Jifunze nahau za lugha ya Kiswahili na mwalimu wa Swahilihub

Fyata mkia – Nyamaza

Fimbo zimemwota mgongoni – Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni

Hamadi kibindoni – Akiba iliyopo kibindoni

Hawapikiki chungu kimoja – Hawapatani kamwe

Kupika majungu – Kufanya mkutano wa siri

Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka – Kumsifu mtu kwa unafiki

Kula mlungula – Kula rushwa

Kupelekwa miyo – Kutiwa [kupelekwa] jandoni

Amekuwa mwalimu   – msemaji sana 

Amemwaga unga – Amefukuzwa kazi……Itaendelea kesho

Author: Gadi Solomon