Jifunze nahau za Kiswahili kutoka kwa Mwalimu wa Swahilihub

Gadi Solomon (Mwalimu wa Kiswahili kwa wageni…BA-Kiswahili)

Simu +255 712127912 Whatsapp

  • Amekula chumvi nyingi –  Ameishi miaka mingi
  • Ahadi ni deni – Timiza ahadi yako
  • Amewachukua wazee wake    –  Anawatunza vizuri wazazi wake
  • Amekuwa popo   – Yu kigeugeu
  • Amevaa miwani   – Amelewa pombe  
  • Amekuwa mwalimu  – Yu msemaji sana 
  • Amemwaga unga    – Amefukuzwa kazi
  • Ana ulimu wa upanga  – Ana maneno makali 
  • Ameongezwa unga  – Amepandishwa cheo
  • Agizia risasi – Piga risasi 
  • Chemsha bongo – Fikiri kwa makini 
  • Kuchungulia  kaburi – Kunusurika kifo  
  • Fyata mkia – Nyamaza
  • Fimbo zimemwota mgongoni – Ana alama ya mapigo ya fimbo mgongoni
  • Hamadi kibindoni – Akiba iliyopo kibindoni
  • Hawapikiki chungu kimoja – Hawapatani kamwe
  • Kupika majungu – Kufanya mkutano wa siri
  • Kumpiga kilemba cha ukoka   –  Kumsifu mtu kwa unafiki
  • Kupelekwa miyomboni – kupelekwa jandoni
  • Kujipalia mkaa – Kujitia matatani
  • Kumeza mate – Kutamani  
  • Kumuuma mtu sikio – Kumnong’oneza mtu jambo la siri
  • Kumpa nyama ya ulimi – Kumdanganya mtu kwa maneno matamu
  • Kumchimba mtu – Kumpeleleza mtu siri yake 
  • Kutia chumvi  katika mazungumzo  –  Kuongea habari za uwongo
  • Vunjika moyo –  Kata tamaa

Itaendelea kesho

Author: Gadi Solomon