Hongera Rais Samia kwa siku ya kuzaliwa

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametimiza miaka 62 ya kuzaliwa akiwa ni Rais wa kwanza mwanamke Tanzania leo tarehe Januari 27, 2022.

Tunampongeza kwa juhudi zake za kuliongoza taifa letu na kuendelea kutunza na kudumisha umoja, amani na mshikamano.

Rais Samia anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa tayari ametoa uongozi kwenye nafasi za maamuzi kwa wanawake wengi.

Rais Samia wakati leo akitimiza umri wa miaka 62 anaweza kujivunia kutekeleza vizuri azimio hilo la Sadc. Tangu uhuru , Taifa halikuwahi kuwa na Katibu wa Bunge mwanamke , lakini sasa yupo Nenelwa Mwihambi, pia hakujawahi kuwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwanamke, lakini sasa yupo Dk Stergomena Lawrene Tax.

Rais Samia alizaliwa Januari 27,1960 Zanzibar na alipata elimu ya msingi kati ya 1966 na 1972 katika shule tofauti visiwa vya Unguja na Pemba.

Author: Gadi Solomon