Mbio za sakafuni

Na Patrick Massawe

Utanguliizi:

Delilah Maurice Shikonyi, mwanadada mrembo akiwa anaendesha gari lake jioni moja alimgonga kwa bahati mbaya mtembea kwa miguu aliyevuka kizembe. Hata hivyo, wakati akiwa katika harakati za kumpa msaada, kundi la wananchi wenye hasira kali lilitokea na kutaka kumwadhibu. Kwa Bahati nzuri akatokea kijana mmoja mwenye misuli, Ben Kanyau  ambaye alimwokoa  na kuondoka naye

katika eneo la tukio na kuepukana na dhahama ile. Mbele ya safari wanajikuta wakiunganisha uhusiano wa kimapenzi. Lakini  kitu ambacho  Delilah hakukijua, Ben alikuwa jambazi la kutisha!  Anamwingiza katika utata mzito na safari ndefu ya mashaka! Endelea kusoma hadithi hii hadi mwisho.

“Asante sana kakangu…” Delilah akamwambia huku akiendelea kuendesha gari.

Delilah na Ben walipoondoka mara baada ya Delilah kusababisha ajali ya kumgonga kijana yule katika Barabara ya Kawawa, Ilala. Umati ule wa watu uliobaki ukawa umeshangaa na kuliangalia lile gari aina ya Toyota Harrier  likitokomea kwa kasi. Hata hawakuwahi kuisoma namba kwa jinsi walivyokuwa wamechanganyikiwa . Vijana wale wa kihuni  wakabaki wakimlaani Ben kwa kumwokoa mwanadada huyo ambaye walitaka kumwadabisha.

“Yule jamaa mshenzi kweli”. Kijana mmoja akamwambia mwenzake.

“Anapenda sana sifa. Anajitia baunsa  mkalamba yule.” Mwenzake akamjibu huku akiwa amekunja sura yake!

“Ah yule si mtu wa chamoto kwani hamumfahamu anajulikana sana. Ukimchezea anakulipua.”

“Ni askari?”

“Hapana. Jambazi.”

“Basi makubwa.”

“Tuwajulishe polisi.”

“Sina muda wa kupoteza. Si unajua mambo ya polisi tena. Unaweza ukageuziwa kibao.”

“Hawawezi kukugeuzia kibao. Siku hizi kuna polisi jamii.”

“Polisi jamii?” Basi wajulishe wewe.”

“Mh tusilumbane. Tumshughulikie majeruhi”. ”Hilo la maana…”

Vijana wale wawili wakasogea hadi katika kile kikundi cha watu waliokuwa wamemzunguka yule kijana majeruhi. Wakati huo alikuwa amekaa chini  akiugulia maumivu wala hakuna mtu aliyekuwa tayari kumtafutia usafiri wa kumwahisha katika hospitali yoyote ya karibu. Damu zilikuwa zinamtoka miguuni na mikononi ambapo aliangukia  baada ya kugongwa na gari lile kiubavu.

“Mpisheni apate hewa.” Mmoja wa vijana wale alisema baada ya kumsogelea.

“Oh” kijana yule alikuwa anaugulia maumivu huku akiyazungusha macho yake kwa watu waliokuwa wamemzunguka.

“Mwahisheni hospitali nyie mnaomzunguka tu” Mzee mmoja wa makamo aliyeonekana muungwana aliwaambia watu wale baada ya kuwaona wamemzuguka tu wakimshangaa.

“Hakuna fedha za kukodi gari mzee. Si unaona wenye magari yao wanapita tu?”

“Ni kweli watu wamekuwa wabaya sana siku hizi! Hapana utu! Tafuteni taksi mimi nitalipa…” Mzee yule akawaambia huku akiingiza mkono wake mfukoni.

Hata hivyo, teksi iliyokwenda kutafutwa haijafika, gari moja la polisi wa doria aina ya Land Rover lilifika katika eneo hilo na kusimama baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa ajali ile. Askari polisi wawili walishuka kuelekea alipokuwa amekaa kijana yule na watu wakaanza kusogea nyuma kuwapisha.

“Pole sana kijana”, Askari mmoja akamwambia kijana  akamwinamia na kumwangalia kijana. “Oh! Aksante sana.” Kijana yule akawaitikia huku akiwaangalia.

“Unaitwa nani?  Askari yule akaanza kumhoji ikiwa ni kuchukua maelezo yake ya awali.

“Naitwa Hashim Ndumu.”
“Umri wako?”

“Miaka ishirini na sita”.

“Unaishi wapi?

Naishi  Buguruni kwa Malapa.

Baada ya kumhoji kijana yule askari akamgeukia mzee aliyekuwa anataka kutoa msaada wa kukodi teski na kumuuliza kama alizisoma zile namba za lile gari lililosababisha ajali.

“Mzee, uliliona lile gari lililomgonga huyu kijana?”

“Ndiyo nimeliona..” Mzee yule alijibu.

“Ni gari ya aina gani?”

“ Ni gari za kisasa…sijui…”  akasita kusita mzee yule.

“Ni Toyota Harrier …” akadakia kijana mmoja.

“Namba zake?”

“Hatukuzisoma”

“Mh sasa tutalipataje? Magari ya Harrier ni mengi hapa jijini. Askari yule akajibu kwa kukata tamaa.

“Ndiyo kosa walilolifanya hawa wananchi.” Akasema askari mwingine.

“Haya unaweza kunyanyuka? Kijana akaulizwa.

“Ndiyo naweza…” Kijana yule akasema huku  akinyanyuka kwa shida kidogo.

“Twende hospitali ukapate matibabu.”

Kijana yule akanyanyuka  huku akisaidiwa na askari polisi na kuingia katika gari. Askari wale wakapanda garini likatiwa moto na kuondolewa kumpeleka majeruhi hospitali ya Amana, Ilala. Baada ya gari lile kuondoka hali ikabaki kama ilivyokuwa mwanzo na gari la Delilah halikuweza kufahamika.

Ben Kanyau alikuwa amejikalia kwenye kiti upande wa kushoto kwenye gari la Delilah wakati Delilah mwenyewe akipangua gea na kuongeza mwendo wa gari. Wakati wote huo hisia zake zilikuwa mbali kwani aliihamishia akili yake yote katika umbo zuri la yule mwanadada mrembo. Ni umbile lililomvutia sana  na hata alipoyahamishia macho yake  tena katika sura yake alivutiwa sana. Gauni lake siyo sahihi kuliita refu  wala halikustahili kuitwa fupi.  Lilikuwa juu ya magoti kwa kiasi kidogo hivyo akayaanika kwa kiasi fulani sehemu ya mapaja yake makubwa kadiri akikanyaga klachi na pedali ya kuongezea mwendo.

