Ushetani wa Alphonce

MTUNZI NA MWANDISHI

Egidius Jack Matungwa

 

Ndege ya papa, ilizunguka mara tatu, juu ya  anga la uwanja wa  ndege, wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Dar. Hiyo ilikuwa ni ishala ya salamu kwa maelfu ya watu waliojumuika uwanjani hapo, wakimgoja mgeni adhimu, kiongozi wa juu kabisa ulimwenguni, wa dini ya Romani Katoliki, baba mtakatifu papa Carol Peter wa 16.

     Ulinzi uliimalishwa. Maofisa wa vyombo vya ulinzi, na wananjeshi wa ngazi tofauti, walisambazwa kila kona ya uwanja, ili kuhakikisha hali ya usalama ni ya kulidhisha.

    Viongozi mbalimbali wa dini na serikali, walijumuika kumpokea papa. Watu ambao hawakuweza kufika hapo uwanjani, walifatilia tukio hilo kwa kutazama na kusikiliza kupitia luninga na radio. Waandishi wa habari walijipanga vema kulilipoti tukio hilo.

    Lilikuwa ni tukio lenye msisimko wa aina yake, lililozikamata vilivyo hisia za watu wengi. Kamera za vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni, zililimulika. Wapo walioshindwa kuvumilia, kiasi cha kujikuta wakibubujikwa na machozi ya furaha, wakati wakiusubiri ujio wa kiongozi huyo. Waliozoea kumuona na kumsikia kwenye vyombo vya habari, pengine hawakuwa wakiamini kwamba, siku hiyo, wangemuona live.

  Ilikuwa ni fursa ya kipekee, inayotokea mara moja-moja sana. Na hiyo siku, ilikuwa moja ya hizo siku adimu, kwa taifa kutembelewa na papa.

  Taratibu, ndege ilianza kushuka chini, ikiitafuta ardhi ya uwanja huo. Kelele za shangwe, vifijo, miruzi na nderemo zilisikika kila mahali. Ilionekana ile ndege ilikuwa ikiendeshwa na rubani mwenye ujuzi na utundu mkubwa wa fani yake. Aliitelemsha kwa mbwembwe, ikiibinuabinua utadhani samaki aogeleavyo majini.

    Manjonjo ya rubani nayo yakaongeza shamrashamra. Hatimaye ikatua. Watu;  “Weeeeeee…” Punde ikaanza kukimbia kwa kutumia tairi zake, ikiliendea eneo la maegesho, ili watu walikuwamo, akiwemo papa, wateremke.

   Kwa nini papa alikuja Tanzania?

   Fununu za hapa na pale juu ya ujio huo zilifukuta. Nyingine ziliongea mema, zipo zilizokuwa kinyume. Umbeya uliopenyeza masikioni mwa watu, na kuvuma kwa kasi ya moto wa kifuu, ni ule uliosema kwamba, papa hakuja kwa jema.

    Ilikuwa ni muendelezo wa ziara zake za kushtukiza, alizozifanya kwenye mataifa mbalimbali duniani. Kwa takribani miaka miwili mfululizo, papa Carol Peter wa 16, alikuwa akifanya ziara za kushitukiza katika mataifa mbalimbali.

    Hakukuwa na tatizo wala halikuwa jambo la ajabu kwa papa kuzuru nchi tofauti tofauti, hususani za kikristo. Ni utaratibu wa kawaida kabisa, kwa mujibu wa hitifaki za kanisa hilo lililoenea ulimwenguni kote. Lakini hizi ziara za kushitukiza, kule kuzuru mataifa flani flani kwa ghafla.Kulikuwa kuna namna!

    Kuligubikwa na siri kubwa iliyojificha chini ya kapeti, siri ambayo ni baadhi tu ya wana hitifaki wa dini hiyo walioifahamu, wakati huo huo waumini wengi walifumbwa. Wengi hawakutakiwa kuifahamu, na hakika, hawakuifahamu!

     Ujio wa papa Carol wa 16 nchini Tanzania.

     Ziara iliyogubikwa utata mtupu…

     Siku hiyo hiyo.., muda huo huo…

     Dakika kumi na tano, kabla dege la  papa halijatua, kipande cha video, kikionyesha uchafu uliyopitiliza wa padre Alphonce, kilisambaa mitandaoni. 

  Aloo!

    Hitifaki ya mapokezi ya papa ilifadhaika, kwa namna kipande hicho cha video chafu za ufuska wa padre Alphonce, kilipoendelea kujizolea watazamaji kwa kila sekunde iliyosonga mbele.

    Video hiyo ilirushwa kwenye moja ya akaunti za you-tube, na ndani ya dakika kumi na tano, kabla dege lililomleta papa halijatua uwanjani, iliweza kutazamwa na zaidi ya watu laki mbili.

    Weweseko lisiloelezeka liliwakumba wakatoliki, pamoja na waumini wa madhehebu na dini nyingine. Ilishangaza sana. Hakuna moyo wa mtu ambaye jicho lake lilipata kuiona video ile, ulitamani kuamini kile ulichokiona.

  Padre Alphonce, ali-maarufu kama father Alphonce, ambaye pia ni makamu wa askofu wa jimbo kuu la Dar es Salaam, Bishops’ vice, alionekana akifanya uovu uliyowaacha hoi bin taaban watazamaji.

  “Ey, hebu ona. Nini hiki?” Fratel Aloyisius alimuonesha Bruda Achilles ile video, kupitia simu yake akiwa amefadhaika sana.

  “Heee! Ndio nini sasa?!” Bruda Achilles alipigwa na mshangao usio kifani, wakati akiropoka, macho yake yalipotuama kwenye simu ya Frateli Achilles.

  “Hebu rudisha nyuma tuone vizuri.” Bruda Achilles alimuomba Frateli Aloyisius. Aloyisius akairudisha nyuma, wakanza kuitazama upya.

   Yaliyoonekana humo…, hakika yalihuzunisha…

   Ndani ya kanisa kubwa la Dar, mida ya usiku. Isingeweza kubainika kwa mtazamaji ilikuwa ni saa ngapi haswa. Ila ilijidhihirisha kwamba ilikuwa ni usiku, kwa giza nene lilionekana nje ya madirisha  ya vioo vya kanisa hilo, na juu kabisa angani, nyota zilionekana zikimetameta, kupitia matundu madogo madogo ya juu ya madirisha.

  Ndani ya chumba kidogo cha matayarisho ya wahudumu wa ibada, kilichopo upande wa nyuma wa ndani ya kanisa, usiku huo, alionekana Sister Benardetha, mtawa wa shirika la damu takatifu ya Yesu. Sister huyo, akiwa nadhifu kwa mavazi ya kitawa aliyojivika, juu yake alijitanda kanga safi yenye picha ya  Bikra Maria mama wa Yesu.

  Ni chumba chenye ukubwa wa wastani. Ndani yake zilionekana shelfu za kuhifadhi mavazi ya mapadre, na vifaa mbalimbali vya kanisa.

  Sister Benardetha, akiwa amejivika kitambaa cha kitawa kichwani mwake, alichukua chombo flani kama kikontena chenye mikate mingi ya sakramenti takatifu. Pembeni yake, kulikuwa na vikombe viwili vya rangi ya dhahabu. Kimoja akakitia mikate isiyotiwa chachu, maalumu kwa ajili ya ushirika wa meza takatifu ya Bwana, inayosimama kama mwili wa Yesu. Na kingine akakitia divai, inayosimama kama damu ya Yesu. Akaichanganya ile divai na maji kidogo, kisha akaitikisa kwa sekunde chache.

  Upande wa pili.., muda huo huo…

  “Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzawa wa tumbo lako amebarikiwa…” Padre Alphonce alionekana akiendelea kusali rozali, huku amepiga magoti kwenye ngazi za kuelekea madhabauni.

  Mkononi alikamata rozali yake, akiwa amevalia kanzu nzuri sana nyeusi, ambayo mara nyingi huvaliwa na mapadre wakiwa nje ya huduma za misa au ibada. Kwa upole na unyenyekevu usioweza kuelezeka, aliendelea kusali rozali, tendo kwa tendo. 

  Wakati akiendelea, Sister Benardetha alitoka kwenye kile chumba alimokuwa, akaanza kuelekea madhabauni. Mikononi alishikilia vile vikombe viwili vyenye rangi ya dhahabu. Alikuwa akivipeleka kuvihifadhi altareni, kwa ajili ya matumizi ya ibada ya kesho yake asubuhi.

  Kutoka kwenye kile chumba hadi madhabauni, ni mwendo wa hatua kadhaa. Muda huo, Padre Alphonce alikuwa amemaliza kusali rozali, na alianza kusali sala ya litania ya Bwana.

  “Bwana utuhurumie.” -Padre Alphonce.

  “Bwana utuhurumie.” -Sister Benardetha.

  Padre Alphonce aligeuza shingo nyuma kumtazama anayeitikia sala yake. Akamuona Sister Benardetha aliyekuwa akijongea kule alikokuwa amepiga magoti.

  “Kristo utuhurumie.” Padre Alphonce aliendelea baada ya kugeuza shingo mbele akiutazama msalaba mkubwa wenye sanamu ya Yesu, unaoning’inia juu ya ukuta wa mbele ya madhabau.

  “Kristo utuhurumie.”

  “Bwana utusikie.”

  “Bwana utusikie.”

  “Kristo utusikie.”

  “Kristo utusikilize.”

  “Bikra Maria mama wa mtoto Yesu.”

  “Utuhurumie.”

  “Utatu mtakatifu Mungu mmoja…”

  Sala iliendelea kwa kupokezana namna ile. Sister Benardetha hatimaye alifika madhabauni akamkaribia Padre Alphonce. Akapanda ngazi za madhabau, akaenda moja kwa moja altareni, huku Padre Alphonce akimkata jicho kali sana.

  Sister Benardetha hakuliona.

  Pale altareni, aliviegesha vile vikombe kwenye kijimeza kidogo kilichojengewa kwa zege, kinachoning’nia nje ya kijimlango mithili ya kijidirisha cha altare. Akapembua kipazia kilichokifunika kile kijimlango, akakifungua.

  Wakati huo, alimsikia Padre Alphonce akinyanyuka kule alipopiga magoti. Akamtazama kwa jicho la pembeni, akamuona akipiga hatua kuelekea pale altareni alipokuwa amesimama yeye. ‘Huyu anafata nini huku?!’

   Wakati akijiuliza lile swali na kuamua kuviingiza vile vikombe kwenye kile kijichumba kidogo cha altare, ili aondoke, alimuona Padre Alphonce akiongeza kasi ya kumfata. Akahisi pengine kuna jambo alilotaka kumuelekeza.

  “Mama Maria wa mtoto Yesu.”

  “Utuhurumie.”  Benardetha aliitikia kama kawaida, huku akistushwa na mkwaruzo wa sauti ya Padre Alphonce ambao hapo awali hakuusikia. ‘Kawaje tena huyu naye!?’

  Hakuendelea kujiuliza. Alistushwa na kikumbo cha mwili wa yule Padre, aliyemvagaa kwa nguvu na kumpakata kwa nyuma yake. “Yesu wangu wa mbinguni!” Sister Benardetha alijikuta akipiga kelele kwa mstuko, huku akishindwa kuvizuia vile vikombe vyenye sakramenti takatifu visianguke na kubwaga vile vilichokuwa vimebebwa ndani yake.

   “Shiiiiiiii…” Alphonce, huku ameiziba midomo yake kwa kidole cha ‘mwalimu’, alimkemea. Mkono wake wa kushoto ukikiachia kitabu cha chuo kidogo cha sala na rozali vikidondoka chini, huku wa kuume ukilifumbata tumbo la yule mtawa kwa nguvu, na kumbania tumboni kwake.

  “Shindwa pepo.” Alipayuka Sister Benardetha.

  Padre Alphonce akatumia kiganja chake cha mkono wa kuume kumziba mdomo kwa nguvu, huku cha mkono wa kushoto kikifanya kazi ya kuyatomasa kwa uchu maungo ya yule mtawa.

  Aisee..!

  Ilikuwa balaa wakati Sister Benardetha akihaha kwa nguvu zake zote kujinasua kwenye ile kadhia. Tayari alishaijua nia ya padre yule aliyeonekana kupandwa na pepo la ngono.

  “Ni…ni…ni…phuuuu, nia, chiiiee…phuuuu…” Sister Benardetha wa shirika la damu takatifu ya Yesu aliendelea kupambana kwa kila namna. Kila alipotaka kujikurupusha kwenye ile mikono ya padre, alijikuta akiishia kutoa pumzi mdomoni. Jitihada zake hazikuwa zikimzalia matunda.

   Padre Alphonce alikuwa na nguvu mfano hakuna. Hakuwa na chembe ya haya wala huruma. Na hata pale Sister Benardetha alipokuwa akizisikia pumzi za yule mtumishi wa Mungu, zilizokuwa zikimtoka puani kwa kuelemewa na mihemko ya ngono, alijua kabisa ule ulikuwa usiku wa balaa lake. Alizidi kuogopa.

  ‘Ee Mungu nisaidie.., nini hiki jamaniii…Eee!?’Sister Benardetha aliomboleza kimoyomoyo huku akibubujikwa na machozi, wakati akiitumia mikono yake kuzikamata barabara kingo za kile kijimeza cha zege cha pale altareni.  Ama kwa hakika alibananika. Na alikuwa kwenye wakati mgumu kwelikweli.

   Padre alizidi kumvuta kwa nyuma, akilazimisha kuiondosha mikono ya yule mtawa kwenye kingo za kile kijimeza cha zege. Benardetha akajitutumua kukaza mikono. Ni nafasi hiyo aliyoitumia fadher Alphonce kukivuta kitenge cha yule mtawa,  akakitupilia mbali. Zoezi la kuyatomasa maungo ya yule dada, likapamba moto. Awamu hii, akikazia eneo la sehemu za siri. Uroho wa ngono ukazidi kumjaa. Akadhamiria kutekeleza alichokikusudia. Kumbaka yule mtawa.

   Kwenye ile purukushani,  Padre Alphonce alimvuta nyuma yule mtawa. Miguu ya  Benardetha iliteleza kwenye mvinyo uliotapakaa sakafuni. Akashindwa kukakamaa, akapiga mweleka uliowapeleka yeye na padre chini. Wakaangukia migongo. Sakafuni alitangulia Padre Alphonce, tumboni akifatiwa na Sister Benardetha aliyelalia mgongo.

   Kila alipofanya namna ya kupaza sauti, sauti haikumtoka yule mtawa. Pepo mchafu lililomvaa padre alikuwa na nguvu kwelikweli.

   Padre alijikakamua  kwa nguvu huku akikenua meno kwa kuuchanua mdomo wake kwa ghadhabu, akamgeua na kumuweka chini yake yule mtawa. Sister Benardetha alilala chali pale sakafuni akiwa amebanwa mwili wake. “Una haja gani nami we shetani. Nani kakutuma uje uninajisi namna hii mwanaharamu wewe? Hii kesi unayojitafutia ni kubwa Father! Na ninaapa…hakya Mungu,  sintasita kukushitaki kwenye uongozi wa juu.”

     Padre Alphonce hakujali!

     Ama hakika siku hiyo, sister Benardetha alipatikana.

     Mala, yowe kubwa la uchungu lilimtoka kinywani yule padre, baada ya Sister Benardetha kumshushia pigo moja kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia goti. Padre aligumia kwa maumivu makali, yaliyomtambaa kwenye mirija ya damu, kutokea kwenye uume, yakiuvaa mwili wote.

     Aliweweseka, na ni wazi pigo lile hakulitalajia. Akalegea baada kuishiwa nguvu kwenye mikono yake iliyokuwa imembana yule mtawa. Maumivu yakiupoka uroho wake wa ngono. Akajiondoa kwenye mwili wa yule binti, akajilaza sakafuni, kando yake bibie Benaderdha. Maumivu yakaendelea kumchonyota, huku akihisi ganzi ikimjaa miguuni.

   ‘Ahsante Yesu.’ Alijisemea kimoyomoyo Sister Benardetha, wakati akiutumia huo mwanya kunyanyuka, akamtoka yule shababi na kutimka mbio. Akafanikiwa kushuka ngazi za madhabau, akiukimbilia mlango  uliokuwa kwenye ukuta wa pembeni, ili atoke nje, moyoni mwake asiamini namna alivyo kiepuka kikombe cha kubakwa na mtumishi mwenzake, tena mbele ya altare takatifu.

    Akaongeza mbio huku jasho jingi likimvuja mwilini, mapigo ya moyo yakipiga kwa nguvu, akipumlia puani na mdomoni kwa taabu.

    Hakufika mbali.

    Ghafla.

    Alisikia kitu kizito kikimpiga kisogoni. Maumivu makali yalikita pale kilipotuama hicho kitu kizito, kisha yakatambaa kichwani pote. Akahisi uzito ukimuelemea kichwani, usoni akiona nyota nyingi zikielea hewani.

    Miguu iliishiwa nguvu, ganzi ikamtambaa mwilini kote. Alipiga magoti yote mawili chini bila kupenda, huku akisikia sauti ya kile kitu kilichompiga kisogoni kikianguka sakafuni.

    Kwa taabu alifanikiwa kugeuza shingo kukitazama, alipokiona, hakuamini kama yule yule Padre Alphonce aliyemfahamu, ndiye aliye mfanyia ushetani wa namna ile, tena kwa kudhamilia.

    Ulikuwa ni msalaba mkubwa wa chuma, wenye uzito wa kilogram ishirini na tano, ukaao juu ya meza ya madhabau.

    Papo hapo, mbele yake, alimuona Padre Alphonce amesimama huku akiwa amemtumbulia macho kwa ghadhab. Usoni akiwa amemfura hasira ya kuua mtu.

   Aloo!

   Macho ya sister Benadertha yalifumbwa kwa kiza kizito, akabwagika sakafuni kama furushi.

   Dhamila ya Padre Alphonce haikukoma, akamuendea palepale kwa uroho uliozidi sana. Akatandaza miguu yake na kumuweka uvunguni mwa mapaja yake. Akapiga magoti akimuinamia. Akalivuta gauni lake la kitawa kwa pupa kuelekea kiunoni. Akamchojoa nguo zake za ndani na kuzitupilia mbali. Akaivuta kanzu yake kwa juu, na kufungua mkanda wa suruali yake haraka haraka.   

   Akambaka yule mtawa!

   Kisha akamlawiti!

   Doh!

   Aisee!

   Alipomaliza ufilauni wake alihamaki vibaya sana. Pepo la ngono lilimtoka. akaanza kujutia ufuska alioutenda mbele ya madhabau takatifu ya Mwenyezi Mungu. Jasho lilimtoka kama mvua, alipokuwa akimtazama kwa woga mkubwa yule mtawa aliyezirai mbele yake.

  Akaona balaa lilishamfika na hakuwa na pakuponea, pindi yule mtawa atakapo zinduka. Alifikiri kwa haraka, akakumbuka vitisho alivyopewa na yule binti dakika chache zilizopita….‘Hii kesi unayojitafutia ni kubwa Father! Na ninaapa…hakya Mungu,  sintasita kukushitaki kwenye uongozi wa juu.’

   Ikambidi afanye maamuzi ya dharula. Maamuzi ambayo yangeweza kumuhakikishia usalama wake.

   Aliinuka na kuelekea upande wa kichwani. Akasimama kidogo, kisha akainama na kumkamata mikono kwa nguvu. Akamburuta, mpaka karibu na madhabau.

    Hapo, palikuwa na kabuli lililohifadhiwa kwa kufunikwa kwa kifuniko cha zege vizuri, kiasi cha kutoonekana kama palikuwa na kabuli. Ni kabuli aliloandaliwa kuzikwa askofu mkuu wa jimbo, ambaye ndiye Kadrinali, pindi atakapofariki.

    Padre Alphonce alikuwa na nguvu zisizo za kawaida, ungedhani ni mtunisha misuli, au mnyanyua vyuma vizito.

    Aliliinamia lile kabuli, akajikakamua misuli kwa nguvu huku akitoa sauti za miguno ya kuvuta mori, akafanikiwa kuufunua mfuniko wake. Kisha akamrudia Sister Benardetha aliyekuwa bado amepoteza fahamu. Akamburuta kwa nguvu zake zote, akamtupia kabulini kisha akalifunika kwa mfuniko wake.

   Haraka sana akaanza safari ya kutoka nje.

    Wakati akiuendea mlango…

  Loo!

  Hakufika mbali.

  Kule mlangoni.

  Aliona…

  Aliona…

 ‘Oh my Godness shiiit…’

  Fadher Alphonce alitoa miguno ya hamaniko, kwa fadhaa isiyoelezeka, huku  akisitisha ile safari wakati macho yake yakikodoka pima kule mlangoni.

  ‘Oh goshhh…holy Mary mother of Christ…shiiiti takatifu…holy shiiiti…’

MIAKA MINGI SANA ILIYOPITA

 

Wakati wa harakati za uchaguzi mkuu nchini Tanzania…

    Taifa liliingia kwenye awamu nyingine ya vuguvugu la uchaguzi mkuu, wa kuwachagua rais, wabunge na madiwani. Ni agenda ya kila baada ya miaka mitano, ambayo kila inapowadia, huja kwa sura na muonekano wake, na msisimko wa aina yake.

 

    Mwaka mwingine wa uchaguzi ulifika, joto la uchaguzi likapanda kila siku. Wachunguzi, wachambuzi na wafatiliaji wa maswala ya uchaguzi duniani, wakaelekeza macho, masikio na akili zao nchini Tanzania.

    Rais na amiri mkuu wa majeshi ya Tanzania, mheshimiwa Makaranga Bruno, alitangaza nia ya kugombea awamu ya pili ya uongozi wake, kwa mujibu wa katiba ya nchi ilivyokuwa ikimruhusu.

    Lakini, ni kipindi ambacho; alikuwa akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kambi ya vyama vya upinzani, na hata ndani ya chama chake mwenyewe, chama tawala. Imani yakekushinda kiti hicho kwa awamu nyingine, ilikuwa ni kiduchu.

    Alionekana mwenye mfadhaiko, aliyepoteza furaha kabisa, mambo yalimgeuka vibaya, kila mlango aliodhani ungempenyezea ushindi, ulifungika.

    Siku moja, ilikuwa mishale ya saa sita mchana, jua kali likiwaka, joto likifukuta kiasi cha kukaraisha. Mheshimiwa Makaranga Bruno alikuwa ikulu ya rais ya Dar es Salaam, akitweta jasho kwa mambo mawili ndani ya wakati mmoja. Kwanza kabisa; jua kali lililokuwa likiwaka siku hiyo.

    Muda mwingi alionekana akizunguka huku na kule, kama aliye wehuka na kupoteza muelekeo. Alihama chumba hiki na kuingia kile. Mkewe Bi. Consolatha Bruno alibaki akimtazama kwa huruma. Alidhani alikuwa akijua kilichomsumbua mumewe, la Hasha, haikuwa hivyo, ama alijua sehemu tu ya maswahibu yaliyomnyima raha mheshimiwa yule.

    Aliamini kwamba, mume wake alikaribia kupatwa na wazimu, kutokana na harakati za uchaguzi zilivyokuwa zikimuendea kombo. Ni kweli, lakini hakufahamu nini cha zaidi kilichomtesa mchana wa siku hiyo.

    Kumbe, alipokuwa usingizini, aliota njozi ya kutisha, iliyo mkatisha tamaa kabisa.

   Alikuwa amelala  kitandani, chumbani mwake. Ghafla, aliona watu wa ajabu wamekizingira kitanda chake.

    Misukule.

    Anawafahamu.

    Watu aliowatoa kafara, akawafanya ndondocha, ili afanikiwe maishani, hususani kifedha na kisiasa.

  Sasa…

  Walimjia mchana ule, kwa njia ya nusu ndoto, nusu halisia.

    Alishtuka kutoka usingizini, akajikulupua kwenye shuka alilokuwa amejifunika gubigubi, bila kujua nini kilimstua. Ndipo alipowaona vizuri.

    Walikuwa wengi, waliojaa na kubanana mule chumbani. Wa rika na haiba tofauti. Walikuwepo ndugu zake, jamaa zake, wengine hakuwa na mahusiano nao ya moja kwa moja. Ila aliwatenda alichowatenda kulingana na alivyokuwa akiagizwa na viongozi wake wakichawi.

   Walikuwepo wazee kwa vijana, wakiume kwa wakike. Wote walikuwa wakimlilia mbele yake, wakimtaka msaada. Walimuomba kwa kumnyooshea mikono mbele, huku machozi ya huzuni na kuomboleza kwingi, yakiwabubujika.

   Miili yao haikuwa na nguvu kama miili ya wanadamu wa kawaida wenye nguvu. Walikuwa wakitetemeka kama walioishiwa nguvu kabisa, huku wakionekana kama wanaotaka kudondokea sakafuni, lakini hawakudondoka.

  “Unatuua Makaranga, una tuua. Tafadhari usitufanyie hivyo… fanya hima kutekeleza unachopaswa kutekeleza ili utuokoe…”Walizidi kumlilia, huku wakizidi kumnyooshea mikono, wakati huo yeye alikuwa ameegama kiubavu pale kitandani, huku mapigo ya moyo yakimpiga mputa kwa hofu.

  “Njaa…njaa…tafadhari Makaranga njaa itaondosha uhai wetu. Tuhurumie tafadhari tunakuomba…usalama wa maisha yetu upo mikononi mwako, nawe unalielewa hilo. Sasa basi; fanya hima utuokoe kabla hatujaangamia . Tafadhari sana, tunakuomba…”

  Wale watu, ambao muda huo hawakuwa wanadamu wakawaida tena, bali misukule, walizidi kumlilia mheshimiwa rais. Wakati wakiendelea kuwasilisha kilio chao, ngozi zao zilizidi kunyongoroka, na kunyofoka nyofoka. Wengine wakaanza kuishiwa nyama kabisa na kubakia mifupa tu, lakini bado waliendelea kuwa na uwezo wa kuongea.

  Mala wakapotea!

  Ndipo rais Makaranga alipostuka kutoka kwenye usingizi asilia, achana na ule alioota.

  Alipatwa na hofu kubwa. Akapoteza furaha kabisa. Akaamka na kuanza kuzunguka zunguka huku na kule. Mke wake akimshuhudia huku akimuhurumia, akiamini kwamba; ni joto la uchaguzi lilikuwa likimtesa mume wake.   

   Hakujua!

*****

  “Kuna ujumbe wa dharula tumeupokea lango kuu mheshimiwa rais, ADC ameniagiza nikufikishie.” Mmoja wa maafisa usalama alimueleza bwana Makaranga na kumkabidhi bahasha. Ililetwa na mtu muhimu sana ambae, rais alishatoa maelekezo kwamba; muda wowote afikapo, asikilizwe na ahudumiwe haraka.

    Rais alipoiona, kabla hajaipokea alistuka sana, jambo lililomshangaza yule afisa usalama aliyeileta. ‘Mbona kastuka?’ Afisa usalama alijiuliza kwa wasiwasi, akidhani pengine rais aliona kitu hatarishi kwenye ile bahasha, na wao kama wana usalama hakuwa wamekiona kabla hawajamuwasilishia, naye akaanza kuogopa.

   Akaigeuza mara mbilimbili akiitazama kwa makini, hakuona chochote kibaya. Na alishangaa pamoja na kushituka kwake rais, bado aliipokea japo kwa wasiwasi uliodhahiri, ulioambatana na kitetemeshi mwili mzima. ‘Mbona kaipokea sasa kama inaviashiria vya hatari?!’

   Wakati afisa usalama aliona akimkabidhi rais bahasha nzuri iliyofungwa vizuri, rais aliona akikabidhiwa pande la ngozi ya mbwa, lililofungashwa hovyo-hovyo. Akalipokea.

    Papo kwa hapo akalifungua, akachomoa kilicho kuwemo. Afisa usalama akaushuhudia mkono wa rais ukichomoa barua iliyoandikwa kwenye karatasi nzuri, wakati rais alichomoa pete kubwa tena nzuri sana.

    Ndipo afisa usalama yule alipoona mambo matatu au manne yakitokea kwa wakati mmoja, tena kwa haraka.

    Mosi, rais Makaranga alikimbiza macho yake kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto, akavitazama vidole, akaishia kufadhaika kwa kitetemeshi.

    Pili, ile barua aliyokuwa ameishikilia rais, ilichakaa na kuwa mbaya mno papo kwa hapo, wakati awali ilikuwa nzuri na mpya. Jambo la tatu ile barua ilichanika yenyewe kimiujiza, huku akimshuhudia Makaranga akiyatumbua macho yake kwa kihoro. Muda huohuo, alimuona mheshimiwa rais akichuruzikwa jasho kama matone ya mvua kwenye kiganja kilichoikamata ile barua.

    Haikuwa hivyo!

    Macho ya rais yalimtoka pima, pale alipoishuhudia ile pete ikipoteza mng’ao wake na kuota kutu. Haikuchukua muda ikameguka na kukatika vipande viwili, lakini sio kwa kiasi cha kuvitenganisha vipande vile, la hasha. Na kile kitendo kiliambatana na kuvuja kwa damu kwenye kiganja cha mkono ulioikamata ile pete, kana kwamba kile kitendo cha kukatika kwa pete kiliambatana na kukatika kwa kiganja chake. Damu ikachuruzika.

     Machozi ya huzuni na kutahayari yalimbubujika palepale bwana Makaranga, wakati afisa usalama aliona jasho likimvuja machoni.

    “Aisee, niitie Adolph mara moja.” Rais alimgeukia na kumuagiza yule afisa usalama aliyekuwa akimtazama kwa fadhaha na hamaniko.

    “Sawa mheshimiwa.” Yule afisa wa jeshi aliitika. Akasimama kikakamavu na kupiga saluti, kisha akatoweka mbele ya uso wa rais. Dakika tano baadae, mtu mmoja aitwae Adolph akiwa amevalia suti ya kijeshi, au kwa jina jingine kombati ya jeshi, alifika mbele ya uwepo wa rais.

    Hali aliyomkuta nayo tu, alielewa jambo baya lilimfika rais. 

    “Tuna safari ya dharula na ya haraka sana. Nahitaji kufika Kilimanjaro hotel. Tumia dakika zisizozidi kumi au kumi na tano, uwe umesha niandalia hiyo safari.” Rais alimpa maagizo mgeni wake aliyeagiza aitiwe.

    “Sawa mkuu. Tunahitaji kuwa na msafara wenye ukubwa gani pengine.” Adolph, aliyekuwa afisa mkuu wa jeshi ngazi ya Kanali, akiwa msaidizi wa rais nafasi ya mkuu wa kambi, au Aide de Camp (ADC) alimuitikia sambamba na kumsaili.

    “Ni mkutano wa faragha na baadhi ya mameneja wangu wa kampeni…campaign managers. Hivyo nahitaji ulinzi tu.” Muheshimiwa rais alimjibu.

    “Sawa mkuu.” ADC Adolph akaitikia, kisha akapigia saluti akiwa amesimama kikakamavu, akatoweka.

*****

    Aide de Camp wa rais, ndiye msimamizi wa ratiba na shughuri za rais ikulu. Ndiye mwenye majukumu ya kuratibu safari zote za rais. Mpokeaji na mkaguzi wa barua za kawaida na barua pepe za rais. Mbebaji wa mikoba, diary na kalamu za rais. Pia husimamia salamu za rais, ikulu na ziarani, pamoja na wageni wake.

    ADC Adolph aliipasha habari hitifaki iliyopaswa kumsindikiza mheshimiwa rais kwenye ile safari yake ya dharula. Kwa jinsi alivyomkuta rais, na mahali alipomtaka amuandalie safari ya kwenda, yaani hoteli ya Kilimanjaro, alielewa alichopaswa kukifanya.

    Kwamba ile haikuwa safari ya kawaida kama zilivyo safari nyingine za rais. La Hasha wa Kalla! Ile ilikuwa ni safari maalumu, kwa ajiri ya jambo maalumu, na rais alitakiwa kusindikizwa na watu maalumu. Hivyo maandalizi ya hapa na pale yakafanyika.

    Kanali komba, mmoja ya wanajeshi wa jeshi la kujenga taifa yaani JKT, akiwa amevalia sare za kijeshi, aliyekuwa na jukumu la kuhakikisha usafi wa gari za pale ikulu, alionekana akifuta vumbi la magari yaliyotegemewa kutumika kwenye ile safari.

    Alitumia tambala, lakini kiuhalisia, alikuwa amevaa kaniki nyeusi, aliyoitanda mabegani kama lubega za kimasai. Mkononi alikuwa na mkia wa fisi, alioutumia kuzichapa zile gari ambazo wengine waliona kama akizifuta au akizikung’uta vumbi. Kila gari aliyoipiga kwa ule mkia, ilibadilika palepale katika ulimwengu wa roho, na kuwa fisi.

    Baadae taarifa ilimfikia rais kwamba, maandalizi ya safari yake yalikuwa tayari.

    Akiwa amevaa mavazi ya ngozi ya mbwa mwitu, tofauti na wengi walivyomuona akiwa amependeza kwa suti nadhifu, mheshimiwa rais alielekea kwenye gari yake…yaani fisi wake. Akampanda na kuketi juu yake, nyuma ya dereva  aliyekuwa tayari ndani ya gari ya rais…juu ya fisi wa rais, akiwa ameyakamata vema maskio ya yule mnyama pori, ambapo katika ulimwengu wa damu na nyama, alionekana amekamata usukani wa ile gari ya kifahari maalumu kwa ajili ya viongozi wakubwa, iliyong’ara kwa rangi nyeusi.

    Dereva naye alikuwa amevaa kaniki nyeusi, na miguuni alivaa viatu vya ngozi vilivyoonekana kama buti za kijeshi. ADC Adolph aliyekuwa amevaa kaniki pia, aliketi nyuma ya rais, japo kwa macho ya kawaida, ailionekana ameketi kiti cha pembeni ya rais.

    Msafara uliondoka ikulu kwa kupitia lango kuu, mbele kabisa ilitangulia pikipiki ya polisi iliyokuwa ikisafisha njia kwa kupiga ving’ora. Havikuwa ving’ora kama tuvijuavyo mimi na wewe. La Hasha wa Kalla. Yalikuwa ni mapembe ya mnyama hatari porini aitwae Nyati, yaliyokuwa yakipulizwa na wale askari waliokuwa kwenye zile pikipiki za kichawi, yaani fisi. 

    Na hata ile gari ya polisi iliyokuwa ikiongoza msafara ikizifatia zile pikipiki, nayo iliendelea kupiga king’ora ambacho katika ulimwengu wa roho, yalikuwa ni mapembe ya Nyati.

    Mwendo kasi wa zile fisi ulikuwa mkali sana, wakati huo wananchi waliopata bahati ya kuushuhudia kwa macho msafara huo ukipita barabarani, waliziona  Land Lover 110 na Land Cruser  za viongozi wenye hadhi ya VIP.

    Waliicha ikulu, wakaelekea Kilimanjaro hotel, ambako ulinzi ulikuwa umeshaimalishwa na wana usalama waliotangulia. Walinzi waliokuwa zamu getini walifungua mageti na kuuruhusu msafara kuingia kwenye viunga vya hoteli ile. Hakuna hata mmoja wao aliyeona kwamba waliziruhusu fisi kupita, badala yake wao pia waliziona landlover 110 ambazo kipindi hicho zilikuwa na hadhi  ya kubeba viongozi wa hadhi ya juu nchini.

Rais Makaranga alitelemka kwenye gari, akaanza kutembea akisindikizwa kwa ukaribu na ADC Adolph, pamoja na baadhi ya wana usalama.

Pale uwanjani, walipokelewa na watu kadhaa waliopendeza kwa mavazi yao mazuri, kumbe yalikuwa ni kaniki na wengine walivaa ngozi za mbwa mwitu. Hakika, wageni na wenyeji wa mkutano huu, katika ulimwengu wa roho hawakuwa kwenye muonekano wa kawaida kabisa.

Walitisha sana.

Muda wote walitumbua macho na mboni zilikuwa za kijani zilizong’aa na kuwaka kama miale ya moto.

Kwa pamoja wakazama ndani ya jengo la ile hoteli, wakaelekea kwenye ukumbi mmoja wa mikutano, wakipitia mapokezi.

*****

Kwa muonekano wa nje, Rais Makaranga alifahamika na wengi kama mtu mwema, mstaarabu na mtakatifu. Lakini ukweli ni kwamba; alikuwa ni mchafu wa tabia shetani alisingiziwa. Japo alikuwa mtu wa dini, alikuwa mshilikina aliye kubuhu, mfano hakuna.

Mkewe bibie Consolatha hakuwa akiujua huu mwenendo wa mume wake, japo kuwa, kuna baadhi ya mambo katika maisha yao, yalikuwa yakimtatanisha. Hakuwahi kumtilia mashaka kwa sababu Makaranga alikuwa mcha Mungu, mcha Mungu kwelikweli!

Makaranga alikuwa mchawi wa kutisha, mshilika wa genge kubwa la wachawi, waliokuwa wakifanya vimbwanga vyao kuzimu ya bahari. Hoteli ya Kilimanjaro, ilikuwa ni moja kati ya vilinge vyao kadhaa, walivyokuwa wakikutania mara kwa mara, hususani kwa ajili ya mikutano ya mazugumzo.

Hitifaki ya wana usalama aliokuwa nao kwenye shughuri zake za kisiasa, wapo waliokuwa wakishilikiana naye kwenye uchawi wake.  Wengine, hakuna walilokuwa wakilifahamu.

Japo alikuwa mtu wa ibada, sadaka na utu wema, Makaranga alipata vyeo vyake vya serikalini kwa kutumia nguvu za giza. Njia moja mbaya kabisa, ni ya kutoa sadaka ya uhai wa wanadamu kuzimu.

Wapo aliowauwa na kumwaga damu zao, ili kukamilisha baadhi ya sheria na taratibu za umoja wao wa wachawi. Lakini pia, wapo aliowaondosha katika ulimwengu wa mwili, kwa kuwageuza misukule, au kwa maneno mengine aliwafanya ndondocha.

Na hiyo siku aliyoelekea na msafara wake pale hotelini Kilimanjaro, alikwenda kwa sababu maalumu. Ujumbe alioletewa ikulu na mjumbe maalumu, ulikuwa hatari sana, ulioambatana na tishio kubwa.

Ile bahasha aliyokabidhiwa, ilikuwa ngozi ya mbwa koko, na barua ambayo yule mwana usalama alimuona akiisoma, ilikuwa ni pete aliyokabidhiwa na wakuu wake wa anga la kichawi, kwa ajiri ya kumfanikisha kwenye mambo yake ya ki uongozi. Hivyo, maana ya ile pete ni uongozi.

Na ndio maana alipoiona, moja kwa moja alipeleka macho yake mkononi, akajitazama kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto. Alipoangalia kidoleni alishtuka sana. Hakuiona pete! Pete yake ya uongozi.

Kuikosa ile pete kidoleni kulimmaanishia kupoteza uongozi aliokuwa nao. Kama rais aliyekuwa kwenye mchakato wa kuwania nafasi yake kupitia uchaguzi uliokuwa njiani, ile ilikuwa ni ishara mbaya sana kwake.

Ile pete kuchakaa na kuwa mbaya, maana yake uongozi wa Makaranga ulikuwa unaenda kupoteza hadhi, thamani na mvuto kwenye jamii. Kama kitu kipatacho kutu kipotezavyo thamani yake ya awali.

Na ile pete kukatika mikononi mwake, kulimaanisha ile nafasi ya uongozi aliyokuwa nao, alikuwa anaenda kuipoteza yeye mwenyewe, na baadae hakutakiwa kumlaumu yeyote. Wanasema mtu mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, na mtoto akililia wembe mpe umkate, ndivyo ilivyomaanisha

Damu iliyochuruzika kiganjani baada ya kukatika kwa ile pete, ili maanisha kwamba; pete kumkatikia kiganjani kuliambatana na kumkata kiganja. Dalili mbaya sana ile. Kwamba; hataishia tu kuupoteza uongozi wake, la Hasha wa Kalla. Itaambatana na umwagaji damu, kisasi, maumivu na majuto.

Huo ulikuwa ni ujumbe mzito wa pili kutoka kilingeni, baada ya ule wa kwanza, waliomtumia kupitia ndoto ya ile misukule iliyokuwa ikimlilia aiokoe kwa kufanya alicho paswa kufanya.

Kuna mahali mambo hayakuwa sawa kwa Bruno, na kama yangeendelea hivyo, matokeo yake yangeleta maumivu na majuto makubwa, si tu kwake, bali hata kwa washilika wa uchawi wake.

Ilikuwa ni siku chungu na ya hatari sana kwake, hususani kwenye mambo yake ya kisiasa. Na ndio maana alimuagiza ADC Adolph, ambaye pia alikuwa mchawi mwenzake, amuandalie ile safari. Safari ya kuelekea hoteli ya Kilimanjaro, kilingeni, ili kujua mustakabari wa urais wake.

Walifika mapokezi ya hoteli ile, wakasaini kitabu cha wageni, kisha wakaelekea kwenye ukumbi wa mkutano wao. Huko, walipokelewa na washilika wao.

Mkutano ulikuwa moto, moto kwelikweli!

*****

Usiku mkubwa…bibie Consolatha alikuwa akikimbizwa na mume wake kipenzi. Kwenye barabara pweke, iliyopo katikati kabisa ya msitu na pori nene. Ulikuwa ni usiku mkubwa, giza zito. Hii ilimpa taabu yule mama kuona alipokuwa akikimbilia.

Bruno yule yule amjuaye, hakuwa katika hali na muonekano aliouzoea kumuona nao. Huyu alikuwa Makaranga wa aina ya tofauti. Lakini ni yule yule mheshimiwa rais, aliyemsababishia yeye kuitwa first lady wa taifa la Tanzania.

Na sasa alitaka kumuua.

“Simama nimesema… si nina kwambia wewe usimame, sasa mbona unanikimbia.” Makaranga alimkoromea huku akizidi kumkimbiza kwa kasi ya ajabu, akiwa na panga lenye makali kuwili.

“Simama wewe mwanamke, mwanaharamu pumbavu kabisa. Utakimbia mpaka wapi… ntakukamata tu. Kila siku umekuwa kikwazo kwangu, nikikuambia unachopaswa kufanya hautaki. Unajitia jeuri. Basi leo utakula jeuri yako.”

“Sisimami…” Bibie Consolatha alijibu huku akiendelea kutimua mbio. “Kosa langu ni nini kwani, kukukatalia kukiua hiki kiumbe kilichoko tumboni mwangu…” Consolatha alijitetea.

Akaendelea, “…nilichokibeba humu tumboni ni ujauzito wa mwanangu, naapa abadani asilani, siwezi kukukubalia umdhuru au umuue mwanangu asiye kuwa na hatia. Siwezi nasema siwezi. Kama umeamua kumuua bora utuue wote. Na kwa uhaini huo, adhabu yake Mungu baba itakuwa juu yako.” Aliendelea kulalama Consolatha.

Wakati huo, Makaranga alikwisha mkaribia kabisa. Kwa bahati mbaya, bibie Consolatha alijikwaa pahala. Kitendo kile hatarishi, kilimsababishia matokeo hasi kwenye zile mbio. Aliweweseka, akapoteza uwezo wa kujidhibiti ili asianguke. Akaanguka kifudifudi, huku akijitahidi kulizuia tumbo lisiguse pale ardhini, akamdhuru mtoto aliyekuwa tumboni. Akafaikiwa.

Akafanikiwa kujikakamua, akajigeuza. Akawa amelalia makalio na kuegemesha mwili kwa kutumia viwiko vilivojiegemeza pale ardhini.

Muda huo huo, Makaranga naye akafika pale.

Consolatha alimshuhudia mumewe amefura uso mzima kwa hasira. Akitweta jasho mwili mzima, ndita zikiwa zumemtapakaa usoni. Akakusanya nguvu huku akitoa miguno ya hasira na kukusanya nguvu. Akanyoosha juu upanga wake, kabla hajaanza kuuteremsha kwa nia ya kulichabanga lile tumbo la yule mwana mama.

“Nawauwa wote barbarian… nguruwe nyinyi.”

Consolatha alipiga yowe la kutaka msaada, bila hata ya kuupata huo msaada wenyewe. Barabara ilikuwa pweke, na hatimaye alianza kulia kilio cha maombolezo ya kukata tamaa. Upanga wa Makaranga ulinyooka vizuri hewani. Na sasa ukaanza kurejea chini, ukielekea tumboni kabisa kumtumbua utumbo.

Ghafla!

Upanga mwingine usiojulikana, ukiwa umekamatwa na mkono usiojulikana, ulishuka kwa spidi kali na kuubatua ule upanga wa rais Makaranga. Upanga wa makaranga ukakatiliwa na kuangukia mbali.

Kutahamaki ile Hammad! Kiumbe wa ajabu akajitokeza.

E bwana ee!

Alikuwa na muonekano wa ajabu, usiofananishwa na kiumbe chochote dunia hii. Makaranga na Consolatha walistaajabu kwa pamoja, walipokuwa wakimtazama kwa hofu yule kiumbe.

Alikuwa nusu mwanadamu, nusu kiumbe asiyejulikana. Aling’ara kama miale ya jua iliyo akisi mwanga kutoka baharini ing’aravyo. Akiwa amejivika mavazi meupe tupu, yenye kumeremeta kama shela ya bibi harusi.

Macho yake makubwa, yaliwaka kama taa kali ya gari iliyowashwa full light. Alikuwa na mwili mkubwa, mwenye urefu usio kuwa wa binadamu wa kawaida.

Upanga wake wenye makali kotekote ukiwa barabara kiganjani mwake, macho yakiwa yamemtoka pima. Aliogopesha kumtazama. Na hata kwa mtu mwenye ujasiri wa kumtazama asingeweza kumtazama, kwa sababu kiuhalisia, ule mng’ao wake binafsi, mavazi ya kumetameta, na macho yake makubwa yaliyowaka zaidi ya taa za full right vilikuwa na uwezo wa kuyaumiza macho kama sio kuyapofusha kabisa.

Makaranga alizungusha macho yake haraka haraka,akiagaza huku na huko, akiutafuta upanga wake uliomponyoka. Akauona. ulijikita hatua kadhaa hivi kutoka pale alipokuwa amesimama.

Akapiga hatua za kuhesabu akiuendea. Alipoufikia, aliinama haraka ili auchukue. Alikuwa kwenye hali ya makabiliano, usoni amefura kwa hasira, na alikuwa tayari kupambana na kile kiumbe.

Alipoinama kuuokota ule upanga, kiganja cha mkono wake kikiwa kimebakisha sentimeta chache sana kuukamata, jambo la ajabu sana lililomuacha yeye na mke wake vinywa wazi lilitokea.

Alipigwa na nguvu kama shoti ya umeme. Au kama radi hivi. Iliyomlarua vibaya ule mkono wake. Akajikuta nguvu zikimuisha, huku ganzi ikimtambaa mkononi, na mkono ule ukapoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Hivyo hata kile alichokikusudia alishindwa kukitekeleza.

Mkono uliraluliwa vibaya na nguvu kama shoti kali ya umeme, akashindwa kuendelea na dhamila yake. Alijikuta akipiga kelele ya maumivu makali, huku akiutumia mkono wake wa kushoto kuupa msaada ule wa kuume kwa kuushika.

“WHAAAT..?!”

Makaranga alipaza sauti ya kiulizo kilichoambatana na mshangao. Ghadhabu ilimpanda kichwani mwake kuliko ile ya awali alipokuwa akimtoa mbio mke wake. Kile kiumbe vivyo hivyo. Yule kiumbe alianza kupiga hatua kumuendea Makaranga ule upande alikokuwa amesimama.

Makaranga naye akawa akipiga hatua kumkwepa yule kiumbe atishaye asimsogelee. Lile zoezi liliwafanya wajikute wakizunguka pale na kwa kumuweka Consolatha katikati, kama mchezo wa watoto wadogo uitwao ukuti ukuti.

Muda huo sasa, walikuwa wakitazamana macho kwa macho, huku wakiwindana kama magimbi yenye shauku ya kularuana kwa kumgombania mtetea.

“Who are you hell…u nani wewe pepo…?” Makaranga alimuhoji yule kiumbe kwa hasira, badala ya kumjibu swali lake, yule kiumbe alipiga hatua moja ndefu, akawa amemfikia Makaranga pale alipokuwa amesimama. Akanyoosha mkono wake usiokuwa na panga, akamkwida kooni kisawasawa. Makaranga alikabika koo barabara. Pumzi zikamshinda kutoka puani, akaanza kuhema kwa taabu sana.

“Huwezi kufanya unachotaka kufanya Makaranga. Wewe ni mjinga na mpumbavu sana. Umeua watu wengi na bado unataka kuua, unaua unaua na unaua. Tangu umeanza kuua umeua wangapi. Na sasa unataka kumuua mwanao wa pekee. PU-MBA-VUUUU…!” Kisha akamuachia huku akimsukumiza nyuma kwa nguvu.

 Makaranga alitoka kwenye ile kabali na kuweweseka huku akiangukia mbali, akibiringika hovyo bila kuwa na uwezo hata chembe ya kumkabali yule kiumbe wa ajabu. Pale chini alikohoa hovyo huku mate yakimtoka kama mbwa.

‘Who hell are you bloody fool…’ Alijiuliza Makaranga Bruno.

“U-nani wewe?” Makaranga alijitutumua kumuuliza, huku akishindwa kuendelea na maswali yake. Kwani mate yalimpalia kwa fujo kooni na kumfanya akohoe tu.

“Mimi ni Michaeli…. malaika wa vita. Nimetumwa na Mungu nije  kumuonyesha mkeo namna ambavyo mwanae aliyeko tumboni anawindwa vikali. Na mbaya wake wa kwanza ni wewe mume wake, baba mzazi wa mtoto… MPUMBAVU WEWE!!!”

“Mimi siogopi wala sijali.” Makaranga alijitutumua kumjibu yule malaika.

“Haina shida. Wewe ujali usijali potelea mbali. Hukumu yako inakungoja akhera. Hata ufanyeje, huna uwezo wa kuishi milele duniani. Utakuja tu, na nikuhakikishie kwamba; hukumu yako inakungoja.” Yule malaika aliyekuwa akizidi kung’ara kwa sura yenye mwanga mkali, na mavazi yanayo metameta, alimtamkia maneno makali.

“I don’t care…” Makaranga alimjibu kwamba hajali.

“It is okay…” Malaika Michael akamjibu. Hakuishia hapo, akaendelea. “Fanya mambo yako yooote, jifiche kwa wanadamu, ila mbingu inakujua Makaranga. Inaujua uovu na mabaya yote unayoyafanya. Usipotubu, na kuifata injiri, hutakaa uione pepo nakuhakikishia. Unayoyafanya ni mbwembwe tu kwa sababu ya pumzi uliyonayo kwa sasa. Dawa yako ni siku ya mwisho parapanda itakapolia.” Malaika Michael alimchachamalia kwelikweli.

“Unanitishia..?!”

 “Sikutishii. Ni wakati wako kumuomba Mungu akupe moyo wa nyama. Moyo wa kujifunza, na kujirudi. Tubu na uiamini injiri, uuone ufalme wa mbingu we mwanaume. Halafu, onyo nakupa. Gusa kwingine kote, achana na huyu mtoto aliyeko kwenye hili tumbo.” Akalisonta tumbo la Consolatha kwa upanga wake.

“Huyo ni mwanangu, na nna haki ya kumfanya chochote.” Makaranga akamjibu jeuri. Wakati huo Alisha jaribu jitihada zake zote kuamka pale chini lakini hazikumzalia matunda. Aliendelea kukohoa kwa nguvu huku akijitutumua kujibizana kwa taabu na yule kiumbe wa ajabu, aliyejitambulisha, kumbe ni malaika. Na kila alipokohoa…mate mengi ya damu yalimtoka kinywani, hili lilimshangaza na kumtisha sana. ‘Nini hiki kanifanya huyu?’

“Unajidanganya Makaranga. Na wanaokushurutisha kumdhuru huyu kiumbe wanakudanganya pia. Na ukiendelea na huo mpango…narudia, ukiendelea na huo mpango…lazima ufe. Nakuhakikishia kifo we baradhuli shetani mwanadamu.

Sina muda wa kubishana na wewe mjinga. Taarifa ndiyo hiyo, huyu sio mwanao. Ni mwana wa Mungu. Ukiendelea kumzonga, mabaya yatakayokupata, utajuta mpaka unaingia kaburini.”

Ghafla…malaika akapotea.

Consolatha akagutuka kutoka usingizini.

Doh…kumbe ni ndoto.

Kisha mwana mama Conso akasikia sauti ikimsemesha moyoni…‘Watu wabaya…wenye nia mbaya…wanamtaka mtoto kwa ubaya…’

‘Mtoto yupi?’

‘Aliyeko tumboni mwako…wamekusudia mabaya juu yake, ili wam-malize.’

Yule mama akafadhaika sana. Ndipo ikamjia kumbukumbu, kwamba;

Ilikuwa ni muda mfupi sana, mara tu baada ya msafara wa mumewe, mheshimiwa rais Makaranga Bruno kutoweka pale ikulu, hali ya ajabu ilimkumba, alipatwa na maluweluwe, kama mauzauza. Akawa kama hajielewielewi hivi.

‘Nimepatwa na nini tena..? Mbona ujauzitohuu  unataka kuniendesha mputa?’  Alijiwazia moyoni mwake, huku akiyapeleka macho yake moja moja tumboni na kuutazama uajuzito wa miezi mitatu aliokuwa nao. Ambao haukuwa umeshaanza kuonekana waziwazi, ila tu kwa hisia za baadhi ya wadakuzi.

 Alikuwa sebuleni mahala pa mapumziko, mara, akawa anaisikia nafsi yake ikimshurutisha aende chumbani akajipumzishe. Akaitii ile sauti.

Akajikongoja, huku kizunguzungu kikimyumbisha. Alipofika tu chumbani kwake, alijitupia kitandani. Usingizi mzito ukamtwaa, ndipo hiyo njozi ya kutisha  yenye maajabu mengi ikifatia.

*****

Chumba mkutano cha wale wachawi, kilipambwa kikapambika kwa mapambo na nakshi za kichawi. Lakini kwa wahudumu wa ile hoteli, na mtu yeyote asiyemuhusika wa ile shughuri, akapata mwanya wa kukiona, aliona mapambo mazuri ya kupendeza kama kumbi za kawaida zipambwavyo.

Kulikuwa na meza kubwa yenye mapana na marefu ya kutosha, iliyozungushiwa viti nane. Vitatu kila upande wa marefu, kimoja kila upande wa mapana, na ilikuwa katikati kabisa ya ule ukumbi. Nyuma ya vile viti, kulikuwa pia na mistari mitatu zaidi ya viti, navyo vilikaliwa na wale wachawi.

Viongozi wa juu pekee ndio waliketi kwenye viti vya mezani, wakati wajumbe waliketi ile mistari mitatu ya nyuma. Makaranga alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wajuu, akitumikia kiti cha ukatibu mkuu wa taifa wa kambonia ile. Hivyo aliketi kwenye moja ya viti vya mstari wa mbele ya meza, nyuma yake alisimama ADC Adolph.

