Hoja Yangu


Hoja yangu wako wapi, si sarufi kushindana,
Meneno huwa situpi, kumbuka nilo yanena,
Kule mambo yako vipi, lilo jema kujuzana,
Tuambieni bayana, nawauza mko wapi,?

Mmeshakuwa wafupi, wenyewe mna pishana,
Yenu mapana yawapi, gauni yasio shona,
Kweli huwa haichupi, urongo una kazana,
Tuambieni bayana, nawauza mko wapi,?

Kwenye hili hunikwepi, hapono tutubanana,
Mwingine utapitapi, ni hoja iso na mana,
Nambiani mko vipi, ya herufi jibu sina,
Tuambieni bayana, nawauza mko wapi.?

Una izara upupi, thama mwashindwa kunena,
Matango yenu yawapi, mlotupa kila kona,
Upituzi haulipi, hojani zama kwa kina,
Tuamhieni bayana, nawauza mko wapi.?

Mie ni nasi si Popi, sijakamilika sana
Makosa niache wapi, vigumu kukosekana,
Nikiuzacho muwapi, kwa yale mlo kinena,
Tuambieni bayana nawauza mko wapi.?

Ukwapi kinache cha ‘pi’, na utao naweka ‘na’
Kaditamati mshipi, si kitu bila ndoana,
Utacho kivua kipi, utaishia kuona,
Tuambieni bayana, nawauza mko wapi?

Author: Gadi Solomon