Akili ya Ben ilikubali kuwa yule alikuwa ni mwanamke mzuri machoni mwa wanaume wanaopenda wanawake wazuri. Fikra za kurusha ndoana  dhidi ya mwanadada yule zikamjia Ben. Ni fikra ambazo kabla hajachukua uamuzi mara Delilah akamwambia kwa sauti nzuri.

“Kakangu..!”

“Naam” Ben akaitika na kumwangalia.

“Sijui nikushukuruje kwa kuniokoa. Nadhani sasa hivi ningekuwa maiti.”

“Hapana. Usingekuwa maiti”. Ben akamwambia huku akicheka.”Lakini naamini usingekuwa na gari lako.”

“Kwa nini?” Delilah akauliza

“Vibaka wangeligombania na kulicharanga vipande vipande. Matairi yangebebwa  na yangechukuliwa  na hata vyoo vyote vingeng’olewa .”Ben akaendelea kumwambia Delilah.

“Mh! Kweli?” Delilah akauliza.

“Ni kweli kabisa. Si ajabu hii redio isingekuwapo. Vibaka wale wengi wao  wana fani ya ufundi wa magari na pale  utawakuta wana zana zote za ufundi. Hivyo hufanya kazi zao kwa kasi kubwa na kwa uhakika. Yaani wao si wa kufanya kazi za kubahatuisha.” Ben alisema kwa msisitizo.

“Mungu wangu!”

“Ndivyo hivyo sista…kama dhoruba ingekukumba ungemwambia nini mzee?”

“Ningefikiria kama angekuwapo” Dalilah akajibu huku akitabasamu kwa mbali. Macho yake alikuwa ameyaelekeza barabarani  asije akafanya kosa jingine tena.

“Unasema kama angekuwapo?” Ben akamuuliza Delilah.

“Ndiyo kama angekuwapo”.
“Una maana gani?”

“Nina maana kuwa hayupo.”

“Kasafiri au?”

“Hapana sina mtu  wa aina hiyo. Sina mwanamume”

“Hivi unasema kweli? Huna mwanamume?”

“Ni kweli. Wala sikuongopei. Ni kwa nini nikuongopee?” Delilah akasema kwa kujiamini na kuongeza.” Wala sidhani kama uongo unaweza  kunisaidia. Ninavyokuambia ndiyo ukweli wenyewe.  Kama huniamini basi sina jingine la kukuambia.”

Ben akainamisha uso wake chini na kutulia kidogo. Halafu akaunyanyua tena huu akiachia tabasamu la mbali na kumwambia Delilah.

“Ni vigumu kuamini.”

“Kuamini nini?”

“Mwanamke mrembo kama wewe hadi leo hujaolewa.”

“Kwani ni ajabu?”Delilah akamkata kauli. Ina maana nimeanza kuzeeka?”

“Hapana…bado wewe ni mbichi kabisa.” Delilah akacheka .

“Si utani sista.” Ben akakatiza.

“Aksante…” Delilah akatamka kwa sauti ya kutamanisha

“Kwani  wanaume wamekuudhi nini hadi uwe hadi  sasa hujawa na mpenzi wako wa kuliwaza?”

“Basi tu. Sijaamua mwemyewe na wala si kwamba wanaumme wamenikosea chochote.

“Naomba basi niwe mumeo mtarajiwa.”
“Unasema?”

“Kama ulivyosikia.”Ben alimwambia Delilah huku amechomeka ombi hilo.

“Siyo vibaya lakini nadhani ni jambo jingine  lililo nje ya uwezo wangu  kwa sasa. Delilah akasema kwa upole akibadili gea   na kupunguza mwendo. Halafu akaendelea.

“Nadhani ni jambo lisilostahili kuchukua nafasi katika maongezi yetu ya leo…hapa nilipo nafikiria jinsi ya kukushukuru.”

“Usijali unaweza kunishukuru hata kwa kauli tu” Ben alimwambia.

“Hapana.” Delilah akapinga. Kazi uliyonifanyia braza ni kubwa. Ujue kwamba hili gari siyo ya mtu mwingine  bali ni langu mwenyewe. Kama ningekumbwa na dhahama   hiyo ya wale vijana  halafu nikabaki hai unadhani ningejisikiaje.

“Yaani hili gari ni lako?” Ben akamuuliza Delilah huku akimwangalia kwa macho yenye mshangao.

“Ndiyo manake.”

“Kumbe basi uko kamili.”

“Wapi kidogo tu. Ni katika kuhangaika na maisha.” Delilah akamwambia kwa sauti kidogo.

“Siyo kidogo sista”

“Ndiyo hivyo.”Delilah akamwambia kwa sauti ndogo na kuendelea.

“Hivi unaitwa nani mkombozi wangu?”

“Naitwa Benard David Kanyau au kwa kifupi naitwa Ben Kanyau kama watu wengine  walivyozoea kuniita.”  

“Nashukuru sana na mimi naitwa Delilah Maurice Shikonyi. Kabila langu ni Mchagga.

“Aisee vizuri sana.”
Ukinywa mfupi ukatawala ndani ya gari baada ya kutambulishana. Wakati huo walikuwa  kwenye taa za trafiki za makutano ya Barabara za Kawawa na Morogoro wakisubiri taa ya kijani iruhusu.

“Hivi wewe unaishi pale Ilala. Delilah akavunja ule ukimya.

“Ndiyo nimeishi pale zaidi ya miaka sita sasa. Na ni sehemu iliyoizoea.”

“Vizuri sana.” Akasema Delilah. Halafu akautumia muda huo wa kusubiri taa ya kijani iwake  na pia kufungua mkoba wake na kutoa pochi iliyokuwa ndani yake. Akaifungua na kutoa fedha kiasi cha laki moja  za noti kumi nyekundu  akamkabidhi Ben akimwambia,

“Tafadhali chukua fedha hii”

“Fedha za nini Delilah?” Ben akamuuliza huku akizishika zile fedha  bila kuonyesha dalili ya kuziweka mfukoni..

“Hiyo ni shukrani kwako.” Delilah akajibu bila  hata kumtazama.

“Shukrani ya nini?” Ben akazidi kumuuliza.

“Na hiyo naamini bado. Shukrani hizi hazijafikia kiwango kunachostahili kulingana na kazi uliyofanya.”

“Hapana Delilah.” Ben akanyoosha mkono na kumrudishia zile fedha na kuongeza,

“Sikufanya vile kwa mategemeo ya kulipwa. Hata hivyo kama hutajali basi kanipatie kinywaji chochote  ili nipooze koo langu.”

