Mfalme wa Kinanda-1

Mwandishi Grey Solver

UTANGULIZI…

Simulizi ya “Mfalme wa kinanda” ni simulizi ya kihistoria ambayo inaelezea namna mfumo wa siasa ya vyama vingi ulivyoingia kwenye nchi za kiafrika na kuratibiwa huku ukiua uzalendo wa viongozi wa kiafrika na kuzorotesha uchumi na afya za wananchi.

Riwaya hii inaeleza kuwa kabla ya mfumo wa uchaguzi wa viongozi wanasiasa kuingizwa Afrika, nchi za kiafrika zilikuwa na mfumo wake wa kiutawala. Nchi za magharibi zikaanza kuwarubuni wanasiasa wa kiafrika ili waige mfumo wao wa siasa na kuwaahidi kuwapa fedha za msaada kwa ajili ya kufanyia uchaguzi na kutatulia shida zingine. Ndipo na wanasiasa wa nchi ya Ntale walipoanza kumshinikiza Mfalme wao ili waingie kwenye mfumo wan chi za magharibi.

Nchi ya Ntale ni nchi iliyopatikana barani Afrika na ilikuwa ikiongozwa na ukoo wa akina Hawanga.

Awali nchi hii ilikuwa na wafalme wawili, ‘mfalme wa nchi’ na ‘mfalme wa kinanda’

Mfalme wa nchi alikuwa ndiye kiongozi mkuu wa nchi na serikali ya Ntale, na alipatikana kwa kurithi ufalme kutoka kwa mfalme aliyepita ndani ya ukoo wa Hawanga. Mtoto anaweza kurithi ufalme kwa baba, au mdogo mtu anaweza kurithi ufalme kwa kaka mtu.

Mfalme wa kinanda alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa juu wa kupiga vyombo vya muziki ikiwemo kinanda, na alijaaliwa karama ya hekima na ushauri. Huyu alikuwa mshauri mkuu wa mfalme wa nchi na alikuwa mtii kwa mfalme. Na alipatikana kwa kurithi kiti vilevile kwa kupitia ukoo wa Ngongonile, lakini tofauti kidogo na mfalme wa nchi.

Kwa kila uzao wa mfalme wa kinanda aliyeko kwenye kiti cha ufalme, mtoto wake mmoja tu ndiye aliyekuwa na ujuzi wa kupiga kinanda hivyo ndiye mfalme wa kinanda mtarajiwa. Na kama mfalme wa kinanda akifariki, huku watoto wake ni wadogo, basi hakutakuwa na ndugu yake atakayerithi kiti cha ufalme wa kinanda kwa maana hawawezi kupiga kinanda. Na haikuwai kutokea mfalme wa kinanda akafariki kabla ya kuzaa watoto. Iliaminika kuwa Mungu aliwapa mfalme wa kinanda nchi ya Ntale kama zawadi, na hakukuwa na mfalme wa kinanda mwingine dunia nzima.

Tamaa ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi ilipelekea mawaziri wa nchi ya Ntale kumuua mfalme wa kinanda ili wapate kumwendesha/kumzidi sauti mfalme. Mawaziri waliamini kuwa kama watamuua mfalme wa kinanda, basi hakutakuwa na mtu mwingine mwenye maono makubwa juu ya mwelekeo wan chi ya Ntale.

Kabla ya kumuua mfalme wa kinanda, waliwapata wafadhili wa kuwapa fedha ya uchaguzi kwa masharti ya kukubaliwa wauze madawa yao ya kulevya Ntale, jambo ambalo mfalme wa kinanda na mfalme walikataa.

Baada ya kumuua mfalme wa kinanda, walifanikiwa kuubadili mfumo wa uongozi na Ntale ikawa inaongozwa na Rais, sio mfalme tena.

Lakini kila kiongozi akawa anafanya alichotaka, wauza madawa ya kulevya wakawatawala kisaikolojia na wananchi wakaanza kupata shida ya kiuchumi na magonjwa yakiwemo madhara ya madawa ya kulevya.