Kulikuwa na makundi mawili yenye muonekano mkutanoni pale. Walikuwepo viongozi. Hao wote walijivika mavazi ya ngozi za mbwa mwitu, kama desturi au vazi la mila yao kwa viongozi. Wajumbe wa kawaida walivaa kaniki nyeusi, walizozitanda mabegani kushuka chini.

Kati yao wachawi wa kawaida, yaani wa jumbe wa mkutano ule, wapo waliokuwa wamesimama kwa ajili ya kuimalisha ulinzi. Mikononi mwao hao walinzi, walikamata mikuki ya kichawi kwa ajiri ya kudhibiti hali yoyote iliyomaanisha tafaruku, ndani ya kikao au nje ya kikao.  Hawa walisimama pembezoni mwa kuta zote za ule ukumbi.

Kama ungebahatika kuwaona, lazima ungetahayari kwa mstuko na hamaniko, au kwa mastaajabu. Walitisha kwa kuwatazama. Muonekano wao haukuwa kama wa wanadamu wa kawaida, mfano kama tulivyo mimi na wewe.

Muda wote waliyatumbua macho yao, na kuyafanya yaonekane makubwa, hususani kwa wale waliokuwa wamesimama kwa ajiri ya kuimarisha ulinzi.

Nyuso zao zilitawaliwa na ghadhabu, na pengine ungejiuliza kilicho waghadhabisha namna ile muda wote ni kipi hasa. Lakini kwao, hiyo ilikuwa ni hulka yao.

Kulikuwa na mwaga hafifu uliosababishwa na mioto iliyokuwa ikiwaka kutokea kwenye vibuyu kadhaa vichache, vilivyofungwa vishungi shingoni. Vibuyu hivyo kuna namna viliwekwa kwenye kuta za kile chumba.

Kile chumba kilioneana kuwa na asili ya giza, pengine kwa sababu muda wote madirisha yake yalizibwa kwa pazia nzito. Na hewa ilipatikana kupitia mashine za kiyoyozi zilizofungwa pale hotelini. Hivyo basi, kulikuwa na giza lililomezwa kidogo sana na ule mwanga uliotokana na moto wa kwenye vile vibuyu.

Humo ndimo mheshimiwa Makaranga Bruno aliwekwa kitimoto na washirika wake wa gamboshi. Alikuwa na tuhuma ya kujibu!

Msimu wake wa kutoa kafara ya damu kutoka kwa mtu wake wakaribu mwenye unasaba unaouma, ulikuwa umejiri. Lakini cha ajabu, siku zilizidi kuyoyoma, bila Makaranga kutekeleza agizo hilo.

Na ni sababu hiyo, hata wale misukule wakamjia ndotoni wakimlilia afanye hima kufanya alichopaswa kufanya. Kwani wao pia, walikuwa wakiitegemea sehemu ya nyama za mtu ambaye angetolewa kafara na huyo muheshimiwa, ili wao waile, njaa isiwauwe.

“Kwa nini?!” Mkuu wa gamboshi, aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha upande mmoja wa mapana ya ile meza, alimtupia swali Makaranga, baada ya kuikumbusha ile hadhira kuhusiana na jukumu lililompasa mwenzao kulitekeleza. Na ilihali anajua fika,  madhara ya kukaidi utaratibu huo.

“Au umeamua maksudi kutukomoa, si ndivyo?! Kwa sababu umesha kipata ulichokuwa unakitaka… Unadhani mwaka huu utapenya kirahisi rahisi tu, kwa sababu umeshaikamata dola? Pole sana baba… kwa hilo….umepotoka sana mzee…” Ghadhabu ya kiongozi yule ilijionyesha wazi wazi usoni pake, wakati akijitahidi kuidhibiti sauti yake isipayuke kwa hasira.

Makaranga, aliyekuwa ameketi kwenye moja kati ya viti vitatu vya upande wa marefu ya ile meza kubwa, nzuri, iliyonakshiwa kwa rangi nzuri ya kahawia, nakshi iliyoifanya ionekane ya bei mbaya sana, aliishiwa nguvu, na hakuwa na la kusema.

“Kukaa kimya maana yake nini… kwamba huna jibu au… tukueleweje…?!”

Makaranga kimya.

“Unajua ni kwa kiasi gani unaiweka kambonia ya wachawi kwenye majaribu mheshimiwa Makaranga…?” Mzee mmoja wa makamo alimjia juu. Huyu alikuwa mwembamba sana, mrefu kiasi na umri ulianza kumtupa mkono.

“Unajua fika kwamba huu ni msimu wako na baadhi ya wenzako kutoa kafara ya damu ya watu wenu wa karibu. Wenzako wooote…wamesha tekeleza…kasoro wewe tu! Oh shiiit dammit to hell… KASORO WEWETU..!” Yule mzee alisistiza kwa uchungu uliosindikizwa na hasira.

“Jamani ndugu zanguni..,” Hatimaye mheshimiwa rais alianza kujitetea, machozi yakimtoka kwa uchungu.   

“Mbona nimesha waeleza sana kuhusiana na hili swala. Ninyi nyote ni mashahidi. Siku zote, miaka yote kwa kiasi gani nimekuwa muaminifu kwenye eneo hilo. Ila kwa kipindi hiki…kuna ugumu uliojitokeza kutokana na aina ya mtu ambaye niliagizwa nimwage damu ya**”  Ghafla, alikatishwa na mvumo mkubwa wa sauti nzito iliyoingilia maelezo yake.

Tetemeko kubwa likaikumba ardhi ya ile hoteli. Mvumo wa upepo mkali kama kimbunga kikitawala kila mahali, hususani kwenye kile chumba cha mkutano. Vitu vikawa vikitetemeka, na vingine vikipeperuka na kutupiliwa mbali. Ni wakati wa ujio wa mungu wao, mwenye nguvu saba, na uwezo wa namna saba za kujitokeza.

Ndipo kiongozi mkuu wa kile kikosi cha kishetani akaanza kuongoza sala ya kumkaribisha mungu huyo, akianza kwa kuzitambua nguvu na uweza saba alizo nazo mungu wao. Shetani mkuu, malikia mkuu wa anga, almaarufu kama Lusifa. 

“Lucifer our lord.” (Lusifa bwana wetu ) Kiongozi alianzisha sala ya mapokezi hayo.

“We acknowledge you.” (Tunakutambua) Waamini wakapokea.

“God of seven power…god of seven might.” (Mungu wa nguvu saba…mungu wa uweza saba)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

Ndipo kiongozi akaanza kuzitaja nguvu hizo, au uweza saba za huyo mungu. Huku waamini wakawaida wakiendelea kuitikia kwa muitikio wao. Na kila nguvu aliyoitaja, ndiyo uweza wake mkuu alionao katika kutekeleza au kufanya mambo yake kama mtawala wa dunia hii. Lakini pia ndio namna azitumiazo kujitokeza mahala popote alipohitaji kuwa.

“The wind.” (Upepo)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“The rain.” (Mvua)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“The land.” (Ardhi)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“Earth quick.” (Tetemeko la ardhi)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“God of crisis and disasters.” (Mungu wa migogoro na majanga)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“God of misunderstanding.” (Mungu wa mafarakano)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

“God of accidents, sickness and diseases.” (Mungu wa ajari, maradhi na magonjwa)

“We acknowledge you.” (Tunakutambua)

Baada ya kuzitaja au kuzitambua nguvu na uweza saba za mungu wao, tayari mungu huyo aliwasili na kuketi katikati yao, baada ya kukiacha kiti chake cha enzi aketiko, kule kuzimu ya bahari.

“Your not serious Mr. president… unacheza na uhai wa watu muheshimiwa rais wala hauko serious abadani asilani…” Sauti nene, nzito na ya kutisha mfano wake hakuna, ilisikika ikiunguruma kwa mwangwi ndani ya kile chumba, bila kujulikana ilikotokea. Kila mmoja akastuka, na kisha kila mmoja akawa kama aliyeielewa, hivyo kila mmoja akajenga umakini na utulivu.

‘The god is speaking…mungu anaongea…’ Ndilo jibu lililopita kichwani mwa kila mchawi ukumbini humo. Kwamba mungu wao, mkuu wa anga la wachawi, kwa heshima nyingine mkuu wa giza, alikuwa amewashukia kwa udhihirisho wa kuzungumza waziwazi.

“Hakuna kisicho wezekana kwenye kambonia ya the god… the dark lord. HAKUNA!” Mungu wao alimfokea Makaranga kwa ghadhabu. “Hivyo visingizio na hayo mengine ni yako, na umeyataka mwenyewe. Tumekueleza mara ngapi kuhusiana na huyo mwanamke wako lakini hukutaka kutusikiliza?”

‘Sio kama sikutaka kuwasikiliza jamani…’ Makaranga alijisemea kimoyomoyo, huku uchungu ukimkereketa kooni. Alikuwa katika hali ya kuona kama anayeonewa, kwa sababu, sababu za yeye kushindwa kutekeleza lile agizo zilikuwa juu ya uwezo wake.

“Sio kama hukutaka kutusikiliza…ila…?!” Mungu alimjia juu muheshimiwa rais kulingana na mawazo aliyokuwa akijiwazia. Mungu alimsikia, kwa sababu alikuwa na huo uwezo, haijalishi alijisemea kimoyomoyo.

“Sacrifice is an order, not a will…, kafara ni agizo sio hiyari.” Mungu Lucifer alimjia juu mheshimiwa, huku sauti yake nzito ikiongeza mkoromo wa ghadhabu.

“So, what can I do your highness… Nifanyeje mkuu.” Makaranga alifungua kinywa na kuzungumza. Wakati huo machozi yalikuwa yakimbubujika kwa uchungu maradufu.

“Nothing to do nothing to have honorable…” Mungu alimjibu kwa ghadhabu. Makaranga akalia kilio cha mwanaume kwa kukata tamaa. Ni kama wenzake walianza kumkatia tamaa. Kwa maana hiyo, kiti chake cha urais kilikuwa mashakani.

“Prince of darkness…say a word to us for our sake.” (Mkuu wa giza, tutamkie neno kwa ajiri yetu) Kiongozi mkuu wa ile kambonia alimsihi mungu wao ambaye sauti yake ilidhihirisha ghadhabu ya kuogopeka aliyokuwa nao.

“Makaranga amuue mwanae aliyeko tumboni kwa mkewe. Kisha mimi nitakunywa damu ya hicho kichanga pindi itakapokuwa ikitoka. Haijalishi wingi wake, hata kama ni tone moja tu, kwangu inatosha. I am a satan, and my will shall be.” Mungu alimjibu kiongozi wa kambonia ya wachawi.

Akaendelea. “Lazima Makaranga akumbuke na atambue, huu ni msimu wake kumtolea mungu mkuu wa giza damu, sio miungu wengine, wala mawakala wangu. Miungu au mawakala wa mungu wanaweza kunywa damu ya mwanadamu yeyote, ndio maana tukamruhusu aweze kuipa damu za makafara ya ajari, majanga na kadharika. Lakini mimi mungu, mungu wenu niwatunzaye, nahitaji damu safi. Damu tamu. Nayo yapaswa kutoka kwa mtu mwenye unasaba wa karibu na huyo anipaye hiyo damu. Tena unasaba unaouma. Kwa sasa Makaranga hana mtu wa namna hiyo, zaidi nimependezwa na kiumbe aliyeko tumboni mwa mke wake.”

“Makaranga umesikia…?!” Mkuu wa umoja ule alimuhoji Makaranga. Kabla Makaranga hajajibu, mungu akamjibia.

“Ndiyo amesikia. Anachojiuliza ni namna ya kutekeleza agizo. Usijali Makaranga, nitakuijia ndotoni kukupatia maelekezo yatakayo kusaidia kunitolea hiyo sadaka. Nakuona unavyopata taabu. Najua unachoogopa. Lakini kaa ukijua, hakuna kinachoshindikana kwangu.”

“Mimi ndiye mungu wenu niwatunzaye usiku na mchana. Ningalipo mimi… ninyi pia mpo. Tena mpo salama salimini.”

Baada ya maneno hayo, mungu akatoweka.

*****

‘Hii ndoto…?!’

Bibie Consolatha alifadhaika na kujisemea moyoni, mara tu baada ya kugutuka kutoka usingizini. Akamshirikisha rafiki yake wa karibu, shoga yake kipenzi, mama Rosemarry. Huyu alikuwa mpishi mkuu wa pale ikulu… chief cooker of the palace.

Mazungumzo yao yalifanyika kwenye chumba cha jiko la ikulu, wakati pilikapilika za mapishi zikiendelea, kwa umakini wakutowawezesha wapishi wengine kusikia mazungumzo yao.

“Kuna haja ya kufanya maombi ya nguvu…inakubidi kuomba sana shoga yangu. Hii ndoto lazima ina maana kubwa.” Mama Rosemarry alimwambia shoga yake mara baada tu ya kufika tamati ya simulizi ya ile ndoto.

“Una maanisha nini shoga?” Bibie Consolatha akamtupia swali moja kwa moja.

“Hiyo ndoto ina ukweli ndani yake. Au mwenzangu hauamini kama kuna ndoto za kweli?”

“Usemi wako una maanisha kwamba mume wangu anataka kumuua mwanangu aliyeko tumboni…si ndiyo…?!”

“Sina maana hiyo shoga…” Mama Rosemarry alimdakia kwa kujistukia. “Ila,” akaendelea, “…mimi nasadiki kwamba; ipo haja ya kufanya maombi mazito. Maombi ya nguvu.”

“Maombi mazito..! Maombi ya nguvu..!” Bibie Consolatha Makaranga alinukuu yale maneno kwa kutoyaelewa. “Ndio maombi gani hayo tena..?!” Akaomba uelewesho.

“Hayo ni maombi ya kuvunja.” Mama Rosemarry akaanza kumfafanulia. Consolatha akatega sikio kwa umakini zaidi, kusikiliza yale maneno ya yule mama aliyemzidi umri kwa zaidi ya miaka 20. Wakati huo Consolatha alikiwa na umri wa miaka 35.

“Maombi ya kuvunja…” mama Rosemarry akaendelea, “…ni maombi ya kukataa kila kazi ya shetani inayosimama kinyume na hatima ya mwanadamu.”

Akaendelea, “Kwenye maisha tunayoishi, tuna ulimwengu wa roho. Huu ni ulimwengu usio onekana kwa macho haya ya kawaida.” Akayasonta macho yake mawili kwa kutumia vidole vya kiganja chake cha kushoto.

“Na  ulimwengu wa mwili, huo ndio ambao kazi zake zote, tunaziona kwa macho ya kawaida. Lakini sasa…mara nyingi, mambo ya ulimwengu wa damu na nyama, au ulimwengu wa mwili kwa jina jingine, ni matokeo au udhihirisho wa mambo yanayoanza kwenye ulimwengu wa roho. Kwa maneno mengine ni sawa na kusema hivi.., mambo yanayo tutokea au yanayo fanyika kwenye ulimwengu wa damu na nyama, huanzia kwenye ulimwengu wa roho.”     

“Hilo nalielewa bibie… swali langu, hayo maelezo yako yana husianaje na ndoto niliyoota?!”

“Swali lako linaonesha ni kwa kiasi gani huielewi vema habari niliyokujuza, japo binafsi yako unaamini kwamba unaielewa. Mtu yeyote anayeielewa vema habari niliyokupa, asingeuliza swali uliloniuliza.”

Consolatha alibaki ameachama midomo wazi kwa bumbuazi aliyojikuta akipigwa, kutokana na maneno ya yule mama mtu mzima.

“Ndoto. Watu wengi wasiokuwa na uelewa kuhusiana na nguvu ya ndoto, huchukulia kawaida sana hicho kitu. Lakini mimi…kamwe siwezi kuichukulia kawaida kabisa. Kwa sababu naijua nguvu yake, faida na madhara. Hupaswi kuchukulia ki masikhara hata kidogo kitu kinachoitwa ndoto.”

Bibie Consolatha kimya!

Mama Rosemarry akaendelea.

“Ndoto ni lango la kiroho lililoko ndani ya mtu, lililoumbwa na Mungu.” Mama Rosemarry akaanza kumpatia elimu ihusuyo ndoto. “Ndoto ni mawasiliano baini ya ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili.” Akameza mate huku akimtazama Consolatha, aliyemtegea sikio kwa makini, kisha akaendelea.

“Kazi ya ndoto ni kupitisha mambo ya kiroho mwilini. Hivyo basi, ni muhimu ukajifunza kuwa makini na ndoto unazoota. Kwani kuna faida katika kujua maana ya ndoto uziotazo, kwa maneno mengine ni vema kuzijua tafsiri za ndoto uziotazo. Na; kuna hasara katika kupuuza ndoto ulizoota au unazoota.”

“Ntayawezaje haya yote shoga?” Consolatha alimuhoji.

“Somo kuhusu ndoto ni pana sana. Ni vema ukatafuta watumishi wa Mungu au ukajenga tabia ya kujisomea vitabu vya wapakwa mafuta wa Mungu, wenye uelewa mzuri kuhusiana na hili. Lakini mwisho na kubwa kuliko yote, biblia pekee, ndiye mwalimu mkuu kuhusiana na somo hili.” Mama Rosemarry alimjibu, akaendelea.

“Ntaangalia namna ya kukusaidia katika hilo, lakini, kwa sasa inabidi tuifanyie kazi kwanza hiyo ndoto uliyoota. Najua wewe ni mgumu kidogo kuelewa habari ya injiri kila mara nikuhabarishapo, hiyo haina shida kabisa. Lakini, ningependa kukukutanisha na mgeni mmoja muhimu sana kanisani kwetu.”

“Mgeni muhimu sana kanisani kwenu…sijakuelewa.”

“Utaelewa. Kanisani kwetu kuna mtumishi wa Mungu, yeye ameitwa kwenye huduma ya utume na unabii. Ndani yake ana karama ya kuombea na kutafsiri ndoto, pamoja na kuona mambo ya ndani ya mtu yaliyojificha. Ni mgeni kutoka Congo, na ndiye muanzilishi wa kanisa letu la Body of Christ international ministry. Atakuwepo kwa miezi mitatu. Hivi tunavyoongea, ana wiki mbili tu tangu amefika. Nadhani ungehudhuria moja kati ya semina zake, jambo jema na la kufaa sana lingefanyika maishani mwako.”

Ukatokea ubishani wa hapa na pale…bibie Consolatha akipinga wazo lile, kwa kutabainisha wasiwasi wake juu ya mfumuko wa makanisa lukuki kila uchwao. Kabla kimya hakijachukua nafasi…

*****

     “In the book of Psalm, the word of God tell us… He sent His word, and heal them, and delivery them from all satanic oppression…” Mtumishi wa Mungu, mtume na nabii Christopher Kabila aliyasema hayo wakati akiendelea kuhubiri.

     (Kwenye kitabu cha Zaburi neno la Mungu linatuambia… Hulituma neno lake, na kuwaponya, na kuwaokoa kutoka kwenye magandamizo yote ya kishetani) Mkarimani wake, mwinjiristi Joshua Antony alimtafsiria.

     Ilikuwa ni ndani ya kanisa la kilokole, liitwalo “The body of Christ International ministry.” Kwa Kiswaili, “Huduma ya kimataifa ya mwili wa Kristo.” Lililopatikana Yombo Buza Dar es Salaam.

     Ilikuwa ni wakati wa ibada ya semina ya neno la Mungu, iliyokuwa ikiendelea kanisani hapo, kwa juma zima mfululizo. Ilikuwa ikiendeshwa na mtumishi huyo wa kimataifa, raia wa nchini Kongo.

     “So…”

    (Kwa hiyo.)

     “Fear not.”

     (Usihofu.)

    “Worry not.”

    (Usiogope.)

     “Why?”

     (Kwa nini?)

      “Our God is a live.”

      (Mungu wetu yu hai.)

      “Put those beautiful hands for Jesus…”

      (Mpatie Yesu hayo makofi mazuri…)

      “Give Him offering of a big clap please…”

     (Mpatie sadaka ya makofi makubwa tafadhari…)

     “ If it’s for Jesus you can do more better…”

      (Kama ni kwa ajiri ya Yesu unaweza kumpigia zaidi.)

      Ibada ilipamba moto. Watu walikuwa wakishangilia na kurukaruka. Kelele za shangwe, miruzi, nderemo na vifijo zilisikika kwa wingi, wakati mpakwa mafuta yule, masihi wa Mungu mwenye kismati cha kukubalika kila mahali aingiapo, akiendelea kuhudumu.

     The body of christ international church, tawi la Yombo Buza, lilikuwa ni kanisa la wastani. Halikuwa kubwa sana wala dogo sana kwa miaka ile. Asili yake au chimbuko lake ni nchini Kongo. Muhasisi wa huduma hiyo ni mtume na nabii James Kabila, ambaye ndiye aliyekuwa amekuja kuhudumu nchini Tanzania, kwenye makao makuu ya kanisa hilo nchini.

     Na siku hiyo wakati akiendelea na mahubiri yake, ndipo hali flani isiyokuwa ya kawaida ilitokea nje ya kanisa. Pikipiki ya kipolisi maalumu kwa ajiri ya kuimarisha ulinzi wa kimsafara iliingia huku ikipiga king’ora. Ikafatiwa na magari matatu ya kifahari, yakiwemo mawili ya kijeshi, ya rangi za kijani iliyoiva.

     Maofisa usalama kadhaa waliteremka na kuimarisha hali ya ulinzi kwa utulivu. Mama Rosemarry na bibie Consolatha, waliteremka kwenye gari aina ya Honda Accord, iliyokuwa katikati ya zile gari za kijeshi. Dada mmoja aliyevalia suti na mawani meusi usoni, akionekana kuwa sambamba zaidi na bibie Cosolatha, alimshikia mikoba, na kuwasindikiza kuingia ndani. Huyo alikuwa mlinzi, au bodyguard wa mke wa rais.

     Wahudumu wa ibada waliokuwa mlangoni kulaki wageni, au ushers kama wajulikanavyo kwa kimombo, waliwasogelea na kuwapokea kwa bashasha. Ndipo walipoingia kwa pamoja kanisani hapo, jioni hiyo, lakini wakiwa wamechelewa kidogo.

      Kwa vile walifika muda ukiwa umewatupa mkono, na kanisa limeshasheheni idadi kubwa ya waumini waliohudhuria ibada, waliona sio vema kuvuruga umakini wa waamini kwa kupita mbele ya watu. Hivyo wakaingilia mlango uliokuwa kwenye ukuta wa pembeni mwa kanisa, upande wa nyuma. Kigezo kwamba bibie Consolatha alikuwa mtu maarafu sana nchini walikizingatia.

     Wakati wakiingia, macho yao yakiwatoka kwa kufata uelekeo waliokuwa wakiongozwa na muhudumu aliyewapokea, lilitokea jambo tofauti kabisa na mategemeo yao. Kutoka kule mbele, madhabauni, nabii na mtume James Kabila aliwaona.

     Ghafla…

     Akasitisha mahubiri, akamakinika nao.

     ‘Ah…nini hii…oh Mungu…’ Hawakuipenda hali ile. Kwani kile kitendo cha mtumishi yule kusita kuendelea kuhubiri, na kubaki amewatazama wao, kiliuteka umakini wa waamini wote mule kanisani. Nao wakageuza shingo zao nyuma, kutazama kilicho mmakinisha mtu wa Mungu, nabii James.

     First lady…

     Heh..! Hakuna jicho la mtu liliyemuona yule mke wa rais, likamtazama mara moja. Kila mmoja alishikwa na mastaajabu asiamini moyo wake kwa kile alichokiona. Mke wa rais wa nchi, aliingia na kuketi kimya kimya akiwa ameongozana na mpishi wake. Wao wanamfahamu kama mama Rosemarry.

     Walishangaa…

     Bibie Consolatha pia alishangaa, hakutegemea kama yule nabii aliyepewa habari zake na shoga yake kwamba ametoka Kongo angeweza kumtambua haraka namna ile, kiasi cha kumfanya aghairishe mahubiri na kubaki amemtazama yeye. Alijisikia vibaya, moyoni akijihukumu kwa kuharibu mfumo wa ibada, na pengine kosa lake lilikuwa kufika katikati ya mahubiri.

     Mama Rosemarry pia alifikiri na kudhani kama mwenzake alivyokuwa akidhani. Kwamba ujio wa mke wa rais umevuruga ibada, na pengine ungeendelea kuivuruga kwa sababu lile kanisa lilikuwa changa, na halikuwa na desturi ya kutembelewa na ugeni mzito kama ule.

     Haikuwa hivyo.

     Nabii James hakuwa ameujua wajihi wa yule mama, la Hasha wa Kalla. Wasiwasi wao tu. Bali wakati wao wanaingia mule ndani kanisani, jambo flani la kitumishi lilipita kichwani mwa yule bwana. Haraka sana, alioneshwa kitu kumuhusu bibie Conso, na papo kwa hapo, Roho wa Mungu akampa ujumbe moja kwa moja mahususi kuhusiana na yule mwanamke aliyekuwa akimtazama. Bibie Consolatha.

     “Wewe mama uliyeingia sasa ivi, mwenye kilemba cha bluu pita hapa mbele.” Nabii alitamka huku akimtazama kwa macho yake yote mawili first lady. Aloo…! Waamini walishangaa sana. Amepata wapi ujasiri wa kumuita namna ile mke wa rais…first lady wa taifa.

     Hawakujua kwamba nabii na mtume Kabila, hakulijua hilo. Bibie Consolatha akatii wito ule kwa kujongea pale madhabauni, huku akisindikizwa na mlinzi wake.

     “Una mimba ya miezi mitatu…” Nabii akaanza kumueleza mara tu baada ya kufika pale mbele. Alikuwa akitumia lugha ya kiingereza akitafsiriwa na yule mkalimani wake. Bibie Conso akapigwa na mshangao.

     ‘Huyu kweli nabii…’ Alijisemea kimoyo moyo.

     “Ndiyo mtumishi.” Consolatha akamjibu kwa lugha ya kiingereza pia, huku mkalimani akiendelea na jukumu lake ipasavyo.

     “Halikuwa swali ili unijibu…” Nabii Kabila akadakia. “Wala sikuhitaji unithibitishie nikuelezacho. Nakuambia nnachokiona, na nina uhakika na nikuambiacho.”

     Bibie Consolatha hoi…

     “Naona taji la kiutawala juu ya kichwa chako…” Nabii akaendelea kutoa unabii huku akitamka yale maneno ya mwisho kwa kuuzungusha mkono wake hewani usawa wa kichwa chake. “Japo sikufahamu, pasina shaka u mtu mkubwa sana wewe. U-nani katika maswala ya kiutawala?” Nabii alizidi kuwastaajabisha waamini na wageni waliohudhuria ibada ile, wakiwemo wale wana usalama waliomsindikiza mke wa rais.

     “Mimi ni mke wa rais wa taifa hili.” 

     “Wow.” Furaha isiyokifani ilimkumba yule mtumishi wa Mungu wakati lile neno la mshangao likimtoka kinywani, akisindikizwa na makofi mengi yaliyopigwa na waamini. Kelele. Nderemo. Vifijo.

     “Jamani makofi mengine mengi zaidi kwa Yesu.” Nabii aliwachochea waamini wazidi kumshangilia Yesu wao. Kelele za shangwe zikarindima maradufu.

     “Yesu yu haiiii…” Nabii alitamka kwa nguvu.

     “Nawe u hai…” Waamini wakajibu kwa nguvu pia.

     “Yesu yu haiiii…”

     “Nawe u hai…”

     “Bwana Yesu asifiweee…”

     “Ameeeeeeeeen…..”

     “Mama…unanifahamu mimi?” Nabii alimtupia swali mke wa rais.

     “Hapana.” Alijibu mke wa rais.

     “Tumewahi kuonana hapo kabla labda?”

     “Hapana.”

     “Unasali kanisani hapa.”

     “Hapana nabii.”

     “Sasa mimi nimeyajuaje yote haya…?!” Nabii Kabila aliwageukia waumini kwa mbwembwe na mikogo alipokuwa akiuliza lile swali la mshangao. Akawa akitembea tembea kwa maringo ya kitumishi pale madhabauni. “Halafu ukiambiwa hapa Mungu yupo bado ukatae…basi bila mashaka kabisa utakuwa na matatizo kwenye akiri zako.” Akamalizia kwa kicheko cha ujasiri.

     “Namuona mama mmoja wa makamo, jina lake la kwanza linaanzia na S…S….Somebody Si Si Si…weewee…”  Nabii alipata kigugumizi kutamka hilo jina.

     “Siwema.” Bibie Consolatha alimsaidia.

     “Alright…na jina lake la pili linaazia na herufi M.”

     “Makaji.” Bibi Consolatha akamdakia pia.

     “Nice.” Nabii akaafikiana naye. Makofi yakaongezeka maradufu.

     “Huyo mama ni rafiki yako mkubwa sana. Namuona mama huyu akikupatia chakula kizuri sana. Unakipokea. Unakila…halafu…ukigeuka nyuma unakitema.”

     “Ni kweli mtu wa Mungu. Siwema Makaji ni rafki yangu sana. Lakini pia ndiye mpishi mkuu wa ikulu.”

     Watu “Weeeeeeeee….”

      “Na ndiye aliyenipa habari zako, na ndiye aliyenileta hapa.”

     Nabii kusikia vile, palepale akaita. “Siwema Makaji pita mbele.” Mama Rosemarry aliamka huko alikokuwa ameketi huku akilia kilio cha kwikwi, kilichoambatana na kunena kwa lugha. Akasogea madhabauni. Wakati huo zile kelele za vifijo na makofi havikukoma.

     “Oh…ooh…wewe ndiye Siwema Makaji?”

     “Ndiyo nabii.”

     “Na sina shaka u-muumini wetu hapa, sura yako ni kama nimewahi kuiona hapa?”

     “Ndiyo nabii.”

     “Ubarikiwe sana kwa kumleta bosi wako leo nyumbani kwa Bwana. Na ama hakika na kuhakikishia, si wewe wala yeye. Kati yenu, hakuna atakaye jutia kwa ujio wenu siku ya leo mahala hapa. Bwana anasema nami waziwazi kwamba; leo ndio siku ya kufunguliwa kwa bosi wako…kama unaamini ongeza makofi mazuri kwa Yesu.”

     Makofi mengi zaidi yakapigwa.

     “Siwema…chakula ambacho Bwana amenionyesha ukimlisha huyu mama, naye ana kila kisha anakitema, sio hicho unachompikia kama chief cooker of the palace. Sio hicho kinachokusababisha mwisho wa mwezi ukinge mkono upokee salary. Hapana. Bwana anasema, umekuwa ukimlisha chakula cha kiroho. That means neno la Mungu. Neno la Mungu ndio chakula cha kiroho…emeeen…”

      “Eeeemeeen…”

      Nabii alipiga kimya akiwatazama wale wamama walioonekana kuafikiana na yale maelezo.

     “Na amekuwa akikipokea hicho chakula, yaani hayo maneno ya Mungu unayokuwa uki mteach. Lakiiiiniii…cha kusikitisha sana, mama huyu hukila kisha hukitema hicho chakula. Yaani huwa analipokea neno, baadae hulipuuzia, na kulichukulia kawaida sana kana kwamba halina maana yoyote katika maisha yake. Na hiyo ndiyo imekuwa silaha aitumiayo shetani kumsulubisha katika maeneo mbalimbali ya maisha yake…kweli au naongopa?”

     “Ni kweli nabii.” Consolatha na Mama Rosemarry walimuitikia kwa pamoja.

     “Na moja kati ya maeneno ambayo adui amekuwa akipata mwanya wa kumpiga kupitia ukaidi wake wa neno la Mungu, amekuwa akipata mimba, na mwisho wa siku ndani ya miezi miwili au mitatu ya ujauzito, zinatoka. Kama naongopa aseme.

     “Usemacho ni kweli mtumishi wa Mungu.” Bibie Consolatha alijibu, safari hii machozi yakimbubujika kama mtoto mdogo. “Na hii uliyoiona, ni mimba yangu ya nne. Nyingine tatu zote nilizozibeba nikiwa ndani ya ndoa yangu…zilitoka zikiwa na aidha miezi miwili au mwezi mmoja.” First lady akafafanua.

     Nabii akaendelea. “Kuna watu wanaofatilia kizazi chako, na kila uzao unaoelekea kuupata, wana kupora kichawi. Lengo sio wewe ukose watoto, la. Shida yao ni kunywa damu za vichanga unaowabeba tumboni mwako. Usiniulize kwa nini inakuwa hivi. Lakini unachopaswa kujua, damu ya wanao wanaokuwa tumboni, kwao ina maana kubwa mno.”

     Nabii akaendelea. “Lakini sasa…safari hii wamenoa nanga kuichukua damu ya hicho kichanga ulichonacho. Kwa sababu uliyembeba humo, ni mkuu. Ni mbarikiwa kuliko uzao wako woteee…na ni mtumishi mkubwa wa Mungu ajaye. Kazungukwa na ulinzi mkubwa wa malaika. Na ndio sababu we mwenyewe umekuwa ukishangaa, mbona awamu hii mimba haiharibiki.”

     “Je, ungependa kumjua muhusika mkuu wa uharibifu wa mimba zako?”

     “Ndiyo nabii.”

     “Yule mwanaume uliyemuota majuzi mchana kwenye ndoto, akikukimbiza na upanga, akitaka kulitumbua tumbo lako, kabla hajatokea malaika Michaeli kukuokoa…ndiye muhusika mkuu wa agenda hii.”

      Mrs. Makaranga alihisi upepo mkali kama kimbunga ukimvagaa na kumchota miguu yake yote miwili. Yowe la mpagao lilimtoka kinywani mwake wakati akirudi kinyumenyume.

     Akaanguka chini. Akasaidiwa na wasaidizi wa ile ibada, waliompokea mgongo na kumzuia asianguke vibaya. Wakamlaza sakafuni taratibu. Akapoteza fahamu.

*****

     Jumapili moja, mishale ya saa saba mchana wa jua kali, wakati mzee Agustine Barua na familia yake wakiwa garini kurejea nyumbani kwao, wakitokea kanisani, njiani, waliendelea kujadiliana namna walivyobarikiwa sana na ibada.

     “Hakika Mungu anamtumia kwa namna ya ajabu na ya tofauti sana pastor Lameck.” Mzee Agustine alimsifia mchungaji wao katikati ya yale mazungumzo, na familia yote ikamuunga mkono.

      “Kweli mwanangu, yule mchungaji yuko moto kwelikweli.” Mama mzazi wa mzee Agustine aliongezea.

      Ndani ya gari lao dogo aina ya Honda Civic, nyuma ya usukani aliketi mzee Agustine Barua, pembeni yake aliketi mke wake. Watoto wao watatu, Joshua, Nassari na Immakulatha waliketi viti vya nyuma kabisa. Wakati siti za katikati waliketi mama mzazi wa mzee Agustine, pamoja na kijakazi wao aitwae Cesilia au Cessy.

     “Ukimtumikia Mungu katika roho na kweli, lazima akutofautishe. Amesema mwenyewe kwenye maandiko yake matakatifu, “Yeyote atakayenitumikia, nami pia nitamuheshimu. Kwa hiyo, pastor Lameck yuko hivyo alivyo kwa sababu Mungu anamuheshimu.” Mama mzazi wa Agustine aliendelea. Akaungwa mkono na wanafamilia wote.

        Safari ya kurudi nyumbani kwao Gongo la Mboto, kutokea Kivule Matembele ya pili, lilipokuwa kanisani lao, ilinogeshwa na nyimbo za injiri zilizokuwa zikikita kwenye spika za gari ya yule mzee. Barabara ya vumbi yenye makorongo na mashimo mengi, ililifanya gari linesenese kila mara. Mazungumzo yalinoga ki-sawasawa, mpaka wakapata ajali.

     Aloo!

     Mzee Barua alichelewa kuliona jiwe kubwa lililokuwa kwenye dimbwi la maji.  Ghafla bila kutaraji, akalivagaa, baada ya kujitahidi kulikwepa bila mafanikio. Bampa la mbele la ile Toyota Escodo likajikita juu yake.

     Ndipo yeye na mwanae mkubwa wa kiume aitwae Joshua, walipolazimika kuvua viatu vyao, na kupandisha suruali zao mpaka magotini, kisha wakatelemka ili kuikagua ile ajari. Walifanya vile ili kukabiliana na maji ya lile dimbwi, ambayo ilikuwa ni lazima wayakanyage.

    Wakiwa nje ya gari, walishuhudia sehemu ya mbele ya gari lao ilibonyea kiasi, na kupoteza muonekano wake mzuri na wakuvutia. Haikuwapa taabu sana. Wakarejea garini, mzee Agustine akainasua gari kutoka pale kwenye jiwe, kisha wakaendelea na safari.

     Baada ya mwendo wa takribani kilometa saba kutoka kwenye lile eneo walipopata ajari, wakawa wameikaribia barabara kubwa ya lami ya Gongo la Mboto, mwendo wa hatua chache lilipo jengo la shirika la mamlaka ya anga.

     Kulikuwa na trafki na polisi kadhaa kwenye makutano ya  barabara ya vumbi, na ile ya lami. Gari mbalimbali zilikuwa zimesimamishwa kandokando mwa barabara na wale askari wa barabarani.

    Ili ashiria hali haikuwa sawa, na ukaguzi yakinifu ulikuwa ukifanyika hususani kwa magari yatokayo barabara ya vumbi.

    Katikati ya makutano ya zile barabara, trafiki mmoja wa kike alikuwa akitoa melekezo kwa madereva, akisimamisha na kuruhusu magari.

    Mmoja kati ya askari wa kiume wa usalama barabarani, alikuwa makini na magari yaliyokuwa yakitokea kwenye ile barabara ya vumbi, upande walikokuwa akina mzee Agustine.

     Alikuwa akitembeatembea pembezoni mwa upande wa kuume mwa ile barabara ya vumbi. Kandokando mwa yale magari yaliyokuwa kwenye foleni, huku akiyatazama kwa makini sana, na nikama kulikuwa na jambo alikuwa akilifatilia.

      Punde, mara tu baada ya macho yake kutua kwenye Toyota Escodo ya mzee Agustine, alistuka kidogo huku akizidisha udadisi. Akaanza kulisogelea huku macho yake yakiwa yameliganda gari ile.

     Akaelekea dirishani kwa dereva, akampa ishara ya kumwamuru aitoe kwenye foleni, kisha aipaki pembeni. Wanafamilia wote wakashangaa…‘Kwa nini?’

     Mzee asiye na makuu, alilichomoa gari lake kwenye foleni na kulisogeza pembeni, huku kichwani akijiuliza kwa nini hasa yule trafki amewataka wao na si gari nyingine zilizokuwa kwenye ile foleni. Maneno ya kulaumu ile hali sanjari na mifyonzo iliwatoka vinywani wale wanafamilia.

     Yule trafki alipiga hatua kulifata lile gari pale lilipokuwa likielekea kupaki.

     “Habari zenu jamani?” Trafki aliwasabahi baada ya kuwafikia. Alikuwa mrefu sana, mweusi sana, mwembamba sana, na alikuwa akizungumza kwa upole sana.

     “Nzuri tu.” Wote walimuitikia kinyonge-nyonge. Hakuna aliyekubliana naye kwa kuwaondosha kwenye foleni. Walikuwa wamechoka mno, na kila mmoja alitamani afike nyumbani haraka, ale, apumzike.

     “Mnatoka wapi, na mnaenda wapi?” Yule askari wa usalama wa barabarani aliuliza huku amemkazia macho makali mzee Agustine.

     “Tunatoka kanisani mkuu, tunarejea nyumbani.” Mzee Agustine alimjibu. Yule trafki akakazana kumtazama usoni mpaka mzee wa watu akapatwa na hofu. ‘Ana nini huyu….mbona ananiangalia sana?’ Na hata wakati swali lile likipita kichwani mwa mzee Agustine, jambo lingine la kuongofya likamfunukia yule mzee kuhusiana na yule askari. Mashaka Macho ya yule trafki, yalijawa na mashaka mkubwa juu yao.

     Yule askari akazidi kumtazama.    

     “Hebu fungua mlango wako mzee.” Trafki alimuamuru kwa sauti ndogo yenye amri, huku akitazama pembeni. Mzee Agustine, mzee wa watu asiye na makuu akatekeleza amri ile. Na hata alipokuwa akitekeleza kile alichoamriwa, aligundua kwamba hali ilikuwa shwari kwa yule askari. Udadisi.

    Macho ya yule askari yalipotuama miguuni mwa mzee Agustine, yalijawa na fadhaa. Mashaka. Wasiwasi. Mzee Agustine aliyagundua yote hayo. Akahisi ile hali ilimkuta yule askari pengine kutokana na namna suruali na miguu yake ilivyokuwa imelowa maji.

     Lakini…

     Pasina shaka mawazo ya yule askari yalienda mbali zaidi. Alitikisa kichwa, kuashilia kwamba; alikuwa amepata jibu la kiulizo alichokuwa nacho.

      Trafki yule alipeleka macho yake huku na kule, akatoa ishara kwa askari wengine waliokuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa, akiwataka wasogee pale alipokuwa. Trafki mmoja wa kike na polisi wawili wa kiume wakasogea wakaungana naye.

    Walisogea kando na kufanya mazungumzo ya faragha kidogo kwa dakika chache. Mpaka muda huo, mzee Agustine alishaanza kupatwa na hofu. Kulikuwa na kila dalili kwamba, mambo hayakuwa mambo.

    Walipomaliza kuteta faragha, wakaanza kulizungunguka lile gari huku wakionyeshana vitu kadhaa, na hili ndilo jambo lililozidi kumtisha mzee wa watu. Cha kushangaza, walipofika mbele ya gari, kukawa na majadala zaidi.

    Agustine aliyafatilia maongezi yao kupitia kioo cha mbele ya gari lake, japo kuwa hakuwa akizisikia sauti zao, lakini ilitosha kumjulisha kwamba, lile bampa la mbele lililoharibika baada ya kugonga jiwe, lilizua mjadala.

    ‘Kwani vipi jamani….mbona mambo yanazidi kuwa mengi…kuna nini?!’ Agustine alijikuta akiwahoji wale askari kimoyomoyo.

    Baadae askari wale waliwarudia wale wanafamilia.  Wakawaweka kizuizini.

    Ndipo wakawaeleza chanzo cha mambo yote yale. Na sababu za purukushani zilizokuwa zikiendelea eneo lile. Na kisa hasa cha ujio wa askari wengi namna ile mchana ule, kwenye makutano yale. Askari wale, waliwapa habari iliyokiacha wazi kila kinywa cha mwanafamilia wa familia ya mzee Agustine.

     Ama kweli dunia ina mambo…na ukistaajabu ya Musa, pasina shaka haujayaona ya Filauni.

*****

     “Khaa!” Ndio neno la kwanza kumtoka kinywani mzee Agustine, baada ya kuteremshwa kwenye gari ndogo ya polisi, na kuliendea kusanyiko kubwa la watu lililokusanyika palepale ile walipopata ajari.

     Alishangaa sana.

     Akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi wanne, waliwapenya watu waliojazana lile eneo, ili ashuhudie jambo ambalo yeye pamoja na ndugu zake walilibishia kwamba halikuwa kweli.

     Wanafamilia wenzake pia walikuwa pamoja naye, midomo yao ikiwa wazi kwa bumbuazi na mastaajabu yasiyoelezeka, kila walipoitafakari hali iliyowaharibia siku yao ghafla.

     Kumbe hawakugonga jiwe kama walivyoona, bali walimgonga binti mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tatu, mwanafunzi wa darasa la sita wa shule ya msingi Ukonga, iliyopo Ukongo Banana. Na binti huyo alidaiwa alikuwa akiishi eneo moja liitwalo Majumba Sita. 

     Doh!

     Wanafamilia nao walilisogelea kusanyiko lile, na kupenyeza mpaka eneo la tukio. Wakapokelewa na vilio vya msiba. Watu walikuwa wakimlilia binti aliyefikwa na mauti, maiti yake ikiwa pale chini imefunikwa kwa kanga.

     Inspekta Obeid Mwakibote, aliifunua ile maiti ili kumuwezesha mtuhumiwa wao kuiona. Mzee Agustine Barua, ambaye alifanana sana sura na muonekano wake na katibu mkuu wa umoja wa mataifa, hayati Koffi Annan, alipigwa na bumbuazi wakati akiitumbulia macho maiti ile, iliyovulia damu, kutoka mdomoni kuangukia shavu la kushoto, macho yake yakiwa yametumbuka, mdomo wake ukiwa wazi kama hayawani.

     “Haiwezekani…hii sio kweli inspekta…hapa sie tuligonga jiwe jamani.”

     “Wewe mzee mtu akikuangalia unaonekana mstaarabu sana, lakini roho yako ni ya kutu nyeusi, tofauti kabisa na mvi zako nzuri zilivyo nyeupe…wakati umemgonga huyu binti tumekushuhudia kwa macho yetu. Wewe na mwanao mlishuka garini, baadae mkarudi na kuondosha gari…sio nyie?” Baba mmoja mwenye umri wa utu uzima alipigilia msumari.

     “We baba una uhakika na unayoyasema?” Mzee Agustine alimjia juu yule mwanaume.

     “Kwa hiyo nakusingizia…sio kweli kwamba wewe…” Hakumalizia utetezi wake, mzee Agustine akamdakia.

     “Jamani…hayo uyasemayo ni kweli, lakini, mimi sikugonga mtu, niligonga jiwe.” Mzee Agustine alijitetea kwa uchungu.

     “Jiwe gani hilo mzee unalolizungumzia, hebu tuonyeshe.”

     Cha kushangaza, mzee Agustine na nduguze waliangaza huku na kule wakilitafuta lile jiwe.

       Hawakuliona.

      Aisee!

      Haya si mauzauza.

      Polisi walipoendelea kuwahoji wananchi waishiyo jirani na eneo lile, kuhusu uwepo wa jiwe hilo eneo lile walikataa. Mzee Agustine akawa amepatikana kwelikweli.

     Wananchi wali wakodolea macho ya kuwazodoa wanafamilia ya Agustine Barua, baada ya kugundua ndiyo aliyemsababishia kifo yule msichana, kisha wakatoweka. Waliwashutumu kuwa wana roho mbaya, kiasi cha kugonga mtu na kumtelekeza namna ile mule majini.

     ‘Halafu eti wametoka kanisani…watu wengine kwa kujifanya malaika kumbe ni mashetani wakubwa…Mungu anawaona.’ Maneno ya kashfa yalisikika hapa na pale.

     Wakati mijadala na mabishano ya hapa na pale yakizidi kuchukua nafasi, inspekta wa polisi, Obeid Mwakibote alikuwa akimtazama kwa makini sana usoni mzee Agustine. Akimdadisi, na kwa kuyafatilia mapokeo ya yule mzee juu ya lile tukio. Alichogundua, ni kama vile kweli yule mzee hakuwa akilitambua lile jambo.

     Hata alipojaribu kupingana na akiri yake iliyoanza kumtetea mzee Agustine, alizidi kupatwa na wasiwasi fulani. Wanafamilia wa mzee Agustine Barua, nao walionesha dalili zilezile. Hakuna walijualo, na lile swala ama kwa hakika lilikuwa geni mno akirini mwao. ‘Mh..! Inawezekanaje hii? Au hawa watu wanaleta sanaa…yup pasina shaka hii ni drama, tena drama kwelikweli.’  Maneno yale yalipita akirini mwa inspekta Obeid Mwakibote yakikinzana na hisia zilizoanza kupata nafasi kwenye ufahamu wake wa akiri. Wakati huo alikuwa akiifunika tena ile maiti kwa kanga, kisha akazidi kumtazama mzee Agustine kwa macho yaliyohoji, ‘una swali jingine…au umeridhika sasa?’

     Kati ya wananchi waliokuwepo pale, wapo waliojinadi kama jamaa wa msichana yule, na wengine walidai kuwa walikuwa wakimfahamu tu.

     Binti mmoja alidai kuwa marehemu aitwae Rhoda Mtaki, pasina shaka alikuwa akielekea nyumbani kwao mchana ule kwa minajiri ya kujisomea. Walikuwa na hiyo miadi, na ni kawaida yao kutembeleana kwa ajili ya kujisomea. Na siku hiyo muda huo, alikuwa akienda kwao Kivule, kwa ajili ya mjadala wa kikundi, (group discussion). Yule binti aitwae Hawa alishuhudia mbele ya umati wa raia pamoja na polisi.

     Wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba; awali hawakujua kwamba lile gari liligonga mtu. Kwani ajari ilitokea ndani ya dimbwi kubwa lililojaa maji yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo. Ila kwa mbali waliishuhudia ile gari ilikwama baada ya kugonga kitu mule majini, ikiambatana na sauti ya kishindo. Nao wakajua ni eidha iligonga jiwe. Kisha wenye gari waliteremka, na kukagua ajari waliyoipata kisha wakarejea garini, wakaondoka zao.

     Mpaka baada ya wao kuondoka, ndipo watu wengine walipogundua kwamba ile gari ilimgonga yule msichana, ambaye kiwiliwili chake kilionekana kikielea majini punde baada ya ile gari kutoweka.

     Ndipo walipopiga namba ya simu ya polisi idara ya usalama barabarani kuwajulisha juu ya tukio lile, huku wakiitaja gari aina ya Honda Civic rangi ya damu ya mzee kuhusika na tukio lile. 

     Ndipo taarifa ile ikatumwa kwa askari wa usalama barabarani waliokuwa zamu eneo lile la maungio ya barabara ya Kivule na ile ya Gongo la Mboto. Pia wakaongezewa msaada wa askari kutoka kituo cha polisi Ukonga. Doria ikaimarishwa eneo husika, na ikazaa matunda kwa kuinasa gari ya mzee Agustine Barua.

     “Mmeamini sasa…au bado tunabishana?!” Sajenti Spark Komba, akiwa ni mmoja wa maaskari waliokuwa pale aliwahoji wale wanandugu waliokuwa pamoja na mzee wao. Akaishia kuyapeleka macho yake kwa mzee Agustine mwenyewe, mtuhumiwa namba moja, aliyesababisha kifo cha yule msichana.

     “Ndiyo huyu muuaji…” Minong’ono ikazidi. Wananchi wachache waliojinadi kuwa waliliishuhudia lile tukio mara tu baada ya kuiona ile gari, walipaza sauti zao za shutuma kwamba ndiyo gari haswaa iliyomgonga yule binti. Na ule uthibitisho wa kubonyea kwa sehemu ya mbele ya gari, kulizidi kuwaamshia uchochezi na uaminisho kwa wale polisi.

     Wanandugu wote waliendelea kupingana na hoja ya wale wananchi, pamoja na polisi waliomtia nguvuni ndugu yao, tangu wakiwa kule barabarani walipoamriwa kupaki gari yao pembeni.

    Ilikuwa ni mara tu baada ya yule trafiki mrefu sana, mwembamba sana na mpole sana, akishirikiana na askari aliowapa ishara wakasogea walipokuwa wameegesha gari, baada ya ukaguzi walioufanya sanjari na mazungumzo yao ya faragha, waliwasomea mashitaka ya kumgonga na kumuua yule msichana.

     Papo kwa hapo walishuhudia askari polisi wengine, akiwemo inspekta Obeid Mwakibote, na sajenti Spark, waliokuwa wamepaki gari yao ndogo aina ya Toyota Mark 2  pembezoni mwa ile barabara, wakiwaijia. Wakampiga pingu mzee wao. Wakamuhamishia kwenye gari yao, huku askari mwingine mwenye cheo cha kluta akiingia kwenye ile gari na kukamata usukani. Wakarudishwa eneo la tukio.

     “Kuanzia muda tuliokutia nguvuni ulikuwa chini ya ulinzi mzee Agustine, na hata sasa uko chini ya ulinzi na unaenda polisi kujibu mashitaka.” Inspekta Obeid Mwakibote alitamka yale maneno yaliyopenya na kuuchoma sawia moyo wa yule mzee mwenye hofu kubwa ya Mungu.

     Siku hiyo, yule mzee mcha Mungu, alilala mahabusu ya kituo cha polisi cha Ukonga Banana, akisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka…

KESI YA MAMA MJANE

      Sauti ya yule msichana, aliyekuwa akilia kila siku, ilipenya masikioni mwa mwandishi wa habari wa gazeti la HEKA HEKA, Comred Bonta kila siku usiku, alipokuwa akikatiza ile njia ya mtaani, akielekea nyumbani kwake. Na kila siku alfajiri, alipokuwa akikatiza ile njia akielekea kazini, aliisikia pia.

      Sauti ya msichana!

Hakujua nini kilimliza yule binti…wala hakuwa anamfahamu.

Alichojua yeye ni kwamba, kila siku akatizapo ile njia, hatua chache kabla hajaifikia ile nyumba ilimotoka ile sauti, alitegemea kuisikia, na hakika aliiskia. ‘Ana nini huyu msichana?!’

Alijikuta akijiuliza siku hiyo alipojikuta akimakinika na kile kilio chenye maombolezo yaliyogubikwa na uchungu dhahiri, bila hata kumuona wala kumfahamu muombolezaji. Lakini, namna sauti ilivyomtoka yule mama mliaji, ilitosha kuvuta picha ni kwa namna gani alikuwa kwenye kipindi kigumu.

‘Pasi na shaka nahitaji kukutana na huyu msichana…pasina shaka ana wakati mgumu sana, nami kama mwanadamu mwenye moyo wa nyama, nahitaji japo kufahamu nini kinamsibu, hata kama iko nje ya uwezo wangu. Kujali, ni zaidi ya fedha na dhahabu.’ Alijisemea moyoni Comred Bonta kwa jina la utani ‘Shushushu,’ kama wafanyakazi wenzake na wapenzi wa kazi zake walivyopendelea kumuita, wakimaanisha, alikuwa mtaalamu katika kutekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari, kwa kufukunyua mambo mazito ya ndani kabisa. Mengi yakiwa ni ya siri.

Siku ya siku ilifika, comred Bonta alimtembelea yule binti nyumbani kwake alipokuwa akiishi. Na ndiyo siku aliyogundua kuwa, hapo alipokuwa akililia kila siku, hapa kuwa nyumbani kwake. Bali yeye pamoja an familia yake, walipewa hifadhi ya kujishikiza kwa muda.

“Karibu sana kaka’ngu… karibu sana.” Yule msichana alimlaki comred Bonta kwa uchangamfu wa kujilazimisha, huku akimkabidhi kigoda cha kukalia. Alionekana ni binti mwenye msiba mkubwa moyoni mwake, huku uso wake uliopambwa kwa sura nzuri yenye kuvutia, ulichuja kwa manung’uniko, huzuni, vilio na uchungu.

“Nimesha karibia dadang’u. Habari za hapa?” Bonta alimsabahi yule binti wakati akijiwekea vizuri kigoda alichokabidhiwa tayari kwa kuketi.

“Hapa hatujambo tu, sijui huko kwenu kaka.”