Mbio za Sakafuni -2

Utangulizi:

Delilah Mourice Shikonyi, mwanadada mrembo akiwa anaendesha gari lake jioni moja alingonga kwa Bahati mbaya mtembea kwa miguu aliyevuka barabara kizembe. Hata hivyo  wakati akiwa katika harakati za kumpa msaada, kundi la wananchi wenye hasira kali liloitokea na kutaka kumwadhibu. Kwa Bahati nzuri alitokea kijana mmoja mwenye misuli , Ben Kinyau ambaye alimwokoa  na kuondoka naye katika eneo la tukio na kuepukana na dhahma ile. Mbele ya safari, wanajikuta wakiunganisha uhusiano wa kimapenzi lakini Delilah hakukijua. Ben alikuwa jambazi la kutisha! Anamwingiza Delilah  katika utata mzito na safari ndefu ya mashaka! Endelea  na hadithi hii ya kusisimua mpaka mwisho wake.

“ Unataka kinywaji gani?” Delilah alimuuliza Ben.

“hata bia moja mbili tatu hivi…”

“unasema bia”

“Ndio manake…a u unnasemaje mwenzangu au wewe hutumii?”

“Mimi natumia…”

“Bali?”

“Hata mimi nakunywa, unadhani ni wapi panafaa kupata kinywaji?”

“Ziko sehemu nyingi tu, hata hapa Magomeni kuna grosari nyingi kila kona.”

“Basi poa kama wewe ni mwenyeji twende sehemu hiyo. Safari ya Kimara nitakwenda hata kesho kwani imeshaingia nuksi.

Wakati huo taa ya kijani ilishawaka na kuruhusu magari yaendayo Kinondoni. Delilah akaliendesha gari kuifuata barabara ile ya Kawawa kama anaelekea Kinondoni hhalafu baada ya mwendo mfupi, Delilah akaliegesha gari kando ya barabara  nje ya grosari iliyoukwa na uhaba wa wateja jioni ile. Ni sehemu ambayo siku za nyuma aliwah kufika na kuridhika na utulivu wa eneo hilo. Naona kwenye grosari hii panafaa…” Delilah akamwambia Ben huku akilipaki gari hilo kando ya barabara sehemu iliyokuwa na nafasi ambapo pia  palikuwa na magari mawili yaliyopaki.

“Hakuna tabu, popote tu ben akamwambia Delilah huku  akiufungua mlango wake wa kushoto.

Wote wawili wakashuka chini . Kabla ya kuelekea  pale kwenye grosari  kwanza kabisa wote wawili  walizungukia upande wa mbele wa lile gari na kuangalia kama limebondeka kutokana na kumgonga yule kijana.Hata hivyo waliliona  likiwa katika hali nzuri. Halikuathirika, hivyo wakaijondoa pale na kuelekea sehemu  ya usawa na grosari  ambapo walichagua sehemu iliyo tupu

Baada ya kukaa tu kimwana Delilah akaagiza vinywaji,  bia kwa kila mmoja. Walihudumiwa na kuendela  kunywa taratibu kila mmoja akiwa na mawazo  kichwani.Na pengine walikuwa wakitupa macho yao kkatika barabara ya kawawa kuangalia jinsi magari yalivyokuwa yakipita kwa wingi jioni ile.

Giza nalo likaanza kuingia.

Nusu saa ilkuwa imepita tangu Ben na Delilah  wafike eneo lile la Magomeni  wakijioatia vinywaji. Akiwa bado na wasiwasi  wa kumgonga mtu, Delilah akavuta pumzi ndeefu kasha akasema kwa sauti ndogo. “Unajua bado nawaza braza…”

“Unawaza nini?” Ben akamuuliza  huku akimwangalia na kuacha kunywa kile kinywaji chake ilichokuawa kwenye glasi.

“Sijui yle kijana  niliyemgonga  ana hali gani masikini.”

“Hayo yameshapita…” Ben akamkatiza.

“Yamepita?”

“Ndiyo kama kafa shauri yake! Mijitu mingine  ikishabwwia unga basi inaona barabara yote ni ya kwao peke yao. Yule atakuwa amebwia unga  sasa umemzidia na haoni njia.”

“Lakini askari wa trafiki hawatanifuatilia?”

“Wanawa eza kukufuatilia kama kuna mtu aliyefanikiwa kusoma namba ya gari. Hhata hivyo, hilo lisikutishe sna.”

“Kwa nini lisinitishe?”Delilah akauliza

“Jiandae tu kwani hakuna linaloshindikana. Tenga fedha kidogo ya kuzungumza nao endapo watakufuatilia. Au unasemaje?”

“Hakuna tatizo, nitazungumza nao kama watakuwa  wamenigundua. Hakuna kinachoshindikana.”

“Hilo ndilo neno, basi poa. Tuendelee na mengine …” Ben akamwambia baada ya kuona  kuwa alikuwa mwanamke mwelewa.

Baada ya maongezi mafupi wakaendelea kunywa huku ukimya ukitawala. Kila mmjoa akiwa na mawazo yake kichwani. Hasa kwa Delilah ambaye amekatizwa  safari yake  ya kwenda Kimara  na baadaye kujikuta ratiba yake imebadilika  na kuizamia katika kinywaji  akiwa na mwanamume  yule aliyemwakoa katika janga la kupigwa na wananchi waliokuwa na hasira kali dhidi yake. Ukweli ni kwamba alikuw anajiona kama mtu aliye katika ndoto kali ya kusisimua.

Lakini kwa upande wa ben alikuwa na wo jingine kabisa.Wazp lake lilikuwa la kutaka kurusha ndoano dhidi ya mwaaanadada yule . yeye alikuwa mgonjwa hasa tena kwa wanawake  warembo, wasafi wanaovutia kama yule Delilah aliyekaa naye . Aliona kana kwamba alikuwa amekutana na nyota  ya jaha kwa kudondoshewa na kimwana huyo. Mungu ampe nini?

Huo ulikuwa ni muda mwafaka wa  wa kujaribu kumwingia nap engine kwa kuifahamu historia yake  kwanza kwani alihisi kuwa mwanadada huyoaalikuwa na nguvu za kuichumi au alikuwa anamilikiwa na ‘shefa la nguvu’ linalimtosheleza kwa kila kitu.

”Delilah,”ben alimwita kwa sauti ndogo.

“Bee” Delilah akaitikia  na kumwangalia Ben.

“Unajua kuwa jina lako ni zuri sana?”

“Kwa nini unasema hivyo?”

“Nina maana ynagu kusema hivyo Delilah.”

“Maana gani?” Delilah akauliza huku akiunda tabasamu jepesi

“ Linanikumbusha mbali sana

“mbali wapi tena?”

