahili

Pelagia Daniel na Gad Solomoni

Kwa mara ya kwanza duniani leo inaadhimisha siku ya Kiswahili duniani 7/7/2022.  Kiswahili kimesheherehekewa duniani kama Siku ya Kiswahili Duniani baada ya Unesco kutenga siku hii kuwa siku ya Kiswahili duniani na kuitambua lugha ya Kiswahili kama mojawapo ya lugha kubwa  zaidi za Afrika na duniani kwa ujumla. Siku hii ilianza kuadhimishwa Julai 1 kwa uzinduzi wa tamasha la utamaduni lililofanyika katika uwanja wa Uhuru kwa siku nne ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.

Julai 6 wizara ya Utamaduni, sanaa na michezo iliandaa mdahalo uliokuwa na mada Kiswahili na ukombozi.

Leo 7 Julai ndio kilele cha maadhimisho ya siku hii yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere yenye kauli mbiu “Kiswahili ni chachu ya Maendeleo na Utangamano Duniani”.

Katika maadhimisho haya mwakilishi kutoka Unesco ametoa salamu za pongezi kwa kukamilisha maadhimisho yaliyotolewa na shirika hilo Novemba 23 mwaka 2021.

Maadhimisho ya siku hii yamehudhuliwa na viongozi wa serikali na mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Daktari Philip Mpango, ambapo amemwakilisha Rais Samia aliyepata udhuru. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ameishukuru Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi nzuri waliyoifanya hasa kuadhimia kufanya maadhimisho haya katika mkoa wa Dar es Salaam.

“Hamjakosea mmeleta shughuli hizi katika mkoa sahihi kwanza tunaposema Kiswahili kilisaidia Tanzania kupata uhuru basi ndo hapa kwa sababu tuna uwanja wa Uhuru” amesema Makala.  

Makamu Mwenyekiti CCM bara Abdrahaman Kinana awaasa Watanzania kuwa chachu ya kukikuza na kueneza Kiswahili hivyo, kutumia wataalamu waliopo nchini.

 Waziri wa elimu ya msingi Afrika kusini Angelina Motshekga na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wametia saini makubaliano ya Kiswahili kufundishwa Afrika kusini.

 “Baada ya kutia saini makubaliano hayo timu zitakaa kuratibu zoezi zima la utekelezaji wa makubaliano hayo” alisema Mkenda. Alimaliza kwa kunukuu shairi la Shaabani Robert Titi la Mama.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amewashukuru na kuwapongeza Watanzania walioshiriki katika zoezi zima la kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani maadhimisho haya yaliodumu kwa siku 7 mfululizo. Ametoa ombi la kujengwa kwa chuo kikuu cha Lugha ya Kiswahili nchini.

Kupitia mtandao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wageni na kuwapongeza kwa kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani, pia amemshukuru Joackim Chisano kwa kuhutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika lugha ya Kiswahili  alipokuwa anaufunga mkutano wa Umoja wa Afrika akiwa anamaliza mda wake akiwa mwenyekiti mwaka 2004. Amesema serikali imejipanga kueneza lugha ya kiswahili na wataalamu watakaotumika watakuwa wahitimu kutoka vyuo vikuu nchini.

Author: Gadi Solomon