“Huko hali ni nzuri tu dada. Tunamshukuru Mungu kwa kweli.” Bonta alimjibu huku akimtazama usoni kwa makini, kichwani akiwa na maswali chungu mzima. Na alijiapiza, ama kwa hakika vyovyote iwavyo, siku hiyo, ilikuwa ni lazima aondoke na majawabu ya maswali yake kuhusiana na huyo mama mliaji, ambaye sasa alishagundua hakuwa mama mtu mzima, bali binti.

“Hii sura sio ngeni sana machoni mwangu, nahisi nimewahi kukuona, ila sikumbuki ni wapi.”

“Eti eeh…” Comred Bonta alimuitikia. Huku akishangazwa na uzuri wa ajabu wa yule binti. Alikuwa mrembo si haba.

“Inawezekana umeshawahi kuniona, japo sura yako ni ngeni machoni pangu. Mimi siishi mbali. Ni jirani yako mtaa wa pili.” Bonta akajieleza kwa kirefu, akimalizia yale maelekezo yake kwa kuunyosha mkono wake wa kuume, kuelekea uelekeo wa mtaa huo aliojinadi kuwa alikuwa akitokea.

“Hivyo eeh…” Yule msichana alimjibu pia. “Basi inawezekana nilishawahi kukuona kwenye pitapita zangu mtaani humu.” Wakaishia kutabasamu. Ni ndani ya muda mfupi mno, ikawa kama damu zao ziliivana. Wakapatana. Wakaelewana. Na kila mmoja akawa rafiki wa mwenzie.

Comred Bonta hakufanya makosa, akautumia mwanya huo kupenyeza hoja yake. Nia yake ilikuwa ni kutaka kujua, kulikoni jirani yake huyo wa mtaa wa kwanza, alikuwa akilia kila siku usiku na asubuhi…

*****

      Mwezi mmoja baadae, tangu ile siku waliyo kutana Bonta na yule dada mliaji, gazeti la Heka Heka lilivunja rekodi ya mauzo. Tathimini ilithibitisha kwamba, Heka Heka liliuzika kuliko magazeti yote nchini, na lilikuwa likiendelea kuuzika.

     Kisa!

     Makala ya kesi ya Magreth Shemweta.

*****

     Siku moja, mama Rosemarry alimshilikisha shoga yake kipenzi bibie Consolatha Makaranga, habari kuhusiana na makala iliyokuwa ikiandikwa na mjukuu wake comred Bonta, kwenye gazeti la Heka Heka. Kesi ya Magreth Shemweta, mjane wa hayati Brigedia Shemweta, Jemedali wa vita!

      “Nimeisoma makala hiyo, na ninaendelea kuifatilia kila Jumanne kwenye gazeti hilo… kwani wewe na mwandishi wa hiyo makala mna unasaba?” Bibie Consolatha Makaranga alimjibu rafiki yake huyo, akamaliza kwa swali.

      “Ndiyooo…” Mama Rosemarry alimuitikia, kisha akaendelea kumfafanulia. “…Bonta ni mjukuu wangu. Mtoto wa kwanza wa binti yangu Rosemarry.”

       “Wow! Mbona sina hizi habari shoga. Ulikuwa wapi kunijuza siku zote hizo?” Consolatha alishadadia kwa furaha. Ni kama vile alipendezwa mno na ile habari kuhusiana na undugu wa mwandishi wa ile makala, na mpishi wake wa siku nyingi pale ikulu.

      Kwanini..!

      Mimi na wewe hatujui.

      “Haijatokea tu tukalizungumzia hilo shoga, mbona Bonta naishi nae. Ni kijana mdogo tu, ila ni hatari kwenye tasnia ya uandishi wa habari. Mpaka anaonewa donge na wenziye!”

      “Ayaa…! Kumbeee…! Mi sijui wala sijawahi kufikiria. Kwa hiyooo, unaponiambia kuwa unaishi na mjukuu wako ndiye huyo Bonta?!”

      “Haswaaa… na hata huyo mama Shemweta anayeandikwa habari yake kupitia makala iitwayo KESI YA MAMA MJANE, haishi mbali nasisi. Ni jirani yetu, wao mtaa wa kwanza, sie wa pili.” Mama Rosemarry alimfafanulia.

      “Alooo!” Consolatha alishangaa sana.  

      “Kumbe ati…!” Alizidi kushangaa.

      “Naomba unikutanishe haraka sana na comred Bonta… binafsi, nahitaji kuifahamu kwa undani hii simulizi iliyoteka hisia za watu wengi, kesi ya mjane wa hayati Brigedia Shemweta.” Consolatha alimwambia.

       “Hapana shaka shoga’angu. Hilo tu, mbona jepesi kuliko hata kazi yangu ya upishi hapa kwako.”

      (Wakacheka kwa pamoja)

*****

      Siku tatu baadae, comred Bonta aliwasili ikulu ya rais ya Dar, kwa ajiri ya minajiri ya kuonana na first lady wa taifa, mama Makaranga Bruno. Ilikuwa ni fursa aliyoifurahia mno. Akainua mikono yake yote miwili juu na kumshukuru Mungu.

      “Hatimaye leo naonana na first lady wa taifa! Hii ni fursa kubwa  mno. Sina budi kuitumia vizuri.” Alijisemea Bonta wakati akizidi kujitoma kwenye viunga vya ikulu.

     Alionana na mke wa rais, wakafanya mazungumzo marefu kuhusiana na ile makala iliyotikisa na kukonga mioyo ya watu wengi, KESI YA MAMA MJANE, mke wa hayati Brigedia Shemweta.

      Kikubwa zaidi, Consolatha alihitaji aipate ile simulizi kwa undani. Bonta hakufanya hajizi.

      Alimsimulia.

      Akamuelezea.

      Yeye mwenyewe pamoja na kuiandika kwenye makala yake, kesi ile ilimgusa sana, akajisikia faraja kuona hata first lady wa nchi imemgusa. Jambo ambalo hakulielewa, ni kipi mama Makaranga alikikusudia baada ya kuupata undani wa kesi ile…

MIAKA MINGI SANA BAADAE… WAKATI ULIOPO

 

     CID Amos Bwire alipaki pikipiki yake kubwa aina ya Baja, nje ya kituo cha polisi cha kati cha Msimbazi Center Kariakoo. Ilikuwa asubuhi mida ya saa mbili na robo. Wakati huo, taarifa kuhusu barua aliyomuandikia mkubwa wake wa kazi, zilisha enea sana masikioni pa wafanyakazi wenzake, na kuwaacha kwenye mastaajabu.

     Alitembea hatua za kuhesabu, akilielekea jengo la kile kituo cha polisi. Njiani akisalimiana na askari wenzake pamoja na raia waliokuwa wakiingia na kutoa mjengoni mule. Alipofika varandani, hatua chache kabala hajazama ndani, alikutana na askari mwenzake. Swahiba wake.

     “Siamini ninacho kisikia. Hivi ni kweliii… au umbea tu?!” Ndivyo alivyodakwa na CID Imelda.

   “Jamani..! Bila hata salamu Imelda?!”

   “Mjini heshima pesa babu weee, salamu kawasalimie bibi na babu yako hukoooo…  kijijini kwenu Sitimbi. Jibu swali langu tafadhari.” Imelda alimcharukia, safari hii akimshikia kiuno cha kishambenga.

   “Ni kweli. Kama ulivyosikia.” Amos alimjibu kwa mkato. Akataka kuingia ndani, Imelda akamzuia kwa kumshika mkono.

   “Kweli hiyo ‘veepeee…?!” Imelda alizidi kumjia juu kwa maneno ya kumshushua, kwa Kiswahili cha mtaani. “…kwa nini umeamua hivyo Amos?” Imelda aliendelea kumbwatukia kwa kiherehere, macho yaliyoonekana kuhuzunishwa na kitendo kile cha Amos kuandika barua ya kuomba kuacha kazi.

   “Ni maamuzi kama maamuzi mengine ya kawaida kabisa, na nimeyaamua kwa utashi wangu mwenyewe, sijashawishiwa wala kushurutishwa na mtu…” Amos akaanza kumfafanulia kama alivyotaka.

    “Najua namna gani imewastua wengi. By the way hali hii niliitegemea, and am ready to handle it.” Amos alimueleza kama masikhara vile, moyoni akimaanisha.

   “No. This is a movie, and, there must be something behind the scene.” Imelda alimpa maneno yale.

     Nje ya kazi, watu hawa ni marafiki wa kubwa na wa muda mrefu, wanapendana sana, lakini pia, wana aminiana mno. Hivyo, Imelda alikuwa akisadiki, hata kama kulikuwa na sababu ya siri sana, iliyompelekea Amos kuchukua maamuzi yale, alipaswa kumshirikisha, kwa sababu yeye ni msiri wake.

     “Hahahaaa…” Amos alicheka sana baada ya kusikia maneno yale. Kwamba yeye kuacha kazi, ilikuwa ni sinema ambayo ilikuwa na siri iliyojificha nyuma yake. Aliyaelewa vema maneno yale na maana yake. Lakini pia, alilielewa kusudi la Imelda. Imelda alitaka kumchoma moyo kwa maneno adhimu, ili amchochee kuweka wazi kile kilichojificha nyuma ya pazia la maamuzi yake.

      Ni kweli.

     Amos hakuongea neno la ziada. Wakazozana vya kuzozana. Baadae wakaachana. Amos Bwire akazama ndani, akijuliana hari na askari wenzake waliokuwa wakimtazama kwa macho yaliyogubikwa na utata, maswali na mashaka.

     Hakujali!

     Alielewa kwa nini hali ilikuwa vile, hivyo hakuwa na sababu ya kushangaa sana. Ndio maana alimwambia CID Imelda yale maneno, “Najua namna gani imewastua wengi, by the way hali hii niliitegemea, and am ready to handle it.”

     Safari ya kuelekea kwenye chumba cha bosi wake ilikuwa ngumu mno asubuhi ile. Sio kwa sababu ilikuwa yenye milima na mabonde. La Hasha wa Kalla. Wakati mgumu, kwa maneno magumu atakayoelezwa na yule mkubwa wake wa kazi. Na maswali magumu, atakayo ulizwa na kutakiwa kuyajibu. Ajiteteeje? Amuelezeje? Ili apate kumuelewa.

     Anamjua bosi wake naye bosi ana mjua vema Amos. Wana juana! Tabia, hulka na mienendo. Kila mmoja ni mtu makini na kazi, asiyehitaji masikhara. Kwa hiyo basi, hata swala la kutaka kuacha kazi, Amos alijua fika kabisa kwamba, mbele ya huyo bosi wake, alipaswa kujipanga.

     Hakukosea.

     Lakini hakuwa na namna. Alishadhamilia alichokidhamilia, na ilimpasa kuufata moyo wake.

     Akajikuta ameshakikamata kitasa cha mlango wa ofisi ya bosi wake, akajitoma ndani. Akamkuta. Alikuwa ameketi kitini, mbele yake kukiwa na meza kubwa ya mbao ya mseplasi, iliyojazana makarabasha kadha wa kadha. Walipotazamana, bosi wake huyo akaukunja uso kitendo kilichozidi kumtia hofu na kumpunguzia ujasiri CID Amos Bwire.

     “Salama mkuu… habari za asubuhi.” CID Amos alimsabahi bosi wake kwa kusimama kikakamavu na kusaluti.

     “Salama. Pita uketi.” Mkuu wake alimuitikia salamu na kumkaribisha kiti, sura yake ikiwa serious. Amos alijisogeza taratibu mpaka kwenye kiti kilichokuwa mbele ya ile meza, akaketi wakitazamana kiubavu.

     “Unaonekana mwenye mashaka afande. Kuna jambo haliko sawa.” Mkuu wake wa kazi alimsaili kwa udadisi wa kisaikolojia.

     “Hapana mkuu. Pasina shaka niko njema kabisa. Nadhani ni mtazamo wako tu.”

     “Una uhakika?”

     “Naam mkuu.”

     “Jana nilikuagiza leo ulipoti ofisini kwangu mala tu utakapofika kazini. Na ndivyo ulivyofanya. Good.” Mkuu wa kazi aliendeleza mazungumzo.

     “Amos…” Akaendelea. Amos alipomsikia akilitaja jina lake, hakumuitikia. Badala yake aligeuza shingo kutazama ukutani alikokuwa ameelekeza macho yake. 

      “Umekuwa nami kazini kwa muda mrefu. Nakujua nje ndani ndani nje kama kiganja changu cha mkono.” Alitamka yale maneno huku akikigeuzageuza kiganja cha mkono wake wa kuume, kisha akautazama sana upande wa mbele wa kile kiganja.

     Akasimama, akaanza kutembea tembea mule ofisini.

     “Wewe ni askari shupavu, mwerevu, mdadisi na mjanja sana.” Akakohoa kidogo.

     “Nataka uniambie… unadhani nini lilikuwa kusudi la mimi kukuita asubuhi hii ofisini kwangu.”

     Kwa mara ya kwanza, Amos alijikuta akimgeuzia uso na kumtazama yule askari mwenye cheo cha Superintendent. Kwa sekunde chache sana alipiga kimya, kabla haja fungua kinywa chake kumjibu.  

     “Nachelea kujibu swali lako mkuu, kwa sababu nahisi umekusudia kunitega ili ninase. Lakini pia, nikisema sijui, ntakuwa muongo. Na uongo, sio desturi yangu, we mwenyewe ni shuhuda. Nnacho dhani, ni mashaka uliyonayo juu ya ombi langu nililoliainisha kwenye barua yangu niliyokuandikia.” CID Amos alimjibu kwa kirefu.

     “Good.” Mkuu alimjibu huku akimtazama kwa matumaini, japo haikumuwia wepesi Amos kuhisi ni aina gani ya matumaini aliyokuwa nayo bosi wake juu yake wakati ule.

     Akaendelea. “Ndio maana awali nilipokwambia, wewe ni askari shupavu, mwerevu, mdadisi na mjanja sana. Sikuwa nikikudhihaki, au nikikusanifu, ama kuku enjoy. I was serious, serious from my heart.”

    Superitendent Kamuli akamsaili tena. “Now tell me my good friend…what’s wrong with you mpaka umedicide kuacha kazi?”

     CID Amos kimya!

     “Anyway.” Superitendet Kamuli akaendelea.

      “Hatima ya maisha yako, ipo mikononi mwako. Mwamuzi wa mustakabari wa maisha yako, ni wewe mwenyewe. Hapana mtu mwenye nguvu ya kukuingilia. Labda kama utakiuka au kuvunja sheria, taratibu au katiba ya nchi.” Akatumia vidole vya mkono wakuume kuzifuta pua zake kwa mikupuo miwili, zikiambatana na kutoa sauti ya kamasi. Kisha akaendelea.

      “Hapo dola, au serikali, itakuwa na nguvu, mamlaka, na uwezo wa kuingilia na kuamua juu ya maisha yako.” Akavuta kiti kingine kilichokuwa kando, akakisogeza na kukitazamasha nakile alichoketi Amos.  Akaketi huku akikunja nne kwa utulivu mkubwa. Sasa wakawa wakitazamana uso kwa uso kwa uzuri kabisa.

     Akaendelea kwa sauti ya upole uliopitiliza, na utulivu wenye ushawishi. “Sitaki tuongee kama staff na mkubwa wake wa kazi. Nataka tuongee kama ndugu. Kama marafiki. Kama mtu na jamaa yake waliyeshibana. Kama kaka na mdogo wake. Talk to me as your blood brother, dare to take me as your spause, niweke wazi usinifiche, wala usinieleze ulichokiandika kwenye barua uliyoniandikia. Niambie ulichokibeba moyoni, duniani tunahitaji wasaidizi wa kubebeana mizigo, na katika hili, kwa ajili yako, wallah naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu nipo tayari. Kwa nini unataka kuacha kazi? Kazi yako ya upolisi. Uliyoisomea kwa msoto mkubwa! Umeipata! Leo unataka kiacha ukiwa na muda mfupi mno tangu uipate. Why Amos…why?!”

     Amos alishusha pumzi ndefu. Wakati mgumu aliokuwa akiuhisi kukutana nao wakati akiiendea ofisi ile, ndio kama huo. Na ama kwa hakika alikuwa kwenye wakati mgumu, wa kujileza na kujitetea. Akapiga moyo konde, akamjibu.

     “Tofauti na sababu niliyoiainisha kwenye barua niliyokuandikia…” Akameza mate kidogo, kisha akaendelea, “…hakuna cha zaidi.”

     Mkuu wake alimtazama kama anayeisoma akili yake, kabla hajatamka sentensi iliyomuacha midomo wazi.“There is a hidden truth under the carpet.” (Kuna ukweli uliojificha chini ya kapeti)

      Khaa!

      Amos hoi…

      Papo hapo Superitendent Kamuli aliamka na kurejea kwenye kiti chake, akaketi. Amos akagwaya. Akapata mstuko wa waziwazi. Ile sentesi. Yale maneno. Yalishabihana na yale aliyomaliza kuyasikia kutoka kwa CID Imelda, muda si mrefu wakati akiingia pale kazini. “…there must be something behind the scene.”

     Wakati kumbukumbu hiyo ikizidi kukivuruga kichwa wake, bosi wake alikuwa akivuta trei ya kuhifadhia mafaili iliyokuwa juu ya meza, ikiwa imesheheni makarabasha lukuki. Kutoka kwenye yale makarabasha, alichomoa bahasha ya kaki yeye ukubwa wa A4.

      Akamkabidhi na kumtaka aipitie akiwa palepale. Ndivyo alivyofanya. CID Amos Bwire hakuamini. Jeshi la polisi lilikuwa limemkubalia ombi lake la kuacha kazi, na kumpa baraka zote. Akanyanyua mikono yake yote juu, akamshukuru Mungu.

      Lakini…

      Huwezi kuamini, furaha hii ilidumu ndani ya dakika tano tu, na dakika ya sita baadae, hali ilikuwa tofauti kabisa, kila kitu kilimgeuka CID Amos Bwire, na kumuacha kwenye mshangao usio na kifani.

      Ama kwa hakika, hakuamini kilichotokea!

*****

       Wiki moja kabla Amos Bwire hajaenda kukutana na Superitendent Kamuli ofisini kwake, alikuwa amewasilisha barua kazini kwake ya kuomba kuacha kazi yake ya upolisi.

       Hatua hii ilimstua kila mfanya kazi aliyemfahamu Amos.

       Haikuwa dhambi.

       Lakini…

       Swali ni, ‘kwa nini aliamua kuacha kazi.’

        Alifahamika kama askari polisi mwenye adiri na kazi yake. Mwenye haiba ya utumishi uliotukuka. Jasiri, hodari, aliyetekeleza majukumu yake kwa uaminifu mkubwa, mwema, asiye na makuu, mwenye utu wema na aliyejua kwa nini alikuwa polisi.

      Katika hali ya kawaida, kutokana na mahaba aliyokuwa nayo kwenye kazi yake hiyo ya upolisi, aliyoitumikia na kupandishwa vyeo mara kadhaa, tena ndani ya vipindi vifupi vifupi, mpaka hatua ya u-inspekta, isingekuwa rahisi kudhani Amos angewahi kufikilia kuachana na upolisi. Lakini eti ghafla, akaomba kustaafishwa.

     Kwanini.

     Na ni hapo ndipo alipougundua umuhimu wake katika jeshi hilo, lenye dhamana ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

    Wakubwa wake wa kazi walimkatalia katukatu. Sio kinafiki. It was serious… hakuna aliyetaka Amos aache kazi.

    “Jeshi la polisi bado linakuhitaji kaka, ni mapema mno kuamua maamuzi hayo…” Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam alimbebeleza wakati wakijadiliana kuhusu swala hilo. Walikuwa ofisini kwa kamanda.

      “Ni kweli mkuu, lakini no way, inanipasa kustaafu sasa, niangalie hamsini zangu. Ni kwa mapenzi mema tu.” CID Amos alimjibu.

       “Mapenzi memaaa…!!!? What kind of mapenzi mema are you talking about? Mapenzi yako mema ni kubaki kazini, na kuendelea kulitumikia taifa, kwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.” Kamanda alimjia juu kwa uchungu mkubwa, usoni akionekana dhahirimoyo wake haukuwa radhi kumpoteza yule kijana.

      “Amos wewe ni jembe lifaalo katika nyakati zote na misimu yote. Haijalishi ni masika, majira ya vuli au kiangazi. Unaweza kulima. Try to think twice please am beging you.”

     “It’s too late to think sir… it’s my in due time to move forward…” (Muda umeenda sana kuendelea kufikiri kaka mkubwa… ni wakati wangu sahihi kusonga mbele) CID Amos alimjia juu kamanda .

     “And it’s too early to call your desire brother, let’s get more time to meditate about it.” (Na pia ni mapema mno kuya thibitisha matamanio yako kaka, hebu na tupate muda zaidi kutafakari kusiana na hili) Kamanda Ignas alimkata maini. Siku hiyo, mpaka wanaagana, hakukuwa na maamuzi rasmi yaliyofikiwa kuhusiana na ile agenda. Na hakukuwa na maamuzi rasmi kwa muda wa juma zima, mpaka ile siku Amos alipoelekea kwa Superitendent Kamuli, na kukabidhiwa barua ya ridhaa ya kuacha kazi. Amos alifanya furaha na shangwe baada ya ombi lake kupitishwa.

     Lakini…

     Kilichofatia muda mfupi sana baadae, kilimfanya Amos ahisi kuwehuka.

*****

     Aliondoka ofisini kwa Superitendent Kamuli, akampigia simu swahiba wake, Inspekta Imelda, akamtaka wakutane nje, ili amshirikishe furaha yake hiyo. Imelda alitimu pale viwanjani, wakaanza kupiga stori zile.

     Ni marafiki walioshibana, furaha ya Amos isingeweza kukamilika kama hakumshirikisha Imelda, wala furaha ya Imelda isingekuwa na maana kama Amos asingeishiriki. Vivyo hivyo katika majanga, changamoto na matatizo ya hapa na pale.

     Wakati wakiendelea kupeana michapo, mara simu ya Amos iliita, alipoitazama, akamfahamu mpigaji. Alikuwa ASP Ignas.

      “Nakuhitaji ofisini mara moja afande.” ASP alimueleza baada ya kujuliana hali. Hakusita, akamueleza best yake kuhusu ile dharula, na kumtaka radhi. Imelda hakuwa na hajizi, akamruhusu aende zake. Alipiga hatua kuelekea mjengoni, akashika kolido na kuuendea mlango wa afisa yule wa polisi, ambaye pia ndiye alikuwa mkuu wa kituo. Akajitoma ndani.

      “Oh! Retired police, your welcome.” (Oh! Polisi mstaafu, karibu)

      “Thanks.” (Ahsante) Amos alimjibu huku akielekea kitini alipokuwa akielekezwa kwa ishara ya mkono na mwenyeji wake. Alizoea kumchukulia kama bosi wake wa kazi, lakini haikuwa hivyo kwa wakati huo. Alijitazama kama polisi mstaafu, na hakuwa chini ya madaraka ya mtu yeyote.

       Alijidanganya.

       ASP Ignas Makame alimkabidhi kijana wake karatasi ya walaka aliyokabidhiwa na Kamanda mkuu wa polisi wa kanda maalumu, RPC Kulindwa.

       Akiwa humo ofisini kwa ASP Ignas Makame, ilimchukua dakika tano Amos Bwire kuusoma mara mbilimbili ujumbe mfupi uliotumwa kwa njia ya barua pepe na Ispekta jeneral Kamugisha Atilio, na kadri alivyokuwa akiusoma nao kumuingia barabara akilini, jasho jingi lilimvuja mwili mzima.

      Ujumbe ule ulisomeka;

      Kwa RPC Kanda maalumu, nimetengua uamuzi wako wa kuridhia ombi la kuacha kazi ya upolisi la askari wako CID Amos Bwire, mpaka hapo maamuzi au ridhaa kutoka kwangu itakapokufikia. Kwa muda huu na kuendelea, CID Amos Bwire aendelee na majukumu yake kama Inspekta.

     Tafadhari zingatia, maamuzi haya yataendelea  mpaka hapo maamuzi au ridhaa kutoka kwangu itakapokufikia.

Nashukuru kwa ushirikiano wako.

IGP

Saini ya IGP

    CID Amos alifadhaika sana baada ya kufika tamati ya ujumbe huo, aliusoma mara tano ili kujiridhisha na kile kilichoandikwa. “Oohh… nooo!!! This is not fair jamani, why so?!” (Ooh… hapanaaa!!! Hii sio haki jamani, kwa nini hasa) CID Amos alinung’unika waziwazi, alivikusanya pamoja vidole vya mkono wake wa kushoto na kufanya ngumi, akaipiga mezani.

    “Cool down young man, hayo ndio maamuzi ya wakubwa, yakupasa kuvuta subira.” Kamanda Ignas  Makame alimtuliza jaziba.

      “Kwani tatizo ni nini hasa… kwa sababu nimefata taratibu zote za kustaafu ajira kwa mujibu wa sharia ya ajira. Kwamba, niko tayari kumlipa mwajiri wangu mshahara wa mwezi mmoja, kwa mujibu wa kustaafu ndani ya saa 24. Sielewi hii milolongo inatoka wapi. Am wondering.” Amos alilalamika,lakini haikusaidia kitu. Akavuta subira, siku zikakatika, haikumzalia matunda. Kila alipojaribu kuulizia maamuzi yaliyofikiwa juu ya ombi lake, mambo yalikuwa yaleyale. Hatimaye akakata tamaa, akapitisha maamuzi magumu.

     Hakwenda kazini kwa muda wa miezi mitatu mfululizo bila kuomba ruhusa, aliporejea, alikabidhiwa barua ya kustaafishwa kwa lazima. Kutokufika kazini miezi mitatu mfululizo bila taarifa, ni kinyume cha sheria ya ajira, na ni kosa linalompatia uhalali muajiri kumtimua kazi mfanyakazi wa namna hiyo. Hivyo ndivyo CID Amos Bwire alivyo fanikisha azima yake ya kuacha kazi.

    Ili kuziba pengo la Amos Bwire, Inspekta Jenerali wa polisi, IGP Kamanzima alimpandisha cheo askari polisi kutoka kituo kikuu cha Temeke Chang’ombe, wa kitengo cha Criminal Identification Department, CID Borry Kihemba, na kuwa Inspekta, kisha akamuhamishia kituo cha polisi Msimbazi Kariakoo.

    Lakini…

    Kitu ambacho Borry mwenyewe na askari wenzake hawa kukifahamu ni kwamba, kulikuwa na siri nzito sana iliyojificha nyuma ya pazia la uteuzi huu.

*****

Nilijiona niko jehanamu baada ya kukata roho. Ufahamu wangu ukanithibitishia ya kwamba kweli nimekata roho. Sikuweza kufumbua macho, kitendo hicho ndicho kilicho niongezea uthibitisho kwamba, sikuwa hai tena. Nilikuwa nimekufa. Marehemu. Niliyelala usingizi wa milele, na katu nisingeamka.

Doh!

‘Sio kweli’ Niliipinga nafsi yangu.

‘Kweliii…unakataa nini sasa. Haupo tena kwenye ulimwengu wa walio hai, wewe ni mfu Kila.’ Nafsi ikazidi kunithibitishia. ‘Aisee, kweli nimekufa. Aloo..! Kumbe mtu akifa anakuwa namna hii…anajitambua, lakini…lakini hawezi tena kujidhihirisha kwenye ulimwengu wa walio hai… ayaaa…’

Daah!

Nilisononeka sana. Sikutaka kufa nikiwa bado kijana namna ile. ‘Sasaaa…kama nimeshakufa niko wapi sasa..?! Mbinguni.., jehanamu au kuzimu… Mboo-mbo-mbo-nna-ka-ma sielewi elewi jama-ni. Mungu na malaika wako wapi sasa…mboo…n…n..na sa…sa…siwa..ooo..nii..oohhshiii?’ Hakika nilihuzunika.

Lakini…

Nilikuja kupata fahamu.

Ikiwa ni wiki ya pili baada ya lile janga la Ubungo external, maelezo haya, ni kwa mujibu wa madaktari wa hospitali ya dokta Kairuki ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Nilikuwa hoi bin taaban, sijiwezi. Hakuna nilichokuwa nikikielewa, wala sikuwa na kumbukumbu za moja kwa moja kuhusiana na maswahibu niliyokumbana nayo. Nilichokuja kukigundua ni kwamba, nilikuwa pale nikipatiwa matibabu chini ya uangalizi mkubwa.

Kumbe sikufa!

Ilianza kama ndoto, kama kweli. Ulikuwa ni utata mtupu. Nikaanza kugutuka usingizini kwa taabu… kwa taabu kwelikweli. Nikawa kama ninaye lazimisha kufumbua macho, nayo yakawa yakikataa katakata kufumbua. Hivyo hivyo kwa taabu, nikajilazimisha, hatimaye yakakukabali kufumbua.

 Kwa mbali nikaanza kupata ufahamu na kuona vitu. Lakini macho yalikuwa mazito, kama vile wingu zito lilitanda mbele na kuyafunika.

“Pole sana rafiki!” Sauti nzuri ya kike ilinisemesha. Nikageuza shingo kuitazama, alikuwa ni binti aliyevalia joho la wauguzi. Ndipo nilipogundua nilikuwa hopitalini.

“Nashukuru.” Nilimjibu kwa taabu, huku nikiangaza huku na kule. Kweli, nilikuwa kwenye chumba kidogo cha kulaza wagonjwa binafsi, (private ward)

“Nimefikaj…” Sikumaliza kumuuliza swali nililotaka kumuuliza, akaniwahi.

“Ngoja nikuitie mwenyeji wako mzungumze vizuri.” Aliyasema hayo huku akigeuka kuelekea mlangoni, akafungua kitasa akatoka zake nje.

Ilichukua dakika kumi baadae, niliposikia mlango wa ile wodi ukifunguliwa.

“Aisee, Mungu mkubwa! Hatimaye umerudi duniani. Hii ni ajabu na kweli.” Sauti ya kiume isiyo nzito wala nyepesi ilinisemesha. Kwa taabu nikajitahidi kuelekeza uso wangu kwa mtu aliyenisemesha. Alikuwa ameshaingia wodini, akasimama kando ya kitanda nilichokuwa nimelala.

“Ha-ti-maye nimerudi..?! Ku-ku-to…ka wapi te…na?!” Nilimuuliza wakati nikijenga utulivu huku nikimtafuta kwenye kumbukumbu zangu. Sikumkumbuka.

Alikuwa mrefu, mwembamba, mweusi, mwenye rafudhi ya kihaya. Nilibaini hakuwa muuguzi kutokana na mavazi yake. Alikuwa nadhifu kwa suti iliyomtoa chicha.

“Ulikuwa mfu wewe.” Aliniambia.

‘Khaa!’ Nilistaajabu.

‘Nilikuwa mfu…halafu ikawaje…nimefufuka katika wafu, ama?!’

“Kwa hiyo sasa hivi sio mfu tena…”

Yup. Mwenyewe si unajiona uko hai tena.” Jamaa alinijibu sikujua kama alijua ni kwa kiasi gani majibu yake yalinitisha.

“Hongera sana jamaa…huwa nasikiaga tu kwamba kuna wanadamu wenye roho ngumu kama ya paka. Ama kwa hakika sasa nimesadiki, sio kwa kusikia tena, bali nimeshuhudia. Wewe ni mmoja wao.”

‘Khaa…anaongea nini huyuuu…mbona simuelewi.”

“Kwani niko wapi hapa… nimefikafikaje… na ninafanya nini hapa… mbona sikumbuki namna nilivyofika hapa. Na…na…mbon…a maumivu yanauchonyota sana mwili…wangu?”

“Upo hospitali ya dokta Kairuki… almaarufu kama Kairuki memorial. Uliletwa ukiwa kwenye hatua ya mwisho ya kutokurejea, yaani hatua ya kifo.”

“Whaaattt…hatua ya mwisho…hatua ya kutokurejea… hatua ya kifo ndio hatua gani tena jama…!” Nilimsaili yule mwanaume.

“Exactry…it was a point of no return…that is a point of death…Pole sana swahiba.”

‘Swahiba?! Tangu lini…’

“Na wewe ni nani kwanza… nimeambiwa naitiwa mwenyeji wangu… ndio wewe?”

“Yup. Ndio mimi.”

“Mwenyeji wangu wa wapi…?”

“Mimi ni raia mwema, hautaksea ukiniita msamalia.”

“Sijakuelewa.”

“Mimi ni mwenyeji wako wa hiyari hapa hospitalini. Pia niko na wenzangu ambao kwa sasa hawapo, wao utawaona hapo baadae. Sisi ni wasamalia wema, tuliokunusuru na balaa kubwa… ulikuwa ufe wewe.”

‘Ni kweli…haukuwa umepita muda mrefu tangu nijihisi niko kwenye ulimwengu wa wafu.’

“Nini kimetokea…ni kipi hasa kimenipata, mpaka niko hapa naugulia maumivu makali namna hii…”

“Pole sana Kilandika… kwa hivyo haukumbuki chochote kilichokupata kabla haujazinduka kutoka kwenye huu usingizi?”

‘Na jina langu unalijua…makubwa…’

“La Hasha! Abadani asilani…sina nikikumbukacho…kwan…i…ni…ni…kimeni…tokea…jama…ni…Haya maumivu haya viipii…oohshhiii…”

Nilikuwa najaribu kujigeuza mgongo, kutokana na maumivu makali sikuweza.Yule jamaa aliniinamia upesi sana, akanikamata mabega akinizuia nisijigeuze.

“No-no-nooo…usifanye hivyo Kila, utajitonesha halafu uzue balaa jingine, tulia hivyo hivyo, nitakueleza kila kitu, naamini, utakumbuka yaliyokusibu.”

Kweli.

Alinisimulia mkasa ulionikuta pale Ubungo external. Ndipo nikakumbuka kila kitu. Kila kitu kilichosababisha niwe pale kwa dokta Kairuki nikiwa katika hali ile kikanifunukia.

Aiseee, ilikuwa ni balaa.

*****

Miluzi ilivuma stendi nzima ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo external. Ilikuwa mishale ya saa sita mchana, wakati basi la Lushanga mali ya kampuni ya Lushanga bus service, likiingia kwa spidi kali.

Nyuma ya usukani aliketi dereva machachari aitwae Majeshi, aliyejipatia umaarufu kwa uendeshaji wake wa mwendo kasi pengine kuliko madereva wengi wa mabasi ya mikoani. Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa muhasisi wa kampuni hiyo, marehemu Lushanga.

Haukuwa muda wa kawaida kwa basi hilo lililokuwa likitokea Geita, kipindi hicho ikiwa wilaya kabla ya kupewa hadhi ya mkoa. Bali lililazimika kuchelewa kutokana na dharula mbaya ililolipata lilipokuwa njiani. Dharula iliyowapelekea wenyeji wa ile stendi kuu kulipokea kwa shangwe za miluzi wakati likiingia viungani hapo. Kwani walikuwa na taarifa ya maswahibu yaliyolisibu basi hilo.

Madereva wa mabasi mbalimbali, makondakta, mateja na wafanya biashara wadogo wadogo wa stendi hiyo, walilikimbilia huku wakilizingira basi hilo, huku wakimlaki kwa shangwe na heko Majeshi alipokuwa akiteremka.

“Hongera Majeshi.” Alipokea pongezi nyingi.

Abiria nao wakatelemka, nyuso zao zikiwa zimesinyaa, wasiamini juu ya ile salama waliyokuwa nayo wakati huo, baada ya kufanikiwa kuupita usiku wa jana yake uliogubikwa hekaheka za kutisha.

Abiria wote waliteremka, kasoro mimi niliyekuwa nimeegemeza kichwa changu kwenye kioo cha dirisha lililopakana na siti niliyokalia.

‘Oh, hatimaye nimefika salama salimini…’ Nilijisemea kimoyo-moyo baada ya kugutuka mawazoni. Akiri ilikuwa mbali, kichwa kiliniwia uzito sanjari na mpwito wa maumivu yaliyosababishwa na mawazo chungu mzima yaliyonikanganya.

Safari nzima, akiri haikunipoa kwa kuwaza na kuwazua mambo kadha wa kadha yaliyougubika ubongo wangu. Mambo mbalimbali ya kutisha niliyokumbana nayo Geita nilikokuwa naishi. Adhima ya ile safari na mambo niliyotegemea kukabiliana nayo jijini Dar.

Hatimaye nilikuwa nimefanikiwa kuingia mji niliopaswa kuingia. Dar, jiji la raha na karaha. Katika kukua kwangu, sikuwahi kufika hata mara moja hapo kabla, ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka ishirini tangu kuondoka kwangu.

Unaweza kujiuliza namaanisha nini? Au je, niliwahi kuishi Dar hapo kabla. Jibu langu ni ndiyo. Na sio tu kuwahi kuishi, mimi ni mzaliwa wa Dar. Nimelelewa Dar nikiwa mtoto mdogo, kabla sijaondoka na kwenda kuishi mbali kabisa nje ya mji huu. Kabla sijaenda kuishi  mafichoni. Na siku hiyo ya ujio wangu njini humo, ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia mkoa huo maarufu wa kibiashara. Sasa nikiwa mgeni wa mji.

Ujio wangu ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kumpa msaada wa kiuwokozi mtu muhimu sana maishani mwangu. Mtu aliyekumbana na madhila magumu kuyasimulia.

Kijana jabari, mrefu, mweusi, mwenye mwili wa wastani ulioimarika kimazoezi, Kilandika Mwampachu a.k.a. Kila, niliinuka kwenye siti yangu iliyokuwa mstari wa tatu kutoka siti ya mwisho wa basi, nikajinyoosha nyoosha viungo vya mwili wangu ili kupunguza uchovu. Kisha nikapeleka mikono yangu kwenye kelia ya kuhifadhia mizigo, nikavuta begi langu nililolihifadhi hapo kama wafanyavyo abiria wengine.

Nikafanikiwa kulitoa. Lilikuwa begi aina ya Volcano, lenye ukubwa wa wastani, lisilokuwa na dalili ya kuwa na mizigo mizito. Na kwa hakika halikuwa na vitu vingi ndani yake. Nilikuwa nimesafiri kisela.   

Niliupeleka mkanda wa lile begi begani, nikalining’iniza hapo. Mpaka muda huo abiria wengi walikuwa wamekwisha kuteremka. Alimanusura ningejikuta niko peke yangu garini. Hali hiyo ilinishitua kidogo, nikabaini kwamba nilikuwa kwenye lindi zito la mawazo. Ndipo nilipoadhimia kuishurutisha akiri yangu iondokane na hiyo hali. Kwani mawazo mengi namna ile, yangeweza kunisababishia hatari kubwa mbeleni.  

Nilikuwa ndani ya kaptura ya kitenge iliyonimpendeza sana. Nilivaa shati la kitenge hicho-hicho, iliyonikamata mwili vizuri na kuyachora vema maungo yangu yaliyo katika kwa mazoezi.

Chini nilivaa viatu vya wazi au sandals. Kofia aina ya kapelo niliigesha juu ya rasta zangu nyingi zilizosokotwa kiume na kuning’inia upande wa nyuma wa kichwa. Kwenye mkono wa kushoto nilivaa saa ya kacha,  na bangiri za kacha moja moja kwa kila mkono. Shingoni pia nilizingirwa na mkufu wa kacha. Ama hakika nilikuwa mpenzi wa vitu vya asili au kacha.

Nilivutia sana siku hiyo, hasahasa kwa muondoko wangu wa kunesanesa kwa kushtua mguu mmoja kisha kuuvuta kama mtu aliyeteguka. Ni miondoko iliyopendelewa sana kutumiwa na wanamuziki wa hiphop au rap, hususani wamarekani weusi.

Kijana nilikuwa brother men, si mchezo.

Nilishuka ngazi za basi lile na kufanikiwa kutoka nje. Usoni nikang’ara zaidi nilipopigwa na jua kali la utosini, lililokuwa likilitokosa jiji la Dar na kupelekea fukuto lenye kukera.

Nilishuhudia namna stendi ile ilivyosheheni mabasi yaliyopangana kwa mistari.

Nje ya basi, mazungumzo juu ya sekeseke lililotuhenyesha usiku wa safari yalishamiri. Dereva Majeshi alishapongezwa na raia pamoja na abiria mpaka kichwa kikamvimba kwa wingi wa sifa.

Upande wangu, mazungumzo yale hayakuwa na umuhimu tena. Wahenga walisha sema yaliyopita si ndwele. Kwa wakati huo, nilihitaji zaidi kuganga ya mbele. Akiri yangu iliyoanza kuitii adhima yangu ya kupunguza mawazo, ilikuwa ikifikiri kilichopaswa kufatia wakati huo.

Ndipo nilipoyapenya yale makundi ya watu yasiyokaukiwa mjadala wa lile sekeseke, nikasogea kando kidogo ili nipate nafasi nzuri kupiga simu niliyopaswa kuipiga, kwa ajili ya hatua iliyotakiwa kufuatia.

Niliomba maelekezo kwa wenyeji wa ile stendi, ili nilipate lango la kutokea nje. Sikuwa mwenyeji wa jiji, kama nilivyotangulia kusema hapo awali. Katika kukua kwangu, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia Dar.

Nilikuwa mgeni wa mji.

Nikaelekezwa. Katika kufuata maelekezo niliyopewa, nilijikuta nimeuacha upande wenye mabasi. Nikasimama kwenye uwazi mpana.

Mbele yangu niliona mielekeo miwili iliyokuwa ikitumiwa na raia kufata malango ya kutoka nje. Uelekeo wa kwanza ni njia iliyoelekea Kasikazini mwa stendi, mwingine ulielekea mashariki mwa stendi. Ule upande wa Mashariki nilitazamana na vibanda kadha wa kadha vya biashara mbalimbali.

Niliduwazwa na ukubwa wa ile stendi, sikuwahi kuona stendi kubwa namna ile hapo kabla. Pilikapilika zilikuwa nyingi, na kulikuwa na kila dalili kwamba, nilikuwa ameingia kwenye mji wenye mishemishe nyingi…kama nilivyowahi kusimuliwa na baadhi ya watu siku za nyuma.

Nikakipeleka kiganja cha mkono wangu wa kuume kwenye mfuko wa kaptura yangu, nikaikamata simu yangu ya mkononi. Wakati nikiichomoa, kabla sijaipeleka usoni ili kupiga, ghafla, macho yangu yaligongana na macho ya dada mmoja mrembo sana, aliyekuwa akinitazama huku kiganjani akichezea simu yake, iliyounganishwa masikioni kwa kutumia ear phone. Mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata mshikio wa sanduku lake la matairi alilolisimamisha.

Wote tukajikuta tukibasamu.

Kwa mara nyingine, Kila mimi, nikafanikiwa kuona kitu cha kipekee mno kwenye kinywa cha yule dada. Mwanya wake…

Aloo…!

Alikuwa ni msichana mzuri mno, mwenye weusi wa rangi ya chokuleti. Si mrefu sana wala mfupi sana. Mwenye mwili wa wastani usiokinaisha kuutazama.

Kutokea pale alipokuwa amesimama, suruali yake ya jinzi rangi ya bluu iliyoiva, yenye matundu magotini kama iliyocharangwa na viwembe, sio kwa bahati mbaya, bali mtindo wa kisasa kwa vijana wa kizazi kipya. Fulana kubwa nyeupe, yenye picha ya mwanamuziki mahili wa miondoko ya Regge, Hayati Lucky Dube. Sweta lake kubwa la rangi ya kijivu alilojifunga kiunoni na kuliacha likining’nia kwenye makalio yake, na raba zake nyeusi zenye michirizi miwili myeupe kila moja, vilimpendeza sana.

Kitambaa kikubwa, chekundu chenye madoa meupe alichojifunga kichwani, hakikuweza kuzificha dredi zake nyingi alizozisokota.

‘Mh…! Huyu mtoto ni shida…’   Nilijisemea kimoyo-moyo wakati miguu yangu ikichapua kumuendea bila hata kujishauri mara mbili.

Namna tulivyokuwa tukitazamana, macho yetu yalikuwa yakiongea kitu. Ile tazamaji ya yule mlimbwende haikuwa ya kawaida, na iliambatana na aibu ya kike yenye kiashiria cha hali fulani ambayo kwa Kila mzee wa totozi, haikuniwia ugumu kuelewa kitu kilichokuwa kikipita akirini mwa yule msichana.

Sasa basi…wakati nikipiga hatua taratibu kumuendea yule mrembo mwenye macho makubwa kama golori, simu yangu ikaita. Nilipoinua mkono kuitazama, nikashituka. Ghafla ikanibidi nisitishe hatua zangu, nikaipokea huku nikigeuza uso huku na kule kwa kuhisi kwamba, huenda mpigaji hakuwa mbali nami.

Sikukosea.

Nilipoipokea tu, nilisikia sauti ya mpigaji ikinielekeza nitazame upande wa Kusini mwa stendi kutokea uelekeo wa Mashariki niliokuwa nikielekea. Nikageuza shingo na kufuata maelekezo.

Nilifanikiwa kumuona dada mmoja mzuri sana. Mrefu, mwembamba, aliyevalia gauni zuri la kitenge lililokomea magotini huku likimkamata vema mwili wake. Akiwa ameushikilia mkono wa mtoto wa kiume mwenye takribani miaka saba hivi, alinipungia mkono. Nikaujibu kwa kumpungia mkono wangu wa kushoto vilevile.

Nikatamani nivuke njia za mabasi zinazokatisha mule stendi ili nimkurubie, lakini nilisita. Kumbukumbuka zilinijulisha kwamba, pembeni yangu, umbali wa takribani mita ishirini hivi, kulikuwa na mrembo niliyekuwa nikimuendea, na pasina shaka yule bibie naye alikuwa akiningoja. Nikageuka kumtazama. Tukatazamana. Jibu likawa kwamba yule bibie kule alikokuwa alikuwa akinigoja.

Nikapagawa.

Huku mrembo mwenye dredi ananingoja. Kule mrembo mwenye mtoto ananingoja. Wote nawahitaji. Na wote ni muhimu kwangu, japo si kwa namna udhaniavyo wewe. Pole weee.

Ninze na yupi nimalize na yupi, nilitatizika.

Wazo la utatuzi wa ule utata likapita kichwani mwangu chapuchapu. Kwamba yule niliyekuwa nikizungumza naye simuni nimuagize anifate kule nilikokuwa. Kwani ilikuwa ni rahisi sana kumpoteza yule mwenye dredi kichwani kuliko yule mwenye mtoto. Ndivyo nilivyofanya, kwa ishara tuliafikiana na yule mwenye mtoto, niliyekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu.

Wakati huo, mrembo mwenye rasta alikuwa akifatilia yale mawasiliano ya ishara kati yangu na dada mwenye mtoto. Yalifanyika kwa ishara za mikono pamoja na vichwa. Ni kama aligundua namna nilivyotatizika baada ya kumuona yule dada wa upande wa Kusini, lakini alivuta subira aone ntakachoamua.

Ndipo alipoadhimia kuendelea kunigoja aliponiona  nikimwita kwa ishara ya mkono yule dada mwenye mtoto, naye akiafikiana nami kwa ishara ya kutikisa kichwa.

Ni muda huohuo, kutokea kule kule walikokuwa wamesimama wale wadada kila mmoja kwa upande wake, kwa pamoja walitahamaki na kupigwa bumbuwazi, macho yakiwakodoka kwa wahka usio elezeka baada ya kuona walichokiona.

Nikiwa sina hili wala lile, umakini wangu ukiwa imevurugwa na wale mabinti wawili wakali, nilipigwa kikumbo kikubwa mgongoni na mtu ambaye sikuwa amemuona, simu yangu ikakwapuliwa kwa nguvu, na kunisababishia maumivu makali sehemu kadhaa za mwili wangu kutokana na lile tukio la kushitukiza.

“Yalaaa…oooh, Mungu wanguuuu…” Yowe la mpagao lilimtoka yule binti mwenye mtoto wakati akimshuhudia yule kibaka akinivamia na kutimka mbio. Vivyo hivyo dada aliyesokota rasta, alijikuta akipiga kelele za hamaniko huku akinisikitikia kwa namna nilivyowahiwa na yule kibaka. 

Yule kibaka alinichezea rafu mbaya sana, niliweweseka huku nikijitahidi kuuzungusha uso wangu huku na kule haraka-haraka ili mwizi wangu asinipotee usoni.

Nilifanikiwa kumuona. Ni bwana mdogo tu, mwenye afya mgogoro, aliyeonekana kuathiriwa na utumiaji wa madawa ya kulevya, alikuwa akitokomea kwenye uchochoro fulani uliosababishwa na mistari ya mabasi yaliyopangana pale stendi.

‘Nakula na wewe sahani moja…’ Sikukubali ujinga. Nikafanya maamuzi ya kumkimbiza bila kufikiri mara mbili. Dakika moja baadae, nilijikuta kwenye ukanda wa majuto mazito, laumu, kilio na maumivu makali. Nikiona bora hata nisingeifukuzia simu yenyewe. Alimanusura yangu, ile simu initoe roho.

Yule kibaka alikuwa mwenyeji wa ile stendi, hivyo haikumpa tabu kunikaribisha jijini mgeni wa mji. Baada ya kukwapua ile simu, aligeuza nyuma na kuanza kukimbilia upande wa Magharibi ya stendi, upande uleule alioniotea.

Na kutoka pale nilipokuwa nimesimama mwili ukitazama Mashariki alipokuwa yule dada mwenye mwanya, nilipogeuza shingo huku na huko, nilimuona mwizi wangu kwa nyuma yangu, na mpaka naamua kumkimbiza, yule mwizi alikuwa akikikunja kona na kutokomea kwenye msongamano wa mabasi yaliyokuwa yamepaki kwa wingi.

Nikakimbia huku nikiipunguzia miguu yangu uzito kwa kuichomoa kutoka kwenye zile sandals nilizokuwa nimezivaa. Nami nikakunja ile kona, huko nako niliweza kumuona yule kibaka.

Nilikuwa nikijiamini sana kwenye swala la mbio, kama ujuavyo, mimi ni mwana riadha. Nikajihakikishia kumtia mikononi mwangu yule kibaka peke yangu bila kumbugudhi mtu, kwa kutaka msaada. ‘Sikupigii kelele za mwizi, peke yangu nakumudu wewe fala…’ Nilijisemea kimoyo-moyo bila kujua kwamba lile lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo baadae nililijutia sana.

Tuliingizana uchochoro huu na ule, tukakimbizana kona hii baada ya ile, baadae nilitahayari hali ilivyonigeukia.

“Mwiziiii…jamani mwiziiii….msaada jamani nisaidieni…” Yule kibaka alipaza sauti yake akiwaomba msaada kundi fulani la vijana lililokuwa akilikurubia.

‘Khaa…! Anataka kufanya nini huyu mjinga…?!” Niliwaza huku moyo ukimpwita kwa hamaniko. Nikaigundua adhima ya yule mjinga. Haraka sana nikataka kujihami kwa kupaza sauti kujitetea dhidi ya zile shutuma. Bahati haikuwa yangu.

Nilikuwa nimesha chelewa sana.

Lol…!

Kilichofatia baada ya hapo,  sikuamini kamwe. “Hapana jamani huyo ndio mwizi kaniiii…..” Nilianza kujitetea utetezi ambao haukunizalia matunda kabisa.

Mmoja ya wale vijana kwenye lile kundi lililokuwa mbele yetu aliniwahi, akasimama katikati ya ule uchochoro kwa kutandaza miguu yake mbele yangu akinizibia njia, tukapigana kikumbo cha nguvu. Mwenzangu alikuwa amejiandaa kwa kitendo kile, kwa hivyo hakutikisika. Lakini kwangu hali ilikuwa tofauti.

Nilihisi maumivu makali maeneo ya kifua, yakitambaa maeneo yote ya juu na ya chini ya mwili.

Papo kwa hapo yule jamaa aliyenizibia njia akanyoosha mikono yake yote miwili, akanisukuma kwa kunipiga nayo kifuani. Sikuwa nimejiandaa pia. Nilisikia maumivu makali sana kifuani,  kwenye mabega na shingoni. Nilipagawa kwa mstuko mkubwa. Nikajikuta nikirudi kinyumenyume huku nikiweweseka kwa hatua chache.

Kabla sijakaa sawa, nilihisi kudakwa kwa nguvu na mikono ya mtu nisiyemjua kule mgongoni. Papo kwa hapo, huko mgongoni nilikodakwa, nilihisi kuna kitu kibaya sana kikifanyika. Baadae, nilihisi wepesi wa ghafla kwenye bega langu la kushoto.

Nikapagawa.

Nilipogeuza shingo kuangalia kilichokuwa kikiendelea, nilipokelewa na konde moja zito kwenye paji langu la uso lililonipa wenge mfano wake hakuna.

Kwa mara nyingine niliweweseka huku nikirudi kinyumenyume, huku nikijizatiti kutokuanguka baada ya kuteleza kisigino. Nikafanikiwa. Sikufika chini. Lakini, papo kwa hapo, mtu mwingine alinidaka mgongo na kunisaidia kuniinua nikasimama wima. Ndipo kwa mara nyingine, kule nyuma, nilihisi kufanyiwa jambo jingine la kikatiri sana. Nikazidi kuchanganyikiwa. Kabla sijafanya chochote, nilihisi miguu yangu ikichotwa ngwara iliyonimudu kunipaisha hewani kama kishada. Nilipaa nikaelea hewani kabla sijashuka chini na kuangukia mgongo na kisogo.

Nilisikia maumivu makali yakinitambaa mwili mzima, nguvu zikinipungua na mwili ukifa ganzi kwa kihoro. Ama hakika mwizi wangu aliniwahi, na alichonifanyia, pasina shaka Mungu alimuona.

Kwa kiasi kikubwa alikuwa amefanikiwa kuniingiza kwenye madhila mengine ambayo sikuwa nimeyatarajia kabisa. Mbali ya yale nilikumbana nayo usiku wa safari. Achilia mbali kashikashi za nyumbani Geita kabla sijaja Dar. Na mazito yaliyonileta Dar hayo ndio achana nayo kabisa.

Nikiwa sijiwezi, hoi bin taaban sina hali, nilikuwa kwenye tafakuri zenye kuongofya, nikigalagala pale chini.

Kilichofatia baada ya hapo.

Aloo…!

Sharobaro mie, mbona niliijutia sana hiyo siku.

Nilipigwa….Nikapigwa….Nikapigwa…Aisee! Kilikuwa ni kipigo cha mbwa mwizi. Kuibiwa niliibiwa mie, na kipigo nikashushiwa mie.

Ilikuwa ni, “Mwizi mwizi…” Kipigo.

“Mwiziii…piga huyo…” Kipigo.

Watu walijaa eneo lile, wengine wakibaki kutazama, wengine wakinishushia kipigo kizito. Nilibondwa na mawe, nikatukanwa matusi yote, na kila aina ya kashifa nilipewa mie.

Nilijaribu sana kujitetea lakini sikupewa nafasi. Nililia hovyo huku nikivuta taswira namna nilivyowahi kushuhudia wezi wakishughurikiwa na wananchi wenye hasira kali. Nikaiona jehanamu ikiniita.