“Kama vitabu vya dini vinavyoeleza  enzi zile za yule mtu aliyekuwa na nguvu sana  kiasi cha kuwashinda adui zake. Ni mtu aliyejulikana kwa jina la Samson ambaye aliponzwa nan a mwanamke  aliyeitwa Delilah na kufanya akamatwe na maadui zake Wafilisti ambao walimng’oa macho yake na ukawa mwisho wake.

“Ah wewe Ben.” Delilah akamkatiza.

“Basi ndio hilo tu.”

“Aisee na jina la kanyau lina maana gani au ni jina la ukoo?”

“hapana hilo sio jina la ukoo.,” Ben akasema na kuendelea. ‘Ni ina ambalo nilikatiwa tangu nikiwa mdogo eli kwa sababu nilikuwa napenda sana kufuga ‘nyau’ yaani mnyama aina yap aka. Basi jina Kanyau likanizoea mpaka leo.”

Wote wakacheka kwa nguvu.

Maongzi yaliyofuata baadaye, Ben alikuwa kinara ambapo hakuzembea kwani alianza kurusha kombora yake dhidi ya mwanadada Delilah kutumia utaalamu  wa hali ya juu.

“Sasa Delilah nisikilze.” Ben akamwambia.

“Nakusilikiza  Ben.”

“Kuna jambo nataka kukuambia.”
“Jambo gani tena?

“Ingawa tumekutana leo tena kibahati baada ya ajali ile sina budi kukueleza dukuduku langu la moyoni mwangu kwa muda huu…huo ndiyo ukweli.”

“Mbona unanichekesha ?” Delilah akamwmbia na kuendelea. “Ni dukuduku gani ulilo nalo moyoni? Kuwa wazi.”

“bila kukuficha nimejikuta nakupendatu. Ni tangu tukutane. Ni Mungu alipanga iwe hivyo

“umesema unanipenda?”

“Ndiy manake.”

“Hebu fafanua…”

“Nimekupenda Delilah. Naomba unikubalie ombi langu  nitakalokuambia ingawa ni nara yetu ya kwzna kukutana.”

“Nimeshakuambia kuwa wazi, ni ombi gani ben?” Delilah akamuuliza Ben ambaye nishai ya pombe ilishamwingia. Na ukweli ni kuwa ameshaelewa nia ya ben akiwa kama mwanamume amemtaka kimapenmzi.

“Naomba kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wewe. Ninakueleza wazi kwani mwenzio nimezidiwa.” 

:Lakini mbona mapema sana?”

“Diyo mapema Delilah.” Ben akaendelea kusema. “Nnaumaini wewe ni mwanamke  mmsomi na unaelewa  nilichosema au unataka nifafanue zaidi?”

“Nimekuelewa sana lakini kwa leo haitawezekana kwani ni lzima kuwe na maandalizi…tutapanga…tufanye siku nyingine.” Delilah akamwambia B

“Oh Delilah yaani mtu njaa kali na chakula nakiona hapahapa halafu unaniambia kesho?”

“Mh na wewe” Delilah akasema baada ya kuona amezidiwa maarifa na Ben. Akakumbuka ile fadhila aliyofanyiwa naye muda siyo mrefu kwa kuokolewa katikati ya lindi la wahuni na vibaka wa Ilala.

“Naomba unielewe Delilah.” Benakaendeklea kusema kwa sauti inayotia huruma ambayo  ilitosha kumlegeza  mwanamke yeyote lakini kwa Delilah akawa ngumu. Usiwe na wasiwasi Ben mambo yatatengenezwa.” Delilah akamwambia Ben huku akimwangalia usoni bila kukwepesha macho yake mazuri.

“Kwa hivyo niwe na matumaini?”

“Ondoa shaka.”Baada ya kujibiwa vile Ben alikuwa na matumaini ya kumnasa mrembo yule aliyemrushia ndoana yake kitaalamu ambayo ilikumana na vikwazo vichache . Ni kweli vilikuwa ni vikwazo  hasa ikizingatia kuwa mwenyewe alikuwa msomi ambaye kuwezi kumwingiz tu akakubaliana na mawazo yako. Safari ya Delilah ya kwenda Kimara ikaishia palepale ambapo ilipotimu saa tatu za usikuiliwakuta wakiwa katika ile grosari wakiendelea kunywa na pia kula nyama choma waliyoaigiza  sehemu nyingine inapochomwa. Kwa muda wote kinara wa maongezi alikuwa Ben ambaye ni muongaji mzuri mwenye mvuto.

Delilah aliunyanyua mkono wake wa kushoto na kuangalia saa yake ya dhahabu. Ilionyesha kuwa imetimu  saa nne  hivyo akamwangalia Ben aliyekuwa anamalizia kinywaji chake kilichokuwa kwenye glasi.

“Naona saa zimekimbia, inatosha kwa leo.” Delilah akamwambia ben.

“Ni kweli ni muda wa kuondoka.” Ben alimwambia

Ndipo Ben na belilah walipoamua kuondoka katika grosari ile. Wakanyanyuka na kuliendela gali lililokuwa kando kidogo. Wotw walikuwa na nishai ya kutosha na kuonekana kauwa ni wapenzi wawili  jinsi  walivyokuwa wakilisogea lile gari.

“Sasa?” Delilah akamuuliza ben

“Unasemaje?” Delilah  naye akamuuliza Ben

“Tunakwenda wapi, kwako au kwangu?” “Twende nyumbani kwangu Mbezi Beach.”

“hakuna tabu maana ulishanihakikishia usalama kuwa uko ‘singo’, twende.

Delilah akaufungua mlango wa upande wa dereva na kuingia ndani huku akifuatiwa na Ben aliyefungua mlango wa upande wa kushoto na kuingia. Delilah akalitia moto gari lile na kuliondoa pale kuelekea Mbezi Beach. Ingawa alikuwa na nishai lakini Delilah alilimudu lile gari bila matatizo yoyote ambapo waliifuata Barabara ya Kawawa kwa mwendo wa wastani kwani amgari yalikuwa mengi hasa mabasi ya daladala yaliyokuwa hayajali Sheria za Usalama Barabarani.

Hata hivyo walifanikiwa kufika katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi  kwenye taa za trafiki ambapo walipinda na kuifuata Barabara hiyo kuelekea Mwenge.. pale waliifuata barabara ya Sam Nujoma kuelekea Mbezi Beach kwa kupitia Mikocheni. Muda woate ben alikuwa akishangaa jinsi alivyoweza kukutana na kimwana yule ambaye alimfunga kamba ya kuunganisha mapennzi kwake anye hakuweka kipingamizi chochote. Ukweli ni kwamba aliona kuwa mtu yule ndiye mzuri atakayemfaa katika shughuli  zake zinazomuweka hapa mjini.

