Jifunze Nahau za lugha ya Kiswahili na Mwalimu wa Swahilihub

1.Kumpa mtu ukweli wake-Kumwambia mtu wazi

2.Pua kukaribiana kushikana na uso-Kukunja uso kwa hasira

3. Sina hali- Sijiwezi 


4.Kupiga uvivu – Kukaa tu bila kazi

 
5.Kupiga kubwa -Kwenda moja kwa moja


6.Kumwekea mtu deko-Kulipiza  kisasi

 
7.Mtu mwenye ndimi mbili-Kigeugeu

 
8.Miamba ya mitishamba-Wanga hodari wa kienyeji


9.Kupiga supu-Tegea

 
10.Kupiga mali- shokaGawana 

 
11.Amekula chumvi nyingi-Ameishi miaka mingi


12.Ahadi ni deni -Timiza ahadi yako


13.Amewachukua wazee wake – Anawatunza vizuri wazazi wake


14.Amekuwa popo – Yu kigeugeu


15.Amevaa miwani- Amelewa pombe [chakari]

  

Author: Gadi Solomon