Wakati nikiparangana na ile kashikashi, muda fulani nikiwa nimeweza kuinuka kwa kuinamia mgongo, huku nikitumia mikono yangu kuuficha uso wangu usidhurike zaidi kwa mawe, kwa mara nyingine, macho yangu yalifanikiwa kuiona sura ya msichana mrembo kuliko wote niliokuwa nimewahi kuwaona duniani.

Yule dada mwenye mwanya.

Safari hii lile taba samu lake halikuwepo. Alikuwa akinlilia huku ameuficha mdomo wake kwa viganja vya mikono yake.

‘Oh mrembo….bahati gani mbaya namna hii…kwa mara ya kwanza nakutana nawe mtoto mzuri namna hii…na kufa ndio nakufa hivi hivi…hata sijafaidi kuuona vema uzuri wako.’

Machozi ya uchungu yalinilengalenga. Sio kwa mateso niliyokuwa nikiyakabili. La Hasha! Bali kuondoka kwenye uwepo wa msichana mzuri kuliko wasichana wote aliowahi kuwaona duniani tangu kuzaliwa kwangu. Nilijua lazima ningekufa tu, na sikutaka kumpoteza mapema namna ile mrembo yule.

Baada ya macho yetu kukutana, yule binti mwenye mwanya hakustahimili kuendelea kuwepo pale. Nilinuona akiuficha uso wake kwa mikono yake, huku akitoweka haraka. Nilisononeka sana. Nikabaini kabisa kwamba, moyo na macho ya yule binti, vilishindwa kustahimili kuendelea kuyashuhudia yale madhila yaliyokuwa yakinikabili.

“Leteni petrol tumalize kazi.” Wananchi wenye hasira kali wakaanza kuambiana.

Nikawasikia.

‘Aisee…yule kibaka kanichezea rafu sio mchezo….leo nakufa najiona hivi hivi…’ Nilizidi kuomboleza moyoni, huku nikihisi nguvu zikizidi kuniishia. Mwili ulivulia damu nyingi, nyingine zikinichuruzika hovyo kila mahali. Nlitapakaa majeraha yaliyoupoteza ule muonekano wangu waki brother men.

Na usharobaro kwisha habari yake.

“Kaka mzuri namna hii…na kupendeza kote anakuwa mwizi…ashooo.” Wanawake walininanga.

“Hapana jamani hajaiba….huyo siyo mwizi…wamemsakizia…” Sauti ya kelele za uchungu na maombolezo ilipenya kwa taabu masikioni mwangu. Nikaitambua. Japo kuwa nilikuwa katika hali ya kutokujiweza.

Nikiwa nimejikunyata ardhini, nikizidi kushambuliwa, nilijitahidi kufumbua macho yangu yaliyoanza kuelemewa na uzito wa maumivu, na damu iliyokuwa ikivuja kwa wingi kwenye paji la uso wangu.

Angalau nimuone huyo aliyekuwa akinitetea, ingawa sikuwa na cha kumlipa. Lakini pia nikijua fika utetezi wake ni bure tu mbele ya wananchi wenye hasira kali. Nilisha muhisi, lakini, nilitamani nijiridhishe.

Kutoka pale chini nilipokuwa nimelala  kiubavu, nikainua uso kwa taabu sana. Ndipo nilipoona jambo lililonirusha roho kwa kihoro. Umbali wa hatua chache kutoka pale nilipokuwa, nilishuhudia watu fulani wakichoma moto tairi la gari, kwa ajili kunichomea.

Kabla sijafanikiwa hata kumuona yule mtetezi wangu, nilihisi kitu chenye uzito mkubwa kikinishukia usoni.

Tofali.

Papohapo nikaanguka chini kabisa na kuanza kukoroma kwa taabu.

Kichwa kiliniwia uzito, na hakukuwa tena na mawasiliano kati ya kiwiliwili na shingo. Nikahisi weusi mzito umetanda usoni. Giza zito likayafumba macho yangu, uwezekano wa kuiona nuru kwa amra nyingine ulifutika ka kabisa.

Nikasikia kitu kingine chenye joto kali kikitua mwilini mwangu.

Lile tairi.

Nikaanza kuungua huku nikizidi kupoteza fahamu. Hakuna nilichokuwa nikikiona tena kwa wakati ule. Zaidi ya kusikia kwa mbali kelele za shangwe na mbija za wananchi waliokuwa yakifurahia kuteketea kwa mwizi.

Doh..!

 Nikavisikia viungo vyote vya mwili vikitengana na kupoteza mawasiliano kimoja baada ya kingine. Hatimaye, kwa mara ya kwanza maishani mwangu, nilimuona Izirael akinikurubia. Malaika yule mtoa roho alininyooshea mkono ishara ya kuniomba roho yangu.

Doh…!

Punde. Taratibu. Niliiona roho ikinitoka, na hivyo ndivyo roho imtokavyo mtu.

Giza nene likaufumba ufahamu wangu.

Nikapiga kimya cha kuongofya.

*****

“Natumai sasa unakumbuka kila kitu?” Yule msamalia alinihoji baada ya kunikumbusha huo mkasa.

“Bila shaka.” Nilimjibu “Wala siamini kama nimeokoka kwenye lile tukio.”

“Haukuokaka…wala haukuwa wa kuokoka.”

“Eti…kwa hivyo nilikufa? Na wewe ni nani sasa…malaika au…kwa hiyo tuko dunia ya wafu, nazungumza na malaika. Kumbe malaika ndivyo mlivyo.”

“No Kila. Haiko hivyo. Uko hai kwenye ulimwengu wa walio hai.”

“Unamaanisha nini unaposema sikuokoka kwenye lile tukio, na sikuwa wa kuokoka, na sasa unasisitiza niko hai. Nini maana yake?”

“Ukisema uliokoka utakuwa unakosea, sema tulikuokoa.”

‘Ukisikia masimango ndio haya sasa…’

“Oh…! Unaniaminisha hivyo ili mpate mnacho stahili. Nashukuruni sana kwa kuniokoa enyi raia wema. Najua shukrani ndio haja ya mioyo yenu. Wako wapi na hao wasamali wenzako, ili nao niwashukuru.”

Jamaa akacheka.

Nikabaki nimemkodolea macho yaliyo maanisha kuwa nataka jawabu la kauli yangu, sio cheko lake. Huwa sipendi kusimangwa.

“Kweli nimeamini…wewe ni mjeuri.” Jamaa alinitamkia. “Anyways…tuachane na hilo…” Akaongeza kusema. Lakini mpaka kufikia hapo, nikawa nimeshahisi kitu. Kwamba kuna neno, au maneno magumu zaidi, alihitaji kuniambia.

Ni kweli.

Jamaa alijitambulisha kwangu vema, kwamba anaitwa Kamugisha Rutta. Ni afisa usalama wa taifa, na alikuwa na mengi ya kuzungumza nami. Na mengi kati ya hayo mengi aliyokusudia kuzungumza nami, yalikuwa ni maneno magumu mno. Hivyo, akanihimiza niwe mvumilivu na mstahimilivu. Nikakubali kumpa nafasi ya kunieleza, nikiwa radhi kumpa ushirikiano alioniomba.

Akaanza kwa kunielezea mimi binafsi kwa namna anavyonifahamu. Na nia yake, pamoja na wasamalia wenzake walioniokoa. Nilishangaa sana, kwa kiasi kikubwa jamaa alikuwa akinifahamu. Alisema, pamoja na kwamba uokozi ilikuwa ni hisani waliyonijalia kama mwanadamu mwenzao, wakijua fika sikustahili ile kadhia, lakini, zaidi sana, lilikuwepo jambo.

*****

Nilizaliwa yapata miaka kadhaa iliyopita, kijiji cha Kasulu mkoani Kigoma. Katika kipindi chote cha kukua kwangu, niliishi na wazazi wangu Kigoma. Nikiwa mtoto wao wa pekee. Tulikuwa na maisha duni. Wazazi wangu waliishi kwa kipato cha kubangaiza. Lakini jambo moja ambalo nilijivunia katika familia yetu, ni upendo uliotawala kati yetu.

Pamoja na hali mbaya ya uchumi, iliyokuwa ikiikabili familia yetu, wazazi wangu walipambana usiku na mchana, kunirithisha urithi wa kudumu. Elimu.

Kila ilipoitwa leo, wazazi wangu hawakuchoka kunihusia nikazanie elimu, ili nije niwatoe kimasomaso siku za usoni.

Kweli, nami sikuwaangusha.

Nilikazana kwelikweli kumshika elimu, wala sikumruhusu aondoke zake, kama biblia takatifu ihasavyo.

Kwa kilimo cha mkono, baba na mama walimudu kunisomesha kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari. Ingawa nilikuwa nikisoma shule za kawaida kabisa za serikali, tena za kata, a.k.a. Kayumba,  bado sikuwaangusha wazee wangu hao. Na kila mtihani niliofanya, niliibuka kidedea kwa matokeo ya kuridhisha. Hilo liliwatia moyo na hamasa wazazi wangu, ya kuendelea kulisukuma jukumu lao la kunisomesha.

Hatimaye nilihitimu kidato cha sita, nikajiunga na chuo kikuu cha ST. Agustine, SAUT, cha Mwanza. Nikasomea masomo ya sayansi ya teknolojia, IT. Nikapata shahada ya kwanza.

Niliipenda taaluma yangu, na ama kwa hakika nayo pia ilinipenda. Niliimudu fani ya IT, lakini zaidi sana, nilikuwa mtundu wa maswala hayo. Kwa hiyo, zaidi ya ujuzi niliochukua darasani, nilizidisha maarifa yangu katika taaluma hiyo, na kunifanya niwe bora zaidi kila uchwao.

Utundu huo, ulinifanya niajiriwe moja kwa moja na mgodi wa madini wa Geita gold mine, GGM. Kwani, jamaa waliokuwa wakinisimamia wakati nikifanya field mahali hapo, waliridhishwa na utaalamu niliokuwa nao.

Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya familia yetu kubadilika. Nilifanya kazi mgodi wa Geita kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000, nikitumikia kitengo nyeti sana cha teknolojia ya mawasiliano. Nilikuwa nikilipwa mshahara mnono na malupulupu kedekede.

Niliishi kwenye nyumba ya kupanga, maeneo ya Msufini, mjini Geita. Nikawa nikiwatumia fedha za kujikimu wazazi wangu huko Geita, kwa kuwawekea kwenye akaunti ya benki niliyowafungulia. Ikumbukwe kwamba, mpaka maisha yanaanza kuninyookea, teknolojia ya kutumiana fedha kwa njia ya simu kidigitali, kitaalamu electronic money, ilikuwa haijaanza nchini.

Miaka ilikatika, wakati maisha yakizidi kutunyookea, ndipo wazazi wangu walipoamua kunieleza siri kubwa, waliyonificha kipindi chote cha kukua kwangu.

Siku moja nilipokuwa katika mapumziko mafupi ya kazi, yaani off ya wiki moja, nikaamua kuwatembelea, nao wakawa wamesha afikiana kunieleza, kile walichodhani kwamba, kilistahili nielezwe kwa wakati huo.

Kwamba, wao, sio wazazi wangu wa kunizaa.

Doh!

Nilistaajabu mno. Nikahuzunika na kuumia mno.

Awali ilikuwa vigumu kunishawishi niyaamini amelezo yao, kwa namna walivyonilea kwa upendo mkubwa. Lakini, hapakuwa na namna wala jinsi. Huo ndio ukweli, na hakukuwa na njia ya kuubadili.

Kwanini hawakunieleza siku zote hizo…na iwe sasa..

Ndipo waliponisimulia simulizi nzima juu ya historia ya maisha ya wazazi wangu huko nyuma, na mpaka mimi nikawa mikononi mwao. Ilikuwa ni simulizi ya kutisha. Ama kwa hakika, moyoni nilikiri kwamba, kibinaadamu, walikuwa na kila sababu ya kutokunieleza habari hiyo katika kukua kwangu. Sikupaswa kufahamu.

Aloo!

Kimbembe kikaja, walikuwa wapi wazazi wangu, kwa muda huo. Hata hao walezi wangu hawakuwa wakifahamu, kwani hawakuwahi kuwasiliana nao tangu waliponichukua na kuanza kunilea. Ila. Walichokuwa wakijua wao, walitengana na wazazi wangu wakiwa Dar es Salaam.

Wakanipa majina ya wazazi wangu. Wakanipa majina ya ndugu wa uzao wa tumbo la wazazi wangu. Ikawa bahati kwamba, kufikia wakati huo, teknolojia na utandawazi vilikuwa vinazid kushamiri nchini na ulimwenguni kote. Tayari, mfumuko wa mitandao ya kijamii ilikuwa ikishika kasi kwelikweli.

Nikajaribu kuyaandika majina ya ndugu wa uzao wa tumbo la mama yangu, kwa namna ya kuyatafuta kwenye mitandao ya kijamii. Ikawa bahati sana kwangu. Baadhi niliwapata, baadhi sikuwapata.

Ndipo nikaanza kuwasiliana na mmoja baada ya mwingine kwa njia ya DM kule instagram, na messenger kule facebook. Nikafanikiwa kuwasiliana vema na dada yangu aitwae Monica, ambaye alikiri juu ya kuzijua taarifa zangu, ila hakuna aliyekuwa akijua mpaka muda huo mahali nilipo, na jina ninalotumia. Kwani mpaka tunatengana, sikuwa nikiitwa Kilandika, au Kila.

Monica alifurahi mno, na akawa na bashasha ya kukutana nami ili tuonane. Bahati mbaya ilikuwa kwangu, kwamba nilikuwa nimebanwa na kazi kwa wakati huo. Bahati nzuri ikawa kwake kwamba, mwenzangu hakuwa na kazi kabisa mpaka muda huo.

Hakuwa amesoma, wala hakuwa na biashara iliyokuwa ikimuingizia kipato. Alikuwa akiishi kwa kutegemea pesa za matumizi, alizokuwa akipewa na mzazi mwenzake, waliyezaa nae mtoto mmoja wa kiume, kisha akakataa kumuoa.

Zaidi sana, kwa wakati ule, alikuwa bize kumuuguza mama yetu aliyekuwa mahututi hospitali ya Muhimbili. Aliniambia mama anaumwa sana na amedhoofu, baada ya figo yake moja kuharibika. Na kwamba, alikuwa akiishi kwa kutumia figo moja. Na kuhusu hali ya uchumi wa nyumbani, aliniambia ilikuwa mbaya kuliko ubaya wenyewe. Niliumia sana.

Nilimtumia nauli Monica, akaja kunitembelea, huku mama akiendelea kuuguzwa na ndugu zangu wengine. Alikuja Geita nilikokuwa nikiishi kikazi. Ndipo niliposadiki kwa namna gani alikuwa ndugu yangu wa damu. Tulifanana mno.

Nilikuwa na wakati mzuri na Monica. Akanisimulia mengi kuhusu maisha yetu, na namna historia inavyonielezea mimi, jinsi nilivyotoweka mikononi mwao. Aisee, niliumia sana.

Lakini kilichonisikitisha zaidi ni kwamba, mpaka muda huo, mama yangu hakuwa na habari kwamba, mwanae nilikuwa nimesha patikana, na nilikuwa nikiwasiliana na ndugu zangu.

Mama alikuwa kwenye koma.

Aisee, nilijikuta nikimlilia sana mama, ingawa sikuwa nimepata kumuona maishani mwangu. Shauku ya kumuona akiwa hai ikanijaa na kuutesa sana moyo wangu.

Alinieleza namna hali ya kiuchumi ilivyokuwa mbaya kwenye familia yetu kwa wakati huo. Tofauti na miaka ya nyuma, ambapo, maisha yalitunyookea na kila kitu kilikuwa sawia. Kabla hatuja hujumiwa.

Akanieleza kwamba; hawakuwa na makazi maalumu. Walikuwa wakiishi kwenye nyumba ya mmoja ya wajomba zetu, aitwae Deostedith “Deo” Malifedha. Mjomba alikuwa ni polisi, akitumikia kitengo cha Field Force Unit, FFU, a.k.a. Fanya Fujo Uone. Huyu ndiye alikuwa msaada wa mwisho kwa ndugu zangu hao. Ndiye alikuwa akiijua kula yao, vaa yao, hata lala yao. Aisee…doh…!

Baadae Monica alirudi Dar, nikimuhakikishia kwamba, likizo iliyokuwa ikifatia, ilikuwa ni lazima niende Dar es Salaam. Na nilimuhakikishia kuwa, nikienda Dar kila kitu kitakuwa safi. Nilichomtaka yeye na ndugu zetu wengine waliokuwa wakimuuguza mama, wajaribu kufanya jitihada ya kutafuta mtu ambaye yuko radhi kuuza figo yake moja, ili mimi nimnunulie mama.

Agizo hilo lilimtisha sana Monica.

Mimi ningewezaje kumudu gharama za kumnunulia mama figo. Figo ni ghali sana.Ni kweli.

Lakini kwa wakati huo, kwangu haikuwa ghari kiasi hicho. Nilikuwa na fedha za kugharamia figo.

Kwa mshahara wa mgodini..?!

Ndipo nilipomuibia siri Monica ili kumtoa hofu na mashaka kwamba, huenda nilikuwa simaanishi katika jambo lile. Kwani, pamoja na kwamba sikuwa nikiishi kimasikini, haikumaanisha nilikuwa na uwezo wa kumnunulia mama figo.

Nikamsimulia simulizi iliyomuacha midomo yake yote wazi. Simulizi ambayo, sikuwahi kufumbua kinywa changu kumshirikisha mtu yeyote, haijalishi nilimuamini kiasi gani.

Monica akawa mtu wangu wa pekee kumuibia siri hiyo.

Ni siri.

Hivyo hata yeye, haikumpasa kumuambia mtu yeyote.

Ndivyo tulivyokubaliana.

*****

Siku ya siku ilitimu, nikawa nimeshajiandaa na safari yangu ya kuelekea Dar, nikitokea wilaya Geita mkoani Mwanza. Kwa sasa Geita ni mkoa.

Nilisafiri kwa kutumia basi la Lushanga, la kampuni ya Lushanga bus service, tukiendeshwa na dereva machachari, Majeshi Lushanga.

Bahati mbaya ikaanzia hapo hapo stendi. Kitendo cha dereva kuiondosha gari, shokapu ikapasuka. Hatukuwa tumetoka hata ndani ya stendi. Ikawachukua saa nne mafundi kufanya matengenezo. Mishale ya saa tano kasarobo, tukaanza tena safari.

Majeshi ni dereva mtukutu katika fani yake hiyo. Ni hodari wa kucheza na usukani, na huwa hakosei wala kusababisha ajali. Hivyo, alimudu kuzifidia saa tulizo zipoteza  pale stendi ya Geita. Mpaka tunaingia Singida, tulikuwa tumeshazifikia basi zilizotutangulia. Aisee, huyu jamaa sio wa mchezo kabisa.

Stendi ya Singida, ndipo tulipopewa nafasi ya kula chakula cha mchana na kupumzika. Nikiwa nateremka garini, niliteremka na dada mmoja mrembo sana. Ndipo nilipobaini kwamba, nilikuwa nimesafiri basi moja na msichana mmoja mkali sana.

Alionekana wa kishua, na hakuwa na kampani yoyote. Nilijitahidi kujenga naye mazoea ya haraka, ili tuzoeane. Alikuwa mgumu kwelikweli. Lakini baadae, akajikuta akilainika. Tukazoeana.

Alinifahamisha jina lake. Anaitwa Ombeni Shemzenadi. Naye alikuwa akielekea Dar, akitokea shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora girls. Kumbe basi alilipandia Tabora. Mpaka tunarejea garini, kila mmoja alikuwa ameshaipenda kampani ya mwenzake, na kuudhiwa na ule umbali tuliotenganisha na siti zetu.

Hatimaye tuliingia stendi ya Morogoro mida mizuri tu, usiku ulikuwa umeshaingia. Tulipotoka hapo, mwendo kama wa kilometa thelathini mbele, tulipigwa tochi na askari wa usalama barabarani. Wakatusimamisha. Wakatuzingua pale, cha maana hakikuonekana. Basi tu. Wakaturuhusu dakika arobaini baadae.

Tulitembea mwendo wa kilometa kadhaa tena, kabla hatuja kutana na kizaazaa. Usiku ulikuwa unazidi kuwa mkubwa, na mahali hapo sikuweza kupajua, kwa sababu nilizokwisha kukueleza hapo awali. Ilikuwa safiri yangu ya kwanza, kuja Dar.

Abiria wote tulistuka na kupatwa na kihoro, baada ya dereva kufunga breki ghafla. Waliokuwa mbele walishikwa na kiwewe kabla hawaja tuambukiza nasi kie kiwewe. Ni baada ya wao kuanza kupiga kelele za hamaniko.

Katikati ya barabara kulitandazwa mawe makubwa. Ghafla. Kundi kubwa la watu wenye silaha za jadi lilitokea mafichoni na kutuzingira  pande zote.

Tulitekwa.

Wale watu wakataka kutuvamia ili watushambulie kwa namna walivyojua wao, na kwa namna walivyokuwa wamejipanga. Lakini, alichokifanya Majeshi, mpaka leo huwa simpatii picha yule jamaa.

Jamaa hakukubali ujinga.

Taa za mbele aliziwasha full right. Kisha akazima ta azote za ndani. Akoki gia za nyuma, kisha akaanza kuliendesha basi kinyume nyume kwa spidi isiyokuwa ya kawaida.

Wale jamaa hawakuamini kilichokuwa kikitokea. Ni naimani asilimia miamoja kwamba, walitahamaki vibaya sana. Mpango wao ulishindwa kimaajabu ambayo hawakuyadhania kabisa.

Ikawababidi waanze kutukimbiza na silaha zao. Abiria wakazidi kupiga mayowe ya woga. Hofu ya kutekwa. Woga wakupata ajali. Kwani alichokuwa akikifanya dereva Majeshi, ni zaidi ya sinema ya action.

Majeshi hakuogopa.

Akazidi kukanyaga pedeli ya mafuta.

Aloo!

Inasemekana aliliendesha basi lile kinyume nyume, umbali wa kilometa sitini. Halikuwa jambo la kawaida wala la jepesi. Si jepesi hata kulisimulia. Lakini ndivyo ilivyokuwa. Na  mwisho wa yote, tulifanikiwa kuwatoka wale majambazi. Salama yetu ikawa ya uhakika mara baada ya kufanikiwa kufika kwenye traffic post, ya wale askari walio tusimamisha muda mrefu wakati ule.

Wote tulimpa Majeshi heko. Alitisha sana.

Tulipowaeleza maswaibu yaliyotusibu, wale askari, kati yao, hakuna hata mmoja  aliyeamini ile habari. Kwamba, tuliwatoka wateka nyara kwa kuwakimbia kinyume-nyume.

Huyo ndiyo Majeshi Lushanga.

*****

Kwa ajili ya usalama wetu, tulilazimika kulala palepale kwenye kile kituo cha wale trafiki, mpaka asubuhi, ndipo tukaruhusiwa kuendelea na safari. Tukiwa hapo, ndiyo nikapata fursa ya kuwa karibu zaidi na rafiki yangu Ombeni. Urafiki wetu ukakolea kwa stori za hapa na pale. Masikhara, utani mwingi, na kadharika.

Kwenye mida ya saa mbili, tuliendelea na safari ya kuelekea Dar. Tukafika saa sita mchana. Yakanisibu yaliyonisibu.

Siku hiyo…

Miluzi ilivuma stendi nzima ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo external. Ilikuwa mishale ya saa sita mchana, wakati basi letu, likiingia kwa spidi kali.

Hatimaye nilikuwa nimefanikiwa kuingia mji niliopaswa kuingia.

Kijana jabari, mrefu, mweusi, mwenye mwili wa wastani ulioimarika kimazoezi, Kilandika Mwampachu a.k.a. Kila, niliinuka kwenye siti yangu iliyokuwa mstari wa tatu kutoka siti ya mwisho wa basi, nikajinyoosha nyoosha viungo vya mwili wangu ili kupunguza uchovu. Kisha nikapeleka mikono yangu kwenye kelia ya kuhifadhia mizigo, nikavuta begi langu nililolihifadhi hapo kama wafanyavyo abiria wengine.

Nikafanikiwa kulitoa. Lilikuwa begi aina ya Volcano, lenye ukubwa wa wastani, lisilokuwa na dalili ya kuwa na mizigo mizito. Na kwa hakika halikuwa na vitu vingi ndani yake. Nilikuwa nimesafiri kisela.   

Niliupeleka mkanda wa lile begi begani, nikalining’iniza hapo. Mpaka muda huo abiria wengi walikuwa wamekwisha kuteremka. Alimanusura ningejikuta niko peke yangu garini. Hali hiyo ilinishitua kidogo, nikabaini kwamba nilikuwa kwenye lindi zito la mawazo. Ndipo nilipoadhimia kuishurutisha akiri yangu iondokane na hiyo hali. Kwani mawazo mengi namna ile, yangeweza kunisababishia hatari kubwa mbeleni.  

Nilishuka ngazi za basi lile na kufanikiwa kutoka nje.

Nje ya basi, mazungumzo juu ya sekeseke lililotuhenyesha usiku wa safari yalishamiri. Dereva Majeshi alishapongezwa na raia pamoja na abiria mpaka kichwa kikamvimba kwa wingi wa sifa.

Upande wangu, mazungumzo yale hayakuwa na umuhimu tena. Wahenga walisha sema yaliyopita si ndwele. Kwa wakati huo, nilihitaji zaidi kuganga ya mbele. Akiri yangu iliyoanza kuitii adhima yangu ya kupunguza mawazo, ilikuwa ikifikiri kilichopaswa kufatia wakati huo.

Ndipo nilipoyapenya yale makundi ya watu yasiyokaukiwa mjadala wa lile sekeseke, nikasogea kando kidogo ili nipate nafasi nzuri kupiga simu niliyopaswa kuipiga, kwa ajili ya hatua iliyotakiwa kufuatia.Nilitaka kumpigia simu mwenyeji wangu.

Niliomba maelekezo kwa wenyeji wa ile stendi, ili nilipate lango la kutokea nje.

Nikaelekezwa.

Katika kufuata maelekezo niliyopewa, nilijikuta nimeuacha upande wenye mabasi. Nikasimama kwenye uwazi mpana.

Mbele yangu niliona mielekeo miwili iliyokuwa ikitumiwa na raia kufata malango ya kutoka nje. Uelekeo wa kwanza ni njia iliyoelekea Kasikazini mwa stendi, mwingine ulielekea Mashariki mwa stendi. Ule upande wa Mashariki nilitazamana na vibanda kadha wa kadha vya biashara mbalimbali.

Niliduwazwa na ukubwa wa ile stendi, sikuwahi kuona stendi kubwa namna ile hapo kabla. Pilikapilika zilikuwa nyingi, na kulikuwa na kila dalili kwamba, nilikuwa ameingia kwenye mji wenye mishemishe nyingi…kama nilivyowahi kusimuliwa na baadhi ya watu siku za nyuma.

Nikakipeleka kiganja cha mkono wangu wa kuume kwenye mfuko wa kaptura yangu, nikaikamata simu yangu ya mkononi. Wakati nikiichomoa, kabla sijaipeleka usoni ili kupiga, ghafla, macho yangu yaligongana na macho ya dada mmoja mrembo sana, aliyekuwa akinitazama huku kiganjani akichezea simu yake, iliyounganishwa masikioni kwa kutumia ear phone. Mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata mshikio wa sanduku lake la matairi alilolisimamisha.

Ombeni Shemzenadi.

Wote tukajikuta tukibasamu.

Sasa basi…wakati nikipiga hatua taratibu kumuendea yule mrembo mwenye macho makubwa kama golori, simu yangu ikaita. Nilipoinua mkono kuitazama, nikashituka. Ghafla ikanibidi nisitishe hatua zangu, nikaipokea huku nikigeuza uso huku na kule kwa kuhisi kwamba, huenda mpigaji hakuwa mbali nami.

Nilihisi, mpigaji, atakuwa ni mwenyeji wangu, tuiyeahidiana aje kunipokea pale stendi.

Sikukosea.

Nilipoipokea tu, nilisikia sauti ya mpigaji ikinielekeza nitazame upande wa Kusini mwa stendi kutokea uelekeo wa Mashariki niliokuwa nikielekea. Nikageuza shingo na kufuata maelekezo.

Nilifanikiwa kumuona dada yangu Monica. akiwa ameushikilia mkono wa mtoto wake wa kiume, alinipungia mkono. Nikaujibu kwa kumpungia mkono wangu wa kushoto vilevile.

Nikatamani nivuke njia za mabasi zinazokatisha mule stendi ili nimkurubie, lakini nilisita. Kumbukumbuka zilinijulisha kwamba, pembeni yangu, umbali wa takribani mita ishirini hivi, alikuwako rafiki yangu kipenzi, Ombeni Shemzenadi, niliyekuwa nikimuendea, na pasina shaka yule bibie naye alikuwa akiningoja. Nikageuka kumtazama. Tukatazamana. Jibu likawa kwamba yule bibie kule alikokuwa, alikuwa akinigoja.

Nikapagawa.

Huku Ombeni ananingoja. Kule dada yangu na mwanae wananingoja. Wote nawahitaji.

Ninze na yupi nimalize na yupi, nilitatizika.

Wazo la utatuzi wa ule utata likapita kichwani mwangu chapuchapu. Kwamba dada yangu Monica nimuagize anifate kule nilikokuwa. Kwani ilikuwa ni rahisi sana kumpoteza Ombeni kuliko dada. Ndivyo nilivyofanya, kwa ishara tuliafikiana na dada Monica.

Wakati huo, Ombeni alikuwa akifatilia yale mawasiliano ya ishara kati yangu na dada.

Ndipo alipoadhimia kuendelea kunigoja aliponiona  nikimwita kwa ishara ya mkono yule dada yangu.

Nikiwa sina hili wala lile, umakini wangu ukiwa imevurugwa na wale mabinti wawili wakali, nilipigwa kikumbo kikubwa mgongoni na mtu ambaye sikuwa amemuona, simu yangu ikakwapuliwa kwa nguvu, na kunisababishia maumivu makali sehemu kadhaa za mwili wangu kutokana na lile tukio la kushitukiza.

Yule kibaka alinichezea rafu mbaya sana, niliweweseka huku nikijitahidi kuuzungusha uso wangu huku na kule haraka-haraka ili mwizi wangu asinipotee usoni.

Nilifanikiwa kumuona.

‘Nakula na wewe sahani moja…’ Sikukubali ujinga. Nikafanya maamuzi ya kumkimbiza bila kufikiri mara mbili. Dakika moja baadae, nilijikuta kwenye ukanda wa majuto mazito, laumu, kilio na maumivu makali. Nikiona bora hata nisingeifukuzia simu yenyewe. Alimanusura yangu, ile simu initoe roho.

Yule kibaka alikuwa mwenyeji wa ile stendi, hivyo haikumpa tabu kunikaribisha jijini mgeni wa mji. Baada ya kukwapua ile simu, aligeuza nyuma na kuanza kukimbilia upande wa Magharibi ya stendi, upande uleule alioniotea.

Na kutoka pale nilipokuwa nimesimama mwili ukitazama Mashariki, nilipogeuza shingo huku na huko, nilimuona mwizi wangu kwa nyuma yangu, na mpaka naamua kumkimbiza, yule mwizi alikuwa akikikunja kona na kutokomea kwenye msongamano wa mabasi yaliyokuwa yamepaki kwa wingi.

Nikakimbia huku nikiipunguzia miguu yangu uzito kwa kuichomoa kutoka kwenye zile sandals nilizokuwa nimezivaa. Nami nikakunja ile kona, huko nako niliweza kumuona yule kibaka.

Nilikuwa nikijiamini sana kwenye swala la mbio, kama ujuavyo, mimi ni mwana riadha. Nikajihakikishia kumtia mikononi mwangu yule kibaka peke yangu bila kumbugudhi mtu, kwa kutaka msaada. ‘Sikupigii kelele za mwizi, peke yangu nakumudu wewe fala…’ Nilijisemea kimoyo-moyo bila kujua kwamba lile lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo baadae nililijutia sana.

Tuliingizana uchochoro huu na ule, tukakimbizana kona hii baada ya ile, baadae nilitahayari hali ilivyonigeukia.

“Mwiziiii…jamani mwiziiii….msaada jamani nisaidieni…” Yule kibaka alipaza sauti yake akiwaomba msaada kundi fulani la vijana lililokuwa akilikurubia.

‘Khaa…! Anataka kufanya nini huyu mjinga…?!” Niliwaza huku moyo ukimpwita kwa hamaniko. Nikaigundua adhima ya yule mjinga. Haraka sana nikataka kujihami kwa kupaza sauti kujitetea dhidi ya zile shutuma. Bahati haikuwa yangu.

Nilikuwa nimesha chelewa sana.

Lol…!

Kilichofatia baada ya hapo,  sikuamini kamwe. “Hapana jamani huyo ndio mwizi kaniiii…..” Nilianza kujitetea utetezi ambao haukunizalia matunda kabisa.

Mmoja ya wale vijana kwenye lile kundi lililokuwa mbele yetu aliniwahi, akasimama katikati ya ule uchochoro kwa kutandaza miguu yake mbele yangu akinizibia njia, tukapigana kikumbo cha nguvu. Mwenzangu alikuwa amejiandaa kwa kitendo kile, kwa hivyo hakutikisika. Lakini kwangu hali ilikuwa tofauti.

Nilihisi maumivu makali maeneo ya kifua, yakitambaa maeneo yote ya juu na ya chini ya mwili.

Papo kwa hapo yule jamaa aliyenizibia njia akanyoosha mikono yake yote miwili, akanisukuma kwa kunipiga nayo kifuani. Sikuwa nimejiandaa pia. Nilisikia maumivu makali sana kifuani,  kwenye mabega na shingoni. Nilipagawa kwa mstuko mkubwa. Nikajikuta nikirudi kinyumenyume huku nikiweweseka kwa hatua chache.

Kabla sijakaa sawa, nilihisi kudakwa kwa nguvu na mikono ya mtu nisiyemjua kule mgongoni. Papo kwa hapo, huko mgongoni nilikodakwa, nilihisi kuna kitu kibaya sana kikifanyika. Baadae, nilihisi wepesi wa ghafla kwenye bega langu la kushoto.

Begi langu, lenye kiasi kikubwa cha pesa, kwa ajili ya kugharamia figo ya mama lilikwapuliwa.

Nikapagawa.

Nilipogeuza shingo kuangalia kilichokuwa kikiendelea, nilipokelewa na konde moja zito kwenye paji langu la uso lililonipa wenge mfano wake hakuna.

Kwa mara nyingine niliweweseka huku nikirudi kinyumenyume, huku nikijizatiti kutokuanguka baada ya kuteleza kisigino. Nikafanikiwa. Sikufika chini. Lakini, papo kwa hapo, mtu mwingine alinidaka mgongo na kunisaidia kuniinua nikasimama wima. Ndipo kwa mara nyingine, kule nyuma, nilihisi kufanyiwa jambo jingine la kikatiri sana. Waleti yangu yenye nyaraka zangu kadhaa, zikiwemo kadi za benki, kadi za anwanina mawasiliano pamoja na vitambulisho, ili kwapuliwa.

Nikazidi kuchanganyikiwa.

Nilipigwa….Nikapigwa….Nikapigwa…Aisee! Kilikuwa ni kipigo cha mbwa mwizi. Kuibiwa niliibiwa mie, na kipigo nikapewa mie.

Ilikuwa ni, “Mwizi mwizi…” Kipigo.

“Mwiziii…piga huyo…” Kipigo.

Wakati nikiparangana na ile kashikashi, muda fulani nikiwa nimeweza kuinuka kwa kuinamia mgongo, huku nikitumia mikono yangu kuuficha uso wangu usidhurike zaidi kwa mawe, kwa mara nyingine, macho yangu yalifanikiwa kuiona sura ya msichana mrembo kuliko wote niliokuwa nimewahi kuwaona duniani.

Ombeni Shemzenadi.

Safari hii, lile tabasamu lake halikuwepo. Alikuwa akinililia huku ameuficha mdomo wake kwa viganja vya mikono yake.

Baada ya macho yetu kukutana, Ombeni hakustahimili kuendelea kuwepo pale. Nilinuona akiuficha uso wake kwa mikono yake, huku akitoweka haraka. Nilisononeka sana. Nikabaini kabisa kwamba, moyo na macho ya yule binti, vilishindwa kustahimili kuendelea kuyashuhudia yale madhila yaliyokuwa yakinikabili.

“Leteni petrol tumalize kazi.” Wananchi wenye hasira kali wakaanza kuambiana.

Nikawasikia.

Na usharobaro wangu kwisha habari yake.

“Kaka mzuri namna hii…na kupendeza kote anakuwa mwizi…ashooo.” Wanawake walininanga.

“Hapana jamani hajaiba….huyo siyo mwizi…wamemsakizia…” Sauti ya kelele za uchungu na maombolezo ilipenya kwa taabu masikioni mwangu. Nikaitambua. Japo kuwa nilikuwa katika hali ya kutokujiweza. Lakini bado niliweza kuitambua sauti ya dada yangu Monica.

Kabla sijafanikiwa hata kumuona, nilihisi kitu chenye uzito mkubwa kikinishukia usoni.

Tofali.

Papohapo nikaanguka chini kabisa na kuanza kukoroma kwa taabu…

*****

Yote haya niliyakumbuka vema, lakini cha ajabu mimi sikupaswa kuyakumbuka. Bali nilikumbushwa na  yule msamalia mwema, aliyekuwa amesimama kando ya kitanda changu, wodini, pale kwa dokta Kairuki.

“Umeyajuaje yote haya… na umewezaje kufahamu mambo yangu mengi kiasi hiki, hata ya miaka ya nyuma?” Nilimsaili yule msamalia mwema, wakati huo, hofu yangu juu yake ilikuwa kubwa mno.

Nilianza kumuogopa.

“Najua mpaka sasa utakuwa unajiuliza maswali mengi kuhusiana na mimi. La. Usiogope. Kwa sasa hebu nikuache upumzike kidogo, kisha nitakapokuja muda mwingine, tutazungumza zaidi.” Jamaa aliishia hapo, akaondoka.

Sikujua kwa nini aliniacha kwenye utata mkubwa namna ile. Ila nilihisi jambo. Pasina shaka, alitaka kunipa muda nizidi kuichemsha akiri yangu, kwa maswali yasiyo kuwa na majibu. Ili atakaporejea, nikiwa na shauku ya kuijua alfa na yee, nimpe ushirikiano aliokuwa akiuhitaji kutoka kwangu.

Sikukosea!

Siku zilikatika, yule jamaa sikumuona tena. Wiki mbili zikapita. Kimya.

Siku moja usiku, hali yangu ikiwa inazidi kuimarika, japo sikuwa na uwezo wa kutembea bila sapoti, kitandani kwangu, nilitembelewa na daktari mwangalizi wangu. Alikuwa ni mama wa kifilipino. Akanipa habari zilizonitisha kidogo.

“We are so grateful to God that, your doing well Kilandika.” (Tunamshukuru Mungu kwamba unaendelea vema Kilandika) Alianza maelezo yake. Kisha akanieleza kwamba, kuna hatua waliyoamua kuichukua, nayo ni kunihamishia hospitali ya Muhimbili.

‘Kwa nini?’

Yule mama aliniambia, kuna changamoto niliyokuwa nayo, ambayo wao wasingeweza kuimudu. Na njia pekee ya kuimaliza, inapatikana hospitali ya Muhimbili, kitengo cha mifupa, MOI.

Niliogopa.

‘Au napelekwa kukatwa mguu?’

Lakini yule mfilipino ni kama aliigundua hofu yangu, akanituliza na kunipa matumaini. Akanihakikishia kwamba, sitakatwa mguu, ila ntapatiwa matibabu yatakayo harakisha uimarikaji wa mifupa yangu iliyoathirika.

Sikuwa na namna. Nikakubaliana naye, kwani hata kama ingekuwa ni kwa ajili ya kukatwa mguu, ningebisha nini, wakati wataalamu ndio walioamua iwe hivyo. Nikaambiwa nijiandae kwa ajili ya safari ya kuelekea Muhimbili, usiku huohuo.

Matayarisho ya hapa na pale yakafanyika, ikiwa ni pamoja na kudungwa sindano. Mida ya saa nne, nilisaidiwa kupelekwa kwenye gari la kubebea wagonjwa, kwa msaada wa machela.

Lakini kichwani sikuweza kuyadhibiti maswali yaliyokuwa yakiniandama. ‘Mbona imekuwa ghafla mno…na kwa nini usiku usiku. Kwani mimi ni mgonjwa wa dharula kiasi cha kuhamishwa hospitali usiku usiku.?’

Yalikuwa ni moja ya maswali kadha wa kadha yaliyonisumbua. Nilisha hoji vipi kuhusu yule msamalia mwema aliyenisaidia, nikaambiwa tangu alipoondoka ile siku hakuwa amerudi tena. Na wao hawakuwa na mawasiliano naye. Ila walinihakikishia kwamba, siku ambayo angekuja kunitembelea, watampatia anwani kamili ya kunipata.

‘Kwa nini amepotea namna ile…Aliniacha njia panda ile siku, kuna mengi nilitamani kuyajua kupitia yeye…sasa…’ Nilibaki kwenye kizungumkuti.

‘Na je asiporudi, nani anaweza kunisaidia kujua nilipokuwa napaswa kwenda. Mimi ni mgeni wa mji, sina ramani, sina mwenyeji, simu, vitambulisho, na kila kitu nilichokuwa nacho, vimeshapotea. Ntakuwa mgeni wa nani mimi jamani?’

Nilibebwa kwenye ambulance, nikisindikizwa na wauguzi watatu.Ule upande wa nyuma nilimo kuwa nimelala kwenye kitanda kidogo cha mgonjwa, kulikuwa na wauguzi wawili wa kike. Kule mbele tofauti na dereva, kulikuwa na muuguzi mmoja wa kiume. Wote humo tulikuwa watanzania. Safari ya kuelekea hospitali ya Muhimbili ikaanza.

Hatukwenda Muhimbili…

*****

Niligutuka usingizini nikiwa na uchovu mwingi. Nilijihisi sikuwa kawaida. Nilikuwa na uchovu ambao mara nyingi humkumba mtu aliyeamka baada ya kuelemewa na usingizi mzito. Kwa hivyo, nilikuwa kwenye usingizi mzito.

Pasina shaka.

‘Kwa nini…?’

Baada ya kuvuta kumbukumbu, nilifanikiwa kuyakumbuka matukio yaliyotukia muda uliopita. Na hatimaye, tulikuwa tukielekea hospitali ya Muhimbili. ‘Lakini hapa sipo hospitalini…achilia mbali Muhimbili’ Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikizidi kuyachunguza mazingira nilimokuwamo.

Yalikuwa ni mazingira mageni kabisa, lakini hayakushabihana na ya kihospitali. Nilikuwa eidha kwenye nyumba ya makazi ya watu, au nyumba ya kulala wageni, guest house.

Nilikuwa nimelala kwenye kitanda cha kifahari mno. Matandiko yake, haikunihitaji mtu kunieleza kwamba yalikuwa ya bei ghari. Samani kadhaa zilizokuwamo mule chumbani, zilikuwa za bei mbaya pia. ‘Wapi hapa nilipo…?’

Na hata wakati maswali mtungo yakizidi kutunga kichwani mwangu, ghafla nilisikia kitasa cha mlango wa kile chumba kikifunguliwa. Akaingia binti mmoja aliyevaia joho la kiuguzi. Nikamkumbuka. Ni mmoja kati ya wale wauguzi niliokuwa nao upande wa nyuma wa ile gari ya kubeba wagonjwa, walionisindikiza tulipokuwa tukitoka kwa doktaKairuki, tukielekea Muhimbili.

“Oh…Kila, naona umezinduka sasa…”

‘Doh…! Kuzinduka tena…kwani nilikuwa nimezimia?’

Yule dada ni kama aligundua namna nilivyotatizika. “Pole sana.” Akanitamkia.

“Pole ya nini?” Nilimuuliza.

“Najua namna mtu awavyo pindi atokapo kwenye usingizi wa kutiwa dawa ya nusu kaputi…ndio maana nakwambia pole sana. Nikisadiki pasina shaka utakuwa umechoka sana.”

“Ni kweli nimechoka sana…” Nikamjibu. “Kumbe mlinitilia dawa ya usingizi…kwa nini basi, nani saa ngapi mlifanya vile?” Nilimfurumushia maswali. ‘Inawezekana walinitilia kupitia ile sindano niliyochomwa wakati tukijiandaa na safari. Nilijijibu.

“Tuyaache hayo, ngoja kidogo.” Alinijibu yule muuguzi, kisha akaelekea mlangoni, akafungua kitasa na kutoka nje. Dakika kumi baadae, mlango ulifunguliwa tena. Safari hii hakuingia yule muuguzi, bali wanaume wawili waliovalia mavazi ya kiraia. Lakini, ilionesha kwamba, walikuwa njema kifedha. Mmoja sikumfahamu, huyu alikuwa mnene kiasi. Lakini yule mwingine nilimkumbuka. Alikuwa ni yule yule msamalia mwema.

‘Oh comred, nice to meet you.’ Yule mgeni wa macho yangu alinichangamkia, na moja kwa moja akaja haraka karibu na kitanda akinipa mkono. Nilijilazimisha kuupokea, moyoni sikuwa na amani hata kidogo. Huku kuitana komred. Naye alinishangaza kidogo.

“Naam Mr. Kila…natumaini unaendelea vema.” Msamalia mwema alinitamkia akiwa amesimama mbali kidogo na kitanda nilichokuwa nimelala, kwa tofauti ya hatua mbili kati yake na yule mgeni mwingine. Nilimkubalia kwa kutikisa kichwa.

“Lakini niko wapi hapa…kwa sababu nilipaswa kuwa Muhimbili hospitalini. Lakini hapa sio…” Sikumalizia sentensi yangu, yule mgeni mpya akanidaka kwa kauli.

“Usijali rafiki. Huu sio wakati wake tena, huu ni wakati mpya na mambo mapya.”

“Etiii?” Nilimaka.

‘Yup.’ Jamaa alijibu huku akitikisa kichwa kwa msistizo.

“Ilibidi iwe hivyo kama ulivyojua. Lakini haikuwa hivyo.” Yule jamaa akaongeza neno huku akisimama wima zaidi, akiifumbata mikono yake pamoja, sanjari na kuifumba midomo yake kwa nguvu na pumzi zikisikika namna zilivyokuwa zikimtoka puani.

Niliduwaa.

Hata yeye alilijua hilo.

“Ni mengi yametokea rafiki.., maswali kwako yamekuwa mengi mno twafahamu, lakini leo, yote yatapata majawabu. Na kila kitu kitawekwa bayana. Na leo, tunaukata mzizi wa fitina.”

“WHAATTT?”

“Yup.”

‘Mzizi wa fitina…’

Nikanyamaza. Nikazidi kumtazama tu. Lakini, kila nilipomtupia macho yule msamalia mwema, niliduwazwa na ukimya wake. Hakuzungumza chochote, kana kwamba hakuwa sehemu yay ale mazungumzo.

Yule mgeni kibonge alichukua hatua ya kukikurubia zaidi kitanda nilichokuwa nimelala. Akaketi kando yangu, juu ya godoro. Tukazungumza….

*****

Akiwa pale kitandani, kibonge akaanzisha mazungumzo rasmi. Kwanza alijitambulisha yeye na kumtambulisha yule mwenzake. Kwamba yeye anaitwa Tibezuka Tibaijuka. Na yule mwingine ni Atilio Mjaki. Wote ni wahaya, marafiki, na wanatumikia kitengo kimoja cha usalama wa taifa.

Wakati Tibezuka alikuwa ni usalama wa taifa namba moja, Mjaki alikuwa usalama wa taifa namba mbili.

Lakini pia wote walistahili kuitwa wasamalia wema, kwani ndio walioshirikiana kuniokoa na kifo pale Ubungo external. Baada ya kujua hivyo, nikamshukuru sana Tibezuka kwa msaada wao, kwani kama sio wao kwa kweli, ningeshakufa siku nyingi.

Hakuishia hapo. Akaendelea. Safari hii akizidi kunichanganya kabisa. Aliniuliza, “Unaukumbuka wizi wa mchanga wa dhahabu, uliotokea GGM miaka michache iliyopita?”

Swali jepesi, jibu lake gumu.

‘What’s going on here?!’

Nilichanganyikiwa vibaya mno. Jamaa alinivuruga kichwa si mchezo.

“Wizi wa mchanga….unahusikaje hapa?” Nilijitutumua kumuhoji, huku nikijitahidi kuikabili hofu yangu isidhihirike wazi wazi bila mafanikio.

“Jibu swali kiongozi.”

‘Whaaat…ati nini…kiongozi…!’

“Yup. Nakumbuka.” Nilimjibu kama alivyotaka, huku nikizidi kumtazama usoni kwa makini, pengine alikuwa ni mmoja kati ya ile timu iliyoshiriki ule wizi. Kumbukumbu zikakataa.

‘Kwa nini aniite kiongozi sambamba na swali kama hilo…?’

Binafsi huwa sipendi majina ya kubambikizwa. “Kaka mkubwa”, mara “kiongozi”, au sijui “Mzee baba,” “bosi”, sijui nani nani huko…akha! Mi kwa kweli huwa sipendi.

Kwa hivyo huyu usalama wa taifa namba moja kuniita vile niliona kama ananichefua tu. Mbaya zaidi sikuelewa maana yake, kama aliamua tu kama wapendavyo vijana wa mjini, au kulikuwa na kitu akimaanisha.

Nilishakihisi hicho kitu.

Haikuwa ajabu kwa mtanzania yeyote kuwa na zile taarifa za wizi wa mchanga wa dhahabu uliotokea mgodi wa geita, Geita Gold Mine, au GGM. Lakini, kwanini anielekezee lile swali moja kwa moja kana kwamba alikuwa na uhakika kwamba nilikuwa na taarifa za kina kuhusiana na ule mchongo.

‘Kwa nini aniite kiongozi…’

“Vema kiongozi, pengine utakuwa unajiuliza nimezijuaje taaria hizi.” Akaendelea kunivuruga.

“Siwezi kushangaa kwa sababu ile ilikuwa issue kubwa, habari zake hazikuwa kificho, kila kitu kiliwekwa wazi na vyombo vya habari zikatangaza.” Nilimjibu jibu la kujihami. Lakini tayari nilikuwa nimeshamstukia, na sikuwa na uhakika kama nilikuwa kwenye mikono salama.

“Kwa mafikara yangu, wizi wa mchanga wa dhahabu GGM, ni moja ya matukio ya wizi mkubwa na wakutisha yaliyowahi kustua umma wa Watanzania, na viunga vyake. Kwa hivyo sina sababu ya kujiuliza umezijuaje taarifa hizo.” Nilimfafanulia. Naye hakuishia hapo.

“Hilo tu, ndilo linalokufanya usishangae nimezijuaje taarifa hizi…una uhakika kiongozi?” Aisee, kwa mara ya kwanza nilikuwa nikaamini kwamba nilikuwa nimepatikana.

‘Ana nini huyu, na mbona udadisi umekuwa mkubwa sana…ni nani huyu?’ Ama kwa hakika, alinivuruga. ‘Halafuuu…! Mbona maswali maswali?!’

Wizi wa mchanga wa dhahabu wa mabilioni ya fedha mgodi wa Geita, ulitokea miaka michache iliyokuwa imepita. Wakati huo, mimi nilikuwa nimeshaanza kazi mgoni hapo.

Habari za kutisha zilitikisa kwenye vyombo vya habari, kwamba, wizi wa mchanga wenye thamani ya mabilioni ya fedha, uliibiwa kwenye chumba maalumu cha kuuhifadhia, kabla ya hauja safirishwa kwenda nje ya nchi, kwa ajili ya mchakato wa kuufanya kuwa dhahabu.

Ni tukio lililowaacha watu wengi midomo wazi, hususani kwa namana ilivyokuwa ikiaminika kwamba, ulinzi ulikuwa mkubwa mno mgodini hapo.

Yalisemwa mengi kuhusiana na lile tukio. Lakini wazawa wengi walilipongeza kwa madai kwamba, wazungu ambao ndio wamiliki wa shughuri zile za uchimbaji wa dhahabu mgodini hapo, walikuwa wakinufaika mno, huku wazawa wakiachiwa mashimo matupu, ilhali hali zao za maisha ni hohehahe.

Msako mkali uliendeshwa kila kona, matangazo yakatangazwa, kwamba, atakaye fanikisha kukamatwa kwa wahusika, atapewa donge nono.

Polisi ikawatia mbaroni baadhi ya washukiwa, lakini hakukufanikiwa kupatikana ushahidi wa moja kwa moja wa kuwatia watu hatiani. Ilikuwa ni misheni iliyoratibiwa kitaalamu, na ikaratibika. Ikafanyika kwa mafanikio makubwa mno.

Nje ya mgodi, watu wakaneemeka ghafla. Wapo walionunua majumba, magari, na matusi mengine mengi kama wasemavyo vijana.

Mimi pia nilikuwa mmoja wa wanufaikaji wa wizi ule. Tena nilinufaika pakubwa, kwa sababu ya majukumu niliyokabidhiwa katika kuutekeleza. Kama mtaalamu wa IT, nilipewa jukumu la kuhakikisha navuruga vyanzo vyote vya teknolojia ya mawasiliano na ulinzi. Hii ilijumuisha kamera za CCTV.

Lakini pia nilitakiwa kuwaongoza watu waliokusudia kuuchota ule mchanga na kuutorosha. Kupitia majukumu hayo, wenzangu wakajikuta wakinibatiza jina la “kiongozi”. Kwenye kuwasiliana kwetu, wakawa wakipendelea sana kuniita hivyo.

Majukumu hayo, niliyatekeleza kwa ufanisi mkubwa, na mafanikio makubwa mno katika ubora wake. Mwisho wa siku nilipata mgao wa milioni mia saba.

Fedha hizo zilikuwa nyingi mno kwangu mimi. Zilitosha kunifanya niishi kwa kufanya matusi pale mjini, au kwingineko. Lakini sikufanya hivyo. Badala yake niliishi kwa kujihadhari sana.

Nilizificha pesa mahala nilikokujua mie, sio benki lakini, wala saccos, au kwenye taasisi yoyote ya kifedha. Nikaendelea na amisha yangu ya kawaida, kwa ajili ya kuepusha kutiliwa shaka. Japo, nilikuwa mmoja kati ya washukiwa tulioswekwa na kusoteshwa rumande, kabla ya kuachiwa kwa kukosekana kwa ushahidi wa kututia hatiani.

Na ndizo fedha zilizonitia jeuri ya kumnunulia mama figo. Kwa hivyo, lile begi nililo kwapuliwa pale Ubungo external, lilikuwa na milioni miamoja za kitanzania, kwa ajili ya mpango wa afya ya mama.

