Kamusi ya Oxford yaingiza maneno 200 ya Kiswahili, lipo Chipsi yai

Na Pelagia Daniel

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) Consolata Mushi amesema lugha ya Kiswahili imetandawaa duniani.

Akizungumza kuhusu kutandawaa kwa lugha ya Kiswahili, Katibu Mtendaji, Mushi amesema Kamusi ya Kiingereza ya Oxford katika toleo lake jipya limeingiza maneno 200 ya lugha ya Kiswahili jana Alhamisi.

Mushi amesema hii ni mara ya pili kwa waandaaji wa kamusi hiyo kuingiza misamiati ya Kiswahili na kuitolea ufafanuzi kwa lugha ya Kiingereza ambapo hapo awali waliweka misamiati mitano pekee.

“Miongoni mwa maneno yaliyoingizwa kwenye kamusi hiyo, ni Chipsi yai, singeli, mamantilie, jembe daladala, chapo, kolabo,” amesema Mushi.

Katibu huyo Mtendaji amesema kwamba hatua hiyo itasaidia utamaduni wa mswahili kufahamika zaidi duniani kutokana na matumizi mapana ya kamusi hiyo kieneo.

Hatua hiyo imekuwa mwendelezo baada ya wiki moja iliyopita dunia kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani

Akizungumzia hatua hiyo mdau wa Kiswahili ameona hio ni hatua nzuri ya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini na duniani kote.

Author: Gadi Solomon