KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

AINA ZA MANENO

Mada hii imetumika kama mfano wa kumsaidia
mwalimu wa kuendelea na ufundishaji wa mada zote
mahUsusi za kidato cha kwanza
Malengo mahususi
Baada ya kupitia sura hii mwalimu ataweza kumwongoza
mwanafunzi aweze
a) Kubainisha aina za maneno
b) Kuumia aina za maneno katika sentensi
c) Kubaini aina za maneno kwa kutumia kamusi
Aina za maneno

a) NOMINO
Waelekeze wanafunzi kutaja vitu halisi na visivyo halisi
au visivoshikika. Wanafunzi watunge sentensi zao
wenyewe na wewe uziandike ubaoni. Maneno viumbe
waliyotaja yako ya vitu halisi, mawazo au tabia fulani.
Maneno ya vitu na yasiyo ya vitu halisi huitwa nomino.
Vitu halisi na visivyo halisi na viumbe vyote huwekwa
katika nomino za kawaida.

Waelekeze wanafunzi waweke maneno yafuatayo katika
aina zake za nomino. Kwa mfano:
Kachumbari, hamu, bata upepo, mzinga, kinanda, jeshi,
Bakita.

b) KIVUMISHI
Kwa kutumia bungua bongo, wanafunzi watunge sentensi
zenye kusifia vitu au jambo. Ziandike ubaoni. Waongoze
wanafunzi kuwa maneno yanayosifia vitu ni vivumishi na
kazi yake ni kutoa taarifa zaidi kuhusu nomino na
viwakilishi.
Kwa mfano:
a) Yule kijana ni mrefu
b) Silaha za maangamizi hazikuonekana huko Iraq.
Unawza ubaini kuwa kuna maneno yenye kai zenye
mwelekeo mmoj lakini yana kazi tofauti kidogo. Neno
yule katika sentensi ya kwanza linafanya kazi gani? Pia
Neno hilo linajibu swali gani? Neno hilo linatoa taarifa
gani kuhusu kijana? Je kusema yule kijana ni sawa na
kusema huyu kijana?
Maneno yule na huyu yanaonesha kijana huyo aliko
nakudokeza umbali na mzungumzaji. Huyu huashiria
kijan yuko karibu na mmzungumzaji. Kwa hiyo maneno

hayo yakitumiwa sambamba na nomino au viwakilishi
huwa vivumishi vionyeshi
Waongoze wanafunzi wachunguze sentensi hizi na
wajibu maswali haya:
a) Ni silaha gani hazikuonekana huko Iraq?
b) Je, kauli za maangamizi ni kivumishi. Fafanua kwa
ufupi.
c) Je kauli za maangamizi inajibu swali gani?
d) Maneno haya yangeondolewa kutoka kwenye
sentensi hiyo ingesomeka silaha hazikuonekana. Ni
wai msomaji akimaliza kusoma sentensi hio atajiuliza
swai: Silaha gazi au zipi?
e) Kwa hiyo, kauli hiyo inatoa maelezo zaid kuhusu
nomino (silaha) inayozingatiwa. Inajibu swali l silaha
zipi? Naarifu juu ya silaha zinazozunumziwa ambazo
hazionekani) Kivumishi hiki kinaundwa na maneno
mawili. Maneno yana kiunganishi za ambacho
kinatawaliwa na –a. Kiuganishi hiki inaweza
kubadilika kulinagana na upatanishi wa kisarufi wa
maneno yaliyo kwenye sentensi hiyo. Kwa hiyo
kiunganishi hicho huweza kuwa cha, la, ya na
mengine yanayotawaliwa na –a unganifu. Kivumishi
chenye umbo hilo huitwa kivumishi cha –a unganifu.
Waeleze wanafunzi waachunguze na kujadili

sentensi na maswali yaliyoambatana nazo kama
ifuatavyo:
Sentensi: Sudan ni nchi kubwa
Je neno kubwa katika sentens hii inafanya kazi gani?
Hiki ni kivumishi kinachotia ifa kwenye nomino
Sudan. Kwa hiyo ni kivumishi cha sifa. Vivumishi vya
sifa ndivyo vingi katika matumizi ya kawaida ya kila
siku.
Maneno kama fupi, vingi, tamu, safi, mbovu, hodari,
nene, nyembamba, nono hayo yote yanaingia katika kundi hili.
Sentensi: Nilimwona nyani mwenye kibiongo
Swali: Yule nyani ana sifa gani?
Yuel nyani ana sifa ya kuwa na kibiongo. Mwenye
kibiongo ni kivumishi kinchotawaliwa na kiangama
–enye. Kiangama hicho kinaweza kubadilika
kulingana na upatanishi wa kisarufi wa nomino
itakayokuwa inazungumzwa.
Kwa mfano: kiti chenye sifingo, pale penye miti
mingi, namba yenye tarakimu.
Sentensi: Wanafunzi watano wa shuleni kwetu
waliingia kidato cha tano mwaka jana
Swali: Neno watano linafanya kazi gani?
Watano ni kivumishi cha idadi.

KIWAKILISHI:
KIwakilishi ni nini? Angalia sentensi hii:
Hao wamechelewa sana. Je, neno hao linafanya kazi
gani? Maneno kama pale, kule, yule, nk tulidokeza
kuwa huonyesha umbali kutoka
mzungumzaji. Maneno kama hapa huyu hawa
huonyeshi ukaribu kutoka kwa mzungumzaji. Lakini
maneno haya hayadokezi mbali tu. Yanadokeza pia
kitu, mahali, au nafsi. Kwa mfano neno pale
linaonyesha mahali palipo mbali kidogo
na mzungumzaji.
Vivyo hivyo neno wale linaeleza watu zaidi ya mtu
mmoja walio mbali zaidi kutoka kwa mzungumzaji.
Kwa hiyo badala ya kutaja majina kama Kishoka na
Shaka wamechelewa sana kuwasili tunasema hao
wamechelewa sana.
Majadiliano yazingatie dhima ya neno hao ambalo
limesimama badala ya watu walio mbali. Si watu
hawa bali ni watu hao.
NAFSI UMOJA WINGI
Ya Kwanza Mimi Sisi
Ya Pili Wewe Nyinyi
Ya Tatu Yeye Wao

Maneno haya ni viwakilishi nafsi huru.
Sentensi: Sisi hatukulima kwao mwaka jana

Leave a Reply