Kwani tayari mtu wa kujitolea figo alikuwa ameshapatikana, na maafikiano yalikuwa si zaidi ya milioni sitini. Milioni arobaini nyingine zilikuwa ni kwa ajili ya misheni nyingine ambayo niliadhimia kuitekeleza nikiwa Dar. Ni misheni kubwa kwa ajili ya jambo kubwa na la siri. Hatari sana, lakini nilikuwa na uhakika kwamba, fedha isingeshindwa na kitu. Aisee, yule kibaka aliyenikwapulia simu pale Ubungo, alinikatili mengi.

Muda ulikuwa umepita tangu wizi wa mchanga GGM kufanyika, na sikuwa nimemsimulia mtu yeyote juu ya ushiriki wangu. Hata walezi wangu kule Kigoma, sikuwaamini katika hili. Nilihofia wangeweza kupata mchecheto wakamwaga mchele kwenye kuku wengi. Niliazimia iwe siri yangu. Na ndivyo ilivyokuwa.

Kwa mara ya kwanza, nilitengua azimio langu kwa kumdokeza siri hii dada yangu Monica, alipokuja kunitembelea. Ndiye mtu pekee uraiani niliyemshirikisha, tofauti na wenzangu tuliokula nao njama ya ule wizi.

Sababu pekee iliyonifanya nimwambie, ilikuwa nikumpa msistizo ili asisite kutafuta mtu ambaye atakuwa tayari kumtolea mama figo, kwa gharama yoyote. Kwani mpaka aliponitembelea kule Geita, bado nilikuwa nikiishi maisha ya kawaida mno, tofauti na mtu anayemiliki mamilioni ya fedha, tena yasiyokuwa ya mkopo.

Sasa basi…kama Tibezuka na Mjaki walikuwa na taarifa za ushiriki wangu, bila shaka Monica alikwenda kinyume na makubaliano yetu. Alishavujisha siri.Ama kweli wahenga walishasema, duniani, hakuna siri ya wawili.

“Najua unajiuliza maswali mengi kuhusiana na haya ninayokueleza, lakini kitu cha kwanza ni muhimu wewe ujue kwamba, hakuna lililokutokea kwa bahati mbaya ile siku unasafiri kutokea Geita kuja Dar.” Usalama wa taifa aliniambia. Akaendelea.

“Kila kitu kilipangwa, kikaratibiwa, na kuratibika, japo si kwa asilimia mia kwa mia. Kuna baadhi ya mambo ni kama yalikuwa yakigeuka kama scene za sinema, yanaanza hivi yanakuja hivi.” Sikumuelewa.

“Unamaanisha nini?” Nilimuhoji.

“Yote haya, ni kazi ya mjomba wako Deosdedith.” Alipotamka hiyo sentensi, nilihisi kizunguzungu kikinichukua pale kitandani na kunibanaisha kona moja ya ukuta, kikanibana kwelikweli, sasa, nisingeweza kufurukuta.

“Unasemaaa…?!” Nilihoji kwa taharuki kubwa, nikiwa nimepagawa zaidi.

“Yes bro, this is it.” Alinijibu huku akiinamisha kichwa kama aliyesikitishwa na maelezo yale, huku akitafakari zaidi. Mimi pia nilijikuta nikiutazamisha uso wangu ukutani kwa juu kidogo, nisijue hata nilichokuwa nikikiwaza. Kichwa changu kilivurugika vibaya mno.

‘Deosdedith Malifedha…! Mjomba wangu…how comes…come ooon…nini kinanitokea mimi Kilandika. Mbona kila kitu kinacho nitokea ni kama movie ya Hollywood.’ Nilijikuta kwenye tafakuri nzito. Ndipo Tibezuka, a.k.a. usalama wa taifa namba moja, akanisimulia kila kitu. Ni mambo mazito.

Kumbe mjomba wetu, niliyeelezewa na dada yangu Monica, kwamba ndiye mfadhili wa familia yetu, alikuwa kinyume nasi, msaliti wa kwanza. Kweli, kikulacho ki nguoni mwako.

Jambo ambalo ndugu zangu hawakuwa wakilifahamu kuhusiana na huyo mtu, ambaye kwao alikuwa mwema kama malaika, alikuwa ni mnafiki. Wa hovyo. Na ndiye muhusika nambari moja wa kuvurugika kwa mukutadha wa maisha ya familia yetu.

Mbaya zaidi, yeye ndiye aliyeratibu kila jambo baya lililotukia nikiwa safarini kuja Dar. Kuanzia Geita stendi, pale basi letu lilipopata hitirafu, iliyo tuchukua saa kadhaa kungojea litengamae.

Morogoro tuliposimamishwa muda mrefu na wale askari wa usalama barabarani. Mpaka kunusurika kutekwa kwetu na majambazi kule porini. Na mbaya zaidi, yeye ndiye aliye kuwa sababu ya mimi kupigwa kipigo cha mbwa mwizi pale stendi ya mabasi yaendayo mikoani, Ubungo.

Mjomba alikuwa akiichezea michezo rafu familia yetu. Kimya kimya, kwa sababu alizozijua yeye. Hata ugonjwa wa mama uliomlaza kitandani kwa muda mrefu, kwake ilikuwa ni ahueni. Shauku yake ilikuwa, mama afe.

Hivyo, baada ya kuambiwa kuhusu ujio wangu, na mimi kuanza kuwasiliana naye, na kumpa mirejesho yote  kuhusiana na mipango ya safari, yeye naye alikusudia yake. Alikusudia kuniua kabisa, ili misaada niliyo ikusudia kwa mama na familia yetu kwa ujumla, ikwame.

Doh!

Mjomba alikuwa katili kwelikweli.

Mpango wa kwanza, aliandaa majambazi wa kuiteka basi ya Lushanga iliyokuwa ikinileta Dar. Ili waniuwe. Katika kujihakikishia ushindi katika hilo, aliwakodi baadhi ya mafundi makenika wa gereji ya Lushanga iliyopo Geita, waitegeshee shokapu ya lile basi, ili punde tu tutakapoanza safari, liharibike. Lengo likiwa kutuchelewesha njiani, ili tufike porini usiku, tutekwe.

Wale askari wa usalama barabarani waliotukalisha muda mrefu pale kituoni kwao bila sababu ya msingi, nao waliandaliwa. Walikuwa ni washirikika wa mjomba, wakishirikiana naye ile njama. Walituchelewesha maksudi, ili usiku uwe mkubwa, mabasi mengine yaendayo mikoani yatupite, tukitekwa, tukose msaada. Hilo walishindwa.

Mpango wa pili ndio ule wa yule kibaka, aliyenikwapua simu Ubungo. Yule naye aliandaliwa, na kutekeleza alichokitekeleza. Lengo lake halikuwa kuniibia simu, bali mimi nife kwa namna alivyofanikiwa kuniingiza kwenye yale madhila.

Lakini nilinusurika… Kivipi?

Kabla ya mpango wa kumtumia yule kibaka, mjomba alianza kwa kuwapanga watu wa usalama wa taifa wanipoteze. Nao ni Tibezuka Tibaijuka na Mjaki. Ni marafiki zake wakubwa. Na waliafikiana kushirikiana kuniangamiza.

Mpango ulikuwa ni wao kuniundia njama, ili nibambikiziwe kesi yoyote itakayonipeleka jela, kisha nikafie huko huko. Njama hii ilikusudiwa kufanyika palepale Ubungo, kabla sijafika hata nyumbani.

Lakini sasa, Tibezuka na Mjaki, nao wakawa na yao mioyoni mwao. Kwa namna ambayo wao walitaka kunitumia mimi, kulingana na namna walivyoamini kwamba nawafaa, waliafikiana kumsaliti mjomba. Hivyo, walikuwa radhi kunidhibiti pale stendi, bila madhila, kisha waniweke mafichoni kama walivyofanya, wanitumie kwenye eneo waliloonelea kwamba nawafaa sana kwenye moja ya misheni yao ya kitaifa. Mjomba si akanyetishwa habari hizo….

Akaona isiwe taabu. Hakuwaeleza chochote jamaa hawa wa usalama wa taifa, badala yake, akaandaa mpango wa siri wa kumtumia yule kibaka bandia. Ili kabla kusudia la usaliti lililopangwa na Tibezuka na Mjaki halijafanikiwa, mambo yageuke mpaka wao washangae.

Na ndivyo ilivyokuwa.

Kumbe, nilipokuwa Ubungo stendi, Tibezuka na Mjaki walikuwepo pia, kutekeleza ombi la mjomba, kama walivyokubaliana, laikini wao nao wakiwa na lao, bila kujua hilo la kwao mjomba kaisha limaizi, na kaisha wageuzia mchezo. Monica na mwanae bila kujua kwamba, niliandaliwa kifo na mjomba aliyekuwa kazini muda huo, alikuja kunipokea.

Na ndipo sasa, kibaka akaniwahi. Yakatokea yaliyotokea, Mjaki na Tibezuka wakiwa hawaamini kabisa namna mchezo ulivyowageuka. Ndipo dakika ya mwisho, wakaamua kuniokoa kwa nguvu, kwa kunitoa kwenye mikono ya wananchi wenye hasira kali.

Na mpaka wanafanikiwa, tayari walikuwa wamesha mpoteza kwenye ile picha Monica, kwa mmoja wao kumpiga pigo lililomfanya apoteze fahamu. Ili asijue kilichoendelea.

Niliondolewa stendi ya Ubungo nikiwa hoi bin taabani, sijiwezi asilani abadani. Nikatoroshewa hospitalini kwa dokta Kairuki, ikiwa ni kwa siri kubwa mno. Na baada ya muda mfupi, taarifa zangu zikiambatana na picha zangu, zilizagaa kwenye vyombo vya habari, kwamba, mwizi aliyejaribu kukwapua simu stendi ya Ubungo, apigwa kipigo cha mbwa mwizi mpaka kufa, maiti yake, imezikwa na manispaa ya jiji la Dar es salaam. 

  Taarifa hizi zilihakikishwa zinawafikia pia ndugu zangu, mjomba Deo, dada Monica, na wengine waliokuwa wakiningoja kwa hamu. Mama hakuweza kutaarifiwa, kwani hakuwa akijitambua. Bado alikuwa kwenye koma.

Hakika huyu msamalia mwema aliniacha hoi kwa maelezo haya, kichwani nikabaki najiuliza maswali lukuki. ‘Kunani mjomba Deo, mpaka afanye yote aliyoyafanya. Tena kwa gharama kubwa namna ile. Kwa sababu kama alikuwa akikodi watu wa kutekeleza njama zake, lazima alikuwa akiwalipa… Ili iweje?’

Baada ya kunisimulia yote hayo, Tibezuka alinitaka turejee kwenye kusudi la wao kumsaliti mjomba. Akaanza kwa kuniuliza swali.

“Unamfahamu, (Akamtaja kiongozi wa kisiasa nchini, mkubwa tu, tena mashuhuri mno.)” Nikastuka.

‘Usalama wa taifa namba moja!’

‘Usalama wa taifa namba mbili!’

‘Mimi!’

‘Mjomba Deo.’

‘Huyo mwanasiasa!’

‘Wizi wa mchanga GGM!’

‘Kuna nini hapa katikati?!’

“Ndiyo namfahamu.” Nilimjibu huku nikimtazama kwa hofu, mashaka yakiwa yameutawala moyo wangu, akiri ikinizunguka kwa kasi mno.

“Basi, maadam unamfahamu, vema.”

“Lakini si zaidi ya kumsikia kwenye vyombo vya habari…naomba nieleweke hapo.” Nilimfafanulia. Naye akanijibu.

“Sawa… hivyo hivyo… hata mimi sikuhitaji awe babu yako ndio uniambie unamfahamu.”

“Enhe, huyo mzee anakujaje kwenye mazungumzo yetu.” Nikamsaili.

“Huyo ndiyo jibu la swali lako la kwa nini tuliadhimia kumsaliti rafiki yetu Deosdedith… Huyo mzee, ndiye sababu ya sisi kukuokoa na kifo pale stendi.” Nilihamaki vibaya sana.

“Eti nini?!”

“Yes… hivyo hivyo ulivyonisikia ndivyo ilivyo.” Tibezuka alinijibu.

“Yule mzee hafai kabisa.” Akaongezea.

“Hafai?!”

“Ndiyo hafai?!”

“Hafai kwa lipi…halafuuu…nyie kuniokoa, kuna husikanaje na kutokufaa kwake?!”

“Tunataka tumpoteze.”

“SAY WHAAAT…?!”

“Hivyo hivyo.”

“Mnataka mumpoteze wangapi…I mean wewe na nani yaani…au huyu mwenzako…?” nilimalizia kwa kumsonta usalama wa taifa namba mbili, Mjaki.

“Na ukiwemo na wewe.” Jamaa alinijibu

‘Mungu wangu…yamekuwa haya tena…eewe Mora wangu naomba unifanyie wepesi tafadhali…mambo gani haya…’

“Aku, aisee mi staki bwana.” Nilijitetea huku nikibetua mabega nikimaanisha sikuwa tayari, ingawa sikuwa nimeelezwa niliopaswa kulifanya, au nilitakiwa kuhusika vipi.

Badala ya kunijibu, jamaa alikaa kimya, kitu kilichozidi kuniacha njia panda. Hakuwa na haraka ya kwenda moja kwa moja kwenye neno kusudiwa. Pengine aliujua uzito wa neno alilotaka kuniambia, ikambidi azunguke mbuyu ili kuniandaa kisaikolojia. Alizidi kutoa maneno ya kumkandamiza yule bwana, na bado hakuniweka wazi, nini kilikuwa kikinipasa baada ya hapo.

“Kwani kawafanyaje jamani…mbona mnamshutumu sana…?” Nilimuuliza huku nikitetemeka, woga ukizidi kukithiri.

“Ah, huyo…! Huyo mzee muone hivyo hivyo, mtu mbaya sana yule. Hafai kama ukoma…”

“Lakini mbona anaonekana mpole na hana shida na mtu. Mara zote amekuwa muungwana na mzalendo kwa taifa lake. Na zaidi sana, amekuwa akisifika kwa uchapakazi wake, hususani miaka miwili ya uwaziri mkuu wake, alifanya mengi mazuri. Tukiachana na kashifa iliyomuondoa madarakani.”

“Unaingizaje wasifu wa uzalendo kwa mtu aliyeondolewa madarakani kwa kashifa?” Tibezuka alinikazia macho, nami nikamkazia macho.

Tukakaziana.

“Aliondolewaaa…?! Alijiondoa…?!” Nilimuijia juu.

“Kuna tofauti gani kati ya kuondolewa na kujiondoa. Hiyo yote ni adhabu ya mkosaji, na yote ni kuwajibika baada ya kutenda dhambi. Tofauti ya mtu anayejiondoa kwenye nafasi na anaye ondolewa, anayejondoa anakuwa amejiwajibisha kabla ya hajawajibishwa, kwa makosa aliyoyafanya, na hiyo haimfanyi kusamehewa maovu yake. Kwa sababu kuwajibika sio toba.” Usalama wa taifa yule alinifafanulia kwa kina, akaendelea.

“Lakini pia, kaa ukifahamu kwamba, huyo mzee unayemtetea hana lolote la maana. Ni mnafiki tu yule…aliyoyafanya aliyafanya kwa makusudi yake. Mzee ni mnafiki sijapata kuona. Ni mzandiki haswa. Hakuna mzandiki mzuri hata siku moja, na ni bora mchawi anaye wanga na anajulikana kwamba ni mlozi moja kwa moja, kuliko mtu mnafki. Mnafki ni zaidi ya mchawi au mshirikina.

“Mi naona mnachuki na hila zenu tu za kisiasa juu yake, hamna lolote la maana. Na kwa namna mnavyomkusudia kwa mabaya, Mungu anawaona.”

“Nakuonya, usipende kumtaja Mungu kwenye mambo kama haya…unadhani ndio tutaogopa kumshughurikia. Kumdeal tuta mdeal, na anachokitafuta aandike maumivu. Maana yake amenoa.” Usalama wa taifa namba moja, alikuwa serious.

“Umezunguka mbuyu kwa muda mrefu…hebu twende moja kwa moja kwenye point. What is the matter?” Nilimwambia, ndipo yule bwana, akaamua kufunguka. Na katika kuniweka sawa, alianza kwa kunipa historia ya chanzo cha mambo yote, mpaka wao kuamua kuniokoa mimi kule stendi, kuna jambo walililikusudia. Kwa maana hiyo, mimi nilikuwa moja kati ya kete yao muhimu katika kukamilisha mipango yao ya kumpoteza yule mwanasiasa tuliyekuwa tukimjadili.

Kabla hajaniambia nini walihitaji kutoka kwangu, alinisimulia mambo mazito sana. Na mpaka anahitimisha simulizi yake, niliapa, kamwe maishani mwangu, sitakaa si tu nishiriki, la, hata kufikiria kushiriki siasa, kamwe!

Waliosema siasa ni mchezo mchafu, walikosea…siasa sio mchezo mchafu, siasa ni zaidi ya mchezo mchafu. Siasa ni mchezo wa hovyo.

HAUFAI…

*****

     Ilikuwa ni baada ya uchaguzi mkuu wa kitaifa, wa kuwachagua madiwani, wabunge na rais, uliofanyika miaka tisa iliyopita. Chama tawala kiliibuka kidedea kwa kuikamata dola kwa awamu nyingine mfululizo tangu kichukue hatamu kwa mara ya kwanza, miongo kadhaa iliyopita. Pia kiliongoza ushindi kwenye nafasi za ubunge na madiwani. Ndipo sasa taratibu nyingine za kiutawala zikatakiwa kuanza kufuatwa, moja wapo ilikuwa ni bunge kumchagua spika wa bunge, na rais kumteua waziri mkuu pamoja na balaza zima la mawaziri. Na hapo ndipo kimbembe kilipoanzia.

   Kumbe bwana, ndani ya chama tawala kuna watu wanaitwa wanamtandao. Mimi sikuwa nikilifahamu hili, mpaka nilipofahamishwa na hawa wasamalia wema walioniokoa kwenye sekeseke la stendi ya Ubungo. “Ashooo… wana mtandao?!” Nilihoji kwa mshangao, sikuwa nimewahi kuijua habari hii juu ya uwepo wa kitu cha namna hiyo, hata hivyo, mimi na siasa wapi na wapi!

   “Yes bro, wanaitwa wanamtandao.” Msamali mwema alinijibu.

    “Ndio akina nani hao?” Nilimuuliza, naye hakuchoka kunielezea.

   Kwamba…

   Wanamtandao, ni kikundi fulani cha watu ndani ya chama tawala, chenye nguvu kubwa ya ushawishi, kinachotoa muongozo wa chama hicho. Kikundi hiki, kinajumuisha viogozi wa juu wa chama na viongozi wake. Watu hawa ndio hutoa dira na muongozo wa kiutawala, kiungozi na kimadaraka. Kwa mfano; linapokuja suala la uchaguzi mkuu, hawa watu, ndio wenye nguvu ya kuamua nani akiwakilishe chama katika kinyang’anyiro cha urais. Kura zao na maamuzi yao, ndio dira ya chama.

   Na zaidi sana, mtu watakaye mpitisha chamani agombee urais, akishinda kiti hicho katika uchaguzi mkuu, kikundi hicho ndicho chenye dhamana ya kumpatia muongozo rais atakaye chaguliwa, namana ya kuongoza nchi, katika namana ya kuendelea kuimarisha misingi ya chama. Moja ya majukumu yake, nikupendekeza na kumpa rais watakaye kuwa wamempitisha, majina ya baraza la mawaziri na wizara zao. Baada ya hapo, jukumu la rais huwa ni kuridhia na kulitangazia taifa yale majina, kana kwamba  yeye ndiye aliyeyateua.

   “Ashooo…” Nilistaajabishwa na maelezo hayo.

    “Usistaajabu sana, hiyo ndiyo siasa, mambo mengi huwa ni ya siri, tena siri kubwa.” Alinijibu msamalia mwema baada ya kuniona namna nilivyosisimkwa kwa maelezo yake, kisha akaendelea kwa kusema, “Ni katika utaratibu huo sasa, ndipo mzizi wa fitina ulipoanza… mpaka leo hii unavyotuona hapa, katika harakati yaku mdeal huyo mzee.”

    Nilikuahidi sitakutajia jina lake mzee huyo, mwenye historia ndefu katika siasa za nchi hii, ila ntatumia moja kati ya wasifu wake kukupasha habari hii. Muheshimiwa huyo, ana asili ya mvi nyingi kichwani pake,  pamoja na umri wake kuwa mkubwa, lakini pasina shaka, mvi zile ni za asili. Ni nyingi mno, hazijachanganyikana na hata punje moja ya unywele mweusi, ili twende sawa, acha tumuite “Bwana Mvi.”

    Msamalia mwema alinieleza kwamba, mwana siasa huyo, ambaye sasa tumeshambatiza jina linalo shabihana vema na wasifu wake mkubwa, Bwana Mvi, alikuwa na uswahiba na mwanasiasa mwenzake mmoja hivi, ambaye naye sitakutajia jina lake halisi, ila kutokana na asili yake ya kupenda kutabasamu muda mwingi, acha tumwite mzee wa tabasamu, a.k.a. Mr. Simile.

    Inasemekana kwamba, mzee wa tabasamu na  Bwana mvi, walikuwa marafiki wakubwa, au washikaji, kama waitanavyo vijana wa kisasa, na ushikaji huu, ulidumu kwa miaka mingi, huku wakijiita boys to men. Aisee, nilishangaa sana kusikia hadithi hii, wanasiasa… boys to men tena…duh! Lakini hatimaye baadaye, hawa boys to men, walijikuta wakiingia kwenye uadui mkubwa usiosemekana.

    Kutoka boys to men, mpaka uadui wa paka na panya… Sio hatari kubwa hiyo!  

    Miaka kumi na tisa iliyopita waliwahi kutaka kugombea urais, lakini mambo yalienda ndivyo sivyo katika hatua za awali za kumtafuta muwakilishi wa chama katika kinyang’aricho cha urais. Ni mambo mengi yaliyochangia wao kutokufanikisha adhima yao, sio kwamba hawakuwa na nguvu ya ushawishi, la Hasha… ila ni mambo ya kisiasa zaidi ndio yaliyopelekea hali ile kutokea. Kwa leo hatutazaungumzia hayo.

    Hawakukata tamaa, walikubaliana kuvuta subira, mpaka baada ya miaka kumi tena, ndipo wangejaribu bahati yao, na ndivyo ilivyo kuwa, miaka tisa iliyopita, baada ya ukomo wa muda wa urais wa rais aliyeingia madarakani miaka kumi na tisa iliyopita, walilejea uringoni, awamu hiyo, wakiwa na makubaliano maalumu ya kimkakati zaidi.

    Bwana Mvi, kwa kujua kiasi gani Mr. Simile alivyokuwa na ushawishi mkubwa, na nguvu kubwa, alikubali  kumuachia  mwezake awanie urais huo, kisha miaka kumi baadae, baada ya utawala wake, Mr. Smile amrithishe kiti hicho adhimu. Maelezo haya yalinifanya nihisi kudata  kama tusemavyo vijana, nikimaanisha nusura nichanganyikiwe.

    “Amrithishe kiti hicho…?! Kwani urais ni ufalme mpaka watu wakubaliane kurithishana, mbona sijawahi kulifahamu hili… na nnavyojua, mtu huwa rais kwa kuchaguliwa na wananchi.”

    “Vema Kiladite, upo sahihi kabisa, lakini kama unakumbuka hapo nyuma, kuna kauli nimekueleza, kwamba, ndani ya siasa, kuna mazingira mengi na michezo mingi mno ya siri, tena siri kubwa. Na labda nikuongezee neno, siasa ni mchezo wa kimkakati zaidi, na ndio maana nimekueleza hapo nyuma kidogo, ujio wa pili wa hawa jamaa kwenye kuwania kiti cha urais, ulikuwa wa kimkakati zaidi.”

    Siasa isikie tu… siasa sio mchezo mchezo…

*****

    Baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika miaka kumi na tisa iliyopita, mbunge aliyelitwaa jimbo la Urambo Mashariki, alilejea jijini Dar.

   Alipofika uwanja wa ndenge wa Dar, baada ya  kuteremka kwenye ndege, alipokea simu iliyomstua sana.

   Alipigiwa na mbunge wa jimbo la Igunga, ambaye, mbali na siasa za muda mrefu, muheshimiwa huyo, alikuwa mfanya biashara mkubwa, tajiri, maarufu na mwenye ushawishi.

    “Hallow muheshimiwa waziri mkuu, pole kwa safari, karibu sana jijini Dar.” Mbunge wa Igunga alimsabahi mwenzake simuni. Mbunge wa Urambo alichelea kuijibu ile salaam, kwani iligubikwa utata mtupu.  

    ‘Hallow muheshimiwa waziri mkuu.., pole sana na safari…, karibu sana jijini Dar… haya mazungumzo mantiki yake ni nini…’ Alijihoji pasi na majibu. ‘Haya ya kuitana waziri mkuu yametoka wapi… kwa nini labda…’ Akapata jibu, ‘lakii-niii… hata kama, mbona sio wakati wake…’ Hakupendezwa!

     ‘Okay, enheee, na hili la “karibu jijini Dar”, kajuaje huyu kwamba nimewasili Dar, yamkini bado niko hapa air port.., au yupo hapa hapa ameniona…’Aliangaza huku na huko akitegemea kumuona huyo mtu, hakumuona!  

     “Naam muheshimiwa, nashukuru nimefika salama, vipi upo hapa Air port?” Mbunge wa Urambo alimjibu kinyonge, akimalizia na swali.

     ‘Walaa, mie nipo Masaki mkuu.” ‘Masaki..! na habari za air port umezijuaje?’

     “Akhaaa… na ukajuaje kwamba mie nimeingia Dar?”

     “Aaaah… bwana eee… kwani wewe haujijui kwa mba u-mtu mkubwa sana kwenye hii nchi… wewe sini waziri mkuu.., waziri mkuu ni mtu mkubwa bwana unayeishi chini ya ulinzi mkali, popote ulipo, utokapo na uendako.”

     ‘Wewe kama nani… IGP.., RPC au usalama wa taifa..!’

     “Lakini bado sijawa.” Mbunge wa Urambo alimjibu kwa huzuni.

     “Ndiyo haujawa, lakini umeshakuwa, maadam wenye nchi wameshaamua na wakiamua ndivyo inavyokuwa wasiwasi wako uko wapi bwana wewe?” Mbunge wa Urambo alikosa neno, akapiga kimya, lakini kwa kweli moyoni mwake hakufurahishwa kabisa na yale mazungumzo, ingawa yalikuwa na ukweli ndani yake, kwake ilikuwa ni mapema mno kuyazungumza namana ile, tena simuni. Japo kuwa mbunge wa Igunga alizungumza kwa bashasha akitegemea mwenzake angefurahia.

     ‘Kwa hiyo hata kama ungetaka kuniteka nyara ungeniteka tu, kama umeweza kujua kwamba nimeingia Dar wakati sijamfahamisha yeyote… hii sio hatari jama…?’ Alikubali kushindwa, akampatia nafasi mpigaji awasilishe hoja yake iliyomsukuma kumpigia ile simu. Alijua fika, zile salamu na bashasha za uwaziri mkuu, mara mtu mkubwa sijui nini nini huko, sizo zilizompelekea muheshimiwa yule kumpigia simu.

     Lazima kuna kitu.

     Lipo neno.

     Ni kweli kabisa, hisia za mbunge wa Urambo zilikuwa sahihi, pale mbunge wa Igunga alipomtaka aghairi safari yake, ili aende Masaki, yalipo makazi yake [yeye mbunge wa Igunga], kwa ajili ya mazungumzo ya lazima sana. Kuambiwa vile, mbunge wa Urambo Mashariki alitahayari sana.

*****

    Alifika Masaki, mchana uleule, kwa gari yake binafsi, akiendeshwa na dereva wake aliyempokea pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar. Moyoni hakuwa na amani kabisa, kiasi kwamba alijishangaa, kwa nini alijikuta amepoteza furaha na amani namna ile.

    Wakati huo huo, moyoni akijua fika kwamba, yeye ndiye waziri mkuu ajaye, hii ni kwa mujibu wa wanamtandao. Wao walikuwa wameshampendekeza kutwaa nafasi hiyo, na rais aliyechaguliwa, mzee wa tabasamu alingojewa kwa ajili ya kumtangaza tu.

    Hivyo basi, kwa namna moja ama nyingine, mbunge wa Igunga hakukosea kumuita yeye waziri mkuu, lakini, haikupasa kuwa kwa namana ile. Yale ni mambo ya siri, hayaropokwi hovyo hovyo namna ile.

*****

    Nyumbani kwa mbunge wa Igunga, mbali na mwenyeji wake, pia alimkuta mgeni mwingine. Huyo alikuwa mbunge wa Mondu, Bwana Mvi. Uwepo huu ulimstua na kumuogopesha kidogo, ghafla akahisi mwili ukimsisimka, hisia kwamba palikuwa na mada nzito zikamjaa ghafla, lakini alijikaza kiume.

     Wale wenyeji walimpokea vizuri, kwa bashasha, huku wakimchangamkia sana, hususani baba mwenye mji. Bwana Mvi alionekana kupoa kidogo, jambo lililomtisha zaidi mbunge wa Igunga, ingawa alijitahidi kuzidhibiti hisia zake machoni mwa wale wanasiasa wenzake machachari.

      Baada ya salamu, utani wa hapa na pale hususani wa kisiasa, mada iliyokusudiwa iliwekwa mezani. Na mchokozaji alikuwa baba mwenye mji.

      “Aisee, kwanza tuseme pole sana kwa usumbufu tuliokusababishia, kwa kukatisha mizunguko yako na kukuleta hapa…” [Mbunge wa Igunga akatikisa kichwa ishara ya kuya kuipokea ile radhi] “…lakini, yote katika yote ni heri tupu, ni kwa ajili ya ujenzi wa taifa letu.” Akameza fundo la mate, kisha akaendelea.

     “Pili tunakushukuru sana kwa kukubali wito wetu… ama kwa hakika umetuheshimu sana, mimi na huyu mwenzangu..,” [Akamgeukia Bwana Mvi. Wakatazamana. Bwana Mvi akaachia tabasamu dogo, huku akitikisa kichwa kumuunga mkono yule mwenyeji wao] “…japo kuwa simuni sikukueleza juu ya uwepo wake mahali hapa, lakini nyie wawili ndio sababu ya kusanyiko hili pengine kuliko hata mimi. [Mbunge wa Igunga akaachia tabasamu la kujilazimisha, huku akili ikamuwasha  kwa shauku ya kutaka kujua nini kinaenda

kuzungumzwa]

      Ndipo baba mwenye mji, akawaelezea taarifa kutoka ngazi ya juu taifani, kutoka kwa rais aliyeapishwa siku si nyingi, Mr. Smile, kwamba, kuna mabadiliko fulani fulani ameyafanya.

      Kwamba, kwa mujibu wa makubaliano waliyoyapitisha wanamtandao, juu ya uteuzi wa watendaji mbalimbali wa serikali, likiwemo baraza la mawaziri, kuna mabadiliko aliyoyaamua muheshimiwa rais.

      Mpaka kufikia hapo, mbunge wa Igunga alihisi vinyweleo vya mwili vikimsisimka isivyo kawaida. Hili jambo wao kama wanamtandao walishalihisi mapema, na walishajiapiza kwamba, kama kweli lingetokea, moto utawaka.

      Mwendesha mada akaendelea kusema, ni katika mabadiliko hayo, rais ametengua pendekezo la waziri mkuu aliyependekezwa na wanamtandao, badala ya mbunge wa Igunga, nafasi hiyo atampa Mr. Mvi

      YAAALAAAAAAAHHHH…!

       OOOH… SALALEEEEE…. MTUMEEE WUUU…!

       Hizi taarifa… narudia hizi taarifa, ndizo moja kati ya taarifa mbaya zilizozuwa kizungumkuti cha utawala mzima wa miaka yake yote aliyodumu madarakani Mr. Smile. Laiti kama angejua nini kingefatia baada yake, asingefanya mageuzi hayo.

*****

     Njia nzima, kichwani mwake aliendelea kurejewa na mazungumzo baina yake na wale wanaume wawili kule Masaki. Uchungu kama utungu wa kuzaa, uliufinyanga moyo wake kiasi cha kupelekea mapigo yake ya moyo yapande juu, (high blood pressure) Ama kwa hakika siku hiyo, wale jamaa walimuweza.

     ‘Kama mmeamua hivyo potelea kote.., hata huo uspika wenu siutaki… potelea mbali.’ Aliikumbuka moja kati ya sentensi alizowatupia wale watu, pale walipomueleza ati, mbadala wa uwaziri mkuu aliokuwa akiutegemea, imeamuliwa awe spika wa bunge.

     “Utagombea uspika wa bunge, na timu ya muheshimiwa rais itahakikisha ushindi ni wako.” Mbunge wa Igunga alimtia moyo.

     “Ati nini…?!” Alimaka mbunge wa Urambo Mashariki.

     “By the way no dought, bunge ni muhimili wa taifa unaojitegemea, ukiwa spika, hakuna tofauti na kuwa waziri mkuu.” Mbunge wa Igunga alikazia.

     “Of course…” Bwana mwenye mvi nyingi akaunga mkono kauli kwa kudakia.

     “Nani kasema hivyo… na kama kweli hivyondivyo ilivyo, kwanini hamkumpa huo uspika huyu ndugu yenu.., [{akimaanisha kwa kumtazama bwana mwenye mvi nyingi}] we mzee mwenye mvi za ukoo unashadadia nini..?! Ati of course.., of courseeee…?! Wakupe wewe basi huo uspika tuione kweli hiyo of course.” 

     “Not like that honorable… we are so humble and apologize for this stuation, sio kusudi letu kukuumiza, ila ni kwa ajili ya kufanikisha mipango kamambe ya baadae…” Mbunge wa Igunga na mwenyeji wa ule mkutano akafafanua, “…imetulazimu kufanya hivi ili kumtengenezea mazingira mazuri Bwana Mvi ya kuchukua nchi baada ya miaka kumi ya utawala wa mzee wa tabasamu,kama ujuavyo, baada ya Mr. Smile, atafata huyu mzee, sasa wazungu wana kamsemo kao kanasema hivi, better the early… maana yake bora mapema, pia haohao wazungu wanasema, preparation is the mother of manifestation… yaani maandalizi ni mama wa udhihirisho. Kwa hiyo, kwa ajili ya udhihirisho wa mafanikio ya mpango mkakati wa miaka kumi ijayo, yatupasa kufanya maandalizi sasa.”

      “Okayyy.., sawa mshenga.., unajifanya unajua sana kupanga mashairi unapoongea hizo ngonjela zako utadhani upo kwenye kikao cha makubaliano ya kutoa mahali. Yaani.., kwa ajili ya udhihilisho wa mpango mkakati wenu binafsi.., ndio muumize wengine..! Sawa! Lakini, muwe na uhakika kwamba, mimi sipendi unafiki na kamwe sitaki unafiki, fanyeni kama mlivyoadhimia mkijua siko upande wenu.., katika hili mmenishurutisha tu. Hivyo basi.., hata  huo uspika wenu siutaki, mpeni mtu mwingine. Mimi ntabaki kuwa mbunge wa kawaida… BASIII!”  Alipomaliza kuyasema hayo, mbunge wa Urambo Mashariki alinyanyuka  akaondoka zake.

      Hatimaye alifika nyumbani kwake, akaelekea moja kwa moja chumbani kwake akalala. Kwa namna akiri yake ilivyo kuwa imevurugika, usingizi mzito ulimtwaa.

*****

     Kama mbunge wa Urambo Mashariki alidhani utani, alijidanganya. Siku ya  siku ilitimu, macho na masikio ya watanzania wengi yalielekezwa kwenye vyombo vya habari. Minong’ono na mazungumzo yalikuwa juu ya taarifa ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kuwa angemtangaza waziri mkuu.

     Muda ulitimu.

     Rais kupitia vyombo vya habari ikulu, alimtangaza waziri mkuu.

     Na aliyepewa wadhifa huo, alikuwa mzee wa mvi nyingi.

     Shangwe na nderemo zilitaradadi kila kona ya nchi.

     Uteuzi huu, pamoja na kuwafurahisha wengi, wengine uliwauma.  

     Hakukuwa na jinsi, uteuzi ulisha fanyika, ukatangazwa, na hata baada ya jina lake kupelekwa bungeni ili kupigiwa kura na wabunge za NDIO au HAPANA, waziri mkuu mteule alipita kwa wingi wa kura za NDIO, za wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

      Taarifa hii ilitangazwa na vyombo vyote vya habari nchini, na vya baadhi nchi za nje. Lakini, pengine kuna kitu ambacho mimi na wewe kwa wakati ule hatukukielewa ingawa kilielezwa sana na waandishi wa habari, “…rais amemteua na kumtangaza waziri mkuu, ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi, amefanikiwa kuwaruka wana mtandao…”

    Hili la kuwaruka au kuwageuka wanamtandao, lilivuma mno. Binafsi sikuelewa maana yake, mpaka nilipo kuja kufahamishwa vema na hawa wana-usalama wa taifa.

     Kumbe wakati ule, baadhi ya waandishi wa habari walifanikiwa kuujua ukweli huu, kwamba, mzee wa mvi nyingi hakuwa pendekezo la wanamtandao katika kukalia kiti kile kikubwa kabisa katika utawala wa nchi hii. Wao walimtaka mbunge wa Urambo Mashariki, mwanaharakati na mwanasiasa wa muda mrefu, msomi wa chuo kikuu adhimu duniani cha Havard. Badala yake, rais akasimamia msimamo wake, akamteua swahiba wake huyo wa miaka nenda miaka rudi. Lengo likiwa ni kumtengenezea mazingira ya kuja kuchukua nchi miaka kumi baadae kwa wepesi kabisa.

      Aje awe rais.

      Rais alikosea sana.

      Maamuzi haya, yalimgharimu sana.

      Sijui kama rais hakujua, au alijua madhara ambayo yangefatia baada ya kitendo chake hicho, na akaamua kudharau. Ninacho fahamu mimi, kile kitendo, kilimgharimu sana yeye, na utawala wake wote wa miaka kumi aliyokikalia kiti cha urais, kiasi kwamba, madhara yale lazima yalikwenda mbali zaidi ya mategemeo au matarajio yake.

*****

      Siku zilisonga, ikafika kipindi cha wabunge kumchagua spika wa bunge. Mbunge wa Urambo Mashariki kwa wakati ule, ambaye kwa sasa ni marehemu, aliandamwa na timu ya rais na swahiba wake waliomgeuka na kumpokonya tonge lake la uwaziri mkuu, safari hii wakimshinikiza agombee uspika wa bunge wakimuhakikishia ushindi. Msomi huyo wa Havard University akakataa katakata.

     Hakuwa akitania, alikuwa akimaanisha. Moyo ulishatumbukia nyongo, hakuwa akiuhitaji huo uspika. Jambo ambalo hakulijua ni kwamba, wakati yeye aliukataa uspika kwa kumaanisha, timu ya rais iliazimia kumpa uspika kwa lazima.

    Ilikuwa ni lazima awe angalau spika, ili kumpoza machungu ya kuukosa uwaziri mkuu, lakini pia kwa ajili ya kumyima upenyo wa kuwa huru kuitesa serikali ya Mr. Smile.

     Kambi ya rais iliamini kwamba, kwa kitendo cha kikatili walichomfanyia mbunge yule, lazima angefikiria kulipiza kisasi, kwa njia yoyote ile, ikiwemo kuwachafua. Sasa basi, njia ya kumbana, ni kumpa madaraka yatakayo mlazimisha kuwa upande wa serikali.

     Kumbe mbunge wa Urambo Mashariki hakuwa na maamuzi ya kukubaliana au kutokukubaliana na pendekezo hilo, ilikuwa ni LAZIMA AWE SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, atake asitake!

     Akakataa.

     Alikataa katu katu, na kila alipotakiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo, aliendelea na msimamo wake.

     Aligoma kuchukua fomu.

     Alidhani masikhara.

     Muda wa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania kiti cha uspika uliyoyoma, mpaka siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la kurejesha fomu hizo ilipofika, Hayati mbunge wa Urambo Mashariki hakuwa amechukua fomu. Upande wa kambi ya rais, hali ilikuwa tete.

      Nusu saa kabla ofisi ya msajili wa wagombea uspika haijafungwa, mbunge wa Urambo akiwa Dodoma, wakati huo shughuri za bunge zilikuwa zikiendelea mkoani humo, hotelini amejipumzisha, alipata ugeni wa ghafla. Alishangaa.

      Alikuwa ni aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kwa wakati huo alikuwa amestaafu nafasi hiyo. Alimjia akiwa amebeba brifkesi. Baada ya salamu, mkuu huyo wa mkoa mstaafu, akampatia ujumbe mzito ulitaka kumtoa roho mbunge yule.

     “Nikiwa kama katibu mkuu wa chama tawala taifa ajaye, nimeagizwa kwako na mwenyekiti wa chama taifa ajaye, kukuhabarisha kwamba, swala la wewe kuwa spika wa bunge halina option. Your ordained to be a parliament speaker, what ever you like it or not…”  Yule baba mtu mzima ambaye mvi zilikuwa zimeanza kukizengea kichwa chake alizungumza kwa kumaanisha. Mbunge wa Urambo Mashariki aligwaya.

     Alimuelewa vema kwa namna alivyojitambulisha, katibu mkuu wa chama tawala ajaye, maana yake ndiye mtu aliyekuwa akiandaliwa kushika nafasi hiyo,  kupitia uchaguzi mkuu wa chama, ambao ungefanyika miaka miwili baada ya hapo, kwa mujibu wa katiba ya chama tawala. Mambo ya siasa hayo!

      Na huyo mwenyekiti wa chama taifa ajaye, ni rais wa Tanzania, Mr. Smile, ambaye kwa mujibu wa chama kilichomuweka madarakani, katika uchaguzi mkuu wa chama uliokuwa ukisubiriwa, alipaswa kuwa mwenyekiti wa chama.

      Mbunge wa Urambo akiwa bado anashangaa shangaa, kutoka kwenye brifkesi yake, mgeni wake alichomoa makarabasha fulani. Akatoa karatasi chache zilizoambatana kwa kubanwa na pini ya mashine ya stepla. Akamkabidhi asome.

     Zilikuwa ni fomu za kuomba kugombea uspika, zilizojazwa kila mahali palipompasa muombaji ajaze, ikiwemo wadhamini. Jina la mgombea lilikuwa lake yeye mbunge wa Urambo Mashariki. Wadhamini na kila kitu kilikuwa tayari, kasoro saini yake tu.

     Mbunge wa Urambo Mashariki alihisi mwili ukimtetemeka, jasho likimvuja kwa wingi kwa hamaniko, ama hakika, alikuwa amepatikana. 

     Uso wa mbunge wa Urambo Mashariki ulisawajika vibaya. “Eti niniiii…?!”  Alihoji kwa mshangao.

     “Yes sir…this is it.” Yule mgeni alimjibu mwenyeji wake, akimaanisha, hiyo ndiyo hali halisi.

      “Hivi you guys, are you out of your mind or…?!” Mbunge wa Urambo alimkemea akimaanisha labda timu ya rais imechanganyikiwa, na alimtusi kwa  yale maneno huku akimtazama moja kwa moja usoni, macho ameyakunja kwa kukunja ndita, kidole cha mwalimu akikizungusha hewani karibu na upande wa kichwa chake akisistiza usemi wake.

     “Mi nahisi mmechanganyikiwa, hamko sawa nyie. Yaani, mmenipora kiti changu, nimetulia nawaangalia tu, sa ivi mni force kugombea uspika!”

     “Sio ugombee..! Uwe spika. Na ushakuwa spika.” Mkuu wa mkoa mstaafu, aliye wahi kutunukiwa  cheo cha uluteni na jeshi la wananchi la Tanzania alimjibu, naye akitumia staili ileile ya kumtazama mwenzake usoni moja kwa moja.

      “SITAKI SASA…”

      “HAIJALISHI… UWE UNATAKA UWE HAUTAKI…tia saini kwenye hizo fomu. Muda unayoyoma, nasubiriwa kuziwasilisha ofisini kwa msajili wa wagombea…ni amri sio ombi.”      

        Aiseee…

        Walitazamana!

         Mbunge wa Urambo alifura kwelikweli, mgeni wake akimtazama kwa kumaanisha, nyusi za macho akizivuta kwenda juu.

         “Saini pleaseee…”

         “Sisaini, kwani lazima?!”

      “Ndiyo ni lazima…Sikiliza bro, haya mambo hayaendi hivyo utakavyo. Hii ni siasa, na wewe umekaa kwenye siasa muda mrefu, nadhani unaijua vema siasa. Kuwa makini kaka, tena uwe mpole, ukijitia mjuaji utakuja kupotezwa, hutakaa uamini.”

        “Unanitishia?”

        “Sikutishi…nikutishe ili iweje, nakueleza ukweli, nikuelezacho ndiyo hali halisi…bado hautaki?”

        Hofu.

        Mashaka.

        Taharuki.

        Wasiwasi.

        Mbunge wa Urambo Mashariki akatia saini.

        Hakukuwa na mazungumzo baada ya hapo, yule mgeni aliaga akaondoka zake, huku akimtakia majukumu mema yajayo ya uspika wa bunge, mbunge wa Urambo Mashariki.

        Siku ya uchaguzi ilifika, majina ya wagombea yakatangazwa. Wabunge wakapiga kura. Matokeo yalipotangazwa, mbunge wa Urambo Mashariki aliibuka kidedea, akifatiwa na spika wa bunge aliyemaliza muda wake, ambaye naye aliwekwa kugombea kama geresha, ambaye siku chache kabla ya uchaguzi aliutangazia umma wa watanzania kwamba hato gombea tena kiti hicho. Eti ghafla, akatangaza nia ya kuwania uspika. Akagombea. Akabwagwa. Mambo yakaishia hapo.

     Hapana, mambo hayakuwa yameisha. Ndiyo kwanza yalikuwa yameanza.

    Aliyedhani mambo yameisha, alijidanganya. Sana tu!

    Ndiyo kwanza, palikuwa pamekucha…

*****

     Mambo hayakuishia hapo, moto uliendelea kufukuta chini kwa chini. Baadae, mbunge wa Urambo na spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, aliungana na wenzake kadhaa walioenguliwa kwenye uteuzi wa nyadhifa mbalimbali.

     Walikuwepo mawaziri ambao rais aliwabadilishia wizara, tofauti na mategemeo yao kulingana na mtandao. Pia wapo waliotoswa kwenye nafasi fulani fulani za madaraka. Wote hawa kwa wingi wao, wakatengeneza umoja wenye lengo la kumuondoa madarakani Mr. Smile kabla hajamaliza miaka yake kumi ya utawala.

     Walikusudia kumdondosha kupitia uchaguzi wa awamu ya pili, baada tu ya miaka mitano ili kumfunza adabu. Na aliyepaswa kuchukua kiti chake, alikuwa ni spika wa bunge. Aiseee…

     Mikakati mbalimbali ikafanyika kufanikisha adhima yao. Wakianza na mkakati mkubwa na maalumu sana wa kuibomoa ngome ya Mr. Smile. Na njia pekee, ilikuwa ni kumtenganisha yeye na nguvu yake kubwa iliyomsaidia sana hata katika harakati za kuelekea ikulu, swahiba wake, mzee wa mvi nyingi. Alooo….

      Wakaandaa mpango wa kumpelekea maneno ya uongo rais, kwamba, waziri mkuu ana mpango kamambe wa kumuondoa madarakani baada ya miaka mitano tu ya utawala wake. Kwamba, hataki kusubiri mpaka miaka kumi kama walivyokubaliana. Ati atagombea urais uchaguzi ulitegemewa kufatia, katikati ya mihula ya utawala wa Mr. Smile, ndio maana anachapa kazi si mchezo.

     Wakati maneno hayo yanamfikia muheshimiwa rais, sifa kemkem kuhusu utendaji kazi uliotukuka zilikuwa zikimuandama waziri mkuu nchini kote. Ni kweli, waziri mkuu alikuwa akichapa kazi kwelikweli.

     Hizi zilikuwa kati ya taarifa mbaya alizowahi kuzisikia mzee wa tabasamu. Aliumia sana. Hakutegemea kama kweli swahiba wake anaweza kumuwazia namna ile. Ili kujiridhisha ikambidi ahoji baadhi ya watu.

     Kosa la kwanza!

     Majibu aliyopewa, yakashabihiana na aliyoambiwa hapo awali. Waziri mkuu anampango wa kugombea urais, akunyang’anye hicho kiti ndani ya miaka mitano, ndio maana anafanya kazi kwa bidii ili kujiongezea thamani kwa watanzania. Muheshimiwa rais hoi!

     Hakujua!

     Kwamba, watu aliowauliza, waliandaliwa na kundi la waasi ili kumpotosha. Rais akadanganywa.

     Anafanyaje sasa…

     Hakuna namna, njia ni moja tu, kumdhibiti jamaa asifanikiwe.

     Ana mdhibiti vipi sasa…

     Njia raisi ya kumvunja nguvu, ni kumuondoa kwenye uwaziri mkuu, kwa sababu huo ndio unaompa nafasi ya kuchapa kazi inayoonekana kwa upana sana machoni mwa watanzania. Ana muondoa je kwenye uwaziri mkuu… Swahiba!

       Kosa la pili!

      Akaambiwa atulize boli wala asipate taabu, akapewa mbinu, na haohao wanafiki. Kutoka mafichoni, yakapekuliwa mafaili yaliyochimbiwa miaka kadhaa iliyopita. Yakawekwa mezani. Kutoka kwenye hayo mafaili, ikatengenezwa kesi kumuhusu yeye waziri mkuu muwindwaji, kwamba aliwahi kutia saini makubaliano fulani, yaliyoliingiza taifa kwenye hasara ya mabilioni ya shilingi.

    Kesi ile akapewa moja kati ya wabunge wa upinzani, akaandaliwa, akapangwa vya kupangwa, akapewa ruhusa na spika wa bunge ailipue bungeni.

    Kichaa kapewa rungu, yule mbunge wa upinzani tena kijana mdogo, machachari katika kuzungumza na kuwasilisha hoja zake, afanye nini zaidi ya kutumia ile fursa jichukulia ujiko. Akatoa hoja bungeni.

    Spika wa bunge aliye kwisha kujinadi kwamba, yeye ndiye spika bora na mfano wa kuigwa kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru, anaruhusu hoja zote za wabunge bila upendeleo wa huyu ni wa chama tawala, na yule ni wa chama cha upinzani, akaruhusu mjadala ufanyike, waziri mkuu kikaangoni moto ukamuwakia.

     Ilikuwa ni kashifa kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania, iliyomchafua mzee wa mvi nyingi, asijue kwamba rais anahusika, aliowageuka akisaidiana na swahiba wake ndio wanao mchoma. Bwana Mvi alitahayari kwelikweli.

      Huku na kule kule na huku, akajikuta katikati ya chumba cha moto. Hana pa kuchomokea, hana msaada, kila aliyemtegemea akawa kinyume nae, alishangaa namna mambo yalivyomgeukia.

      Tume ya uchunguzi iliundwa na spika wa bunge, nayo ikarudisha majibu. Waziri mkuu akaonekana mkosaji. Fisadi. Kuona hivyo, muheshimiwa waziri mkuu akaona isiwe taabu, akaamua kuwajibika kama kiongozi.

     Akasimama bungeni na kuongea, kwamba amemuandikia barua rais ya kujiuzuru uwaziri mkuu, akasema, “…najua tatizo sio…{akataja jina la ile kashifa iliyokuwa ikimsulubu}, tatizo ni uwaziri mkuu, let me grand them their wish…” akamalizia kwa kimombo, akimaanisha acha awapatie hitaji lao.

     Inaonekana mpaka kufikia hapo, muheshimiwa huyo aliyekalia kuti kavu, alikuwa amesha baini nini sababu ya akina fulani na fulani kushadadia kwamba yeye ni fisadi, kahusika na upotevu wa mabilioni ya watanzania. Lakini hakuwa amejua kwamba, mshikaji wake alishatiwa ndimu, na sasa ilikuwa ikimpa kimuhemuhe cha kuhakikisha anamshuhudia mmoja ya wana boys to men anapotezwa kwenye ramani ya siasa. 

     Wakati akimtumia rais ile barua ya kujiuzuru, kumbe moyoni alitegemea swahiba wake huyo atakataa ombi lake na kumsimama kidete kumtetea ili aendelee kushika hatamu ya uwaziri mkuu. Si alimwambia usihofu, we andika barua ya kuniomba kwamba umeamua kujiuzuru uwaziri mkuu, kisha mimi ntalihutubia taifa, nitabatilisha ombi lako, kisha ntawaambia watanzania tuwe na subira wakati tukifikiri namna ya kulitatua hilo. Bwana Mvi akakubali. Alijidanganya!

     Kilichofatia, mara tu baada ya rais kuipata barua hiyo, aliisundia kwenye droo zake ikulu, akanyanyua mikono juu, akamshukuru Mungu. Akapata ahueni.

     Alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na ile kashifa, akaueleza umma wa watanzania kuhusiana na waziri mkuu kumuandikia barua ya kutaka kuwajibika kama kiongozi. Akasema kwa moyo mweupe, ameridhia ombi hilo, na atamteua waziri mkuu mwingine.

     Bwana Mvi hoi!

    Watanzania hoi!

    Rais kamgeuka swahiba wake…

    Huo ndio ukawa mwisho wa ushikaji wa boys to men.

    Baada ya hapo, mambo mengine mengi yaliendelea, mengi yalisemwa, mengi yalipita, lakini, rais alijikuta katika wakati mgumu sana kiutawala, bila shaka aliijutia sana dhambi ya kuwageuka wanamtandao.

     Spika wa bunge na timu yake ikafanikisha mpango A. Mikakati kadha wa kadha ikaendelea, ikiwa ni pamoja na kuanzisha chama chao chenye lengo la kumtoa Mr. Smile madarakani.

     Wakati huo Mr. Smile naye hakuwa poyoyo, alishawagutukia wabaya hao mipango yao, akafanya ya kufanya, chama cha akina spika wa bunge kikakosa usajiri. Kukosa usajiri, kikakosa sifa na vigezo vya kushiriki uchaguzi wa muhula wa pili wa utawala wa hasidi wao mkuu. Kikapotezwa. Jamaa wakadhitiwa wakadhibitika.

       Waziri mkuu mstaafu naye akaanzisha harakati zake za yeye  kama yeye, safari ya kuelekea ikulu. Alikuwa na nguvu ya ushawishi sio kidogo. Kwa kadri muda wa uchaguzi mkuu ulivyokuwa ukisogea, Mr. Smile alizidi kumgwaya jamaa. Alijua fika, kama adui yake huyo atachukua nchi, kwa mabaya aliyomfanyia, asingemuacha salama.

     Ikambidi naye apambane kiume kumdhibiti. Nguvu ya mzee mwenye mvi zake za asili, ilikuwa kubwa na ya kutisha sio mchezo. Mzee wa tabasamu alitishika sio kidogo.