Watoto wa mfalme wa kinanda aliyepita walikuwa wawili, wa kike mmoja na wa kiume mmoja, na hakukuwa na hata mmoja aliyeweza kupiga kinanda kati yao. Na mfalme wa kinanda peke yake ndiye mwenye uwezo wa kuipambania nchi bila kuogopa na akashinda.

Je atapatikana mfalme mwingine wa kinanda? Usikose kuisoma riwaya hii iliyosheheni mikasa ya kisiasa, mapenzi na uchawi

.*****************************************************************

Endelea….

“Vipi mrembo, mbona unajigeuza geuza tu kitandani. Hulali leo?”
“Najitahidi kulala lakini sipati usingizi mme wangu. Naomba nipigie kinanda ili nilale”
“Umeanza na kudeka kwako, unataka nipige kinanda ili ulale au uanze mambo yako ya ajabu ajabu”
“Aah, hayo mambo ya ajabu umeyasema wewe, mimi nimesema nipigie kinanda ili nilale. Usiponipigia mimi utampigia nani, au una wake wengine jeshini huko”
“Sasa yamekuwa hayo! Ngoja nikupigie ugomvi uishe”
Kapteni Ngongonile aliamka kutoka kitandani majira ya saa tano usiku, na kukiendea kinanda chake kilichokuwa pembeni mlemle chumbani. Hakuweza kukataa kupiga kinanda kwa maana tayari alishamzoesha kumpigia kinanda mke wake Anna au mama Lupala mara kwa mara.
Alikitoa kitambaa kilichofunika kinanda na kuanza kupiga ala za wimbo wa wasanii maarufu wa nchi za magharibi “Clinton Cerejo & Dominique Cerejo” uliojulikana kwa jina “I just wanna spend my life with you”
Like a dream you can’t explain
Love can chase the bidding of your heart
Like the sunshine in the rain
Love can make your whole world fall apart
But I want it now
I just wanna spend my life with you
Time will show me how
Suddenly everything has turned me inside out
Suddenly loves the thing that i can’t live without

You’re my dream, my love, my life
I just wanna spend my life with you
You’re the one who makes me smile
I just wanna spend my life with you
Gotta love some how
I just wanna spend my life with you
You can show me how………….
Kapteni Ngongonile alipiga kinanda kwa hisia kali za kimapenzi.
“We usinitanie, unadhani mwenye hisia ni wewe peke yako” alijisemea kimoyomoyo Anna na kuinuka kitandani. Alimsogelea kapteni Ngongonile ambaye alikaa kwenye kiti akipiga kinanda na kumkumbatia kwa nyuma, huku shingo yake akiiegemeza mabegani kwa kapteni Ngongonile.
Kapteni Ngongonile hakujali mkao ule, aliendelea kupiga kinanda na kuimba kwa hisia.
What have you done to me
Is this how it’s meant to be
Can’t control this feeling in my heart
I can see paradise, glowing inside your eyes
And I know you feel it in your heart
But I want it now
I just wanna spend my life with you
Time will show me how
Suddenly everything has turned me inside out
Suddenly loves the thing that i can’t live without

You’re my dream, my love, my life
I just wanna spend my life with you
You’re the one who makes me smile
I just wanna spend my life with you
Gotta love some how
I just wanna spend my life with you
You can show me how………….

Ohhh….love is a crazy thing,
It’s like when you wanna sing
And the words are deep inside your soul
When somebody comes along together
You sing a song you just let the music take control
And I want it now, I just wanna spend my life with you
You can show me how
Suddenly everything has turned me inside out
Suddenly loves the thing that i can’t live without

You’re my dream, my love, my life
I just wanna spend my life with you
You’re the one who makes me smile
I just wanna spend my life with you
Gotta love some how
I just wanna spend my life with you
You can show me how

“Kweli wewe ni mfalme wa kinanda, kumbe mfalme (mfalme wa nchi ya Ntale) hakukosea kukupa jina hili. Nakupenda sana”
Anna alimkumbatia kapteni Ngongonile kwa mahaba, na kumsukumia kitandani.

Itaendelea….

Kwa maoni, ushauri wasiliana na mwandishi kwa namba 0756926416

Author: Gadi Solomon