Fahamu nahau za Kiswahili na maana zake

1. Vimba kichwa -Kuwa mkaidi.

2. Kutia kiraka- Fichia siri mtu.

3. Kumlainisha mtu – Kumwambia mtu maneno ya ushawishi.

4. Kutia utambi –kuchochea jambo.

5. Kumeza maneno moyoni – kuficha siri

6. Kula njama – kufanya jambo kwa siri

7. Pangu pakavu tia mchuzi – maskini.

8. Kumwonyesha mgongo – kujificha.

9. Kuona cha mtema kuni – kupata mateso.

10. Maneno ya uani – maneno ya porojo.

11. Mkubwa jalala – kila lawama hupitia kwa mkubwa.

12. Mkaa jikono – mvivu wa kutembea.

13. Paka mafuta kwa mgongo wa chupa – danganya

14. Mtu mwenye ndimi mbili – kigeugeu

15. Kupiga supu – tegea.

16. Kupiga mali shoka – gawana, fuja mali

17. Kula chumvi nyingi – ishi miaka mingi.

18. Kuwa popo – kuwa kigeugeu

19. Vaa miwani/chapa maji – lewa pombe

20. Kuchungulia kaburi – mahututi nusura ya kufa

21. Ponda mali – fuja mali/tumia mali vibaya.

22. Hamadi kibindoni – akiba iliyopo kibindoni.

23. Hawapikiki chungu kimoja -hawapatani.

24. Kupika majungu – kufanya mazungumzo ya siri

25. Vika kilemba cha ukoka – kumpa mtu sifa asizostahili.

26. Kujipalia makaa – kujitia matatani

27. Mwaga unga – fukuzwa kazini.

28. Ongezewa unga – pandishwa cheo.

29. Uma mtu sikio – kumnong’ononeza mtu jambo la siri.

30. Chimba mtu – kumpeleleza mtu siri zake.

31. Kutia chumvi – kuongeza Habari za uongo.

32. Kula vumbi/mumbi/mwata – pata tabu

33. Kodoa macho – tazama sana kutokana na mshangao.

34. Kutoka shoti – Kimbia kwa kasi sana.

35. Kushtaki njaa – kula.

36. Kutiwa mbaroni/kutiwa nguvuni – kushikwa au kukamatwa na polisi.

37. Kuweka nadhiri- kutoa ahadi

38. Fua dafu – faulu.

39. Lilia ngoa – onea wivu kutokana na hali fulani nzuri.

40. Chimba mikwara – fanyia mtu vitisho.

41. Pigwa kalamu – achishwa kazi.

42. Zunguka mbuyu/kula rushwa– honga

43. Kanyaga chechele – potea njia.

44. Chukuliwa na chechele – sahau.

45.

Author: Gadi Solomon