     Katika uchaguzi wa kumpata rais atakayeingia madarakani kumrithi mzee wa tabasamu, aliyekuwa akimaliza muda wake, mapambano makali yalifanyika ndani ya chama tawala, lakini kikubwa ilikuwa kumdhibiti mtu mmoja aliyekuwa na wafuasi wengi na ushawishi mkubwa, bwana mvi. Mzee wa kutabasamu akafanikiwa kumdhibiti rafiki yake wa zamani, hasidi wake mkubwa wa zama hizi, japo ilikuwa kwa mbinde sana.

   Mzee mwenye mvi zake za asili akakosa nafasi ya kugombea urais, baada ya kunyimwa ridhaa hiyo na chama chake. Huku na huko huko na huku, akahama chama!

    Hakukubali kushindwa.

    Ameuota urais kwa zaidi ya miaka 20. 

   Akahamia moja ya chama cha upinzani kilichokuwa na ushawishi mkubwa, kilichoungana na baadhi ya vyama vyenzake vya upinzani, na kujenga umoja wao wenye nia ya kuking’oa chama tawala madarakani.

   Huko nako nyota ya mzee mwenye mvi nyingi ikaendelea kung’ara, awamu hiyo maradufu zaidi. Umoja wa vyama vya upinzani vikampitisha kugombea urais kwa tiketi ya chama alichohamia. Weee…

    Sio siri, hali ya chama tawala ikawa hatarini, kukawa na kila dalili kwamba, utawala wa chama tawala unaenda kukoma. Jamaa alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi, alikuwa tishio kubwa kwa chama tawala. Ikabidi mikakati mikubwa mikubwa ya kumdhibiti muheshimiwa waziri mkuu mstaafu huyo zifanyike. Na ni katika mikakati hiyo, moja wapo, niliitafutwa mimi kupitia wale wanausalama wa taifa.

    Kazi yangu ilikuwa ni moja tu, kupitia fani yangu ya maswala ya IT, kama nilivyoweza kufanikisha wizi wa mchanga wa mgodi wa GGM, nilipaswa kuhakikisha nafanikisha zoezi la kuchakachua matokeo ya kura za bwana mvi.

   Bwana Mvi alionekana kuwa tishio, na kulikuwa na kila dalili ya kupata kura ambazo zingetosha kumpeleka ikulu. Hili halikutakiwa kabisa. Hivyo basi, mimi na wenzangu kadhaa tuliyopewa jukumu hilo, tulipaswa kuhakikisha tunabatilisha matokeo ya kura alizo pigiwa yule mtu aliyeonekana kama adui wa taifa, kwa njia ya mtandao.

    Hilo tu!

*****

Naweza kusema kwamba, wale usalama wa taifa walinipatia kwelikweli, hakuna kinacho nishinda kwenye maswala ya IT. Kwa namna walivyo ninusuru na kifo kilicho ratibiwa na mjomba wangu, mdogo wa damu wa mama yangu, tumbo moja toka nitoke, sikuwa na namna zaidi ya kuwarudishia fadhila.

Kweli, niliutumia ujuzi wangu wote, pengine na utundu wangu wote niliokuwa nao. Nikaifanya kazi yao vema. Wao wenyewe waliifurahia mno kazi yangu, na hawakujuta kunitumia. Nililipwa ujira wangu stahiki, kama tulivyokubaliana. Ujira mnono!

Namshukuru sana Mungu, watu hawa hawakuwa wasumbufu lilipokuja swala la malipo. Tukafika tamati ya kazi kwa ushindi mkubwa, kwani mwisho wa siku, yule mwanasiasa aliyekuwa akitutoa jasho, Bwana Mvi, aliambulia patupu.

Tulimshinda kwa kishindo.

Akatoka kapa.

Kwa mara nyingine, chama tawala kikaendelea kushika madaraka ya juu kabisa kitaifa, kwa kuikamata dola, kikawa na ridhaa ya kuongoza nchi.

Ni katika kutekeleza majukumu yangu, ndipo nilipojua siasa sio swala la kuzungumzia ki juu juu. Watu wengi huko mitaani wanaizungumzia siasa utadhani wanaijua.

Siasa sio ile tunayoipigia zoga kwenye vijiwe vya kahawa, tukipoteza muda wa kurudi nyumbani tukikwepa kelele na magomvi ya wake zetu, hapana. Siasa halisi ni siasa ya ndani. Achana kabisa na siasa hususani kama huijui, siasa ina wenyewe.

Mwisho kabisa, niliachana na wale watu kwa amani asilimia mia moja.

Lakini…

Walinipatia sharti moja gumu mno, lililo nisononesha na kuumiza sana moyo wangu.

Niliujutia ushirika wangu na hawa watu.

      Kuanzia siku hiyo tuliyopitisha maafikiano hayo, niliishi kwa kujisimanga sana mimi mwenyewe. Nilijutia kuingia maagano na watu waliokuja kuniweka kwenye wakati mgumu namna ile.

     Ama kwa hakika, sikuwa na uhakika wa kuweza kuitekeleza amri yao, kwani ili uumizaa sana moyo wangu, wakati huo huo, kigezo cha, ni  watu hatari kiasi gani walionipa ile amri nikikizangatia. Sana tu!

MIEZI KADHAA BAADAE

      Msitu wa mabwepande! Mpita njia mmoja aitwae Majaliwa, au baba Ezekiel, akiwa amelewa chakali, ndiye mtu pekee aliyeweza kushuhudia tukio la kutisha usiku ule.

     Akiwa amelewa tapatapa tilalila, akipiga miluzi ovyo, na kuimba nyimbo zisizoeleweka, alijikuta pombe yote ikimtoka kichwani, ghafla, wakati akifatilia tukio la ajabu, lililommakinisha isivyo kawaida yake. Na ama hakika kila alichokiona, kuna wakati kilimfanya ajihisi anaota ndoto.

   Aliacha kuimba nyimbo zake zisizoeleweka. Miluzi yake ya hovyo ikakoma. Akabaki ameduwaa, kimya kimya, hatua kwa hatua, kwa tahadhari ya kutogundulika uwepo wake mahala pale, akafatilia tukio lote lililompiga bumbuwazi.

   Ulikuwa ni siku mkubwa, mida ya saa tisa. Manyunyu ya mvua iliyonyesha kutwa nzima, pamoja na ule usiku, yaliendelea kuchuruzika. Ikiwa ni saa chache kupita tangu mvua kubwa isitishe kunyesha. Giza zito liliugubika msitu wa Mabwepande, uliopo pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam, barabara ya Bagamoyo.

  Gari aina ya Toyota Hiluxe double caben, rangi nyeusi iliyoiva, ikiwa imefungwa vioo vyake vyote, ilikuwa ikipita kwenye barabara kubwa ya pori hilo usiku huo, muda huo. Hali ilikuwa ni ya utulivu usioweza kufananishwa, na upweke wa mandhari ile usioelezeka.

  Ni katikati kabisa ya eneo ambalo, kwa mtu wa kawaida lingemtisha kulikatiza mida hiyo. Lakini ile gari ilikatiza, tena polepole kwa mwendo wa madaha.

  Mtu mmoja asiyejulikana, aliendelea kunyonga usukani kwa mkono mmoja wa kuume, bila tashititi wala hofu.  Mkono wake wa kushoto mara kadhaa aliutumia kukamata ufito wa sigara yake kubwa ya ki Marekani, maarufu kama American cigaretee, aliyokuwa akiivuta kinywani mwake kwa kuunyonya ufito wake utadhani alikuwa akinyonya pipi aina ya rollpop.  

  Aliiacha barabara, akaiingiza ile gari katikati kabisa ya pori la ule msitu unaoogopeka. Msitu uliogubikwa historia mbovu chungu mzima. Msitu wa maovu mengi.

   Aliipaki ile gari mahali fulani, jirani kabisa na shimo kubwa. Lile shimo, lenye urefu wa futi sita na upana wa futi mbili, kwenda chini lilikuwa na urefu wa futi nne au tano. Lililoonekana lilichimbwa siku si nyingi. Kwa sababu udongo uliokusanyika kando, kwa maana ya udongo ulioondolewa wakati wa kuchimbwa kwake, ulikuwa mbichi, na haukuwa umeshikamana kabisa. Na haikuwa ajabu kwamba; lilikuwa limechimbwa siku hiyo hiyo!

  Yule bwana, alipopaki ile gari, alizima injini kisha akatoa roki za milango. Akatelemka kwa kutanguliza mguu wa kuume chini. Akaidondosha sigara yake ardhini, akaizima kwa kuisagasaga kwa buti yake kubwa aliyoivaa. Kisha akashusha mguu wa kushoto, akatoka garini na kufunga mlango.

   Akiwa ndani ya jaketi lake maalumu kwa ajiri ya kumstiri na mvua, rain coat kwa kimombo, alijitikisa tikisa mwili wake ili kuufanya uchangamke. Kisha akaanza kupiga hatua za kuhesabu, akiuendea mlango wa nyuma wa ile Toyota Hilux double caben.

   Akaufungua.

   Akaanza kuhangaika kunyanyua furushi la mfuko wa plastiki, lililotapakaa damu ndani yake. Akafanikiwa kuliondosha ndani ya gari, akalibwaga chini. Lilikuwa kubwa haswaa. Alishusha pumzi kuashilia lilikuwa zito kwelikweli.

   Ndipo akatoa koleo na jembe. Navyo pia alivibwaga pale ardhini. Akaanza kuliburuta lile furushi, ambalo ndani yake haikujulikana kulikuwa na nini. Akalisogeza mpaka kando ya lile shimo, akalitupia ndani yake. Akalirudia jembe na koleo, akaanza kuvitumia kulifukia lile shimo.

   Jamaa alikuwa jabali mwenye nguvu kwelikweli. Haikumchukua muda kukamilisha ile kazi. Akarudisha zana zake garini, akazipaki vema. Naye akajitoma ndani. Akawasha gari, akapandisha mafuta, akaiondosha kwa mwendo mkali. Tofauti kabisa na ule aliokuja nao. Yote hayo, yalishuhudiwa na yule mlevi, ambaye mpaka wakati huo, ulevi ulikuwa umemwisha kwa wahka.

*****

“Ngoo…ngoo…ngooo…” “Ngooo…ngooo…ngoo…” Sauti kubwa ya kugongewa mlango wa sebuleni, ilimkera bi Chausiku Majaliwa. Muda huo, yeye na wanae walikuwa wamekwisha jipumzisha kwa usingizi mzito, kasoro mme wake aliyekuwa hajarejea, tangu alipoondoka mchana wa siku hiyo.

Haikuwa ajabu, kwani ndio kasumba ya Majaliwa. Siku zote amekuwa na kawaida ya kuondoka na kurejea usiku mkubwa, akiwa amelewa chakali tilalila kwa pombe za kienyeji.

“Mama Eze fungua mlango haraka, fungua mlango haraka sana.” Mama Ezekiel akastaajabu. Imekuwaje siku hiyo mumewe agonge mlango kwa kumuita jina lake. “Fungua mlango mke wangu, tafadhari.”

‘Makubwa… leo naitwa mke wangu.’ Alijisemea kimoyo moyo yule mama wa watoto sita. Alishazoea kuitwa wewe mbwa kasoro mkia, wewe ng’ombe, fungua mlango. Ikawaje siku hiyo akaitwa mke. Tena mke wangu.

‘Kuna kitu.’

Alizidi kujiwazia wakati akiinuka kwenye kitanda chao cha chuma, kilichotandazwa spring katikati kwenye eneo la kulaza godoro. Na godoro lililozwa kwenye hizo springi, lilikuwa la pamba lililochakaa mno. “Oh! Mme wangu…nakuja jamani pole pole.”

Akawasha karabai. Akajitanda kanga. ‘Mtu unajua fika kwamba huo mlango ni mbovu, unagonga kama unakimbizwa, maana yake nini? Au unataka kuumalizia kabisa tuwe tuna lala mlango wazi?’ Akafyonza huku akitoka chumbani, akaelekea mlangoni alikokuwa akigonga mume wake. Na kadri alivyokuwa akiusogelea mlango, ndivyo kasi ya ugongaji ikazidi. Na kadri fujo za kiugongaji zilivyozidi, ndivyo alivyozidi kumchefuka.

Na abadani asilani, pamoja na kwamba alishakuwa muhanga wa kudumu wa changamoto hiyo, ya kurudiwa yumbani na mume wake mida hiyo, kwa fujo nyingi, kamwe ile hali hakuwahi kuizoea.

“Mume wangu unafujo wewe, khaa!” Yule mwana mama alilalama wakati akiufungua ule mlango uliojiozea kwa kutafunwa na michwa, usio kuwa na tegemeo la kufanyiwa marekebisho leo wala kesho. Kwani baba mwenye mji hakuwa na cha maana akiwazacho. Maisha yake yote, ni yeye na pombe, pombe na yeye.

Aliufikia mlango, moyoni akiwa na faraja kidogo, angalau siku hiyo hakuitwa nyau, mbwa, au ng’ombe. Na kwa mara ya kwanza, aliitwa mke wangu. Sio siku yake ya bahati hiyo jama!

Alipofungua, akitazamia kukutana na mume wake, alistuka mno. Almanusura aanguke kwa kihoro. Mgongaji hakuwa mume wake. Alikuwa ni mwanaume mwingine kabisa.

“Kaaa! Ni macho yanguuu… au naota?!”

“Ni kweli na hakika shem, ni mimi ndiye niliyekuwa nagonga kwa kugeza sauti ya mumeo, ili uwahi kufungua. Siku nyingine kuwa makini sana, utakuja kufungulia majambazi.” Kijana mmoja aitwae Masumbuko alizungumza. Mama Ezekiel akabaki akitetemeka kwa kihoro. Ama hakika alichokiona hakukitegemea. Na kwa namna alivyo ivaa ile kanga kwa kuiegesha, kulimfanya ajisikie aibu.

“Kumbe unajua fika kwamba mimi ni shemeji yako, sasa kisa cha kuwa unanitongoza ni nini? Na usivyo na haya wala usiyejua vibaya mwanaume wewe, umeamua kuniijia usiku usiku nyumbani kwangu ili?! Kwa kuwa unajua kwamba mume wangu hayupo ndio ntakukubalia huo upuuzi wako…?! Baba umenoa, hapa andika maumivu. Kukuhakikishia maneno yangu, kufumba na kufumbua, nahesabu moja mpaka tatu, naomba uwe umeondoke haraka sa…”

“M…mh…! We mwanamke punguza jaziba. Kwa hiyo.., we kila ukiniona unawaza kutongozwa tu?”

“Kwani huwa una jipya gani zaidi ya kuninyima raha. Kila siku,  kila saa, kila mahali niendako ni kunifatilia tu kwa huo upuuzi wako.”

“Sawa basi nimekubali, lakini leo ndio utaujua huo upuuzi wangu. Nimekuja kukupasha habari. Cha pombe wako kaokotwa hukooo, njia panda ya Mabwepande. Yuko hoi bin taaban hajitambui, wasamalia wema wamemkimbiza hospitali ya Mwananyamala. Kazi kwako, kwa heri.” Masumbuko alipomaliza kutoa maelezo hayo, akaanza kuondoka. Mama Majaliwa akamtaka arudi.

“Sasa ndio nini shemeji. Hivi unaweza kunipa taarifa ya namna hiyo kienyeji enyeji halafu unajiondokea tu. Hakuna ufafanuzi wala mazungumzo ya kina.”

“Mazungumzo gani ya kina utakayozungumza na mpuuzi. Mi sikila siku nakufukuzia kukueleza upuuzi wangu. Upuuzi gani ntakao endelea kuuzungumza hapa ukanielewa.”

“Kwa hiyo we usiambiwe ukweli kisa utanuna. Kwani uongo, huwa haunitongozi wewe…” Hakumalizia sentesi yake, Masumbuko akamdakia.

“Kweli mama. Na umesema unanihesabia moja mpaka tatu niwe nimeshaondoka, ndio kama hivyo naondoka. Au hiyo tatu bado haijatimia”

“Hebu acha mambo yako wewe mwanaume. Kuwa serious. Ni kweli uliyoyasema au unanizingua tu?!”

“Khaaa…! Kweli ee.”

Mama Ezekiel machozi yakaanza kumlengalenga. “Amepatwa na nini jamani mume wangu?” Alihoji huku akianza kuomboleza.

“Inahisiwa amegongwa na gari. Kapasuka vibaya kisogoni na ana majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwilini. Sijui hata kama atapona”

“Looh! Pombe hizo. Jamani mwanaume huyu atakuja kuniua kwa presha mimi. Kila siku namwambia hizo pombe za kuwa zinamrudisha nyumbani usiku, ipo siku atatuletea balaa sisi.” Alizidi kulalama yule mwana mama.

“Akipona ndio umkanye sasa, anatupa shida sisi. Hii ni mida ya kujipumzisha na ‘mabae’ wetu, badala yake ona sasa tunavyohangaika.”

Wakazungumza kwa kirefu, kisha wakakubaliana waelekee hospitali ya Mwananyamala kesho yake asubuhi, ili kumjulia hali majeruhi.

*****

Konstebo wa polisi Kova Mura, alitoka ofisi anayofanyia kazi, akaelekea moja kwa moja ofisini kwa Superintendent Mwita Marwa. “Jambo afande.” Alimsalimu huku akisaluti, mara tu baada ya kuingia kwenye ofisi hiyo, ndani ya kituo cha polisi cha Wazo Hill Tegeta.

“Jambo. Karibu, pita uketi.” Ndivyo Superintendent Mwita Marwa alivyo mlaki mgeni wake. Naye alikuwa ameketi kwenye kiti chake cha mbao kilichokuwa kikitazamana na meza ya mbao ya seplus.

“Nimeitikia wito wako mkuu.”

“Pasina shaka. Nimekuita hapa, kuna dharula imejitokeza afande.” Superitendent Mwita alianza kumpa maelekezo. “Kuna tukio limetokea usiku wa kuamkia leo…” Pua zake zika tanuka na kusinyaa, ukimya mfupi ukapita. “Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni cha pombe aliyepindukia, amekutwa njia panda ya barabara ya Mabwepande. Amelala hoi bin taaban, hajitambui wala hajiwezi. Na kuna kila kiashiria kwamba, atakuwa aligongwa na gari.”

Wakatazamana usoni, mpaka muda huo Konstebo Kova Mura hakuwa amekusudia kutia neno lolote. Aliendelea kuwa mtulivu, akiyafatilia kwa umakini mkubwa, maelezo ya mkubwa wake wa kazi.

“Sasa basi…” Superitendent Mwita aliendelea, “…nakuagiza uende hospitali ya Mwananyamala sasa hivi. Wodi ya majeruhi, ukafanye uchunguzi wa hali ya majeruhi huyo, pia ufanye upelelezi, kufikia jioni ya leo, uwe na majawabu ya awali kuhusiana na tukio hilo.”

“Ni akina nani waliofikisha habari hizi hapa kituoni?”

“Wasamalia wema waliomuokota, na ndio waliomkimbiza hospitalini. Kisha waakagawana majukumu. Wengine wakaleta lipoti hapa.”

“Hao wasamalia waliomuokota na kumkimbiza hospitali, na kufikisha lipoti hapa pasi nashaka wanamtambua majeruhi. Ama?”

“Of course… Ni mwana kijiji mwenzao, na ndio waliotupa ushuhuda kwamba, majeruhi ni cha pombe aliyepindukia.”

“Awali umeniambia kwamba, inahisiwa majeruhi atakuwa aligongwa na gari…” Superitendet Mwita Marwa akamuunga mkono kwa kutikisa kichwa. “Inahisiwa, kwa hivyo hakuna uhakika huo. Kwa nini inahisiwa hivyo, na si vinginevyo?”

“Ni kulingana na mazingira aliyokutwa majeruhi.” Mwita akaanza kufafanua. “Amekutwa amelala chali, kwa mtindo wa kuanguka na kujipigiza vibaya ardhini.” Akaendelea. “Ameumia sana tumboni na kisogoni, damu nyingi ikimtoka mdomoni… Na. Kumeonekana alama za msuguano wa tairi za gari jirani na alipoangukia majeruhi huyo.”

“Oke… majeruhi huyo anaitwa nani?”

“Anaitwa Majaliwa Makanyaga.”

“Oke… nadhani nina maswali mengi ya kuanza nayo. Na haita kuwa busara kukutupia mzigo huo. Kwa sasa, niruhusu nielekee hospitalini kwanza, huko alikolazwa cha pombe.”

“Nakuruhusu. Nakutakia kila la heri na mafanikio mema kwenye jukumu hili.”

“Shukrani mkuu. Tegemea lipoti nzuri kutoka kwangu kabla jua halija zama.”

“Nakuamini Kova.”

*****

Gari aina ya Spacio, mali ya Konstebo Kova Mura, ilikuwa kwenye mwendo kasi mkubwa. Uskani ulishikiliwa na Kova Mura mwenyewe, wakati kiti cha pembeni yake aliketi askari mwingine. Alikuwa ni Private Hamis Abdallah.

Walishuka kilima cha Wazo, almaarufu kama Wazo Hill. Walipofika Tegete Kibaoni, walikamata barabara ya Bagamoyo kwa kukunja kulia, moja kwa moja upande wa kuelekea mjini.

Dakika arobaini na tano baadae, walikuwa maeneo ya stendi ya Makumbusho, wakiikamata barabara ya vumbi, inayo elekea hospitali ya Mwananyamala. Dakika chache sana baadae, walikuwa wamepaki gari hiyo, eneo la kuegesha magari ya wageni, lililomo ndani ya hospitali hiyo.

Waliteremka, na kuhakikisha wameiacha gari katika hali ya usalama. Wakapiga hatua za miguu kuelekea wodi ya majeruhi. Walipofika, walipokelewa na nesi mmoja ambaye walijitambulisha kwake, pamoja na nia ya ujio wao hospitalini hapo. Nesi yule bila kuwapotezea muda, moja kwa moja aliwapeleka kwenye chumba cha mganga wa zamu. Akawakabidhi kwa dokta Peter.

“Habari za kazi dokta?” Kwa pamoja walimsabahi wakati wakimkabidhi vitambulisho vyao vya kazi.

“Nzuri tu, sijui nyie ndugu zangu?” Dokta Peter aliziitikia salamu zao kwa pamoja, wakati akiwaonyesha viti waketi. Akavipokea vile vitambulisho na kuanza kuvipitia, kimoja baada ya kingine. Ndipo alipogundua kwamba, ule ulikuwa ni ugeni wa kiserikari, polisi kutoka kituo cha polisi cha Wazo Hill Tegeta.

“Hatujambo.” Walimuitikia. “Sisi ni askari polisi kutoka kituo cha Wazo Hill Tegeta.” Konstebo Kova Mura alianza kujieleza. “Tupo hapa kikazi. Tumepewa lipoti juu ya uwepo wa majeruhi anayehisiwa aligongwa na gari usiku wa kuamkia leo, eneo la njia panda ya Mabwepande. Sijui kama una hizi taarifa dokta.” Akaweka kituo.

“Oh…! Pasina shaka mkuu. Majeruhi huyo tunaye, amepokelewa na wenzangu waliokuwa zamu ya usiku alfajiri kwenye mida ya saa kumi na moja.

“Okay.” Kova aliitikia.

Dokta Peter akakazia huku akitikisa kichwa, “Yup.”

“Vipi anaendeleaje?” Private Hamis Abdallah alimsaili dokta Peter, wakiwa wametazamana usoni.

“Hali yake ni mbaya sana. Waswahili wanasema, hali ya mgonjwa ni tia maji tia maji…” Konstebo Kova na Private Hamis wakatazamana. Dokta akaendelea, “…hajitambui, na pumzi zinamtoka kwa shida sana. Pia mapigo yake ya moyo yako chini mno.”

“Tunaweza kumuona?” Konstebo Kova alihoji.

“Bila shaka wakuu.”

Wakanyanyuka vitini, wakaelekea wodini kwenye kitanda alicholala majeruhi huyo.

Alikuwa kwenye moja ya vitanda kadhaa vilivyo kuwemo kwenye ile wodi ya jumla. Kando yake alikuwepo mama mmoja, ambaye dokta aliwatambulisha kwake, kama mke wa yule majeruhi. Pia aliambatana na watoto wake watatu kati ya sita aliozaa na mumewe. Wakike wawili, wakiume mmoja. Pia aliambatana na mdogo wa mume wake aitwae Masumbuko, yaani shemeji mtu. Huyu ndiye aliyempelekea mke wa majeruhi habari za balaa lililomkuta mumewe.

“Pole sana mama kwa matatizo.” Wale askari walimsabahi mke wa Majeruhi.

“Nashukuruni jamani.” Aliwajibu yule mama kwa sauti iliyokauka kwa kulia sana.

“Sisi ni polisi kutoka kituo cha Wazo, tupo hapa kufatilia hali na tukio la mume wako. Tayari tumeshapokea lipoti ya awali kuhusiana ya tukio hili kutoka kwa wasamalia wema. Ni faraja yetu tumekukuta. Tunahitaji kuzungumza na wewe mawili matatu mama.” Konstebo Kova alimueleza kwa kirefu yule mama.

“Haina shida baba,” aliwajibu yule mama huku uso ameutazamisha chini, kama anayewaonea haya wale askari.

“Labda kwa kuanza, ungetueleza kwa kifupi, kuanzia kuondoka kwa mume wako nyumbani, mpaka kupatikana kwake katika mazingira aliyokutwa, ilikuwaje?”

“Baba…” Yule mwana mama alianza kueleza. “…mume wangu huyu, ni kawaida yake kuondoka nyumbani mchana, kuelekea kwenye mataputapu na kuturudia nyumbani usiku mkubwa amelewa tapatapa. Hajiwezi. Hajielewi. Harufu ya pombe ni yake, mikojo ni yake. Kwa kweli sisi wanawake wengine tulioko kwenye ndoa, tuna vumilia mengi sana.” Machozi yakaanza kumbubujika mama wa watu.

“Pole sana mama.” Wale polisi walijikuta wakimpoza kwa pamoja, kama waliokubaliana.

“Ahsanteni… ndio misalaba tuliyoumbiwa wengine, na tumeshaipokea.”

“Mataputapu ndio nini mama?” Konstebo Kova alimuuliza.

“Ni pombe za kienyeji baba.”

“Ooohh… okay, pole sana.”

“Nashukuru.”

“Enhee…!” Kova akamtaka aendelee na mada.

“Sasa… hiyo jana. Ameondoka zake vizuri kama kawaida yake…” mama akaendelea kuwaeleza, “…na hakurejea tena. Mpaka nilipogongewa mlango na shemeji yangu huyo mnayemuona hapo…” Akawasontea Masumbuko “…ndiye aliyenipasha habari hizi. Na mpaka sasa hivi, sijajua nini hasa kimempata. Zaidi ya hisia za watu waliomuokota kwamba, atakuwa aligongwa na gari.”

“Zaidi ya hapo, huna ulijualo.” Kova alisistiza. Yule mama akamjibu, “Sina baba.”

Konstebo Kova na Private Hamis wakatazamana. Vichwa vikawauma kwa kuchanganyikiwa. Kesi ile iliwaingiza kwenye kizungumkuti, hususani kutokana na kwamba majeruhi alikuwa hoi bin taaban, asiye na dalili ya kuamka kwa muda huo. Pili, mtu aliyemgonga na gari, alitoweka eneo la tukio na hakujulikani alipo kuwa.

Itakuwaje.

Wale maaskari waliomba wapewe faragha watete kidogo. Dokta Peter akarejea ofisini kwake, wakawaacha mke wa majeruhi na wanae waliokuwepo pale.

“Aisee… hii kesi ni ya aina yake afande. Naanza kuona ugumu wa jukumu lililoko mbele yetu, au we mwenzangu unaonaje?” Konstebo Kova Mura alianza kumueleza Private Hamis waliposogea kando kidogo.

“Mkuu. Niko upande wako kwa asilimia zote kabisa. Hapa tulipo naona giza, mbele napo naona giza. Sijui hata tunaanzia wapi.”

“Kesi mbaya sana hii, lakini we had no choice, we should handle it.” Kova alimwambia Hamis. Akaendelea, “…sasa…ninachokiona hapa, we baki hapa hospitali. Msubiri huyu majeruhi mpaka azinduke, then umuhoji kilichojiri. Mimi niache nimchukue huyo shemeji wa mke wa majeruhi, anipeleke kwenye msitu wa Mabwepande eneo la tukio, nikafanye uchunguzi wangu. Nimekwambia Superitendent  Mwita anataka lipoti ya awali ya kesi hii, kabla jua halijazama. I hope you know him.”

“Exactrly.” Afande Hamis akamkubalia kauli. Wakayapanga ya kuyapanga. Wakafikia muafaka. Konstebo akazungumza na Masumbuko, na kumtaka waongozane mpaka alipookotwa yule majeruhi. Masumbuko hakuwa na kipingamizi. Wakaagana na mke wa majeruhi, wakaondoka wakimuacha Private Hamis.

Walifika eneo la kuegesha magari, wakaingia kwenye ile Spacio waliyokuja nayo. Kova akakanyaga mafuta, safari ya kuelekea msitu wa Mabwepande ikashika hatamu.

*****

Walifika njia panda ya Mabwepande, eneo alipookotwa baba Ezekiel kwa mujibu wa maelekezo ya Masumbuko. Konstebo akaanza uchunguzi wake kwa mujibu wa mbinu zake za kipolisi.

Akalikagua kwa ustadi lile eneo. Akianzia na mahala alipokutwa amelala baba Ezekiel. Ni kweli kulikuwa na kuchimbika kwa udongo kulikosababishwa na tairi za gari. Gari yenyewe sio kubwa sana wala ndogo sana.

Akaanza kuzifatilia zile alama za yale matairi, kwenye ile barabara yenye tope jingi lililosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha. Akatembea hatua kadhaa kurudi nyuma, akabaini kitu. Kwamba kuna tairi za gari zilizoacha barabara na kuingia kwenye shamba moja wapo eneo lile. Na huko mbele hakukuwa na barabara ya inayo toka, kwa mujibu wa maelezo ya Masumbuko, aliyompatia yule askari.

“Kama unasema huko mbele barabara haitoki, unadhani ilikuwa inaenda wapi hii gari?” Konstebo Kova Mura alimuhoji Masumbuko, huku ameyafinya macho yake kwa mashaka.

“Siwezi kujua afande. Ndio kwanzaa na mimi nayaona haya matairi yakikatisha uelekeo huu.” Masumbuko alimpa jibu lililozidi kummakinisha yule askari.

“Hebu nifate.” Konstebo Kova Mura akamtaka Masumbuko waendelee kwa pamoja kuzifatilia zile alama za yale mataili ya gari. Wakazifatilia huku Konstebo akijiaminisha moyoni kwamba, kama kweli barabara mbele haitoki, lazima kuna umbali usiokuwa mrefu sana, zile alama zingekoma.

Hakukosea!

Walifika mahala ambapo, zile alama hazikuendelea. Zaidi kukawa na mizunguko mingi ya alama zile, zilizooashilia kwamba, lile gari lilikuwa likizunguka zunguka pale, hususani kwa kukata kona.

‘Lilikuwa linatafuta nini huku hili gari, usiku huo?’ Yule askari alijiuliza pasina majibu. Alimakinika zaidi na sehemu iliyoonekana kama ilichimbwa na kufukiwa masiku si mengi, kama si muda mrefu uliopita. Akaingiwa na wasiwasi.

“Nini hiki…tuta sio tuta…!” Alinong’ona konstebo.

Akasogea zaidi pale, Masumbuko akiwa kando yake hatua kwa hatua. Kwenye kitabu chake kidogo, akiandika kila alichodhani ni cha muhimu kukiandika. Masumbuko alimshuhudia yule askari akichora baadhi ya michoro kwenye hicho kijitabu chake, ambayo ni kama aliielewa kwa upande mmoja, na ni kama hakuielewa kwa upande mwingine.

Baada ya udadisi wa hapa na pale, wakakata shauri la kuondoka. Konstebo alimsindikiza Masumbuko mpaka nyumbani kwake, wakiwa tayari wamesha badilishana namba zao za simu, kwa makubaliano ya kuendelea kupeana taarifa ya kila kitakachojiri. Kisha yeye konstebo, akaendelea na safari, akirejea ofisini.

Akiwa njiani, alipokea simu ya Private Hamis.

“Nipe lipoti afande.” Konstebo Kova Mura alimdaka usemi Private Mwita Marwa.

“Huku mambo sio mambo mkuu…”

“What has happened comred. Nini kimetokea?”

“Majeruhi amefariki bhana, aisee bull shiit to hell.”

“What…?!” Konstebo Kova alipagawa. “Amefariki..?! Shahidi namba moja huyo jamani, haya mambo vipi holy shiiit…”

“Yaani mkuu we acha tu, ila nimefanikiwa kuzungumza nae  a little bit. Nimepata kitu kidogo kutoka kwake.”

“Aloo…! Kumbe umeongea naye, excellent, kwa hiyo kuna muda alizinduka?”

“Ndiyo mkuu. Na ni kama Mungu alimzindua kwa makusudi ya kuongea na sisi kabla hajamchukua kabisa, kwenye makazi yake ya milele. Yaani baada ya kuzungumza naye tu, jamaa akakata roho, kaenda zake ahera, oh my God.., can you imagine?!”

“Yes I can imagine. Maskini… apumzike kwa amani cha pombe na pombe zake.”

“Amina. Inabidi tuonane tuongee kwa kina, kuna kitu nyuma ya kifo cha huyu jamaa. Something else is hidden behind his death. The guy is killed… Jamaa ameuwawa kwa maksudi, ajari ya maksudi.”

“Oh yes, ama hakika tunahaja ya kukutana now now, habari unayonipa, ina click  vizuri kwenye ubongo wangu.”

Wakakubaliana wakutane ofisini muda huo huo.

*****

Walikutana ofisini, baada ya Hamis kutoka hospitalini. Wakapeana lipoti. Hamis akamueleza namna alivyofanikiwa kuzungumza na baba Ezekiel muda mfupi kabla hajakata roho.

Majaliwa alimuelezea yule askari tukio zima, alilolishuhudia huku likimrusha roho, na kumuondosha pombe zote kichwani. Tangu anaiona ile Toyota Hilux ikikata kona kuelekea shambani, na lile zoezi la kuzikwa kwa lile furushi.

Akasema, wakati lile gari likitoweka kwa spidi kali, akiwa amejificha, lilipompita alijikuta akiteleza na kuangukia barabarani. Akajikakamua kunyanyuka, lakini ni kama yule mtu aliyekuwa akiendesha alimuona.

Akasitisha safari yake. Akaanza kurudisha gari kinyumenyume. Alipoona vile alisimama haraka ili kumkwepa. Ndipo jamaa aliongeza kasi mpaka alipomgonga kwa kutumia upande wa nyuma wa gari yake.  Akaanguka na kupoteza fahamu. Hakujua nini kiliendelea, mpaka muda huo alipokuwa hapo hospitalini.

Baada ya maelezo hayo, Majaliwa au baba Ezekiel, alilalamika kuzidiwa na maumivu, akaomba apumzike. Akalala na hakuamka tena, mpaka lipoti ya wauguzi ilipothibitisha kuwa kesha kufa.

Wakati wote huo, Konstebo alikuwa kimya, akiyaoanisha maelezo hayo ya Private Hamis, na yale mambo yaliyomtatanisha kule kwenye msitu wa Mabwepande…

Alasiri yake, wananchi wa Mabwepande, wakishilikiana na polisi, walilifukua lile eneo. Wakakuta furushi lile lililozikwa na mtu asiyejulikana.

Ndani yake, kulikuwa na kiwiliwili cha mtu mmoja aliyekadiliwa kuwa ni kijana, kwa mujibu wa ngozi yake, alihisiwa kuwa pengine ni muhindustani. Kichwa chake hakikuwepo, kiwiliwili kilianzia shingoni mpaka miguuni.

Balaa kwelikweli!

*****

    Asubuhi moja, mfanya biashara maarufu wa kihindi, bilionea Darkshina Ghosh, alikuwa mitaa ya katikati ya mji maeneo ya Posta mpya ya jijini Dar. Kwenye shangingi yake ya bei mbaya, aina ya Range Rover, aliambatana na mlinzi wake wa Kihindi, Jayanthi Murthy.

Hatimaye dereva wao Muhindi, Indu Mala Malhotra alipaki gari pembeni mwa barabara, jirani kabisa na jengo la Posta mpya. Darkshina Ghosh na Jayanthi Murthy walitelemka na kuelekea kwenye lile jengo.

Kama kawaida yake, Darkshina alijikongoja kwa kuchechemea mguu mmoja, akisaidiana na mkongojo wake. Walipofika dirisha la huduma ya vifurushi, (pasels), Darkshina alimkabidhi muhudumu kalatasi ndogo yenye maelezo juu ya uwepo wa mzigo wake mahali hapo.

  Yule binti aliipitia ile karatasi, kisha akawaomba wampe dakika tano atakuwa amesha kamilisha taratibu za kuwakabidhi mzigo wao. Wakakubali. Takribani dakika tano au saba hivi baadae, yule binti alirejea na mzigo wenye muonekano kama boksi hivi, lililofunikwa vizuri kwa karatasi nzuri za rangi, kama zifungwavyo zawadi rasmi. Akawakabidhi.

  Darkshina Ghosh akampa ishara kwa macho Jayanthi Murthy aupokee, Jayanthi Murthy akaupokea kwa niaba ya bosi wake. Wakakamilisha baadhi ya taratibu za makabidhiano na yule muhudumu, ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi kidogo cha fedha, kwa ajili ya kulipia gharama za ile huduma, kisha wakarejea kwenye gari, wakatoweka maeneo yale.

  Hawakusafiri umbali mrefu, kutoka pale mpaka Moven Pick Hotel, ambako Darkshina alikuwa na miadi na baadhi ya wafanya biashara wenzake. Yeye alitelemka na kuingia hotelini kwa ajili ya kutekeleza miadi, akawaruhusu vijana wake warudi nyumbani pamoja na ule mzigo, ambao bado hakuwa amejua una nini ndani yake. Jayanthi Murthy na Indu Mara Malhotra wakaendelea na safari yao mpaka nyumbani kwa bosi wao Masaki.

  Usiku mida ya saa mbili, Darkshina Ghosh alirejea na vijana wake waliomfata na gari kule mjini. Wakiwa sebuleni, akaagiza apatiwe ule mzigo. Jayanthi Murthy akaelekea kwenye moja ya vyumba vya nyumba ile, punde akarejea na lile boksi, akamkabidhi bosi wake.

  Muda huo Darkshina Ghosh alikuwa bize kuvuta kiko yake huku akitoa moshi kwa wingi puani, akiwa ameketi kwenye sofa, na joho lake zuri la kinaijeria likimpendeza vema, mkongojo wake akiwa ameuegamisha upande wa pembeni mwa sofa.

  Bodygurd Jayanthi Murthy alisimama mbele yake akitaka kumkabidhi ule mzigo, Darkshina Ghosh akamuenyesha kwa ishala ya macho auweke juu ya meza iliyokuwa pale sebuleni, kisha akampa ishara nyingine aufungue. Akaufungua.

  Lilikuwa ni boksi kubwa zuri lililofunikwa vizuri kwa karatasi maalumu za kufungia zawadi. Lilifungwa na kufanya muonekano wa kizawadi. Alipofanikiwa kupembua mifuniko yake, bodygurd Jayanthi Murthy alijikuta akiruka pembeni kwa woga wa waziwazi huku akiachia kelele ya hamaki. Darkshina Ghosh na Indu Mala Malhotra waliokuwa wakimfatilia hatua kwa hatua walipigwa na mshangao pale walipomuona mwenzao akibaha namna ile.

  “What’s wrong young man?” (Nini tatizo kijana) Bosi Darkshina Ghosh alihoji kwa wasiwasi. Jasho lilimchuruzika kwa wingi yule bodyguard, wakati akijikaza na  kuanza kupiga hatua za kunyatia kurudi pale mezani macho yakiwa yamemtoka pima, kwa hofu ya kukitazama kilichokuwa mule kwenye lile boksi.

  ‘Naota ama ni kweli?’ yule bodyguard wa Darkshina Ghosh alijiuliza kimoyo moyo wakati akilinyatia lile boksi kwa woga.

  “Jesus!” Hatimaye aliropoka kwa nguvu, wakati huo Indu Mara Malhotra alikuwa akilinyatia lile boksi kwa woga pia. Darkshina Ghosh naye vivyo hivyo. Ndipo kelele za taharuki zilipokitawala kile chumba, kila mmoja ikimtoka kwa namna alivyomtoka. Walichokiona mule kwenye boksi, kiliwatisha na kuwaacha kwenye mastaajabu yasiyoelezeka.

*****

  “This is the game, and we must play it.” (Huu ni mchezo, na nilazima tuucheze) Bodygurd Jayanthi Murthy aliropoka kwa kiholo, wakati akimkabidhi bosi wake kadi ya mawasiliano…business card.

  “With this man, we can play this game, and surely…we shall win it.” (Pamoja na huyu jamaa, tunaweza kuucheza huu mchezo, na hakika…tutaushinda.) Alisistiza bodygurd Jayanthi Murthy.

  “Call him…fanya faster faster.” Darkshina Ghosh alimuamuru punde baada ya kuisoma ile kadi, na kuliona jina la muhusika wa hizo namba zilizoandikwa.

  Bodygurd Jayanthi Murthy alichomoa simu kwenye mfuko wa suruali yake ya jinsi iliyombana, akaanza kuibofya, akilitafuta jina la mtu mwenye zile namba zilizopo kwenye ile kadi ya mawasiliano. Wakati huo Darkshina Ghosh alikuwa akizunguka zunguka kwa chechemea yake pale sebuleni, huku sauti ya mkongojo wake ikisikika kwa nguvu kila ulipokita sakafuni. Ikawa mara aketi sofani, mara asimame na kuzunguka zunguka pale ukumbuni. Alichanganyikiwa kwelikweli.

  Simu ya upande wa pili wa ile ya bodyguard iliita, sekunde chache baadae ikapokelewa. “Hallo…”  Jayanthi aliendelea na mazungumzo na mtu wa upande wa pili. Yule aliyempigia.

  “Yes man. Kuna dharula imetokea hapa nyumbani kwa bosi wangu, tunakuhitaji usiku huu huu tafadhali.” Akatulia. Akasikiliza majibu ya upende wa pili.

  “Dharula ipi hiyo jamaa…na mbona muda umeenda sana, ntawezaje kutoka usiku mkubwa namna hii mkuu?!”

  “Ni kweli muda umeenda sana, na usiku ni mkubwa. Lakini hii ni dharula na dharula siku zote hutatuliwa ki dharula.

 “Naelewa mkuu…lakini…” bodygurd hakumpa nafasi ya kujitetea.      “Tusitumie muda mwingi kwa kubishana man…fanya kama hisani tafadhari niko chini ya miguu yak…” Naye mtu wa upande wa pili hakumpatia nafasi ya kumalizia kauli yake.

  “Poa man. Tusifike huko kwenye kuanza kusujudiana. Nipe dakika kama ishirini hivi, nadhani ntakuwa nimeshafika hapo.”

  “Poa.”

   Muda wote huo Indu Mara Malhotra alikuwa ameketi kwa kujiinamia kwenye sofa, akiri ikimzunguka kwa kuchanganyikiwa. Kama isingekuwa kumuhofia bosi wake, au kumuheshimu, angekimbia na kupotea eneo hilo. Kitu alichokiona kwenye lile boksi, hakuwahi kukiona maishani mwake mwote, na wala hakuwa na mategemeo ya kuja kukiona tena, kitu cha namna ile siku nyingine maishani mwake.

  Nusu saa baadae mlio mkubwa wa pikipiki ulisikika nje ya uzio wa geti la ile kasri. Jayanthi Murthy akatoka nje ya ile sebule, akaelekea kule nje, akashilikiana na walinzi waliokuwa zamu ya usiku kuilinda ile nyumba, kumpokea mgeni.

  Wakati huo simu yake ya mkononi iliita, akaitoa kwenye mfuko wa suruali alipokuwa ameshailejesha, alipoitazama, akaliona jina la aliyekuwa akimpigia. Ndiye mtu aliyemtazamia. Akaipokea kwa furaha.

  “Yes man, hope umefika…nimelisikia Baja yako.”

  “Yeah, nipo hapa nje mkuu.”

  “Poa mkuu, nakuja sasa hivi kukupokea.”

  Akawa ameshafika nje, akawashuhudia walinzi wakizengea zengea getini wakimakinika na ule ujio wa ile pikipiki, bado hawakuwa wamelifungua.

  “Oya askari, mfungulieni huyo mtu.”

  “Poa poa mkuu.” Mlinzi mmoja alimuitikia huku kazi ya kufungua geti ikianza mara moja. Aliingia Amos Bwire na pikipiki yake kubwa, akaipaki pale bustanini. Jayanthi Murthy akiwa pembeni kumlaki kwa bashasha kubwa.

  “A’salaam alleikum.” Jayanthi Murthy alimsabahi. “Wallei’kumsalaam.” Amos Bwire akamuitikia kwa tabasamu huku wakipeana mikono kwa nguvu, sanjari na kutikisana kama wanaopimana nguvu. “Bora umekuja kaka. Kuna jambo la kutisha sana, tunahitaji msaada wako kulitatua.”

  “Unanitisha bwashehe.”

  “Nisikutishe. Maadam issue yenyewe iko ndani ya uwezo wako.”

  Wakazama ndani, pale sebuleni. Wakasalimiana na wote waliokuwamo, kisha Jayanthi Murthy akamsogeza pale mezani kwenye lile boksi, akamfunulia. Amos Bwire alipoona kilichokuwemo, alimanusura apae hewani kwa kihoro. Kelele kubwa ya hamaniko ilimtoka, macho yakimtumbuka kwa woga, pale alipokiona kichwa cha mwanadamu kimehifadhiwa kwa kupachikwa ndani ya lile boksi.

‘Kichwa cha mtu, ndani ya boksi…Nini maana yake hii?!’

“Ni nini hicho nyie watu?! Shiiit to hell.” Amos Bwire alihoji kwa butwaa iliyochangamana na hofu kubwa. Jasho lilianza kumtoka mwilini kwa wahka.

“Detective, ndio maana uko hapa saa hizi. Ndio maana tumekuita. Kila unayemuona hapa, hakuna ajuaye kuhusu hicho ulichokiona.” Darkshina Ghosh alimueleza Amos Bwire kwa sauti ndogo ya upole.

“Nyie watu waajaabu sana, kwa hiyo kunikurupua kote, kunistishia usingizi wangu, mnakuja kunionyesha nini hiki?! Hivi we Jayanthi, umepata wapi ujasiri wa kuniita nije niangalie kitu cha namna hii. Haujui ni vibaya kumtazamisha mwenzako kitu au picha za kuongofya namna hii, tena bila ridhaa yangu?” Akameza mate, kisha akanyoosha mkono akilisonta lile boksi “Nini hicho hapo…?!” Akazungusha macho akiwatazama watu wote mule ndani kwa zamu, “…huo sini uchuro!”

“Come down brother…” Jayanthi Murthy akataka kuanza kumtaka radhi, Amos hakumpa nafasi. “Hakuna cha Come down brother hapa, the issue niku comfess kwamba what you did to me it’s too wrong. Full stop.” Amos alifoka.

“Okay Amos, apologize…hasa hasa nisamehe zaidi mimi niliyekupigia simu, ndiye niliye mshawishi mkuu wangu tukuite.”

“Okay, let’s cut shortly a long story…tufupishe hadithi, nini kinaendelea? Am scared.” Amos akamtaka ufafanuzi wa kile kilichokuwa mbele yao.

“Amos…sisi sote humu ndani tumetishika…” Jayanthi Murthy alianza kumuelezea, hatua kwa hatua. Namna bosi wake alivyowataka yeye na dereva wampeleke Posta.  Ni baada ya kupokea ujumbe uliomjulisha kwamba, kulikuwa na mzigo wake uliotumwa kwa njia ya Posta, na alitakiwa kuufata.

Akamsimulia mlolongo mzima wa matukio, mpaka kufikia pale muda huo. Na kichwa kilichokutwa mule kwenye boksi, ni cha mtoto wa pili kutoka mwisho wa Darkshina Ghosh. Na kichwa kile, kilihifadhiwa vizuri, kwa kupachikiwa flana ya jezi ya mpira wa miguu, ya klabu ya Chersie, kwenye kingo za lile boksi.

“Detective Amos, jukumu nnalotaka kukupatia ni moja tu. Fanya juu chini, kila uliwezalo, nimjue aliyeniulia mwanangu, na kunitumia kichwa chake kwenye boksi. Ni hilo tu.” Darkshina Ghosh alimueleza Amosi Bwire, a.k.a. mpelelezi binafsi, huku akinyanyuka kwa kujizoazoa pale sofani. “Nakuja.” Alitamka huku akiukamata mkongojo wake vema, akatoweka pale sebuleni, akaelekea chumbani kwake.

Aliporejea, alikuwa na brifkesi yenye kitita kikubwa cha fedha, akamkabidhi Amos Bwire, kama kianzio cha malipo ya jukumu alilomtaka amtekelezee. Alimtaka amchunguzia kifo cha mwanae, na aliyemtumia ile zawadi ya kichwa cha mwanae kwenye boksi, kwa njia ya Posta.

Alimpa sharti moja. Iwe siri, wala polisi hawakutakiwa kufahamishwa chochote. Jambo hilo, lililomshangaza sana mpelelezi wa kulipwa, Amos Bwire. Kwa tukio kubwa na zito namna ile, Darkshina Ghosh alikataa kata kata kuwashilikisha polisi. ‘Kwa nini?’

Kazi yake Amos ilikuwa ni hiyo tu, kuwajua au kumjua, watu au mtu, aliyehusika au waliohusika na mauaji ya kinyama ya mwanae, aliyekuwa shabiki mkubwa wa timu ya mpira wa miguu, klabu ya Uingereza ya Chersea.

*****

Njia nzima alizongwa na mawazo chungu mzima, kuhusiana na kile alichokishuhudia nyumbani kwa Darkshina Ghosh, pamoja na yale majukumu aliyokabidhiwa na yule bilionea. ‘Polisi hawatakiwi kujua chochote…’ Hili onyo lilimtatiza sana Amos. Alichokiona kilikuwa ni kitu kikubwa na katika hali ya kawaida, Darkshina alitakiwa kuwaeleza polisi ili wafanye nafasi yao, lakini alikataa katukatu abadani asilani.

Mbele ya pikipiki yake aliipakata ile brifkesi iliyojaa noti nyekundu za elfu kumikumi za kutosha, akiwa ameifunika kwa jaketi lake kubwa la kujikinga na baridi. Na hakuwa amezihesabu zile fedha, ila kwa muonekano tu, alijihakikishia, zilikuwa ni zaidi ya malipo ya kawaida ya kazi zake. Japo mteja wake alimuhakikishia, yale yalikuwa ni malipo ya awali tu…Advance.

Ghafla akamkumbuka mpenzi wake Mwanaidi. ‘Oh my God, sijui atakuwa katika hali gani uko huyu bibie.’ Alijisemea kimoyo moyo. Hakujua nini kilimsibu, ghafla tu, akaanza kuyakumbuka matukio ya nyuma. Tangu siku alipo kutana na yule mrembo kwa mara ya kwanza, mpaka muda huo alipokuwa akirejea nyumbani kwake, akiwa na utajiri wa ghafla usiku huo.

Akavuta kumbukumbu…

ESCAPE ONE

Usiku. Tamasha kubwa la burudani, maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo, UNIVERSITY BASH, lilifana ukumbi wa Escape One, uliopo Mikocheni. Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam, walijumuika kwa pamoja kushiriki burudani hiyo maalumu kwa ajili yao. Wengi wao walitoka chuo cha biashara cha IFM, na chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Tamasha lile, liliandaliwa na kituo kikubwa cha habari na burudani nchini, cha Clouds FM. Djay Mo’ Fire aliwarusha roho wahudhuriaji wa tamasha lile, kwa kupiga nyimbo ‘kali’ za Bongo flavor na zile za ‘majuu.’

Wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya walio alikwa kutoa shoo, hawakuwaangusha waandaaji wa lile tamasha. Walifanya shoo zao za kukata na shoka. Hakika ilikuwa siku ya kipekee sana, usiku wa burudani pasina kifani. Usiku wa university bash. Ulinzi ulikuwa wa kutosha, jeshi la polisi lilijipanga kudhibiti kila aina ya uhalifu.

Mishale ya saa sita unusu, Hellen aliyekuwa akisoma chuo kikuu cha biashara cha IFM, aliwafahamisha rafiki zake alioongozana nao tamashani, kwamba amechoka, na alihitaji kurejea hosteli kupumzika.

“Unazingua Hellen, mambo gani hayo? Hii ndio mida ya sakata rhumba, we unaongelea kurudi nyumbani!” Agnes, aliyekuwa ameketi naye meza moja, wakila na kunywa ‘alimzodoa.’

“Tatizo lake huyu naye mtoto wa mama sana, mi ndio maana huwa sipendagi kuongozana nae kwenye harakati kama hizi. Hakawii kukukata stimu.” Linda akadakiza.

“Jamani! Yanatoka wapi hayo yote. Kwani mimi nimemshurutisha mtu aondoke disko. Mimi naondoka peke yangu, nyie endeleeni kukata rhumba mpaka kuchwe, kimpango wenu.”

“Swala sio kuondoka peke yako bibie…” Linda alimjia juu. “…issue hapa ni kwa nini uondoke kabla ya mida ya wanga. Tumekuja wote, unaondokaje peke yako kwa mfano labda?! Au mwanga wewe?”

“Oyaa…mimi sioni hata cha maana tunachobishania.” Hellen alitia neno kabla hajamgeukia Agnes. “Oya, nipe ear phone zangu mi nijikatae.”

“Usimpe.” Linda akaweka zuio huku akimkata jicho kali Agnes. Kisha akamgeukia Hellen na kumtazama kwa sanifu. Hellen hakumjali Linda, alisha mzoea, ni msichana mwenye asili ya ukorofi. Akamuelekezea macho yake yote Agnes, ambaye naye hakuonesha nia ya kumpa hizo ear phone.

“Aggy…si nimekuomba ear phone…”

“Sina ear phone za mtu mie.”

“Unasemaje wewe…?!”

“Amekwambia hana…” Linda alitaka kumjibia Hellen kijeuri, Hellen hakumpa nafasi.

“Halafu we malaya usiniletee shoboshobo zako hapa.” Hellen alimfokea Linda kwa ghadhabu. Alishachoshwa na masumbufu ya huyo binti aliyekuwa sababu za yeye kuendelea kuchelewa kupumzika, wakati uchovu ulikuwa ukimnyima raha.

“We k**a unaniita mi nani…? (Akamzabua kofi)”

E bwana ee…!

Uliibuka ugomvi mkubwa na hakuna aliyeweza kuuamua. Si unayajua tena mapigano ya wasichana yalivyo.

“Msiwaachanishe hao wamechukuliana bwana, msiwaamue kabisa. Atakaye mshinda mwenzake, ndiye mmiliki wa bwana anayepiganiwa.” Kijana mmoja mfupi sana, akaropoka wakati mapigano yale yakiendelea.

