
Gad Solomoni (Mwalimu wa Kiswahili ……BA kiswahili)
simu + 255 712127912
- Amekuwa popo – Yu kigeugeu
Amevaa miwani – Amelewa pombe
Amekuwa mwalimu – Yu msemaji sana
Amemwaga unga – Amefukuzwa kazi
Ana ulimu wa upanga – Ana maneno makali
Ameongezwa unga – Amepandishwa cheo
Agizia risasi – Piga risasi
Chemsha bongo – Fikiri kwa makini
Kuchungulia kaburi – Kunusurika kifo-
Fyata mkia – Nyamaza
Fimbo zimemwota mgongoni -Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni
Hamadi kibindoni – Akiba iliyopo kibindoni
Hawapikiki chungu kimoja -Hawapatani kamwe
Kupika majungu – Kufanya mkutano wa siri
Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka – Kumsifu mtu kwa unafiki
Kula mlungula – Kula rushwa
Kupelekwa miyomboni – Kutiwa [kupelekwa] jandoni
Kujipalia mkaa – Kujitia matatani
Kumeza [zea] mate – Kutamani
Kumuuma mtu sikio – Kumnong’oneza mtu jambo la siri
Kumpa nyama ya ulimi -Kumdanganya mtu kwa maneno matamu
Kumchimba mtu – Kumpeleleza mtu siri yake
Kutia chumvi katika mazungumzo – Kuongea habari za uwongo
Vunjika moyo – Kata tamaa
Yalimkata maini – Yalimtia uchungu
Kujikosoa – Kujisahihisha
Kutia utambi – Kuchochea ugomvi
Kumeza maneno – Kutunza siri
Kula njama – Kufanya mkutano wa siri
Kumkalia mtu kitako – Kumsema/kumsengenya
-
Kupiga vijembe – Kumsema mtu kwa fumbo
Kiinua mgongo – Malipo ya pongezi/uzeeni
Kazi ya majungu – Kazi ya kumpatia mtu posho
Kaza kamba – Usikate tamaa
Kumwonyesha mgongo – Kujificha
Kuona cha mtema kuni – Kupata mateso
Maneno ya uwani – Maneno yasiyo na maana/porojo
Mate ya fisi – Kata tamaa kupita kiasi
Mbiu ya Mgambo – Tangazo
Mungu amemnyooshea kidole – Mungu amemuadhibu
Mkubwa jalala – Kila lawama hupitia kwa mkubwa
Mkaa jikoni – Mvivu wa kutembea
Ndege mbaya – Bahati mbaya
Paka mafuta kwa mgongo wa chupa – Danganya
Maoni Mapya