Mwisho.

Mbio za Sakafuni -3

Utangulizi:

Delilah Mourice Shikonyi, mwanadada mrembo akiwa anaendesha gari lake jioni moja alingonga kwa Bahati mbaya mtembea kwa miguu aliyevuka barabara kizembe. Hata hivyo  wakati akiwa katika harakati za kumpa msaada, kundi la wananchi wenye hasira kali lilitokea na kutaka kumwadhibu. Kwa Bahati nzuri alitokea kijana mmoja mwenye misuli, Ben Kinyau ambaye alimwokoa  na kuondoka naye katika eneo la tukio na kuepukana na dhahma ile. Mbele ya safari, wanajikuta wakiunganisha uhusiano wa kimapenzi lakini Delilah hakukijua. Ben alikuwa jambazi la kutisha! Anamwingiza Delilah  katika utata mzito na safari ndefu ya mashaka! Endelea  na hadithi hii ya kusisimua mpaka mwisho wake.

“Unataka kinywaji gani?” Delilah alimuuliza Ben.

“Hata bia moja mbili tatu hivi…”

“Unasema bia”

“Ndio manake…au unasemaje mwenzangu au wewe hutumii?”

“Mimi natumia…”

“Bali?”

“Hata mimi nakunywa, unadhani ni wapi panafaa kupata kinywaji?”

“Ziko sehemu nyingi tu, hata hapa Magomeni kuna grosari nyingi kila kona.”

“Basi poa kama wewe ni mwenyeji twende sehemu hiyo. Safari ya Kimara nitakwenda hata kesho kwani imeshaingia nuksi.

Wakati huo taa ya kijani ilishawaka na kuruhusu magari yaendayo Kinondoni. Delilah akaliendesha gari kuifuata barabara ile ya Kawawa kama anaelekea Kinondoni halafu baada ya mwendo mfupi, Delilah akaliegesha gari kando ya barabara  nje ya grosari iliyoukwa na uhaba wa wateja jioni ile. Ni sehemu ambayo siku za nyuma aliwah kufika na kuridhika na utulivu wa eneo hilo. Naona kwenye grosari hii panafaa…” Delilah akamwambia Ben huku akilipaki gari hilo kando ya barabara sehemu iliyokuwa na nafasi ambapo pia  palikuwa na magari mawili yaliyopaki.

“Hakuna tabu, popote tu Ben akamwambia Delilah huku  akiufungua mlango wake wa kushoto.

Wote wawili wakashuka chini . Kabla ya kuelekea  pale kwenye grosari  kwanza kabisa wote wawili  walizungukia upande wa mbele wa lile gari na kuangalia kama limebondeka kutokana na kumgonga yule kijana. Hata hivyo waliliona  likiwa katika hali nzuri. Halikuathirika, hivyo wakaiondoa pale na kuelekea sehemu  ya usawa na grosari  ambapo walichagua sehemu iliyo tupu

Baada ya kukaa tu kimwana Delilah akaagiza vinywaji, bia kwa kila mmoja. Walihudumiwa na kuendela  kunywa taratibu kila mmoja akiwa na mawazo  kichwani. Na pengine walikuwa wakitupa macho yao katika barabara ya kawawa kuangalia jinsi magari yalivyokuwa yakipita kwa wingi jioni ile.

Giza nalo likaanza kuingia.

Nusu saa ilikuwa imepita tangu Ben na Delilah  wafike eneo lile la Magomeni  wakijipatia vinywaji. Akiwa bado na wasiwasi  wa kumgonga mtu, Delilah akavuta pumzi ndeefu kasha akasema kwa sauti ndogo. “Unajua bado nawaza braza…”

“Unawaza nini?” Ben akamuuliza  huku akimwangalia na kuacha kunywa kile kinywaji chake ilichokuawa kwenye glasi.

“Sijui yule kijana  niliyemgonga  ana hali gani masikini.”

“Hayo yameshapita…” Ben akamkatiza.

“Yamepita?”

“Ndiyo kama kafa shauri yake! Mijitu mingine  ikishabwwia unga basi inaona barabara yote ni ya kwao peke yao. Yule atakuwa amebwia unga  sasa umemzidia na haoni njia.”

“Lakini askari wa trafiki hawatanifuatilia?”

“Wanaweza kukufuatilia kama kuna mtu aliyefanikiwa kusoma namba ya gari. Hata hivyo, hilo lisikutishe sna.”

“Kwa nini lisinitishe?”Delilah akauliza

“Jiandae tu kwani hakuna linaloshindikana. Tenga fedha kidogo ya kuzungumza nao endapo watakufuatilia. Au unasemaje?”

“Hakuna tatizo, nitazungumza nao kama watakuwa  wamenigundua. Hakuna kinachoshindikana.”

“Hilo ndilo neno, basi poa. Tuendelee na mengine …” Ben akamwambia baada ya kuona  kuwa alikuwa mwanamke mwelewa.

Baada ya maongezi mafupi wakaendelea kunywa huku ukimya ukitawala. Kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani. Hasa kwa Delilah ambaye amekatizwa  safari yake  ya kwenda Kimara  na baadaye kujikuta ratiba yake imebadilika  na kuizamia katika kinywaji  akiwa na mwanamume  yule aliyemwakoa katika janga la kupigwa na wananchi waliokuwa na hasira kali dhidi yake. Ukweli ni kwamba alikuwa najiona kama mtu aliye katika ndoto kali ya kusisimua.

Lakini kwa upande wa mwingine alikuwa na wazo jingine kabisa. Wazo lake lilikuwa la kutaka kurusha ndoana dhidi ya mwanadada yule. yeye alikuwa mgonjwa hasa tena kwa wanawake  warembo, wasafi, wanaovutia kama yule Delilah aliyekaa naye. Aliona kana kwamba alikuwa amekutana na nyota  ya jaha kwa kudondoshewa na kimwana huyo. Mungu ampe nini?

Huo ulikuwa ni muda mwafaka wa  wa kujaribu kumwingia nap engine kwa kuifahamu historia yake  kwanza kwani alihisi kuwa mwanadada huyoaalikuwa na nguvu za kuichumi au alikuwa anamilikiwa na ‘shefa la nguvu’ linalimtosheleza kwa kila kitu.

”Delilah,” Ben alimwita kwa sauti ndogo.

“Bee” Delilah akaitikia  na kumwangalia Ben.

“Unajua kuwa jina lako ni zuri sana?”

“Kwa nini unasema hivyo?”

“Nina maana yangu kusema hivyo Delilah.”