“We nayeee…nani kakwambia wanagombania bwana.” Mwanaidi, aliyekuwa mmoja wa washirika wa ile meza ya akina Hellen akamzodoa yule kijana mfupi.

“Khaaa…! Kwa hiyo we hujui kwamba, mimi ndiye nnayepiganiwa hapo?!”

“Mh! We naye Kimburu shuti upiganiwe na nani?”

KOSA.

Yule jamaa alimchota ngwara moja matata sana Mwanaidi. Ile ngwara ilimmudu yule binti, ikampaisha hewani. Akaweweseka kabla hajaanguka chini kwa kishindo kikubwa, huku akikipigiza vibaya kisogo pale chini.

Mwanaidi kimya!

“Kauaa…kauaa…” Kelele za hamaniko zililindima. Kila mtu akashawishika kusogelea lile eneo, hata aliyehisi usumbufu kulisogelea hapo kabla, akasogea. Yule jamaa aliyempiga ngwara Mwanaidi akapoa kwa fadhaha.

‘Nimeua.’

 Hata hakujua ni muda gani alijikuta mikononi mwa polisi, mikono ikiwa ndani ya pingu. Akaongozwa mpaka kwenye karandinga la polisi. Siku hiyo, aliyotegemea kuimalizia kwa uzuri wa burudani ya university bash pale Escape One, akaimalizia lupango.

La Haula! Alijilaumu sana. Hakujua alimkosea nini Mungu, mpaka aumalize kwa madhila mazito namna ile bila kutarajia, ule usiku wa furaha.

Mwanaidi alizinduka baada ya kupewa huduma ya kwanza na wenzake pale ukumbini, chini ya ulinzi wa polisi. Akasimama. Akasema yuko sawa, japo alilalamika kwa kuhisi maumivu makali kisogoni, na maeneo ya uti wa mgongo.

“Sina haja ya kwenda hospitali, najiweza.” Alimjibu afande Amos Bwire aliyekuwa akifatilia hali yake pale ukumbini, tangu alipoanguka.

“Utaendelea na disko?” Amos alimtupia swali.

“La Hasha wa Kalla! Hii sherehe siihitaji tena. Huyu mseng* kanialibia muddy. Ngoja niende tu nyumbani, hii siku ishakuwa na mkosi.”

“Umenena vema, jiandae nikupe eskoti mpaka nje, nihakikishe unapata usafiri ukiwa salama.” Afande Amos alimsemesha taratibu.

“Sawa kaka. Nashukuru sana kwa msaada wako.”

“Shaka ondoa, ndio majukumu yetu ya kazi. Sasa sijui unakitu unahitaji kuchukua kabla haujaondoka.”

Mwanaidi hakumjibu neno, akayaelekeza macho yake kwa Siwema, aliyekuwa pembeni yake. “Mkoba wangu?”

“Nnao.”

“Poa. Nipe. We endelea na party, mi naelekea home.”

“Si tuondoke wote.”

“No Siwema,we endelea na party. Ntakupa nauli ya kurudia. Usikatishe burudani yako kwa ajili yangu.”

“Okay. Poa.” Siwema, binti waliyekuwa nae meza moja alimjibu kinyongenyonge huku akimkabidhi Mwanaidi ule mkoba wake. Mwanaidi akaufungua na kutoa noti tatu za elfu kumikumi, akamkabidhi Siwema kwa ajili ya nauli. Wakaagana na kuachana. Mwanaidi akatoka akiwa chini ya uangalizi wa CID Amos Bwire.

“Yule ni ndugu yako au?” Amos alimsaili wakati wakipiga hatua za kujivutavuta kuelekea nje ya ukumbi.

“Nani, Siwema?”

“Yup.”

“No. She is my best friend.”

“Wow..! Just friends!”

“Yeah..! Kwani vipi?”

“Hapana. Mnaonekana mnapendana sana.”

“Yeah…ni kweli. Yule mseng* ameshaondoka au?”

“Nani…aliyekuumiza.”

“Ndiyo.”

“Ah…masiku mengi. Saivi anapumulia nyuma ya nondo za lupango.”

“(Akamtukania mama yake) mseng* yule, leo angeniua ndio angejua kuita maji mma.”

“Ah! Si unawajua vijana wa mjini. Wakishaona mademu sifa zinawaponza. Pole sana, huyo tuachie sisi tutamfunza adabu.” Amos Bwire alimjibu kwa kujiamini. Wakafika nje. “So…unachukua bodaboda…au bajaji?”

“No, nna usafiri wangu. Private car.” Mwanaidi alimjibu huku akimsontea mahali alipoegesha gari yake. Wakajongea taratibu, mpaka pale walipobakiza kama mita tatu hivi na alikopaki ile gari yake. Mwanaidi akamshukuru sana yule askari huku akimpa noti mbili za elfu kumikumi. Hapo ndipo Amos alipojilidhisha kwamba, yule binti alikuwa njema kiuchumi.

“Nashukuru sana.” Afande Amos alizipokea zile hela huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio, akipumua kwa namna ya tofauti kabisa. Yule binti zaidi ya kuonekana kuwa ni mtoto wa ‘kishua,’ alikuwa mrembo sana. Mrefu mwembamba, mwenye mvuto wa kimahaba.

Chuchu zake zilizochongoka, zilichomoza vema kwenye gauni lake fupi lililombana, huku kwa chini lilimkomea juu ya magoti. Jamaa akatamani kuomba namba, akajistukia!

Wakaagana na kuachana. Mwanaidi akapiga hatua zaidi kulisogelea gari, ghafla mguu mmoja ukateleza. Akajitahidi kujidhibiti asianguke. Hakufaulu, akaanguka. CID Amos Bwire akausikia ukelele wa yule binti. “U’ wiiii…” Alipogeuka, kamuona akigaagaa chini alipopiga mueleka. Akamrudia.

“Oh! Kulikoni tena mrembo…? Pole sana mama.” Amos akambembeleza wakati akipenyeza mikono yake makwapani mwa yule binti, akamnyanyua na kuanza kumfuta vumbi lililomtapakaa.

Wakati akimfuta…

Viganja vya mwanaume yule vikitalii juu ya nguo za yule dada, wote walijikuta wakipatwa na hali isiyokuwa ya kawaida. Msisimko aliouhisi Mwanaidi, alihisi nguvu kama shoti ya umeme ikimlarua.

“Nashukuru sana kaka, naona siku ya leo Mungu hataki tutengane mimi na wewe.”

Kicheko.
“Umeona ee…kabisa yaani. Hata mimi nimeshaona.” Wakacheka.

“Umenisaidia sana, hope Mungu amenikutanisha na rafiki mwema usiku wa leo.”

“Pasina shaka. Ondoa hofu mrembo. Ni mwanaume mpumbavu tu, asiyejua kuthamini vitu vizuri, ndiye mwenye ujasiri wa kukuacha mrembo kama wewe uteseke.” Mwanaidi aliisikiliza kwa utulivu sentesi ile, huku akikenua meno. Kisha akacheka.

“Chukua namba yangu basi, tutazidi kuwasiliana rafiki mwema.” Mwanaidi aliambatanisha tabasamu alipokuwa akimtamkia ile sentensi, aidha kwa kujua au kwa kutokujua, ni kwa kiasi gani iliuburudisha moyo wa yule askari.

Wakapeana namba. Wakaagana tena, kisha wakaachana. Haikuchukua wiki mbili, urafiki wao uliwaingiza kwenye dimbwi zito la mahaba. Wakadumu kwenye mahusiano mpaka kipindi Amos anajiuzuru kazi ya upolisi.

Na hata huo usiku wakati Amos akipokea simu ya Jayanthi Murthy, alikuwa na Mwanaidi nyumbani kwake wakichombezana.

“Umesema nani anakuita?” Mwanaidi alimuhoji kwa hamaniko.

“Jayanthi Murthy, ni bodyguard wa mfanyabiashara flani, anaitwa Darkshina Ghosh.” Amos alimjibu.

“Darkshina Ghosh..!” Mwanaidi alistuka sana. Amos akaibaini ile hali, ila ni kama yule binti naye alijistukia, akaamua kupoteza lengo.

“Kulikoni… mbona umestuka sana, na umelitaja jina lake kana kwamba limezoeleka kinywani mwako?” Amos akamuhoji huku akikaza kamba za viatu vyake.

“Aaah… nooo… nimeshangazwa tu kuona una haraka na huo wito ilhali mtoto wako mzuri niko hapa, na haikupi homa kunitelekeza peke yangu kwenye hili bangaloo, wakati ungeweza kumpa miadi hata kesho mngeonana.”  Mwanaidi alimjibu kwa upole ulioambatana na wasiwasi flani, hali iliyomtia wasiwasi pia Amos Bwire.

“Ni kweli usemayo honey, lakini msistizo alionipa huyu jamaa yangu, nahisi kuna jambo zito kidogo.”

“Ndiyo uniache peke yangu humu ndani… usiku huu wote… kweli jamani! Mtu unayempenda unaweza kunifanyia hivi. Mbona haiingii akirini?!” Mwanaidi alizidi kulalamika.

“Usijali baby, ni majukumu ya kazi mpenzi wangu. Si unajua mi mtoto wa kiume. Napambana ili mtoto mzuri upate kula.”

“Hata kama.”

Amos alitumia nguvu kuondoka, akaondoka bila ridhaa ya yule binti. Na ule muda, alipokuwa akirejea nyumbani kwake na blifkesi yenye mamilioni aliyokabidhiwa na Jayanthi Murthy, akaongeza mwendo kasi baada ya kukumbuka namna walivyoachana na Mwanaidi.

Mwanaidi hakuwa ameiridhia ile safari.

Hatimaye alifika nyumbani. Alipoingia ndani, hakumkuta Mwanaidi. Alistaajabu sana. Akamtafuta kila chumba bila mafanikio. Akapiga simu yake, haikupatikana. Ndipo alipobaini ni kwa kiasi gani, alimkwaza yule mrembo kwa kung’ang’ania kuitikia wito wa swahiba wake Jayanthi.

‘Lakini pia, aliposikia jina la Darkshina Ghosh, alistuka sana. Kwa nini nilipoanza kwa kumtaja Jayanthi Murthy hakustuka?!’

Alijikaza kulichukulia kawaida hilo swala, japo lilimtia mashaka. Akalala akiwa na wasiwasi mkubwa wa kulipoteza penzi lake.

*****

      Ulipita usiku aliokutana na yule bilionea wa kihindi, aliyemkabidhi dili na dau la mamilioni, mpelelezi Amos Bwire alidamka mapema sana alfajiri. Akajiandaa na kuelekea kazini kwake. Kwenye ofisi yake inayojihusisha na maswala ya kipelelezi, aliyoifungua mara tu, baada ya kuachana na kazi ya upolisi. Kampuni ya Amos Private Ditactive inc, ilikuwa ndani ya jengo la Blue Peal, Ubungo Plaza, iliyopo Ubungo.

Alikuwa na miadi ya kukutana na Darkshina Ghosh, kama walivyokubaliana usiku wa jana yake. Kwamba Darkshina, angelipoti ofisini kwake asubuhi hiyo, kwa ajiri ya usaili wa awali, utakaomsaidia yeye Amos kuanza kutekeleza jukumu alilompatia.

Alipaki pikipiki yake sehemu ya maegesho ya jengo la Ubungo plaza. Akaingia ndani, akaelekea kwenye eneo lenye lifti. Akajitoma na kupanda mpaka ghorofa ya sita. Huko ndiko ilikokuwa ofisi yake. Ofisi ya Detective Amos Bwire. Mpelelezi wa kujitegemea.

Alifikia mapokezi, akalakiwa na katibu muhutasi wake, aitwae Noella. Wakasabahiana kwa kuchangamkiana. Amos na msaidizi wake huyu, walikuwa wakielewana sana. Walipendana, wakazoeana huku bidii na hali ya kazi ikiwa ya hali ya juu kwao wote.

“Taarifa yoyote mpya?” Amos alimuhoji Noella baada ya salamu. Noella akakataa kwa kutikisa kichwa.

“Okay. Nategemea kukutana na mgeni asubuhi ya leo, ni muhindustani, anaitwa Darkshina Ghosh. Akifika, mruhusu anione tafadhari.”

“Sawa bosi.”

Akajitoma kwenye ofisi yake, iliyopo nyuma ya mapokezi. Mida ya saa tatu, Darkshina Ghosh aliwasili. Noella akampokea na kumjulisha bosi wake kwa njia ya simu ya mezani, kisha akamruhusu aingie kwa Amos.

“Oh..! Komredi. Karibu sana. Amos Bwire alipaza sauti yake kumlaki mgeni wake kwa bashasha.

“Ahsante sana komredi.”  Darkshina Ghosh akaupokea ule ukaribisho kwa bashasha pia.

“Pasina shaka sisi ni makomredi sasa, kwa sababu tumeshaunganishwa na jukumu kubwa la pamoja.”

Kicheko.

“Hakika komredi.”

“Karibu kiti uketi.”

“Shukrani sana.”

Darkshina Ghosh akaketi. Wakawa wakitazamana usoni kwa uzuri kabisa. Ilimchukua sekunde chache mno yule muhindustani, kuuthibisha ubora na uzuri wa ile ofisi, iliyoshehenezwa kwa samani ghari za kuvutia.

“Ofisi yako nzuri sana kijana.”

“Oh..! Nashukuru sana mzee wangu, kidogo najaribu jaribu.”

“Haujaribu, unafanya kweli. Hivi ndivyo kijana wa kisasa anavyo takiwa kuwa. Kufanya vitu vya kimaendeleo, na sio kuendekeza mambo yasiyo na maana. Uhuni na anasa zisizo na tija. Safi sana kijana.”

Amos akajenga uso wenye aibu kidogo, kama awavyo mtu yeyote asifiwapo na mtu anayemzidi, pengine kiumri, hadhi au mali. “Nashukuru sana mzee. Kwa mara nyingine tena niseme karibu sana. Hapa ndio ofisini kwangu.”

“Nashukuru sana. Pasina shaka nimesha karibia.” Darkshina Ghosh alimuitikia, kisha moja kwa moja akaelekea kwenye mada. “Awali ya yote, nikutake radhi kwa kadhia iliyotokea jana. Nasadiki hukupendezwa na kile kitendo cha kukutazamisha kitu tulichokutazamisha usiku ule. Bila shaka hatukukutendea haki. Kwa hilo, nianze kwa kusema tusamehe sana, mimi pamoja na rafiki yako Jayanthi.” Darkshina alijieleza kwa upole uliopitiliza, na muonekano wa ustaarabu usiopimika.

“Oh! Mbona hilo lilipita hiyo hiyo jana.” Amos alimjibu kwa utulivu, huku akistaajabishwa na ustaarabu wa yule tajiri.

“Yeah… Ni kweli. Hata mimi nasadiki hivyo. Ila mimi huwa naamini kwamba, kumjali mgonjwa ni bora zaidi ya kumtibu. Mambo mepesi ni sahihi kuyachukulia kwa wepesi wake, na mazito, ni kwa uzito wake. Lile jambo lilikuwa zito, hivyo kama mtu makini ninayejali, nisingeweza au nisingependa kulichukulia kwa wepesi.”

“Nimekuelewa vema mzee wangu. Ondoa shaka kabisa. Mpaka kufikia hapa, mimi nina amani na moyo wangu ni mweupe kabisa. Nilipoghafirika sikuficha hisia zangu, nadhani niliweka kila kitu bayana, nanyi mkatambua dhahili namna nilivyoghafirika. Kwa hivyo ninaposema yameisha…ni wazi namaanisha.” Akaweka kituo, kisha akaendelea.

“Ninachokifikiria kwa sasa, ni kuhusu jukumu ulilonipa, na namna ya kulitekeleza. Hilo lingine hebu tusilipe nafasi, ili maisha yaendelee.”

“Sawa. Nafurahi kusikia hivyo.”

Amos akamuitikia, “Karibu.” Kisha akaendelea. “Enhee… hebu tuanze na point iliyotukusanya hapa.” Akayafinya macho yake, na kujenga umakini. “Tukio la jana! Mimi bado sijalielewa kabisa.” Amos Bwire akaweka kituo, huku akimtazama Darkshina kwa shauku ya kusikia kutoka kwake. 

Darkshina Ghosh akaongea kwa majonzi, “Detective…mimi mwenyewe vivyo hivyo. Niko kwenye sinto fahamu huwezi amini. Ni kizungumkuti”

“Nini kilitokea, mpaka ukawa na kichwa cha mwanao katika mazingira yale?”

Darkshina akamsimulia mlolongo mzima wa matukio, tangu siku alipotumiwa ujumbe na shirika la posta kwa njia ya teleksi, kwamba, kuna mzigo wake umetumwa kwa njia ya posta, na alipaswa kuufata. Ndipo asubuhi ya siku hiyo akauendea, akiwa na wale vijana wake.

Hakuufungua, akaendelea na ratiba zake za siku hiyo mjini. Mpaka huo usiku aliporejea nyumbani, na kuomba akabidhiwe.

Ndipo alipokutana na hicho kioja. Kichwa cha mwanae kikiwa kimekaushwa kwa kuokwa, kisha kikahifadhiwa kwenye boksi la chuma.

“Uliwezaje kubaini mara moja kwamba ni kichwa cha mwanao, wakati kilikuwa kimeokwa?”

“Mosi, mwanangu kapotea katika mazingira ya kutatanisha yapata wiki nzima sasa. Rafiki zake wanasema, mara ya mwisho walikuwa nae Mlimani City cinemax, usiku wakitazama mpira wa ligi kuu ya Uingereza, ya La Liga. Siku hiyo, kulikuwa na mchuano mkali kati ya timu ya Manchester United  na Chersea. Mwanangu alikuwa shabiki mkubwa wa Chersea. Na siku hiyo, alivaa jezi ya timu hiyo.”

“Kwa maneno hayo, mwanao alitekwa usiku wa siku hiyo, wakati akitoka mpirani. Na ndio maana waliokuletea kichwa chake, wameweza kuambatanisha na jezi ya Chersea…hiyo ni kumaanisha kwamba, walimuwinda, wakamteka na kumuua.”

“Nasadiki vivyo hivyo.”

“Unadhani kwa nini waliomuua wamemuua mwanao? Na kwa nini wakuletee kichwa chake?” Kimya kikapita, wakati Amos akimtazama mgeni wake kwa macho ya udadisi, kisha akaendelea. “Sijui kama utapingana na mawazo yangu, kwamba mwanao kauwawa kwa ajiri ya kukukomoa. Kifo cha mwanao ni kisasi. His death is retribution… reprisal”

 “Bila shaka Amos…this is a revenge…it maight be a vengeance.” Darkshina Ghosh akaunga mkono mawazo ya Amos Bwire kwa msistizo.

“Unamtifuano na nani, au akina nani mzee Darkshina?! Amos alimtupia swali huku amemkazia macho makali yule muhindi, ambaye akili yake ilionekana kuweweseka kwa swali lile.

“Sina mtifuano na mtu yeyote.”

“Sio kweli.” Amos alimdakia huku akizidi kumtazama kwa macho yake makali, yenye udadisi mkubwa. Alikuwa makini kuisoma saikolojia ya yule mzee. “Lazima kuna mahali hapako sawa mzee Dark. Tukio hili, sio la kawaida kabisa. Na kama ulivyo tangulia kusema hapo awali, mambo mepesi kwa wepesi wake, na magumu kwa ugumu wake. Issue kama hii, haiwezi kutokea kirahisi rahisi namna hiyo.”

“Ni kweli komredi. Inawezekana usemacho, kama rafiki yako amesha kueleza kwa undani kidogo kuhusiana na mimi. Mimi ni mfanya biashara mkubwa, Darkshina Ghosh nafahamika kama bilionea. Sasa…katika haya mambo yetu ya kibiashara, tunakumbana na mambo mengi swahiba. Chuki bila sababu, wivu wa kimaendeleo, mashindano, minyukano, na mengine mengi kama hayo. So what your saying it maight be true. But for me… I know nothing.”

Amos alikuwa mtulivu sana wakati akiusikiliza utetezi wa mteja wake, juu ya hoja aliyombana. Kimya kikapita, kabla hajafungua mdomo na kumtupia swali, “Una mke?”

“Hapana.”

“Kwa nini?”

“Mke nilikuwa nae, ila alishafariki miaka mingi iliyopita.”

“Okay…pole sana. Naye alikuwa Muhindi?”

“Nashukuru sana…yeah, alikuwa Muhindi kama mimi.”

“Ulifanikiwa kuzaa nae watoto wangapi?”

“Wanne.”

“Akiwemo marehemu uliyetumiwa kichwa chake.”

“Ndiyo.”

“Hope una hawara, right?”

“Very true.”

“Anaitwa nani?”

“Amanda.”

“Umezaa nae?”

“Hapana.”

“Mnaishi wote, right?”

“No.”

“Okay…yeye ana jishughulisha na nini?”

“Ameajiriwa kama Chief accountant, makao makuu ya TRA, kule Posta.”

“Aisee! Kumbe ni muhasibu mkuu mamlaka ya mapato Tanzania! Naweza kupata…aaamm….anyway, basi.” Amos alitaka kumuomba kitu, lakini akasita.

“Kupata nini komredi?” Mteja wake alimuuliza baada ya kuona amesita kuwasilisha ombi lake.

“Ah…hapana. Acha tu.”

“Sema komredi.”

“Usijali. Kwa sasa tuishie hapo, unaweza kwenda. Ntakucheki muda mwingine ntakapokuhitaji.”

“Sawa.”

Darkshina Ghosh akanyanyuka tayari kwa kuondoka. Ndipo Amos alipomuuliza swali alilokusudia kumuuliza, japo alijifanya alisahau. Hakutaka kulifanya kuwa swali rasmi, ili akipate vema kilichomo kichwani kwa mteja wake.

“Uliniambia hautaki kuwashilikisha polisi hili swala, kwa nini labda?”

“Polisi mambo mengi kijana, sihitaji complications.”

“Una maanisha hata taarifa ya kupotea kwa mwanao huku wataarifu jamaa.”

“Nooo… niliwataarifu. Lakini hili la kichwa cha mwanangu limenigusa sana, na sitaki kabisa kuwashirikisha hao jamaa. Nahisi wataniwekea usiku tu. Nataka kwa nguvu zangu mwenyewe, niwabaini waliohusika.”

“Kisha..?” Amos alidakia.

“I will know what to do. Niachie mimi, ntajua ntakachokifanya. Mimi nimekupa jukumu moja tu, kuwabaini au kumbaini anayehusika na huu unyama. Na ntakupa ujira ambao haujawahi kulipwa na mteja mwingine, na pengine haitakaa ije itokee, ulipwe ujira wa namna hiyo katika kazi yako hii, milele.”

Maneno hayo yalimfanya Amos amtazame mteja wake kwa muda, kabla hajashusha pumzi ndefu, iliyofatiwa na neno moja tu, “Sawa.”

*****

     Baada ya Darkshina Ghosh kuondoka, Amos alimuita katibu muhutasi wake ofisini mwake. Wakafanya mazungumzo takribani dakika ishirini. Akautumia muda huo kumueleza Noella kuhusiana na ugeni ulioondoka pale ofisini.

     Noella akakiri kwa kinywa chake juu ya ugumu alioutazamia, kwa wao kama kampuni binafsi ya kipelelezi, katika kufanikisha adhima ya mteja wao, Darkshina Ghosh. Wakapeana mikakati ya kuanza kutekeleza lile jukumu.

    Mbinu ambazo Noella alishauri waanze nazo, ziliamsha ari ya kazi ya Amos. Mara zote, amekuwa akijivunia sana utendaji kazi wa huyo binti. Noella alitokea kuwa msaada mkubwa kwa Amos kama mpelelezi binafsi, na kama kampuni kwa ujumla. Alikuwa ni binti mwerevu, mjanja na mwenye ari ya kazi muda wote.

     Mbinu ya kwanza; ilimpasa asubuhi hiyo hiyo Noella kuondoka pale ofisini, ili aelekee mjini Posta. Kwa kutumia gari ndogo ya ofisi, Toyota Spasho, aliondoka ofisini kwa ridhaa ya bosi wake. Akiwa barabarani, kichwani aliyakumbuka mazungumzo yake na bosi wake asubuhi ile.

     Aliyatafakari maelezo aliyopewa kuhusiana na zawadi aliyotumiwa mteja wao kwa njia ya posta. Ndipo sura ya Darkshina Ghosh akiwa nae mapokezi muda ule ikamjia kwa upya.

      ‘Huu ni utata…tena utata kwelikweli. Kwa nini huyu muhindi hataki issue kubwa namna hii iwafikie polisi. Ati anasema kwamba polisi watamuwekea usiku…mnh…hilo tu?! Mbona haiingii akirini..?!’ Kichwani aliendelea kutafakari, tafakuri iliyotunga mimba ya maswali mtungo, ambayo bado muda wake wa kujifungua na kuzaa majawabu haukuwa umewadia.

        Barabarani alikumbana na foleni za hapa na pale, kutokana na msongamano mkubwa wa magari. Na mara kadhaa alisimama kwenye foleni za kwenye mataa ya trafiki. Saa mbili baadae, alikuwa kwenye viunga vya jengo la mamlaka ya mapato Tanzania, TRA makao makuu.

*****

Usiku mkubwa. Kwa mara nyingine, Amos Bwire alipaki pikipiki yake nje ya uzio wa kasri la Darkshina Ghosh. Mbele ya lango kubwa, walinzi waliokuwa zamu, tayari wakiwa na taarifa za ujio wake, walimfungulia na kumruhusu kuingia.

Jamaa akaiingiza Baja yake na kuipaki sehemu ya maegesho ya vyombo vya moto, iliyojengelewa kwa vyuma vilivyosimikwa na kufunikwa kwa matenti ya kisasa kwa juu. Akagonga mlango, akafunguliwa na kujitoma sebuleni. Hapo aliwakuta Darkshina Ghosh, Indu Mala Malhotra na Jayanthi Murthy.

Nyuso zao zilionyesha mambo hayakuwa mambo, japo kuwa walijikaza na kumkaribisha vizuri, kabla ya kumuongoza sehemu yenye ngazi za kuelekea ghorofani. Wakakwea pamoja, wakielekea kwenye moja ya vyumba vya kulala wageni vya jumba hilo. Wakajitoma humo, moja kwa moja Jayanthi Murthy akakielekea kitanda pekee kilichokuwamo.

Kilikuwa chenye ukubwa wa futi tano kwa sita, kizuri, kilichotandikwa kwa umaridadi. Akapepumbua matandiko yake na kunyanyua godoro, akaliegemeza ukutani. Kilichoonekana uvunguni…

“Toba roho yangu!” Amos Bwire alipayuka huku akiifunika midomo yake kwa kiganja cha mkono wake wa kuume. Macho yake yalimkodoka akizitazama maiti mbili zilizochinjwa shingoni, zikiwa zimelala uvunguni mwa kitanda.

“I can’t believe this…what is this, holy temptation.”Amos aliendelea kupayuka. Hakuwa akiamini alichokuwa akikiona.  Ndipo alipoijua sababu ya wale watu kumuita kwa mara nyingine, nyumbani kwao usiku mkubwa namna ile. Ilikuwa ili aje ashuhudie mauzauza kwa mara nyingine.  

Maiti za vijana wawili wa kiume wakitanzania, zililazwa vema pale sakafuni. Sehemu ya juu ya miili yao, hawakuwa na mavazi, kuanzia matumboni kushuka chini, walisitiriwa na shuka moja. Kwa maelezo ya Ghosh, walizikuta maiti zile pale zikiwa uchi wa mnyama jioni hiyo, baada ya kupokea ujumbe kwa njia ya simu ya mezani, walipopigiwa na mtu wasiyemfahamu, ambaye hakuwa radhi kujitambulisha kwao.

Macho ya Amos yalizidisha umakini kutazama kando mwa maiti ya pili kutoka ukutani. Palikuwa na jambia refu limegandia damu, lenye makali kuwili.

“La la la laaaa…aisee…” Amos aliendelea kufadhaika. Aliingia ndani ya uzio wa kitanda, akaikurubia maiti iliyopakana na lile jambia. Akaiinamia huku akitoa leso mfukoni mwa suruali yake. Akazitazama kwa makini maiti zile, kisha akiwa ameifumbata ile leso kiganjani mwake, akalikamata lile jambia. Kuna kitu alikiona kilichoyavuta macho yake.

Ubavuni mwake liliandikwa ujumbe ulichongwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali. ‘Nitaua tena.’ Ulisomeka ujumbe wenyewe. Alitumia muda mrefu kulitazama kwa umakini, pengine kuliko hata muda alioutumia kuzitazama zile maiti. Yeye mwenyewe alijishangaa, kwa namna alivyo kuwa makini zaidi na lile jambia kuliko wale marehemu.

Jayanthi Murthy alilishusha lile godoro baada ya Amos kurejea nje ya uzio wa kitanda, akiwa amelirudisha jambia mahala pake. Akakitandika vema kile kitanda, na kukirejesha kwenye muonekano wake wa awali. Matukio hayo, yalikuwa yakimstaajabisha sana Amos, ilimchukua muda mrefu kuwatafakari wale wahindi aliokuwa akifanya nao kazi. Walikuwa ni binadamu wa aina gani wenye ujasiri usiokuwa wa kawaida namna ile. ‘Bila shaka walikuwa wachawi waliokubuhu.’

“Unawafahamu hawa marehemu?” Amos alimtazama usoni bosi wake, akimaanisha lile lilikuwa swali lake.

“Ndiyo nawafahamu, ni wanangu hawa.” Jayanthi Murthy alimjibu.

“Ni wanao…?!” Amos aling’aka. Jayanthi akaelewa sababu ya mpelelezi yule kung’aka namna ile.

“Yup, ni wanangu, nilizaa na mtanzania. Mama yao sio mama yake na Kann.” Jayanthi alifafanua, Amos akawa amemuelewa vema. Kann ni yule mtoto wa Jayanthi, aliyeuwawa, kisha kichwa chake kikatumwa kwa njia ya posta kikiwa ndani ya boksi.

Maelezo ya Jayanthi hayakuishia hapo, akamweleza zaidi kwamba, jumla amezaa watoto sita, na wanawake wanne tofauti. Mwanamke wa kihindustani, aliyemzalia hayati Kann. Wale marehemu wawili chini ya godoro, nao wana mama yao mtanzania. Ana watoto wawili wengine, wakike na wakiume aliozaa na mwanamke mwingine wa kitanzania. Na marehemu mkewe aliyezaa nae mtoto mmoja muhindi.

Kwa mara nyingine, Amos Bwire alijikuta akimtafakari bila majawabu mteja wake, baada ya kumpa msimamo wake kuhusiana na vile vioja vilivyokuwa vikiendelea, kwamba hana mpango wa kuwashirikisha polisi.

“Hii ajabu sana Darkshina, hata kama hauumani utendaji kazi wao, ni sawa, lakini wao pia wana nafasi yao. Japo kufahamu ni haki ya  msingi ya jeshi la polisi. Hivi unadhani siku wakibaini hii hali, na ukawa haujawapa ripoti, utakuwa salama kweli?”

“Shida iko wapi Amos?” Darkshina alimuhoji kwa sauti ya jeuri yenye kukoroma.

“Shida ipo bosi…lazima nikueleze ukweli huu. Kumbuka kabla sijawa mpelelezi binafsi, nilikuwa polisi. Nazijua taratibu zinazopaswa kufatwa katika mazingira kama haya. Ni muhimu ukawaeleza polisi, la sivyo, siku wakijua…mi sitakuwemo.”

“A-nhaa…kama huo ndio wasiwasi wako ondoa shaka. Wewe huusiki kwa jambo jingine lolote, zaidi ya jukumu nililokupa. Kuwabaini watu wanaohusika na mchezo huu mchafu. Nikiwabaini….Aloo…” Darkshina Ghosh alisistiza kwa kuuma midomo yake kwa hasira, huku akiinamisha kichwa chini, na kukitikisa kwa masikitiko.

“Utawafanyaje?” Amos alilazimika kumuuliza swali ambalo alijua lingemkera yule mzee, lakini hakuwa na namna. Alikuwa kwenye wakati mgumu kuyajua mawazo ya yule muhindi kuhusiana na yale matukio na upelelezi wake bila kuwashirikisha polisi ungeishia kwenye maamuzi gani.

“Kwa namna yoyote ile, adhabu yao itakulazimu ujichukulie sheria mkononi…ndio maana yake.” Amos alimkazia macho usoni wakati akijaribu kuyachota mawazo ya mteja wake. “Hilo nalo ni kosa ki sheria… tena kosa kubwa haswaa. Na halita kuacha salama.”

“Una maanisha nini Amos… mbona sikuelewi?”

“Najua ni vigumu kunielewa kulingana na msimamo wako… lakini… ipo siku utanielewa. Ninachokitaka mimi, washirikishe polisi mzee, kabla mambo maji hayajazidi unga.”

“Nadhani kazi niliyokupatia imekushinda. Unaonaje tukisitisha biashara yetu.”

“Walaa, kazi haijanishinda, na biashara hatusitishi. What am saying is for your sake…nikuelezacho ni kwa ajili yako mzazi.”

“Sihitaji maelezo yako, nnachohitaji ni majibu ya kazi yangu niliyokupa,  fullstop!” Mzee Darkshina Ghosh alifoka huku mate yakimtoka na kumrukia usoni Amos. Amos akaimaizi hasira ya mteja wake. Haikuwa ya mchezo-mchezo. Akakubali kushindwa, akaaga na kuondoka.

*****

Alifika nyumbani kwake mida ya saa tisa, akapaki pikipiki yake kwenye banda alilokuwa akiihifadhi kila siku. Ndani ya uzio wa nyumba aliyopanga.

Akaelekea varandani kwenye mlango. Akapachika ufunguo kwenye kitasa, akaufungua kisha akajitoma sebuleni. Giza lilikuwa zito. Akaelekea ukutani kwenye swichi ya taa ya pale sebuleni, akaibofya, balbu ikafanya nuru.

Ndipo alipoona kitu kilichomstua na kumtisha, alimanusra aanguke chini kwa kihoro.

Pumzi zilimtoka kwa fujo, wakati mapigo ya moyo yakimwenda mbio, alipojikuta akitazamana na mwanadada mgeni machoni mwake. Mwenye mwili mkubwa wa wastani, mrembo si haba. Hakuwa amewahi kumuona hapo kabla, na hakujua aliingiajeingiaje nyumbani kwake  usiku ule.

Moyo ulimthibitishia kwamba; alipoondoka; hakuacha mtu yeyote ndani. Alikomea kitasa kwa ufunguo, ufunguo aliondoka nao, alirudi nao, na aliutumia kufungua kitasa kilichokuwa kimekomewa kama alivyokiacha.

Doh!

Yule mrembo alikuwa amejibweteka kibwege kwenye sofa ya mtu moja iliyokuwa konani mwa ile sebule, asiye na chembe ya woga wala waiwasi, kana kwamba alikuwa kwake, au alikuwa mwenyeji mwenye uhalali na mahala pale. Ile hali, ikazidi kumuingizia ubaridi mwili mzima Amos Bwire.

“U-nani wewe, na umeigiajeingiaje nyumbani kwangu?” Amos alimuhoji kwa kufoka.

“Hiyo ndiyo salamu?!” Binti alimtupia swali badala ya kujibu maswali. “Mmm…” Akazidi kuhoji huku akimkazia macho yake makubwa ya kirembo, nyusi akizichanua kwenda juu. “Au hivyo ndivyo ulivyofundwa na wazazi wako…ukikuta wenyeji ugenini unaanza kwa kuwakaripia badala ya kuwasalimu…ustaarabu wawapi huo Amos?”

“Whaaaat?!” Amos Bwire alipiga kelele baada ya kusikia jina lake likimtoka kinywani yule binti aliyekuwa ameketi sofani, awamu hii akianza kusimama kibabe kana kwamba yuko tayari kwa lolote. Alikaa kisharishari.

‘Baradhuli mkubwa huyu, kumbe ananijua…ni nani huyu…na anataka nini kwangu?’

“Unajiuliza mimi ni nani…na nnataka nini kwako…?”

Akamcheka.

“Usijali mwanaume, utanijua, japo sitahitaji kujitambulisha,  pia utajua kilichonileta kwako. Ila sio kwa staili hiyo babu ee, upo?”  Amos akamuelewa alichomaanisha kwa yale maneno yake ya mwisho, “…Ila sio kwa staili hiyo babu ee.., upo?” Alikuwa akimtahadharisha kwamba atamfahamu kistaarabu na sio kwa kumpelengesha.

“We mpumbavu nini? Yaani uvamie kwangu halafu unipangie namna ya kuku treate? Holy shiiit shenzi type…Unachopaswa ni kuwa mpole na mnyenyekevu. Upo kwangu na nina weza kukufanya chochote na sheria ikanirinda.”

Binti akamsogelea zaidi, akamsimamia kiubavu huku akimtazama bila kupepesa macho. Sogeleaji hii, ilimfanya kila mmoja ahisi kugusa kidogo kifua cha mwenzie.

Upande wa mkono wa kushoto wa yule mrembo, ulikuwa wima ukipakana kwa karibu kabisa na kifua cha Amos aliyekuwa akimtazama kwa makini yule msichana asiye mfahamu. Yule msichana alimsogezea uso wake usoni, ni tofauti ya takribani nusu sentimeta, pua zao zingegusana, akamtolea maneno ya maudhi.

“Oh…kumbe mwoga ee…!”

Akamcheka tena.

“Una-o-goooopwa, kumbe mbwa koko…unabweka tu. Lione, unadhani na mimi nakugwaya kama hao mbulula uliozoea kuwatisha, acha hizo mambo zako za ki k**a babu hii mashine kubwa.”

Amos Bwire hakuweza kuyasikia vema yale maneno ya shombo, kwani wakati binti akimtolea mbovu, akili yake ilikuwa bize kudadisi uso wa yule msichana anayejiamnini kupindukia.

Naye binti akaubaini udadisi uliomjaa yule jamaa. Wakati anamalizia kauli yake ya mwisho aliukwepesha uso wake pembeni, ili nia ya Amos isifanikiwe. Kwa bahati mbaya sana, alikuwa amesha chelewa.

‘Sura hii…sijawahi kukutana nayo hapo kabla, lakini kuna mahali nimewahi kuiona…’ Alikuwa akidadisi Amos, lakini ghafla aliitambua.   

‘Amanda…crazy irrogant…, nilikuwa nina uhakika kwamba una husika kwenye hii mission, mshenzi wewe…ila kwanza nilitaka kujiridhisha.”

“Sawa. Ushenzi ndio asili yangu. Nashukuru umeshanifahamu, kama nilivyokuahidi hapo awali, kwamba utanijua tu japo sitahitaji kujitambulisha, kwani mi ni mtu mashuhuri. Am celebrity.

“Celebrity wa wapi? We mshenzi tu. Huna u-celebrity wowote. Wewe ni nyang’au kama nyang’au wengine tu.” Amos alimjia juu.

“Sawa. Unaongea sana Amos. Sasa hivi unajifanya kunibeza, lakini umesahau kwamba, huyu nyang’au ndio aliyekusababisha utumie gharama kumtuma karani wako aje kunichunguza na kunipiga picha kwa siri kazini, kana kwamba mmekuwa waandishi wa magazeti ya udaku. Halafu unajitia unajua sheria, sheria gani inakuruhusu kumpiga mtu picha kwa kumvizia.”

“Kwa hiyo, unatakaje labda?” Amos alimoji akiwa ameghadhabika vilivyos.

“Haujui…?! Kwamba ni kinyume cha sheria kumpiga mtu picha bila ridhaa yake.” Amos alibaki kimya akifatilia kwa makini mienendo na tambo za yule dada. Kichwani akakumbuka ile siku alipotembelewa na mteja wake ofisini kwa mara ya kwanza, Darkshina Ghosh, katikati ya mazungumzo, yeye Amos alitaka kumuomba kitu…

“Naweza kupata…aaamm….anyway, basi.” Amos alitaka kumuomba kitu, lakini akasita.

“Kupata nini komredi?” Mteja wake alimuuliza baada ya kuona amesita kuwasilisha ombi lake.

“Ah… hapana. Acha tu.”

“Sema komredi.”

“Usijali. Kwa sasa tuishie hapo, unaweza kwenda. Ntakucheki muda mwingine ntakapokuhitaji.”

“Sawa.”

Siku hiyo, Amos alitaka kumuomba picha mnato ya huyo hawara yake aliyemtaja kwa jina la Amanda, akirini akiwa amesha muhesabu kama mmoja ya watu wakuwafatilia. (Suspect)Alisita kuwasilisha ombi lake, kwa kuwa anaijua nguvu ya mapenzi. Alihisi Jayanthi angemueleza hawara yake mambo yalivyokuwa yakienda, na kama kweli Amanda angekuwa ana husika, angejipanga kumkwepa. Ama kumkabiri.

Hakukosea.

Akaamua kumtumia katibu muhutasi wake, Noella. Moja ya majukumu aliyompa ile siku alipomtuma aende Posta mpya, kwenye ofisi za makao makuu ya TRA, ilikuwa ni kupeleleza nyendo za mtumishi aitwae Amanda, na kumpiga picha za siri ili kuipata sura yake. Ndivyo alivyofanya Noella.

Na ni baada ya kuzikumbuka picha alizowasilishiwa na Noella, Amos aliibaini sura ya huyo mvamizi wa nyumbani kwake usiku huo, alipokwa akimdadisi kwa makini. Amanda, a.k.a. crazy irrogant, jina la bandia alilompachika muda punde ulopita. Huyu ndiye hawara yake Darkshina Ghosh. Jambo ambalo si Amos wala Noella aliyelijua ni kwamba; Amanda ni shida!!!

“Nadhani hitaji la kunifamu tumeshamalizana. Bado la pili, nalo ndilo la muhimu. Kwa nini nimekuja kwako.”   

“Sihitaji kujua.”

“Ni lazima ujue Amos…si ulikuwa unajiuliza nini kimenileta hapa kwako.”

“We nani amekwambia nilijiuliza hivyo?”

“Unadhani na mimi ni jinga kama Darkshina na wenzake. Wale hawana akiri. Mimi nina akiri. Mimi ni muinterejensia kuliko wewe. Nina uwezo mkubwa wa kuisoma akiri ya mtu, kujua nini anawaza, na kipi kinapita kwenye ufahamu wake, just kwa kukutazama tu.” Akafyonza mfyonyo mrefu.

“Na kuanzia sasa, majukumu ya Darkshina Ghosh utayatekeleza chini yangu, kwa kufuata maelekezo yangu.” Alikazia Amanda.

“Unasemaje wewe?” Amos aling’aka.

“Habari ndo hiyo, vinginevyo utakufa siku si zako mwanaharamu wewe.” Amanda alimfokea sanjari na kumnyooshea kidole kwa msisitizo. Amos alishangaa sana. ‘Anajiamini nini huyu?’

“Na huyo Malaya wako uliyemtuma aje kunichunguza kazini kwangu, sijui kunipeleleza nini uko mnajuana wenyewe, mwambie akome akomae, anikome kama alivyokoma kunyonya kwenye titi la mama yake. PUMBAVU ZENU WOTE.” Amanda alizidi kufoka.

Amos Bwire alizidi kupigwa na bumbuazi. ‘Ameyajuaje yote haya?!’

“Unaniangalia…we nikodolee tu hiyo mi macho yako kama mjusi kabanwa na mlango. Mi ndio Amanda babu, shangingi la mjini. Ukimsikia mwingine huyo ni photocopy.”

Amos Bwire alitahayari!

*****

   Wakati CID Borry Kihemba akiapishwa kuwa inspekta, na kulipoti kituo chake kipya cha kazi cha Msimbazi centre Kariakoo, wilayani Bihalamuro mkoni Kagera kwenye kambi ya wakimbizi, hali ilikuwa tete, patashika nguo kuchanika.

   Kijana mmoja alijikuta mikononi mwa polisi akihenyeshwa mputa mputa kwa kipigo kizito sanjari na maswali magumu. Polisi kambini humo, walimshikilia kijana huyo, kwa kile walichodai kumtilia mashaka, kutokana na nyendo zake kutoeleweka, lakini pia kwa kosa la kukutwa akizengea zengea kwenye mahema ya wakimbizi wanamokaa wanawake na watoto wachanga tu, kwa sababu maalumu, na wanaume hawakuruhusiwa kuyazungukia, bali kwa kibali maalumu. 

   Askari polisi, Koplo Wasiwasi aliye kabidhiwa jukumu la kumshughurikia mharifu huyo, aliendelea kukabiliana naye.

   “Unaitwa nani weweeee…?” Lilikuwa ni swali moja lililoulizwa mara tatu na afande Wasiwasi kwa mtuhumiwa. Mtuhumiwa hakujibu. Afande Wasiwasi alichomoka kaunta kwa spidi kali, akamuendea pale alipokuwa amejikunyata yule mtuhumiwa, akampiga makofi mawili kwenye mashavu ya pande zote. Makofi yale yalitosha kumchangamsha jamaa na kumfanya akiri imkae sawa.

   “Sema unaitwa nani weweee…” Afande Wasiwasi anavyoipenda hiyo “weweee…”  Acha tu! Anavyoitamka sasa, kama ungebahatisha kumsikia, ungefurahi na roho yako. Pale kituoni ndio ushakuwa msemo wa askari wenzake, kila muda utasikia “Weweee…weweee…”

   “Eddy.” Kijana alijibu.

   “Eddy ndio nini…huna baba huna mama, kazi tu HEDDII’ hedi bichwa lako.” Askari yule mtata alimkoromea huku akimgeza kwa kubana pua, akamalizia kwa kufyonza huku macho ameyatumbua utadhani mjusi kabanwa na mlango.

   “Edson Anzael.”

   “Leta kitambulisho chako huko…mtu mwenyewe ulivyo kaa-kaa hueleweki, nina wasiwasi na wewe kabisa. Kama sio Al shabab, basi Boko haram! ”

   Edson “Eddy” Anzael kwa mujibu wa utambulisho wake, alijipapasa kwenye mifuko ya suruali, akachomoa pochi, humo akatoa kitambulisho cha mkazi chenye rangi ya kijani, akamkabidhi yule askari mbabe mbabe.

   “Ulikuwa unafanya nini kule weweeee?!” Koplo Wasiwasi alizidi kumuuliza, ikiwa ni mara ya pili bila kupewa majibu.

   Yule kijana aliyekuwa amevaa suruali ya jinzi ya bluu iliyoiva, shati la mikono mifupi lililopambwa kwa drafti za rangi mchanganyiko, aliendelea kuuficha uso wake kwa kukifumbata kichwa chake kwenye magoti aliyoyakusanya pamoja, sakafuni alipokuwa ameketi kwa kujiinamia. Ni kwenye ukumbi mdogo, uliomo ndani ya kituo kidogo cha polisi cha kambi ile.

   Kulia kwake, ndipo ilipokuwepo kaunta ya mapokezi, alikosimama afande jeuri, katili wa kuogopeka. Afande Wasiwasi.

   Alikuwa ni askari mwenye sura ndogo nyeusi, mrefu kidogo mfupi kidogo, mwenye mwili mdogo mdogo tu, lakini asiyependa masikhara kabisa.

   “Si nakuuliza weweeee…kwamba haunisikii.., jeuriii.., au dharau..?!”

   Kimya.

   “PHAAA!” Kofi.

   “AYAAAAAH.” Yule kijana alipiga ukunga, maumivu makali aliyoyasikia, yaliambatana na mishipa ya kichwa kumtutumuka, huku akishuhudia nyota nyingi zikielea hewani baada ya afande yule kuchomoka pale kaunta,, akamuendea na kumlamba kofi la kelbu.

   “Nilikuwa namtafuta ndugu yangu.”

   “Shenzi zako paka shume wewe…mpaka upigwe mbata ndio ujue kujibu, eeh..?! Nyambafu!” Wakatazamana kama paka na panya. Afande wasiwasi akarudi kaunta

   “Ndugu yako anaitwa nani?”

   “Ester Manyiru.” Edson aliongopa.

   “Ni nani yako?”

   “Dada yangu?” Kwa mara nyingine akaongopa.

   “Naye ni mtanzania, au mkimbizi?”

   “Jama, nimekwambia ni dada yangu, mimi niwe mtanzania yeye mkimbizi wapi na wapi?!” Yule mtuhumiwa jeuri alimjia juu afande Wasiwasi badala ya kumjibu. Lakini siku hiyo, alikuwa amepatikana mikononi mwa askari jeuri mwenzake. Walijeuriana!

   “PUMBAVU WEWE…ninapo kuuliza maswali yangu sihitaji maswali yako, nataka majibu…shenzi type mbwa koko…jibu upesi huko.”

    “Ni mtanzania.”

    “Sasa…kilichokuwa kinakushinda kujibu ni nini hasa…kwani wewe kuwa mtanzania dada yako akawa mkimbizi cha ajabu nini? Au kipi nashindikana hapo..?! Je kama mama ako alichepuka na mrwanda au mrundi, mi ntajuaje? Kunguru beti wewe.” Maneno hayo yalimuudhi vilivyo Edson, alitamani amrukie yule askari amrarue vipande vipande, lakini hakuwa na namna.

   “Sikiliza we pusi, huko ulikokuwa, hema namba kumi mpaka kumi na tano ni maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya wanawake wanaonyonyesha watoto wao wachanga tu. Ni utaratibu uliotolewa na shirika la afya ulimwenguni, Word Health Organisation-WHO. Ni mpango mkakati wa kuwaepusha watoto na ugonjwa wa tetekuwanga, uliolipuka na kusambaa kambini hapa kwa kasi. Mwanaume yeyote, haruhusiwi kusogelea… Au na wewe unanyonyesha?!” Kwa mara nyingine Edson akachefukwa na lile swali la shombo la yule askari.

   Usaili ukaendelea, muda wote kijana Edson, kwa sababu alizozijua yeye, alilazimika kutoa majibu ya uongo. Mpaka muda huo masaa yalizidi kuyoyoma. Alichodhamiria kukifanya kambini pale, hakuwa amekifanya, zaidi ya kuishia mikononi mwa polisi.

   Kila alipoifikiria hatari iliyokuwa mbele yake asipo tekeleza yampasayo kambini pale, alihisi kuchanganyikiwa. Alifahamu fika, kwamba; huko mbeleni, mambo yangezidi kumuharibikia na hali yake ingeenda kuwa mbaya zaidi.

   Sasa…

   Muda ulizidi kumtupa mkono!

   Hofu.

   Mashaka.

   Tahayari.

    Alikata tamaa ya kuishi kabisa. Mambo yalimuendea ndivyo sivyo, na maswali ya afande Wasiwasi yalikuwa mengi mno, tena yenye kukera. Hivyo hivyo waliburuzana kibishi, baadae askari yule aliamua kumfanyia hisani mtuhumiwa wake.

   Alichokifanya, asijue mtu aliyekuwa pembeni yake ni hatari kiasi gani, ama pengine yale majina ya Boko haram na Al Shabab yalimfaa kiasi gani, alimuelekeza wapi anaweza kwenda akamuulizia huyo ndugu yake Ester na kumpata kwa wepesi.

   Edson alimshukuru yule askari kwa hisani ile, wakaagana, akaondoka zake. Alichokifanya kijana Edson, badala ya kwenda alikoelekezwa na afande Wasiwasi ili kumpata ndugu yake Ester, alirudi tena kule kwenye yale mahema alikokutwa akatiwa nguvuni.

   Aliyafikia.

   Muda ulikuwa umeenda sana. Giza liliufunika mji, usiku ulikuwa umeingia.

   Alidhamiria kutekeleza jukumu lake bila kujali hatari iliyokuwa mbele yake. Binafsi alisadiki kwamba, hatari ya kutokamilisha majukumu yaliyomtoa mkoani Dar es salaam na kumfikisha pale, ilikuwa kubwa maradufu, zaidi ya kutiwa kizuizini na vyombo vya usalama kambini hapo.

   Lakini…

   Yaliyomkuta huko…alijuta kuzaliwa…

*****

Akiwa amejiremba akarembeka kama mwanamwari kigoli, alitembea haraka haraka kuelekea kwenye yale mahema alikozuiliwa kurudi, ili aonane na mtu aliyemfanya aende kambini hapo. Edson Anzael “Eddy”, aliyejivika mavazi ya kike ili asistukiwe, akirini alikuwa amevurugwa vibaya sana.

Lazima nionane na huyu msichana leoleo, la sivyo itani-cost.’ Alijisemea huku akipumua kwa nguvu.

Maelezo ya afande Wasiwasi, kwamba hema namba kumi mpaka kumi na tano yametengwa maalumu kwa ajili ya wa mama wenye watoto wanao nyonya, yalimpa uhakika kwamba, mwanamke aliyekuwa akimsaka kwa udi na uvumba, atakuwa huko.

Aliikumbuka sehemu ya habari aliyoisoma kwenye gazeti la MWANANCHI, “…binti huyo, amehifadhiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya bihalamuro, hema namba kumi na tatu.” Alipoikumbuka, ile habari, jambo jipya likamfunukia, ‘Aaah…kumbe hema namba kumi na kumi na tano  ni kwa ajili ya wamama wanao nyonyesha…huyu nae ana mtoto anaye nyonya…aisee,’ akakaza mwendo. Dakika chache baadae, alifika viungani hapo, akaanza kuzengea kwa tahadhari.

Aliliona hema namba kumi na tatu. Moyo ukamlipuka, mapigo ya moyo yakaanza kupiga mputa. Alihisi mwili ukimtetemeka wakati akitafuta namna ya kuzamia humo. Akatulia kusikiliza hali ya hewa, ilikuwa ya utulivu na ukimya uliopitiliza. Akajikaza kiume, kwa kutumia moja ya mlango wa hema lile, alijitoma ndani.

Sekunde tano nyingi, akawekwa chini ya ulinzi!

Aiseee!

Kumbe, yeye pasina kujua lolote, kuna watu walikabidhiwa jukumu la kuendelea kufatilia nyendo zake. Kutoka pale  kituo cha polisi, alikuwa chini ya uangalizi mkali wa wapelelezi. Wakati ana jiremba, anabadili mavazi yake na kujivika ya kike, mpaka anaanza safari ya kurudi kule alikozuiliwa, alifatiliwa. Alipojitoma hemani, akakamatwa!

Mbiu ikapigwa, watu wakafurika eneo hilo. Akawekwa mtu kati, akasulubiwa mfano wake hakuna. Wakati akipelekwa polisi, aliendelea kupigwa kipigo cha mbwa mwizi.

Lakini…hakutakiwa kurejeshwa polisi, alitakiwa apigwe mpaka afe. Ndio agizo la siri walilopewa na polisi wale wananchi wapelelezi waliokabidhiwa lile jukumu la kumfatilia.

 Alipewa kipigo kizito, sanjari na maswali magumu yaliyomshinda kuyajibu. Wakati huo huo, mawingu ya mvua yalikuwa yakitanda kwa wingi angani. Milio ya radi na miale yake vililindima kwa fujo angani. Ghafla, mvua kubwa ikanyesha.

