Historia ya mtunzi mashuhuri Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi amezaliwa mkoa wa Mwanza. Amezaliwa 13 Aprili 1944 katika kijiji cha Namagondo kisiwani Ukerewe. Euphrase Kezilahabi ni mwandishi kutoka nchini Tanzania. Euphrase kezilahabi Lugha yake ya kwanza ni Kikerewe lakini huandika hasa kwa Kiswahili ambacho amekipanua kwa kutumia mitindo ya lugha yake ya asili. Baba yake anafahamika kwa jina la Vincent Tilibuzya. Baba yake Euphrase Kezilahabi alikuwa msimamizi wa kijiji. Euphrase Kezilahabi alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma katika shule ya msingi Nakasayenge. Tangu 1957 alisoma Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.

Mwaka1967 alijiandikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akasoma shahada ya ualimu na fasihi hadi alipohitimu mwaka 1970. Mwaka huo huo 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro. Baadae akahamishiwa katika shule ya sekondari Mkwawa mkoani Iringa.

Mwaka1971 alirudi chuo kikuu cha Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo. Alisoma shahada ya uzamili (M.A) hapo hapo chuo kikuu cha Dar es salaam. Moja ya kazi zake za kidhamifu ni tasinifu iliyohusu riwaya za Shaaban Robert. Mwaka 1974 akawa mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Akaendelea na masomo ya uzamifu (PhD) huko nchini Marekani, katika Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison. Alitoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu “African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation”. Mpaka ana fariki alikuwa ni Profesa katika chuo cha Botswana.

Maandiko ya Euphrase Kezilahabi

Riwaya alizoandika

Riwaya ya Rosa Mistika: ni riwaya iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka 1976. Riwaya hii imekuwa na matoleo matatu, toleo la kwanza lilitoka mwaka 1976 na kuchapishwa nchini Kenya (Nairobi) na kuchapishwa na East Afrika literature Bureau. toleo la pili ilichapwa tena 1980 Nairobi Kenya na kuchapishwa tena na literature Bereau, ilichapwa tena kwa mara ya mwisho riwaya hii ya Rose mistika 1988 nchini Tanzania na Dar-es-salaam university Press. Riwaya hii imegusia masuala ya utoaji mimba kwa wasichana wadogo, mapenzi katika umri mdogo, ukosefu wamaadili kwa viongozi wa uma mfano mhusika padre.

Riwaya ya dunia uwanja wafujo: imechapishwa mwaka 1975 na vide-publisher. Riwaya hii inasawiri maisha halisi ya Tanzania. Riwaya hii inaelezea jinsi maisha yaliyopo duniani ni sawa na fujo kwani kila mtu anayekuja duniani huleta fujo zake na baadae kutoweka. Mwandishi Euphrase Kezirahabi anaelezea katika jamii kila mtu anakuja duniani kufanya fujo zake na kusababisha matatizo mbalimbali katika jamii yake kama mauaji, ukabila, umalaya, uchawi, ubakaji, ulevi wa kupindukia.

Riwaya ya gamba la nyoka: riwaya hii imechapishwa mwaka 1979 na East Afrika publisher. Riwaya hii inaonyesha jinsi maamuzi ya kisiasa yasiotafakariwa yanavyoweza kuwa na athari mbaya kwa wanyonge na wakulima. Ni riwaya inayotashtiti sera zinazoongozwa na ubinafsi, kisasi na pupa ya utekelezaji. Hii riwaya inayotumia sitiari na taswira zenye uwezo mkubwa wa kuibua hisia kali na itakayozichokonoa fikira za msomaji hususani kwa namna inavyoupembua unafiki katika matendo ya waja.

Riwaya ya Kichwa maji: riwaya hii imechapishwa mwaka 1974 /2008 na vide-muwa publisher limited. Kichwa maji ni riwaya ya kisasa ambayo imejikita zaidi katika nadharia ya utamaushi (udhanaishi) katika kuangalia maisha ya sasa. Riwaya hii ina sura nane. Kwa ujumla mwandishi amegusia vitu kama bughudha, mahangaiko, tabu na karaha anazo kumbana nazo mtu kwenye jamii anayoishi.

Riwaya zake nyingi anazoandika mwandishi Euphrase Kezirahabi zimejikita katika riwaya dhati. Riwaya zake nyingi huwa anatumia lugha za kifasaha, nyoofu, adilifu na zisizo na matusi vile vile riwaya zake huwa zinakubalika na sehemu kubwa ya jamii. Pia riwaya zake huwa na mambo nyeti, adhimu na yenye thamani katika jamii.

Riwaya nyingine alizowahi kuziandika mwandishi Euphrase Kezilahabi ni:

Nagona (1987/1990) Dar essalaam university press, Dar es salaam.

Mzingile (1991)Dares salaam University Press, Dar essaalm.

Mashairi aliyoandika Euphrase Kezilahabi

Kichomi (1974) iliyochapishwa Nairobi Lusaka ibadani: Heinemann, Karibu Ndani (1988) Dares Salaam university press na Dhifa

Tamthiliya aliyoandika Euphrase Kezilahabi

Kaptula la Marx (1978/1999)kaptula la Marx Dar es salaam: Dar esslaam University Press.

Mchango wa Euphrase Kezilahabi katika fasihi ya Kiswahili

Euphrase Kezilahabi ni mwandishi ambaye anachukuliwa kuwa ndiye mrithi wa mwandishi nguli Shaaban Robert. Ni mwandishi ambaye ametoa mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili. Mwandishi huyu ndiye mwanzilishi wa ushairi huru (free verse) katika Kiswahili alipoandika vitabu vya ushairi vya kichomi (1974) na karibu ndani (1988).

Euphrase Kezilahabi anajulikana kwa ushujaa wake wa kujaribu mitindo mbalimbali ya uandishi wa vitabu. Ukisoma vitabu vyake kama Rose Mistika, Dunia Uwanja wa fujo, Kichwa maji, Gamba la nyoka na tamthiliya ya Kaptula la marx utakutana na chembe chembe mpya katika nyanja mbalimbali hasa katika matuzo ya falsafa mfano riwaya ya Mzingile na Nagona. Msomaji wa vitabu hivi viwili lazima awe na uelewa wa falsafa za kimagharibi kama (existemutialism, epistemology, metaphysics, psychoanalysis, aesthetics na phenomenology) na pia falsafa za Kiafrika kama unataka kuelewa chochote kinachozungumzwa katika vitabu vyake.

Author: Gadi Solomon