“Maana gani?” Delilah akauliza huku akiunda tabasamu jepesi

“Linanikumbusha mbali sana

“Mbali wapi tena?”

“Kama vitabu vya dini vinavyoeleza  enzi zile za yule mtu aliyekuwa na nguvu sana  kiasi cha kuwashinda adui zake. Ni mtu aliyejulikana kwa jina la Samson ambaye aliponzwa na mwanamke  aliyeitwa Delilah na kufanya akamatwe na maadui zake Wafilisti ambao walimng’oa macho yake na ukawa mwisho wake.

“Ah wewe Ben.” Delilah akamkatiza.

“Basi ndio hilo tu.”

“Aisee na jina la Kanyau lina maana gani au ni jina la ukoo?”

“Hapana hilo sio jina la ukoo.,” Ben akasema na kuendelea. ‘Ni jina ambalo nilikatiwa tangu nikiwa mdogo eti kwa sababu nilikuwa napenda sana kufuga ‘nyau’ yaani mnyama aina ya paka. Basi jina Kanyau likanizoea mpaka leo.”

Wote wakacheka kwa nguvu.

Maongzi yaliyofuata baadaye, Ben alikuwa kinara ambapo hakuzembea kwani alianza kurusha kombora lake dhidi ya mwanadada Delilah kutumia utaalamu  wa hali ya juu.

“Sasa Delilah nisikilize.” Ben akamwambia.

“Nakusilikiza  Ben.”

“Kuna jambo nataka kukuambia.”
“Jambo gani tena?

“Ingawa tumekutana leo tena kibahati baada ya ajali ile sina budi kukueleza dukuduku langu la moyoni mwangu kwa muda huu…huo ndiyo ukweli.”

“Mbona unanichekesha ?” Delilah akamwmbia na kuendelea. “Ni dukuduku gani ulilo nalo moyoni? Kuwa wazi.”

“Bila kukuficha nimejikuta nakupenda tu. Ni tangu tukutane. Ni Mungu alipanga iwe hivyo

“Umesema unanipenda?”

“Ndiyo manake.”

“Hebu fafanua…”

“Nimekupenda Delilah. Naomba unikubalie ombi langu  nitakalokuambia ingawa ni mara yetu ya kwanza kukutana.”

“Nimeshakuambia kuwa wazi, ni ombi gani Ben?” Delilah akamuuliza Ben ambaye nishai ya pombe ilishamwingia. Na ukweli ni kuwa ameshaelewa nia ya Ben akiwa kama mwanamume amemtaka kimapenzi.

“Naomba kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wewe. Ninakueleza wazi kwani mwenzio nimezidiwa.” 

Lakini mbona mapema sana?”

“Ndiyo mapema Delilah.” Ben akaendelea kusema. “Natumaini wewe ni mwanamke  msomi na unaelewa  nilichosema au unataka nifafanue zaidi?”

“Nimekuelewa sana lakini kwa leo haitawezekana kwani ni lazima kuwe na maandalizi…tutapanga…tufanye siku nyingine.” Delilah akamwambia B

“Oh Delilah yaani mtu njaa kali na chakula nakiona hapahapa halafu unaniambia kesho?”

“Mh na wewe” Delilah akasema baada ya kuona amezidiwa maarifa na Ben. Akakumbuka ile fadhila aliyofanyiwa naye muda siyo mrefu kwa kuokolewa katikati ya lindi la wahuni na vibaka wa Ilala.

“Naomba unielewe Delilah.” Ben akaendelea kusema kwa sauti inayotia huruma ambayo  ilitosha kumlegeza  mwanamke yeyote lakini kwa Delilah akawa mgumu. Usiwe na wasiwasi Ben mambo yatatengenezwa.” Delilah akamwambia Ben huku akimwangalia usoni bila kukwepesha macho yake mazuri.

“Kwa hivyo niwe na matumaini?”

“Ondoa shaka.”Baada ya kujibiwa vile Ben alikuwa na matumaini ya kumnasa mrembo yule aliyemrushia ndoana yake kitaalamu ambayo ilikuma na vikwazo vichache . Ni kweli vilikuwa ni vikwazo  hasa ikizingatia kuwa mwenyewe alikuwa msomi ambaye kuwezi kumwingiza tu akakubaliana na mawazo yako. Safari ya Delilah ya kwenda Kimara ikaishia palepale ambapo ilipotimu saa tatu za usiku iliwakuta wakiwa katika ile grosari wakiendelea kunywa na pia kula nyama choma waliyoiagiza  sehemu nyingine inapochomwa. Kwa muda wote kinara wa maongezi alikuwa Ben ambaye ni muongaji mzuri mwenye mvuto.

Delilah aliunyanyua mkono wake wa kushoto na kuangalia saa yake ya dhahabu. Ilionyesha kuwa imetimu  saa nne  hivyo akamwangalia Ben aliyekuwa anamalizia kinywaji chake kilichokuwa kwenye glasi.

“Naona saa zimekimbia, inatosha kwa leo.” Delilah akamwambia Ben.

“Ni kweli ni muda wa kuondoka.” Ben alimwambia

Ndipo Ben na Delilah walipoamua kuondoka katika grosari ile. Wakanyanyuka na kuliendela gali lililokuwa kando kidogo. Wote walikuwa na nishai ya kutosha na kuonekana kuwa ni wapenzi wawili  jinsi  walivyokuwa wakilisogea lile gari.

“Sasa?” Delilah akamuuliza Ben

“Unasemaje?” Delilah  naye akamuuliza Ben

“Tunakwenda wapi, kwako au kwangu?” “Twende nyumbani kwangu Mbezi Beach.”

“Hakuna tabu maana ulishanihakikishia usalama kuwa uko ‘singo’, twende.

Delilah akaufungua mlango wa upande wa dereva na kuingia ndani huku akifuatiwa na Ben aliyefungua mlango wa upande wa kushoto na kuingia. Delilah akalitia moto gari lile na kuliondoa pale kuelekea Mbezi Beach. Ingawa alikuwa na nishai lakini Delilah alilimudu lile gari bila matatizo yoyote ambapo waliifuata Barabara ya Kawawa kwa mwendo wa wastani kwani magari yalikuwa mengi hasa mabasi ya daladala yaliyokuwa hayajali Sheria za Usalama Barabarani.

Hata hivyo walifanikiwa kufika katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi  kwenye taa za trafiki ambapo walipinda na kuifuata Barabara hiyo kuelekea Mwenge.. Pale waliifuata Barabara ya Sam Nujoma kuelekea Mbezi Beach kwa kupitia Mikocheni. Muda wote Ben alikuwa akishangaa jinsi alivyoweza kukutana na kimwana yule ambaye alimfunga kamba ya kuunganisha mapenzi kwake naye hakuweka kipingamizi chochote. Ukweli ni kwamba aliona kuwa mtu yule ndiye mzuri atakayemfaa katika shughuli  zake zinazomuweka hapa mjini.