Hali ilipozidi kuwa mbaya, akajitahidi kufurukuta mpaka akawatoka wale watu. Akatimka mbio.

Wakamkimbiza.

Hawakumpata!

Alifanikiwa kuwapotea, kwa sababu usiku ulikuwa mkubwa, mvua iliyoanza ghafla ilikuwa ikinyesha kwa nguvu, giza nalo lilikuwa zito.

Alikimbia sana. Akafanikiwa kutoroka kambini bila kumpata mtu aliyekuwa akimtafuta. Alifika barabara ya lami, akakimbilia na kudandia kwa nyuma lori moja lililokuwa likipita. Dereva wa lori bila kujua kuwa nyuma ya lori palikuwa na mtu amedandia kwa siri, aliendelea kukaza mwendo.

Safari ilikuwa ndefu, Edson asijue wapi alikuwa akipelekwa, alichokitaka yeye kwa wakati huo, ni kuiepusha nafsi yake na mauti.

Baadae walifika mahali ambako hakukuwa na mvua wala dalili ya mvua kabisa. Walikuwa mbali sana na kambi ya wakimbizi ya Biharamulo. Hofu ikaanza kumshika Edson, akijiuliza wapi alipokuwa akielekea, na atarudije alikotokea.

Usiku ulizidi kuwa mkubwa, lakini hakuacha kushikilia vyuma vya mlango wa nyuma ya lori. Mahali walifika, milio ya lisasi, mabomu na milipuko ya fataki ikawa inasikika kwa nguvu kutokea mbali na kule walikokuwa. 

Edson aligundua kitu.

Walikuwa jirani na nchi ya Burundi.

Kilikuwa ni kipindi cha machafuko ya kisiasa nchini Burundi, yaliyopelekea vitendo vya  uvunjifu wa amani, baada ya rais Pierre Nkulunzinza wa nchi hiyo, kung’ang’ania madaraka ya urais kwa nguvu, yaliyopasa kukoma mwaka 2015 kwa mujibu wa muongozo wa katiba ya nchi hiyo.

Ripoti ya vyombo vya habari duniani, ilikuwa ikilipoti namna hali ya usalama nchini humo ilivyokuwa   mbaya. Vitendo vya wananchi walikuwa wakimpinga mtawala huyo, waliendesha maandamano kila kona ya nchi, sanjari na kuchoma matairi barabarani. Hali hiyo, ilisababisha mpambano mkali, kati ya wananchi na vyombo vya usalama.

Kwa siku kadhaa, vurugu hizo zilikuwa zikiendelea mpaka mida ya usiku.

Edson alitahayari.             

Safari iliendelea. Baada ya mwendo mrefu, ghafla, mlipuko mkubwa na wa kuongofya uliwakumba. Lile lori lilirushwa hewani kama kishada. Likiwa hewani, lilimeguka katikati na kufanyika mapande mawili, lilibiringika mara kadhaa, kabla ya kushuka chini na kujibamiza vibaya sana.

Edson Anzael, alitupwa juu umbali mkubwa na kuelea hewani kama puto, akadondokea mbali kwenye eneo lenye nyasi nyingi.

Bomu!

Mitego ya waasi wa nchini Burundi…

Walikuwa mpakani mwa Tanzania na Burundi…aisee!

Alisikia maumivu makali yakiuchonyota mwili wake wote, kichwa kilimuwia uzito kwa ganzi iliyomtapakaa mwilini, fahamu zikitaka kumuhama. Akahisi kukata roho.

Akihofia usalama wake, alinyanyuka akatimua mbio. Alikimbia sana, akikatiza kwenye pori lilopakana na ile barabara, asijue alikuwa akielekea wapi, mpaka alipojikuta yuko chini ya ulinzi mkali.

Tochi kali za watu waliotokea mafichoni zilimmulika mgongoni kutokea kule alikotokea, kisha sauti iliyomuamrisha asimame palepale alipokuwa ikasikika. Alisimama kwa woga bila kugeuka.

“Unaelekea wapi huko wewe…?!” Sauti kutoka kwa wale watu ilikoroma. Kimya.

“PWAAAA!” Moja kati ya bunduki za wale wanajeshi ilifyatuliwa risasi, mlio wake ukarindima hewani. Edson akashtuka vibaya, woga ukimjaa maradufu.

“Geukia huku.” Sauti nyingine iliunguruma. Edson akageuka. Sasa.., mianga mikali ya zile tochi ilimmulika sawia usoni na kumkera vibaya sana. Akavikusanya viganja vya mikono yake usoni kujikinga na ile miale iliyomchoma na kumuumiza macho. Ndipo alipobaini wale watu wote walivaa sare za jeshi, sanjari na zile tochi, walikuwa pia na mitutu ya bunduki iliyonyooshwa kumuelekea alikokuwa. Edson alibabaika kwelikweli.

‘Duuh..! Ni nini hiki tena jamani?! Nimeyakanyagajee.., au ntakuwa nimevamia kambi ya jeshi niniii..?!’ Edson alijiwazia. Hofu kubwa ilimjaa, ujasiri ukampungua.

 “Rudi huku, unapajua unakokimbilia lakini…au una puyanga tu kama hayawani?” Hakujibu, wala hakusogea.

“Rudi huku weweee…acha ubishi.”

‘Kwani kuna nini huku…mbona hawaji kunikamata?!’

Wakati akiri ikiwaza na kuwazua kwa kukimbizana bila majibu, alisikia sauti fulani nyuma yake. Akastuka. Maji.

“Waaaaahhh…” Sauti ile iliendelea kuvuma.

Maji yanaporomoka…

“Waaaaah.” Sauti ile iliendelea kuvuma.

‘Mh…mbona kama ni…mbona kama ni…aisee..la la laaa…” Edson akajua amepatikana, baada ya kugundua kwamba, sauti ile, ilikuwa ni mvumo wa maji ya mto. Kumbe alikuwa akikimbilia mtoni.

“Una kimbilia mtoni ili ujiue au umekuwa samaki unataka uogelaa…maana tuna kwambia uje huku hautaki, au tuichabange hiyo miguu yako kwa risasi ndio ujue tuna maanisha?!”

“Halafu amesimama kwenye ngema inayomeguka kila siku mshenzi yule, sasa sijui akiporomokea huko nani atamuokoa?” Sauti nyingine ilisema.

‘Khaa…!’ Eddy alizidi kutishika.

Hakuamini kwamba alikuwa akikimbilia kifo.

“Jisalimishe uko kwenye hatari we jinga, hii ni amri wala sio ombi. Njoo huku, na ukijitia jeuri utakufa bila kupata hata nukta ya kuliita jina la Mora wako. Nyambafu!

Vitisho vilizidi kuwa vingi. Akawaza cha kufanya, hakuwa na namna. Sasa basi, baada ya kubaini wazi kwamba alikuwa kwenye hatari kubwa, ya eidha kuuwawa kwa risasi za wale wanajeshi, au kwa kusombwa na maji ya ule mto ambao hakuwa amefanikiwa kuutia machoni, akajua alipaswa kujiokoa. Na njia pekee, ilikuwa ni kujisalimisha mikononi mwa wale wanajeshi waliomzingira…kuliko kifo!

Akawa mpole.

Akaanza, kupiga hatua kuwaendea wale wanajeshi kama walivyo muamuru ili ajisalimishe.

Alichelewa…

*****

Katikati ya kijiji pweke chenye makazi machache ya wakaazi, ndani ya nyumba ndogo ya kifukara, iliyojengwa kwa udongo ikaezekwa kwa makuti, alikuwemo dada mmoja mwenye umri wa miaka takribani 27.

Kwenye chumba kilichotandwa na wingi wa nyumba za buibui,  chenye mwanga hafifu kutokana na madirisha yake madogo ya miti, ndimo alimokuwamo. Mbali na chumba hicho, ile nyumba, pia ilikuwa na sebule ndogo na chumba kingine kilichopakana na ile sebule.

Kule nje, kweneye uwanja ulio kingwa kwa uzio wa nyasi, palijengwa choo na jiko la mabati yaliyojaa kutu kuanzia chini mpaka juu, [{full suit}].

Aliketi aliketi kwa kunyoosha miguu yake, kwenye sakafu ya udongo isiyojua sementi inafananaje, akitwanga majani fulani ya kijani kwenye kinu. Kisha akawa anayatoa yale majani aliyoyatwanga, anayakamua kwa kiganja cha mkono wake, na maji yaliyochuruzika, aliyaelekeza yamwagikie kwenye chungu alichokuwa nacho kando ya miguu yake.

Alijichokea mwenyewe kwa dhiki, shida na matatizo chungu mzima. Mavazi aliyojivika yalikuwa yakimaskini mno. Kwa namna maisha yalivyompiga, hakuonekana na uzuri wowote. Lakini, kwa wanaume wakware wanaojua kumuangalia vema msichana aliyeko katika hali yoyote, huyu dada alikuwa ni mzuri si haba.

Uzuri na urembo wake ulifichama kwenye mioshi na masizi ya kuni aliyozoea kushinda nayo kutwa nzima. Umbo lake la haja, lenye mvuto wa kutamanisha ki-ngono, [{sex girl}], lilifichama kwenye mavazi yake yaliyochakaa, kiasi cha kupoteza mvuto wa kuyatazama.

Wakati akiendelea na ile shughuri, ghafla, alistushwa na sauti ya mtu aliyepiga chafya kutoka kwenye kile chumba kingine. Alishangaa…Kulikoni?

Alinyuka upesi akapiga hatua za haraka haraka kuelekea kule chafya ilikotokea. Alipofika, aliachia tabasamu pana, akinyoosha mikono juu na kumshukuru Mungu.

“Jamani Wow…Mungu mkubwa jamani acheneni Mungu aitwe Mungu.” Alitamka yale maneno kwa sauti ya chini huku akizidi kukikurubia kitanda cha kamba na miti alipokuwa amelala mwanaume mmoja, aliyepoteza fahamu karibu ya kufa.

Aliketi kitandani, jirani kabisa na yule mgonjwa. Hatimaye umeamka.., wow…pole sana jamani…” Alitamka kwa furaha kubwa. 

Pale kitandani, yule mgonjwa hakuweza kujibu wala kuongea chochote, zaidi sana aligumia kwa maumivu makali. Alionekana kupigwa bumbuazi kama mwenda wazimu, asiejua alikuwa wapi, wala alichokuwa akikifanya.

Alifumbua macho yake kwa taabu, kama mlevi. Akaanza kutoa miguno ya maumivu. Akataka kuamka. Yule dada akawahi kumzuia.

“Taratibu kaka…hali yako sio nzuri kiasi hicho.” Yule binti alitamka, yule kaka akashangaa.”

‘Hali yangu sio nzuri…kivipi? Kwani hapa niko wapi, nafanya nini…na ni kipi hasa kimenipata…mbona…mbona…mbo…daah aisee…” Yule jamaa alihisi maumivu makali mwili mzima. Lakini, kuna sehemu mbili za mwili wake alihisi pakipwita zaidi. Kwenye paji la uso, upande wa kuume wa tumbo. Alikuwa akihisi kitu kama panga kali likimkatakata.

Yule binti alimtazama yule jamaa, naye jamaa alibaki kumtazama yule binti. Walitazamana!

 Wakati msichana yule alionekana kufurahikwa na hali ya yule mwanaume, yule mwanaume alibaki kimya. Asiyecheka, asiyenuna, yupo yupo tu alimradi. Na walipokuwa wakitazamana, swali fulani kuhusiana na yule binti lilipita kichwani mwa yule mwanaume. ‘Ni nani huyu?’

Hali iliendelea vile mpaka baada ya siku tatu, ndipo kidogo walipoweza kuzungumza japo kwa taabu.

Yule dada ndiye aliyeanza kujitambulisha kwa yule kaka, wasifu wake, na namna alivyompata yule kaka. Maelezo yake, ndiyo yaliyomzindua yule kijana.

Akakumbuka…                

*****

Siku ile…

Vitisho vilizidi kuwa vingi. Akawaza cha kufanya, hakuwa na namna. Sasa basi, baada ya kubaini wazi kwamba alikuwa kwenye hatari kubwa, ya eidha kuuwawa kwa risasi za wale wanajeshi, au kwa kusombwa na maji ya ule mto ambao hakuwa amefanikiwa kuutia machoni, akajua alipaswa kujiokoa. Na njia pekee, ilikuwa ni kujisalimisha mikononi mwa wale wanajeshi waliomzingira…kuliko kifo!

Akawa mpole.

Akaanza, kupiga hatua kuwaendea wale wanajeshi kama walivyo muamuru, ili ajisalimishe.

Kwa bahati mbaya sana, alikuwa amesha chelewa.

Alitaka kupiga hatua ya kwanza, mguu ukamsaliti. Ndipo alipohisi hali isiyokuwa ya kawaida pale ardhini. Palikuwa na badiliko la ajabu. Mguu badala ya kwenda mbele, ulirudi nyuma. Hakuurudisha yeye.

Kama hakuurudisha yeye…nini basi kilitokea?

Udongo wa ile sehemu ulitita kidogo, na kuuvutia nyuma mguu wake. Akapiga hatua nyingine kwa mguu mwingine, mambo yakawa yaleyale. ‘Whaaat?’

 “Halafu amesimama kwenye ngema inayomeguka kila siku mshenzi yule, sasa sijui akiporomokea huko nani atamuokoa?”

Yale maneno yalijirudia kwenye ufahamu wake, kabla hajagundua kwamba alikuwa amesha chelewa sana. Hakuamini kilichomfika, ila hiyo ndiyo ikawa hali halisi.

Ki-utani-utani udongo ulizidi kutitia, na kama masikhara vile ngema, yaani dongo kubwa la sehemu ya ukingo wa mto lilimeguka, likaanza kuporomokea mtoni, huku ikimshinikiza naye kuambatana nalo. Hakuamini kilichokuwa kikimfika. Alichokisikia kutokea kwenye lile kundi la wanajeshi ni sauti za hamaniko zilisikika kwa fujo.

“Hey…nini hicho kinatokea…oya…ya…oya.., hataariii… ayaaaaah…” Kelele za wanajeshi zilikuwa nyingi, lakini hazikulizuia lile dongo alilosimamia Edson Anzael lisiangukie mtoni. Likiwa pamoja naye, kabla halijamuacha akielea hewani.

Edson alipiga kelele za hamaniko, “Mama weeee…nakufaaaa, mamaaa…lalalalaa, ayaaaah….”

“PWAAAAA…”

Sauti nzito ilisikika baada ya ule udongo kuyafikia maji, maji nayo yakaruka hewani kama tsunami, Edson naye akafatia.

Kutoka kwenye ile ngema, mapande mengine mengi ya udongo yalifatia na kumbamiza vibaya Edson kule majini alikokuwa akitapatapa, yakamzamisha kilindini kabisa mwa yale maji. Ama kwa hakika, ule udongo ulidhamilia kumzika jamaa mzima mzima.

Edson asiyejua kuogelea wala kujiokoa kwa namna yoyote na ajali ya maji, alijikuta akinywa maji mengi wakati akizidi kutitia chini, kabla hajaibuka juu huku akiparangana kuiokoa roho yake. Akatitia tena, akaibuka tena. Kisha, maporomoko makubwa ya ule mto, yalimsomba kwa nguvu na kumpeleka asikokujua. Hakuwa na namna wala muamana. Akiwa majini, kwenye ile hekaheka, Edson aliamini kweli siku za mwanadamu za kuishi zina ukomo. Kwa mara ya kwanza maishani mwake, alikiona kifo kikiyatwaa maisha yake.

*****

“Basi hukufa Edson, uliokolewa na wananchi waishio kandokando ya ule mto…Mungu bado ana haja nawe hapa duniani.” Yalikuwa ni maneno ya yule dada aliyekuwa akimpatia matibabu kwa njia ya kienyeji, aliyejitambulisha kwake kwa jina la Angel.

“Siamini Angel…siamni kama bado niko kwenye dunia ya walio hai, sio kwa dhahama ile.”

“Ni kweli, inaonekana ulipitia hatari kubwa sana, kusombwa na maji ya ule mto kisha kuokoka sio kitu lahisi, lakini kwa Mungu hakuna kinacho shindikana.” Angel alisistiza.

“Ule mto una asili ya mawe mengi, pasina shaka ndio yaliyokukata usoni na tumbo lako la kuume…ulikutwa damu nyingi zikimwagika sana kwenye majeraha haya.” Angel alimwambia Edson, huku akiyasonta yale majeraha, kisha akarejea kumuelezea kwa kina namna alivyokutwa kando ya ule mto.

Alikutwa amelowa maji na damu, akiwa amezirai hoi bin taaban, mwili wake umejikita kwenye furushi la takataka lililonasa kwenye ukingo wa mto, akadhibitiwa na mawe yaliyoota upenuni mwa mto ule.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa pona yake, vinginevyo, Edson Anzael-Eddy, angefia mule majini.

*****

   Kati ya wananchi waliokuwepo wakati wa uokozi wa Edson, Angel ndiye aliyejitolea kumpa hifadhi majeruhi yule, aliyekionja kikombe cha mauti, kisha akakataa kukinywa. Akampa matibabu kwa dawa za miti shamba, mpaka wiki moja baadae alipozinduka.

   Edson alimshukuru sana yule binti kwa wema na fadhili zake. Edson hakuthubutu kumueleza ukweli wa chanzo cha ile kadhia aliyokumbana nayo. Alimdanganya mambo mengi tu kwa sababu zilizomlazimu kudanganya.

   Lakini Angel alimueleza ukweli wa maisha yake, kwamba, yeye kiasili ni mrundi, ambaye wazazi wake walinunua uraia wa Tanzania. Maisha yao yamekuwa ya kifukara miaka nenda miaka rudi, kiasi cha kupelekea yeye Angel kukosa kitu cha muhimu mno alichokihitaji sana maishani mwake. Elimu.

   Miaka kadhaa iliyopita waliikimbia nchi yao ya Burundi kutokana mapigano yaliyosababishwa na machafuko ya kisiasa, yaliyopelekea vita vilivyodumu kwa muda mrefu, vilivyokuwa vikiendeshwa na makundi yanayoipinga serikari ya mwenyekiti wa chama cha The National Council for the Defense of Democracy-Force for the Defense of Democracy, (CNDD-FDD),rais Pierre Nkuluzinza. Wazazi wake Angel walifia Tanzania miaka michache iliyopita kwa sababu mbalimbali za kibinadamu.

   Mwisho kabisa, walikubaliana kuishi pamoja kwa  muda wote wa matibabu, kisha baaada ya hapo, Edson angerejea nyumbani kwake mjini Mwanza anakoishi.

   Angel alimpeleka Edson kwa wakala wa mitandao ya simu, akarudisha namba yake ya simu aliyoipoteza kwenye zile hekaheka. Kuanzia hapo, akawa anatumia njia ya kidijitali kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zake za benki, kwenda kwenye simu kisha anatoa kwa wakala. Kuanzia hapo, maisha ya Angel na yule bwana yakawa mazuri.

   Edson alikuwa na akiba ya fedha nyingi, wala swala hilo halikumtia wasiwasi kabisa. Angel akajikuta fadhila aliyomfadhili yule mwanaume ikimlipa maradufu. Haikuchukua muda, uzuri, urembo na mvuto wa Angel ulifichuka kutoka mafichoni. Edson akatahayari kwa namna yule msichana alivyoumbwa akaumbika. Alishangaa sana. Kuanzia hapo, jicho la Edson likawa likimtazama kwa namna ya tofauti yule binti. Taratibu hali fulani isiyokuwa ya kawaida ikamuingia Angel, akajishangaa namna alivyojikuta akianza kumuonea aibu yule mwanaume. Na kila walipotazamana, Edson akawa akipagawa mfano wake hakuna.

   Mara nyingi alipokuwa akilala, fikra na mawazo yakawa yakimkanganya yule jamaa. ‘Mtoto ni mrembo, kaumbwa akaumbika. Umbo lake hatari si mchezo…anitazamapo, yale macho sasa.’

   Msukumo wa kumueleza Angel namna anavyojisikia kuhusu yeye ukamjaa, lakini ataanzaje kumtongoza dada’ke.

   Katika namna ambayo kila mmoja wao asingeweza kuelezea ilianzaje, wawili hawa walijikuta wakizama penzini. Wakawa wapenzi!

   Penzi lao likawa tamu sana. Edson hakuwa na mke, Angel hakuwa na mume, pingamizi litoke wapi.

   Ili kudumisha mapenzi yao hayo, wakakubaliana kwamba, watakuja kuoana kwa ndoa kabisa.

   Edson akafarijika mno kumpata yule mrembo. Angel vivyo hivyo, alijiona mwenye bahati kumpata Edson, kijana handsome, sex, mwenye ukwasi wa kutosha.

   Lakini…

   Wakati hayo yote hayo yanaendelea, Edson hakuwa na amani kiasi hicho. Aliwaza hatima ya maisha yake iliyokuwa hatarini.

   Aliikumbuka safari yake ya kambi ya wakimbizi ya Ngara. Kuna jambo la muhimu sana lilimpeleka huko, wala hakulifanikisha. Matokeo yake akajikuta kwenye mapambano mazito ya kuiokoa roho yake.

   Maisha yake na Angel pale kijijini yalikuwa mazuri mno, lakini, yalikosa furaha kabisa kwa sababu alibeba siri nzito mno moyoni mwake. Siri iliyotesa maisha yake!

   Siku moja, wakiwa pamoja nyumbani kwao, baada ya kuivunja amri ya sita, Angel alimuaga Edson kwamba anaenda porini kukusanya kuni. Wakabusiana, wakaagana na kuachana kwa mahaba mazito. Angel aliyezama kwenye dimbwi zito la mapenzi, alimuahidi mwenzake kuwa hata chelewa kurudi, ili awahi kumpikia chakula kizuri.

   Walikubaliana hivyo.

   Angel aliondoka, akarejea baada ya saa tatu. Alipofika, hakumkuta mpenzi wake. Akamuita hakuitika. Akamtafuta hakumuona. Alipotazama sanduku la nguo alilolinunua pale kijijini na kulitumia kuhifadhi nguo zake, lilikuwepo, na nguo zake zilikuwepo.

   Akampigia simu kwa simu ya mkononi aliyonunuliwa na huyo huyo mpenzi wake. Haikupatikana. Akavuta subira akijipa moyo kwamba, huenda Edson ametoka kidogo matembezini. Alingoja na kungoja.

   Edson hakurudi tena…

*****

   Muda uliyoyoma, usiku ukazidi kuwa mkubwa. Dalili ya Edson kurudi haikuwepo. Angel akakata tama. Akataka kulipoti polisi, lakini sharia ya nchi haikumruhusu. Sharia inasema, mtu mzima akipotea, atafutwe na wahusika kwa muda usiopungua saa ishirini na nne, kabla ya kutoa lipoti polisi. Ikambidi afanye upekuzi yakinifu mule ndani. Ndipo alipokutana na karatasi ndogo imekunjwa ikahifadhiwa chini ya mto. Ilimtoa machozi.

   Iliandikwa ujumbe…

   Kwako mpenzi Angel,

Mimi hapa Edson Anzael. Pole sana kwa ujumbe huu, ambao naamini utakuumiza kama sio kukuliza kabisa. Najua unanipenda sana, najua ni kiasi gani umeweka tumaini juu yangu. Najua ni ndoto yako na matamanio ya moyo wako kwamba siku moja tuje tuoane. Lakini kumradhi sana love kwa kukuumiza. Naomba nikueleze tu ukweli kwamba; mimi ni mme wa mtu. Tena mume wa ndoa ya kanisani kabisa.

   Wakati ule tulipoanzisha mahusiano yetu, sikudhani kama tungefika huku tulikofika. Tumefika kwenye kilele cha juu kabisa cha mahaba. Na ndio sababu nimeona bora niokoe jahazi, nikuache kwa kupoteza kabisa mawasiliano yangu mimi na wewe. La sivyo, najua hatuwezi kuwa marafiki eti kwa kigezo cha kusitisha mahusiano ya maloveee…

   Hapana pasina shaka hatutoweza. Hivyo, basi nimeondoka, nimerudi kwetu Mwanza waliko mke na watoto wangu. Yaliyotokea baini yangu na wewe, acha ibaki story. Nimekuwekea milioni tano kwenye akaunti yako ya benki niliyokufungulia, utazitumiaje, ni wewe tu upendavyo. Nakutakia kila la kheri, Mungu akubariki, na akujalie mwanzo mpya wa maisha mapya bila mimi. Na mwisho wa siku akupe mume mwema. Nakushukuru mno kwa fadhili zako, na mapenzi yako motomoto. Ama kwa hakika, unastahili kupendwa. Una haki ya kuwa mke wa mtu.

   Ntayamiss mahaba yako, ntayamiss makumbatio yako, ntamiss kiss na jinsi tulivyokuwa tuki sex. Lol, ama kwa hakika, tumekuwa na siku chache zilizoweka alama kubwa maishani mwetu. Lakini yote kwa yote ni kwa wema. Nisamehe sana mpenzi kwa kukuumiza.

      Byee byee,                                      

mie mpenzi wako nikupendaye kwa dhati,

Edson.

   Mpaka anamaliza kuusoma ujumbe ule, Angel alikuwa ametepeta kwa kulowa machozi mwili mzima. Akahisi dunia imemgeuka, imemsaliti na kumtelekeza peke yake kwenye sayari isiyojulikana. Alilia sana!

   “Kwa nini umenitenda hivi jamani mimi, kwani nini Edson, kwa nini?! Au kwa sababu mimi yatima? Au kwa vile sijasoma, au huu umasikini wangu jamani baby, si ulisema unanipenda hivi hivi nilivyo sasa imekuwaje tena? Hata kama una mke na watoto mimi bado nakupenda, lol…hahahaahhaa….” Alilia sana Angel, wakati huohuo akilini mwake kulipita wimbo aliokuwa akiupenda sana, wa mwanamama Natalia Cole…. Uitwao I miss you like crazy…

      Japo kuwa hakuwa na uwezo mzuri wa kukizungumza kiingereza, lakini mashairi ya wimbo huo, aliyamudu vema. 

   Even though its been so long, my love for you keeps going strong,

   I remember the things that we used to do, a kiss in the rain till the sun shine through,

   I’d try to deny it, but A’m still in love with you.

I miss you like crazy..,,

I miss you like crazy..,

Ever since you went away

Every hour of every day,

I miss you like crazy..,,

I miss you like crazy..,

No matter what I say or do,

There’s just no getting over you.

   I can see the love shining in your eyes,

   And it comes as such a sweet suprise

   If seeng’s believing its worthy,

   the wait so hold me, and tell me its not too late,

   We’re so good together,

   We’re starting forever now,

   And I miss you like crazy.

I miss you like crazy..,,

I miss you like crazy..,

Ever since you went away

Every hour of every day,

I miss you like crazy..,,

I miss you baby..,

A love like ours will never end,

Just touch me and We’re there again.

   Just one night  and we’ll have that magic felling like we used to do,

   Hold on tight and whatever comes our way we’re gonna make it through,  

 If seeng’s believing its worthy,

   the wait so hold me, and tell me its not too late,

   We’re so good together,

   We’re starting forever now,

   And I miss you like crazy.

I miss you like crazy..,,

I miss you like crazy..,

Ever since you went away

Every hour of every day,

I miss you like crazy..,,

I miss you baby..,

No matter what I say or do,

There’s just no getting over you.

And I miss you (baby),

And I miss you (baby),

All the tender love you gave me,

   When a felling getting this strong,

   You know the really thing come along

   And I miss you I miss you like crazy baby, only you’re should be “you are” sweet love can save me, I miss you like crazy, a love like ours will never end,

   Just touch me and we’re there again,

   Miss you like crazy, I miss you like crazy,

   Yaani umenikimbia na kuniacha peke yangu kwenye hiki kijiji pweke, mfariji wangu ewe msaada wangu, hata hizo fedha za nini sasa. Mimi sihitaji fedha zako Eddy nakuhitaji wewe. Umeniacha peke yangu bado unajiita mpenzi wangu, eti, mie mpenzi wako nikupendaye kwa dhati,

Kweli jamani ya kweli hayo… aah lalalaa…usiende Mwanza love baki na mimi…” Alilalama binti wa watu. Lakini ghafla!  Alisikia sauti nzito ya kiume ikiunguruma kutoka kwenye mlango wa kuingilia hicho chumba alimokuwa akilala na Edson.

   “Hajaenda Mwanza huyo!” Angel alistuka baada ya kuisikia sentesi hayo. Kutahamaki, alistukia amelengwa na mdomo wa bastola kutokea kulekule mlangoni.

   Aliogopa sana!

*****

   Edson Anzael  “Eddy,” alizikwea kwa kiherehere ngazi za hospitali ya Rabininsia Memorial iliyopo Tegeta, maeneo ya Namanga jijini Dar. Uso wake ulikuwa umesawajika balaa. Kichwa kilimuwia uzito kwa uchovu uliosababishwa na wingi wa mawazo, huku moyo ukipiga mapigo yake pasina utulivu.

   Alichanganyikiwa!

   Alikuwa amepatikana.

   Kumbukumbu juu ya mambo yaliyokuwa yakimkabili mfurulizo hazikumtoka. Hakuwa na nukta ya kukipumzisha kichwa chake kuwaza. Mambo yalikuwa yakimuendea kombo, na kama angefanya mzaa, usalama wa maisha yake ulikuwa hatarini.

   Alifika kwenye korido ya ghorofa ya tatu, akaanza kuitafuta wodi ya wanawake na watoto. Alimuona muuguzi mmoja wa kike, akajikaza kuificha hali yake yakutahayari, akamkaribia na kumuuliza ilipo wodi ya wanawake na watoto. Muuguzi yule akamuelekeza. Edson akafata maelekezo yale, akaipata. Moyo ukamlipuka “PAAAAHHH!!!”

   Kwa sekunde kadhaa aliganda akiwa amesimama nje ya chumba ambacho mbele yake, kulikuwa na mlango wenye maandishi yaliyosomeka kimombo, ‘women and chirldren ward,’ yaani wodi ya wanawake na watoto.

   Alisisimka, akwa amesimama umbali wa hatua tatu kutoka ulipo ule mlango, na mgongo wake ukiugusa ukuta wa nyuma yake. Kwenye kolido lile palisheheni pilikapilika za mipishano ya wagonjwa, wageni na wauguzi. Hofu ilizidi kumkabili lakini maswaibu nayo yalikuwa yamemzidi, akajikaza kiume, akaukurubia ule mlango. Akakamata kitasa, akajitoma ndani.

   Alipozama tu ndani ya kile chumba, macho yake yalipambana na vitanda vya wagonjwa vilivyopangwa vema kwa mistari miwili iliyotenganishwa na uwazi uliofanya njia ya katikati. Humo akawashuhudia wa mama na watoto waliolazwa, wauguzi wachache pamoja na wageni.

   Hakutaka kupoteza muda, moja kwa moja akaanza kupiga hatua kukiendea kitanda alichokikusudia, alipolazwa mtu aliye sababisha yeye akawa pale muda ule.

   Hakuwa amewahi kukiona hapo kabla, wala hakuwa amewahi kufika hospitalini pale hapo kabla. Lakini, kichwani alikuwa na maelekezo yakumfikisha kwenye lengo.

   Alifika kwenye kile kitanda, cha tatu kutoka mlangoni, upande wa Magharibi Kaskazini mwa ile wodi. Hapakuwa na mtu, wala hapakuwa na dalili yoyote ya kuwapo na mtu.

   Matandiko ya kitanda kile yalitandikwa vizuri mno, wala hakukuwa na mikunjo ya aina yoyote ambayo ingeashiria pengine labda kulikuwa na mtu anayelala na huenda ametoka kidogo.

   ‘Siyo kweli… nimechezewa kekundu?’ Edson alijiwazia moyoni huku akihisi uchizi ukimuanza. Alichanganyikiwa kwelikweli. Sasa, hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi. Akakaza moyo asije kuwehuka.

   ‘Nini maana ya haya mambo.., wamekusudia nini hawa jamaa… eeeh?!’ Alikuwa akizungukazunguka mule wodini wakati akijiuliza maswali pasina majibu. Alitamani kumuona huyo mgonjwa aliyekuwa amelazwa kwenye kile kitanda cha tatu kutoka mlangoni, upande wa Magharibi Kasikazini mwa ile wodi. Alikuwa mtu wa muhimu mno kwake kwa muda huo. Alimuhitaji sana.

   Wakati akijaribu kutafakari hatua gani achukue, wazo likapita kichwani mwake. Awaendee wauguzi waliokuwa zamu mule wodini, awaulize pengine wana taarifa za huyo mgonjwa ambaye kwake hakuwa na shaka kabisa kwamba hakuwa mgonjwa, bali mtego, sio aliotegewa bali aliosogezewa masudi ili sio umnase bali ajinase mwenyewe.

   Akaanza kuisogelea sehemu ya wauguzi, hatua chache kabla hajaifikia, mara simu yake ya mkononi iliyokuwa kwenye mfuko wa suruali yake ya jinzi ikaita. Ni kama iliita maksudi, lol! Akaichomoa, akaitazama, akakuta mpigaji anatumia namba mpya. Akastuka. Akasita kuipokea. Lakini hakuona kama ingekuwa sahihi kutokuipokea, akajikaza kiume akaipokea. Alipomaliza kuzungumza, jambo jipya lililomshangaza na kumuacha midomo wazi lilimfunukia. Akapagawa.

   Mpigaji alikuwa ni mwanamke, au labda binti ambaye hakutaka kujitambulisha kwake moja kwa moja ni nani. Ila, alimpa maelekezo ya hatua za kuchukua kwa wakati ule aliokuwa mule wodini.

   ‘Nani huyu… na amejuaje kwamba muda huu nimo humu wodini, tena anauhakika wa asilimia miamoja. Hawa jamaa wamedhamilia kunichezea mimi drama, au sivyo. Lakini, mbona kama huyu yuko kinyume na hawa watu wabaya.’ 

   Alitamani kumpuuzia mtu aliyetoka kuzungumza naye kwenye simu. Moyo ukamsaliti, ukimshurutisha kutii, hususani kila alipojaribu kuivutia kumbukumbu ile sauti. Akajikuta ameahirisha kuwaendea wale wauguzi wa zamu ili kupata taarifa za yule mgonjwa wao aliyekuwa amelazwa kwenye kile kitanda ambacho sasa, hakikuwa na dalili ya kuwa na mtu akilaliaye kwa muda wa karibuni. Akatoka nje ya ile wodi ‘mkukumkuku,’ mpaka koridoni.

   Pilikapilika za hapa na pale zilikuwa zikiendelea, wakati macho yake yalipokuwa yakishuhudia tukio lililomfunua mdomo na kumuacha kinywa wazi kwa sekunde chache.

   Kutoka pale alipokuwa, mita chache mbele yake kulikuwa na chumba chenye lifti. Muda huo, aliweza kuishuhudia lifti ile ikiwa inafunguka, baadhi ya watu wakitoka na wengine wakiingia. Lakini sasa, katika watu walioingia, walikuwa ni wauguzi wa kike wawili, waliojifunika nyuso zao kwa vitambaa maalumu vya kujizuia na magonjwa ya kuambukiza. Vitambaa vile viliwaacha wazi sehemu ndogo sana ya nyuso zao.

   Walikuwa wakimsindikiza mgonjwa kwa kusukuma kiti cha magurudumu alichokalia.

   Kwa mbali… aliweza kuwaona.

   Kwa bahati mbaya, umbali ule ulimzuia kuwafahamu wale wauguzi pamoja na mgonjwa wao, japo kuwa alihisi kumfahamu yule mgonjwa, ingawa hakuwa amefanikiwa kumuona vema.

   Na kama yule mgonjwa ndiye yule mtu amdhaniaye, basi pasina shaka hata wale wauguzi hawatakuwa wauguzi, bali wamejifanya wauguzi kwa sababu maalumu wanaoijua wao. Na wamefanya vile maksudi ili hali wakijua fika kwamba muda ule yeye Edson anawaona.

   Kwa nini…

   Alipiga hatua za haraka kuiendea ile lifti lakini alichelewa. Sekunde chache aliishuhudia milango ya ile lifti ikijifunga, wakati huo, mmoja kati ya wale wauguzi aligeuka wima akatazama moja kwa moja kwenye ule uwazi uliotengenezwa na milango ya lifti.

   Sasa milango ya lifti ilikuwa ikikutana ili kujifunga na ni muda huohuo yule muuguzi alipozidi kukaza macho yake kuelekea nje ya ile lifti. Siyo bure, kuna kitu alikuwa akikitazama kule nje, ama kuna mtu alikuwa akimtazama.

   Muuguzi yule aliinua mkono wake wa kuume moja kwa moja akaupeleka usoni pake. Akakichomoa kile kitambaa kilichomziba uso. Wakati huohuo, lifti ilikuwa ikielekea kujifunga kabisa, na wakati ikijifunga, tayari yule muuguzi alikuwa amekwishakitoa kitambaa usoni pake.

   Edson Anzael “Eddy,” alikuwa akifatilia lile tukio kwa umakini mkubwa kana kwamba alilitegemea. Ndipo sasa macho yake yalipo mtumbuka kwa kihoro, moyo ukamlipuka na kupiga “PAAAHHH!!!”

   Aliiona vema ile sura ya yule muuguzi.

   Hakuibahatisha…

   Yule sio muuguzi wala sio mtu wa jinsia ya kike.

   Yule ni mwanaume… na anamjua… lol.

   Lifti ilijifunga, Edson akatazama kwnye kingo za milango ya lifti, panapo waka taa zianazoonyesha hesabu ya ngazi inazotembea lifti. Akabaini ilikuwa ikipanda juu. Hakutaka kupoteza muda, akaazimia kukwea ngazi ili aikimbilie, akiamni kuwa, maadamu wale wauguzi feki na mgonjwa wao feki wanalikuwa wakikokotana na kijibaisikeli cha wagonjwa, lazima angewawahi na kuwapata huko waendako. Ghorofa ya ngapi sasa…

   “Potelea mbali itafahamika mbele kwa mbele,” alilopoka kwa nguvu mpaka watu waliokuwa jirani naye wakamsikia. Akalibaini hilo kutokana na umakini uliotengenezwa ghafla na watu wale.

   Hakujali.

   Akawapotezea.

   Akatimka mbio kuziendea ngazi, alifahamu zilipokuwa kwani wakati alipokuwa akiifata lifti, aliziona. Zilikuwa kwenye ukuta uleule aliokuwa ameuegemea alipokuwa amesimama kolidoni nje ya wodi ya wanawake na watoto. Ilikuwa ni nyuma hatua chache sana kutoka pale alipokuwa.

   Aliziendea, akazifikia, akazikwea. Hakufika mbali, sauti laini ya mtoto wa kike iliyopaza ikiliita jina lake ilimstua.

   Edson akastuka, akageuka akiwa ngazi ya tatu kutoka pale koridoni. Akamuona msichana aliyemuita.

   “Hapana tafadhari… usiende huko, ni hatari kwako na kwangu pia… pleaseee babangu’nakuomba.” Ile sauti ilimsihi ikiomboleza. Edson alishangaa, aakai huo, hakuwa na uhakika kama aliyasikia vema maneno ya yule msichana, na kama kweli aliyasikia basi hakuyaelewa kabisa. Alilipagawa vilivyo baada ya kuiona sura ya yule mlimbwende aliyekuwa amesimama mbele yake.

   “WHAAAATTT… I can’t believe my eyes, ni kweli ninachokiona au naota?” Edson alizungumza kwa kumung’unya maneno lakini yule msichana aliyasikia.

   “Hii sio ndoto Eddy, Mungu kaukutanisha tena kwa mara nyingine, ena awamu hii, ni kwa kusudi maalumu.” Yule msichana alimjibu huku machozi yakimbubujika. Edson alishuka zile ngazi huku akihisi kutetemeka na kuishiwa nguvu. Sasa naye alishindwa kuyazuia machozi yake kulia.

   Wakalia.

   Wakati huo Edson alimsogelea yule mrembo, mrembo kweli si haba. Wakalakiana kwa kukumbatiana huku machozi yakiwabubujika utadhani wamefikwa na msiba mzito. Ni hapo ndipo Edson akaamini kwamba hakuwa ndotoni. Harufu ya joto la yule msichana aliimjia upya akaimbuka vema.

   “Angela.., umefikaje huku.., umepajuaje hapa.., na umejueje kwamba mimi niko hapa… na nini maana ya kauli yako kwamba nikienda huko ni hatari kwangu na…” Edson alimtwisha mtungo wa maswali lakini Angela hakumruhusu kuendelea.

   “Huu sio wakati sahihi wa kujibu maswali yako. Kwanza tuondoke hapa. Tupotee kabisa.” Angela alimjibu.

   ‘Whaaattt…’ Edson alipagawa.

   Angela hakumpa muda zaidi, alimshika mkono na kumvuta kwa ishara kwamba amfate waondoke. Edson alijikuta akiafiki kama zuzu maamuzi ya yule msichana aliyewahi kuwa mpenzi wake, kabla hajavunja mahusiano yao kwa kumtoroka na kumuacha solemba peke yake kwenye kijiji pweke. 

   Wakaondoka. Wakatoweka na kupotea kabisa pale hospitalini.

*****

   Ile siku…

   Baada ya Padre Alphonce kumbaka na kumzika sister Benadertha akiwa hai, wakati akipiga hatua kuuelekea mlango wa kutoka nje ya kanisa….

  ‘Oh goshhh…holy Mary mother of Christ… shiiiti takatifu… holy shiiiti…’ Alilaumu sana. Wakati huo kiganja cha mkono wake wa kuume kilikuwa usoni pake akiyafikicha macho, ili yawe na uwezo wa kung’amua, iwapo alichokiona kilikuwa ni kweli, ama wenge.

      Milango yote ya kanisa ilikuwa imefungwa kwa kukomewa vema na makomeo, hivyo padre Alphonce hakuwa na hofu ya kufumwa wakati akifanya ushetani ule. Lakini.

   Lol…kama bahati mbaya hivi, aliona kitu kama kiwiliwili, au kivuli cha mtu kikitoweka kwa spidi kali kutoka kwenye dirisha lililopakana na mlango aliokuwa akiuelekea.

   ‘Oh! My God… nimefumwa… kuna mshenzi kaniona holy shiit… shiiiti takatifu.’  Alijikemea kimoyomoyo. ‘Mambo yameharibika.., ni nani yule? Au macho yangu yamenidanganya?’ Alitaka kujitia moyo, kwamba huenda alichokiona kilikuwa ni tofauti na dhahania yake.

Akakaza mwendo kuusogelea mlango. Alipoufikia, haraka haraka akachungulia nje, akitamani amuone mtu aliyekuwa akimfatilia. Hakumuona. Wala hakuona kitu chochote cha tofauti.

Hofu.

Alirudi parokiani, kwenye nyumba ya mapadre alipokuwa akiishi. Moyoni akiwa na teseko la fadhaa kwa unyama alioutenda. Kumbaka, kumlawiti, na kumzika kaburini sister Benardertha akiwa hai. Usiku ule, alilala kwa shida, na ama kwa hakika, usiku ulimpita kwa taabu. Mawazo yaliyoutesa mtima wake, hofu na mashaka vilimsulubisha.

*****

   Siku moja asubuhi, mishale ya saa tatu, padre Alphonce alikuwa ofisini kwake akizungumza na muumini mmoja mmoja aliyefika parokiani kwa minajili ya kupata huduma ya kipadre. Mgeni wa tatu aliyeingia alikuwa ni kijana mmoja mwenye takribani umri wa miaka 35.

   Wakati wote aliokuwepo eneo la nje ya ofisi akingoja ruhusa ya katibu muhtasi ili aonane na padre, alionekana kuwa mpole na mnyenyekevu, kiasi kwamba katibu muhtasi, alihisi kumuonea wivu mke wa yule kijana, kwamba kapata mwanaume wa maana. Alionekana gentleman.

   Dakika mbili baada ya kumruhusu kuingia ofisini kwa padre, katibu muhtasi alibadiri mtazamo wake, sasa, ule msemo kwamba watu wa pole ni wa kuogopwa, ulimganda kichwani kwa kila sekunde iliyosonga mbele.

   Kumbe jamaa hakuja kwa wema bwana! Alikuwa amemjia padre Alphonce kwa shutuma ya kujihusisha kimapenzi na mke wake, aliyefunga nae ndoa miaka miwili iliyopita, na huyo huyo padre Alphonce ndiye aliye wafungisha ndoa.
   Ugomvi ulikuwa mkubwa. Watu wakafurika. Walikuwepo watumishi wa pale parokiani, waumini waliokuja kwa ajili ya kuonana na mapdre na wapiti njia waliosikia lile sekeseke. Katika ugomvi ule, padre Alphonce alizikana katukatu zile shutuma.

Waligombelezewa hatimaye ugomvi uliisha. Padre Alphonce alijisikia vibaya sana. Akarejea kwenye nyumba ya mapadre walikokuwa wakiishi na wenzake, akiwa amefadhaika mno.

   Alipoingia chumbani kwake, alikuta gazeti la MWANANCHI likiwa kitandani. Hakustuka, lilikuwa ni jukumu la msaidizi wao wa ndani kumpokelea gazeti hilo kila siku, kutoka kwa muuzaji waliyekwisha kupatana nae awe akimletea, kisha, kila mwisho wa mwezi, hujumuisha hesabu na kufanya malipo ya jumla. Siku hiyo juu ya gazeti hilo, kulikuwa na habari ndogo iliyo mrusha roho kisawawa. 

   Ukiachana na lile sekeseke alilokumbana nalo ofisini, habari ile, ilizidi kumuharibia kabisa siku yake padre Alphonce…

*****

   “Habari gani hiyo love?” Angel alimsaili padre Alphonce. Alphonce hakumjibu, badala yake aliwasha kompyuta mpakato yake, akaiunganisha na intaneti, kisha akabofya sehemu ya barua pepe ya kampuni ya Yahoo. Akaingia kwenye akaunti yake ya barua pepe.

   Humo, akafungua moja ya ujumbe aliojitumia mwenyewe, yaani attachment kwa lugha ya kitaaalamu. Akamgeuzia Angel ile kompyuta mpakato, au laptop kwa kizungu ili ashuhudie kwa macho yake…ule ujumbe.

   Angel akashangaa.

   Ilikuwa ni sehemu ya juu ya gazeti la MWANANCHI, lililobebwa na kichwa cha habari,

BINTI WA KIITALIANO AKWAMA NA MWANAE MPAKANI

Adai kutelekezwa na mwenyeji wake aishiye Tanzania,

Apata hifadhi ya muda kambi ya wakimbizi ya Ngara baada ya hali ya mwanae kubadilika ghafla,

Aomba msaada wa wasamalia wema kumnusuru na mateso anayoyapata.

   Kisha habari kwa kina ikaanza kutiririka chini ya yale maneno. Nafasi haikutosha, ikaandikwa inaendelea ukurasa wa 3.   

   Habari hii, iliambatana na picha husika, ikimuonyesha huyo binti wa kiitaliano, akiwa amempakata mwanae wa kike mwenye takribani miaka mitano. Angel akazidi kushangaa.

   “Inahusiana nini na haya yanayotokea Alphonce.” Angel alimuuliza.

   “Kuna mahusiano makubwa mno Angel, haya ni mambo yangu binafsi, sikuwahi kutamani kumueleza mtu yeyote. Lakini, kwa hali ilipofika, na kwa mujibu wa mahusiano yetu, sina budi kukueleza.” Padre Alphonce alizungumza kwa uchungu mkubwa, machoni akilengwa lengwa na machozi, kiasi cha kumuogopesha zaidi Angel. Angel akajikaza kusikiliza.

   Huku akionekana hakuwa radhi kulizungumzia hilo, ila ilimlazimu tu, Alphonce alimsimulia simulizi iliyomtia simanzi kubwa Angel.

   “Huyu binti anaitwa Carolina, ni muitaliano aishiye Italia. Nafahamiana naye. Tulijuana nikiwa chuoni Italia, tayari nikiwa padre, baada ya kupata ufadhili wa kusomea digrii ya udaktari nchini humo.”   

   “Wakati huo, yeye alikuwa akisomea utawa katika seminari moja nchini humo. Tulifahamiana kwa sababu yeye na wanafunzi wenzake walikuwa na tabia ya kutembelea jumba la mapadre waishio Vatican, makao makuu ya kanisa letu la Roman Katoliki kufanya usafi kila jumamosi. Na ni jumba hilo nilipokuwa nikiishi kipindi chote cha masomo yangu.

   Tulifahamiana na Carolina.

   Tukatokea kupendana sana.

   Ghafla.

   Tukaanzisha mahusiano ya kimapenzi kwa siri kubwa mno, kwani ilikuwa ni hatari mno kwake kama mwanafunzi wa utawa, na mie kama padre. Wakati huo, sikuwa na cheo nilicho nacho sasa cha umakamu wa askofu, yaani vice bishop.

   Baadae msichana huyo alipata mimba. Hapo ndipo mambo yalipo haribika kabisa. Jambo lililonishangaza, nadhani ni kwa namna alivyokuwa akinipenda kwa dhati, kwa hiari yake mwenyewe, Carolina aliadhimia kunifichia siri.

   Tulishirikiana kujaribu kuitoa ile mimba, hatukufanikiwa. Mpaka ikabainika na uongozi wa chuo alichokuwa akisoma. Carolina akafukuzwa chuo. Ndoto yake kubwa na ya miaka mingi ikazimika kama mshumaa. Niliumia sana kwa ajili ya Carolina.

   Aliamua kuachana na habari ya masomo, akajikita kwenye biashara. Nilimpa mtaji mkubwa, fedha nilikuwa nayo si mchezo. Fedha unayoniona nayo sasa, sijaanza kuimiliki hivi karibuni. Nina hela nyingi mno.

   Mpaka naondoka Itali, mimi na Carolina tulikuwa tukiwasiliana vizuri tu. Niliwajibika vema katika gharama za malezi ya mtoto. Mpaka nilipokuja kukutana na habari hii gazetini.”

   Padre Alphonce alimaliza kumsimulia. Angel machozi yalikuwa yakimlenga. Alphonce hakujua iwapo yalikuwa ni machozi ya wivu wa mapenzi, au alikuwa akimuonea huruma kwa hadithi ile.

   “Lol…makubwa. Sasaaa…tatizo ni nini hasa mpaka haya ya Carolina kukwama mpakani, mara sijui kuhifadhiwa kambi ya wakimbizi yakatokea, ili hali umeniambia mawasiliano yako na mzazi mwenzako yalikuwa mazuri…” Namna sauti yake ilivyokwaruza alipoyatamka maneno “mzazi mwenzako”, ndipo Alphonce alipoelewa sababu ya machozi ya yule msichana. Wivu.

   “…na yanahusianaje na huku kukimbizana kwako na hawa watu wabaya?!” Angel alimalizia maswali yake.

    “Awali nilikuwa nimehisi vingine, ila kwa mujibu wa hizi habari ulizoniletea sasa nimeelewa vema ni nini kinaendelea. Kuna mambo yanaendelea, pasina shaka watu hawa wanaotaka kuishinikiza Tanzania isaini makubaliano ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja, wamefanikiwa kizifahamu habari kuhusu mimi na Carolina. Nao watakuwa wamefanikiwa kumshawishi Carolina anisaliti ili wamtumie kama chambo ili wafanikishe mipango yao…hii ni strategic plan to accomplish the mission.” Aliyasema hayo wakati mambo mengi yakipita akirini mwake. Alihisi kuwehuka.

   “Hayo maneno ya mwisho sijakuelewa, si unajua mi mwenzio shule ilinipita kushoto.” Alijitetea Angel. Edson akaumizwa na ile sentesi, alishafahamu ni kwa kiasi gani swala la kutokupata elimu lilivyokuwa likimsononesha Angel. Akamfafanulia.

   “Huu ni mpango mkakati wa kufanikisha mpango.”

   “Unadhani Carolina amehongwa ili akusaliti?” Angel akamtupia swali.

   “Hakika.” Edson alijibu kwa uhakika.

   “Wakati we mwenyewe unamuhudumia vizuri.” Angel akaongezea neno. Edson akamjibu.

   “Sio kwa kiasi cha fedha atakazokuwa amelipwa na hawa watu. Kumbuka hii ni njama ya kimataifa, inayo husisha dola kubwa la Uingereza. Mimi na wewe hatujui nani hasa yuko nyuma ya shinikizo hili la kuzitaka nchi za kiafrika ziunge mkono usagaji na ushoga.”

   “Duh!” Angel alishusha pumzi na miguno ya kukata tamaa. Akaendelea, “Ulisema awali ulihisi vingine, ulihisi nini, pengine inaweza ikawa hiyo ndiyo sababu, tofauti na hili ulidhanialo?” Angel akamtupia swali.

   Alphonce akajikuta akipata kigugumizi na kupepesa macho. “Aaaam, hapana, tuachane na hayo kwa sababu hayana maana tena kwa sasa.” Alijibu Aliphonce, moyoni akijiambia.., ‘Awali nilihisi issue ya kumbaka, kumlawiti na kumzika mzima mzima mtawa Benadertha ndio sababu ya kutafutwa kwangu na hawa watu wabaya. Kwa sababu siku ile.., niliona kitu kama kivuli cha mtu kikitokomea pale mlangoni, sasa…kama mambo yenyewe ni haya ya kuwala kiboga hawa mashoga, kidogo itakuwa ahueni kwamba mambo sio mabaya kama nilivyodhani. Bora kashifa ya kujamiiana na mashoga kuliko kesi ya ubakaji, ufilaji  na mauaji kama nilivyomtenda Benadertha.’

   Wakiwa pale kitandani, wote akiri zilivurugika, wasijue nini hatima ya mambo yale, na kwa namna gani Alphonce angefanikiwa kuishawishi serikari ya Tanzania

ikubaliane na shinikizo la wazungu, ili anusurike na aibu ya ule uchafu.  

   Mara hali za miili yao ikaanza kubadilika. Pamoja na wakati mgumu waliokuwa nao, bado kila mmoja alihisi kuuhitaji mwili wa mwenzake. Nguvu ya mapenzi haijawahi kushindwa na jambo lolote.

   Wakaanza kutomasana, kabla hawajazama penzini. Kwa mara nyngine, kila mmoja akajikuta mwilini mwa mwenzake aliyemkosa kwa muda, bila kutegemea. Kila aliyewahi kudhani hatompata mwenziye tena, habari ilimuendea tofauti.

   Awamu hii, hakuna mushikeli wowote uliyowaingilia. Walifanikiwa kupeana raha ya dunia. Baada ya hapo usingizi mzito uliwachukua. Walilala fofo, mpaka walipoamka baada ya kustushwa na mstuko wa kishindo kizito cha mlango wa chumba chao uliobomolewa kwa nguvu, kisha watu watatu wenye silaha za moto wakawavamia…

Inaendelea…

Mawasiliano na mwandishi wa riwaya hii:

Instagram; egidiusjack5 Facebook; Egidius Jack

Email egidiusjack@gmail.com Mob;0715499002Author: admin