Mbio za Sakafuni -4

Delilah Maurice Shikonyi mwanadada mrembo akiwa akiendesha gari lake jioni, alimgonga mtembea kwa miguu aliyevuka barabara kizembe. Hata hivyo akati akiwa katika harakati za kumpa msaada kundi la wananchi lilijitokeza ghafla na kutaka kumwadhibu.

Kachero Inspekta James na Delilah wakabaki pale ofisini wakimsubiri Mhasibu Mkuu Othman Mbega afike pale tayari kwa mahojiano. Muda wote ule Delilah hakuwa na amani kabisa rohoni mwake kwani hakujua hatima yake wakati ameshafikishwa ndani ya  himaya ya dola. Angeweza kunusurika na mkasa ule  ulioanza kutishia maisha yake. Hakujua ni nini kitatokea. Alisubiri miujiza. Lakini ni miujiza gani inaweza kutokea  ya kumwokoa yeye akiwa ni mtuhumiwa  nambari moja? Machozi yakaendelea kumbubujika kwa wingi! Othman Mbega, Mhasibu Mkuu wa kampuni ile ya kuuza magari alibaki ameduwaa kwa muda pale ndani ya ofisi yake mara tu  baada ya Kachero Inspekta James   kukata simu ile aliyokuwa amempigia  kumjulisha afike kituo cha Polisi Chang’ombe  mara moja. Aliuliza kuna tatizo gani? Swali lile lilimjia kichwani  mara kadhaa ndani ya dakika moja lakini hakuweza kupata jibu lolote akijua kuwa atalipata huko huko  kituoni.

Bila kupoteza muda  Othman Mbega alitoka ofisini kwake na kuelekea nje sehemu ya maegesho ya magari. Akaliegesha gari lake aina ya Toyota Landcruiser Prado na kupanda kuelekea  kituoni kama alivyokuwa ameelekezwa. Ingawa magari yalikuwa ni mengi barabarani hakukawia kufika  kwenye kituo kile  cha polisi. Akalipaki gari lake sehemu ya maegesho halafu akashuka na kuelekea ndani ya ofisi ya Kachero Inspekta James  iliyokuwa katika jengo lile na pia ilikuwa inatazamana na  upande wa mbele  wa kituo. 

Othman Mbega  akaiendea  ofisi ile  na kugonga mlango mara mbili na kisha kuingia ndani. Kwa wasiwasi kidogo akitegemea kumkuta  James peke yake. Kitu cha kwana kilichomshtua na mumshangaza Mbega ni baada ya kumkuta Delilah akiwa amekaa ndani ya ofisi ile aliyoelekezwa mara tu alipozungumza  na askari polisi mmoja aliyekuwa pale mapokezi mwanzoni mwa lango kuu. Delilah hakuwa  katika hali ya kawaida  akionekana kuchafuka na macho kuwa mekundu!

Delilah alikuwa amekaa katika kiti  kilichotazamana na meza iliyokuwa amekaa  Kachero Inspekta James. Delilah alimwangalia bosi wake kwa sura iliyojaa hofu. Wakaangaliana kidogo halafu Delilah  akainamisha uso wake. Ni kitu gani kimemsibu? Mbega akajiuliza.

Karibu! Karibu Bw. Mbega. Inspekta James alimkaribisha.

“Ahsante…”Mbega akajibu akionekana bado amechanganyikiwa.. halafu akavuta kiti kingine na kukaa taratibu macho yakiwa yametazamana kwa zamu na Delilah pamoja na James. Baada ya kukaa akapumua  kwa nguvu huku akijaribu kuutoa wasiwasi aliokuwa nao.  Alijiona kama vile alikuwa  na ndoto ya ajabu.

“Ndiyo Bwana Mbega… kuna tatizo “ Kachero  Inspekta James  akamwambia kwa sauti ndogo na huku akitabasamu kidogo.

“Tatizo gani”? Othamn Mbega akauliza.

“Ni tatiizo” James akasema na kuongeza huku akigeuza zile karatasi zilizokuwa mezani kwake na kuenndelea. “Siyo ndogo wala kubwa  kupindukia.  Kwanza naomba uniambie, je, unamfahamu huyu dada aliyeko hapa”? 

“Ndiyo namfahamu.” Mbega akasema kwa haraka.  

“Anasema yeye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Ahmed Motors, je, ni kweli?”

“NI kweli kabisa.”

“Na wewe ni mfanyakazi wa kampuni hiyo?”

“Naomba kitambulisho chako”

“Sawa. Othman Mbega akatoa kitambulisho cha kazi na kumpatia Kachero Inspekta James. Baada ya kukipitia akakitazama  kidogo na kumrudishia huku akimgeukia  Delilah na kumwambia,”Hebu naomba na cha kwako.”

 “Sikuja nacho.”

“Umekiacha wapi?”

 “Nimekiacha ndani ya mkoba wangu ofisini.”

“Vizuri.” Kachero Innspekta James  akasema huku akiwatazama  kwa zamu. Kisha akamwambia Mbega, “Bwana Mbega kuna taarifa yoyote  uliyoipata kabla ya mimi kukupigia simu?”

“Taarifa kuhusu nini?”Mbega akauliza kwa mshangao!

 “Kuhusu huyu mfanyakazi mwenzako Delilah?” ‘Taarifa gani?”
“Wewe si bosi wake”

“Ndivyo ilivyo”

“ Alipotoka ofisini  ulikuwa na taarifa.”
“Ndiyo taarifa hiyo ninayo.”

“Alikuwa na ruti ya wapi?”

“Alikuwa na safari ya kwenda benki.”
“Kufanya nini?”

“Kwani yeye hajakupa maelezo.”Mbega akauliza huku akiwa amekunja uso.

“Yeye ni yeye na wewe ni wewe kama Mbega tafadhali naomba unielewe.”

“Alikuwa anapeleka fedha.”
Zilikuwa kiasi gani?”

“Shilingi milioni mia nne.”

Kachero Inspekta James akaandika kidogo katika karatasi halafu  akashusha pumzi ndefu na kumkazia macho Mbega.

Akamwambia kwa sauti nzito isiyokuwa na masihara ndani yake.

“Basi kwa mujibu wa keshia wako ni kwamba fedha hizo zimeporwa.”

“Unasemaje?” Othman Mbega akauliza kidogo huku akisimama. Hakuamini masikio yake. Akamtumbulia macho James  kama vile alikuwa  amemwambia habari mpya kutoka kuzimu.

Habari ya kutisha!

“Ndiyo ukweli wenyewe“ Kachero Inspekta James  akaendelea kusisitiza.

“Delilah! Delilah! ni kweli hayo?” Othman Mbega akamgeukia Delilah na kumuuliza.

“Ni kweli bosi” Delilah akasema kwa sauti ya udhaifu.

“Hapana! Haiwezekani! Othman Mbega akasema huku akigonga meza! Pua zikatanuka  na vinyweleo vikasimama  kama mbwa aliyekasirika.

“Basi imewezekna.”Kachero Inspekta James akamwambia.

“Siamini “

“Tulia nikwambie”

“Huwezi kuniambia kitu! Yaani hapa nimechanganyikiwa.”

Kachero James akataka Delilah atoe maelezo yake tena. Ni maelezo ambayo  yaliendelea kumchanganya Mbega kwa kiasi kikubwa  ambapo alimtazama James  kwa macho makali  na jasho jingi kumtoka. Halafu akamuuliza:

“Kwa hivyo ni kipi kinaendelea?”

“Itabidi tuwazuilie wote wawili kwa ajili ya upelelezi zaidi. Huo ndiyo utaratibu wetu.” James akamwambia  akipigapiga kalamu yake juu ya meza.

“Unasema?” Othman Mbega akahamaki :
“Mungu wangu.” Delilah naye akasema!

“Ndivyo hivyo hakuna jinsi. Na waliopora fedha hizo watapatikana tu.” Taarifa zimezagaa kila kona na pia fedha zitapatikana tu.

“Fedha zipatikane?” Mbega akauliza.

“Ndiyo zitapatikana  kwani inaelekea majambazi hao hawajatoka nje ya jiji. Askari wetu wako katika msako mkali.”

“Zikiwa mikononi mwa majambazi  labda iwe miujiza!”

Mbega akasema huku akijiinamia  na kushika jama.

Ama kweli  haikuwa ni kauli ya kumpa matumaini makubwa Othman Mbega akihofia kupoteza ajira yake. Kwa vyovyote  akijua kwamba taarifa zile zingemfikia mmiliki wa kampuni ile  Ahmed Barwan Karama aliyeko Dubai, Falme za Kiarabu basi miongoni mwa hatua dhidi yake ni  kufukuzwa kazi. Na pia angekuwa miongoni mwa watu ambao wangelisaidia Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu msaada ambao angeutoa akiwa mahabusu

Ni hatari sana.

Othman Mbega  alivuta pumzi ndefu na kuzishusha halafu akamwambia Kachero Inspekta James “Afande una uhakika gani wa  maneno yako? Unadhani watu hao hawakujiandaa kikamilifu kabla ya kufanya uporaji huo?”

“Ni kweli walijiandaa, lakini hilo lisikutishe.  Nakuhakikishia kuwa tuko kazini hivi sasa. Hata kama siyo leo lakini lazima tuwatie mbaroni tu.”

“Sijui.”Othmani Mbega akasema huku akiona kama tukio lile lilikuwa ni hadithi ya kuudhi masikioni mwake. Hakika alikuwa  amechanganyikiwa. Hakuamini kwa asilimia mia moja kwamba fedha zile zingepatikana ndiyo ukweli wenyewe.

Muda wote redio ya mawasiliano iliyokuwa pale mezani  ilikuwa  ikieleza jinsi askari polisi walivyokuwa katika  harakati za kufuatilia  tukio lile  kwa kutumia askari wa miguu, pikipiki na magari. Hatua nyingine iliyofutata ilikuwa  ni kuwaweka chini ya ulinzi Delilah na bosi wake Othman Mbega ili kujua  ukweli wa mambo ambao Delilah aliujua fika.

Ben Kanyau  aliyekuwa amedondokea mle ndani ya bonde kubwa lenye vichaka vilivyofungamana kiasi cha makachero wa polisi kumtafuta na kumkosa  alikuja kupata  fahamu baada ya saa mbili kupita. Wakati huo usiku ulikwishaingia na kwa muda huo alikuwa juu ya nyasi na maumivu aliyoyahisi zaidi kuliko mengine ni jaraha la riasi aliyopigwa na mmoja wa makachro  waliokuwa wanamfuatilia.

Pia kwa mbali Ben alihisi maumivu mengine  ya kiuno chake  ambayo hayakuwa makali sana. Taratibu alijiinua na  kukaa huku  amezugukwa na giza kiasi kwamba alishindwa kuona kitu chochote kilichokuwa karibu naye. Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha huku akiwaza jinsi alivyoweza kuwakwepa makachero wale baada ya kuangukia ndani ya bonde na wala hakujua walielekea wapi baada ya kumkosa.

Kwa vyovyote vile alijua kuwa  walikuwa wanaendelea na msako wao mpaka wamtie mbaroni jambo ambalo hakutaka kabisa.
Maumivu ya begani yalizidi kumuuma hivyo akanyanyua mkono wake na kushika  sehemu hiyo iliyokuwa na jeraha. Kwa mara ya kwanza ndipo alipohisi joto na mnato wa damu iliyokuwa ikimtoka  kwa wingi. Ndipo alipotambua kuwa alikuwa ameumia sana.

Moyoni mwake Ben aliwalaani makachero wale wa polisi  waliompiga risasi. Aliponyanyua uso wake pazia jeusi lililojitandaza mbele ya macho yake  lilitoweka  na nuru ya mbalamwezi iliyokuwa imejitokeza. Akanyanyuka  na kuanza kuondoka katika eneo lile  kwa mwendo wa kuchechemea na maumivu ya kiunoni  aliyahisi  zaidi kama mtu aliyechomwa na msumari wenye mcha butu  nyuma ya nyonga.

Akajishika kiunoni  ambapo aliuma meno na kupepesuka na kwa hatua za polepole  akauendea ule mkoba uliokuwa na rundo la fedha na kuuchukua. Alipokuwa anaondoka  katika eneo lile akaichomeka bastola yake kiunoni na kujaribu kuvuta hatua ndefu. Maumivu ya jeraha lile la risasi pamoja na la kiunoni yalimfanya aume meno. Kwa mbali alisikia kizunguzungu.

Ben akaichukua simu yake iliyokuwa dani ya suruali yake. Hii ni simu alishukuru kwamba  haikuweza kudondoka  wakati alipokuwa  akiangukia kule bondeni na muda wote alikuwa ameizima  wakati walipokuwa katika harakati za uporaji wa fedha zile. Halafu akaiwasha na kuangalia saa ambapo ilimwonyesha  ni saa tatu za usiku. Muda ulikuwa umekwenda sana.

Mwisho.  

Author: admin