KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

Historia fupi ya mabadiliko ya mtalaa wa somo la Kiswahili

Somo la Kiswahili lilianza kufundishwa katika shule za msingi mwaka 1901 wakati wa utawala wa Kijerumani. Wakati huo, Kiswahili kilitumika katika jeshi la Tanganyika na katika dini na biashara. Kumbuka kuwa lugha ya Kiswahili ilikuwa inazungumzwa nchini hata
kabla ya kuja kwa wakoloni wa Kiarabu na
Kizungu.
Wakati wa utawala wa Waingereza yaani mwaka 2020 Kiswahili kiliendelea kufundishwa katika shule za msingi. Kilikuwa ni lugha ya kufundishia katika madarasa ya
chini.

Madarasa hayo ni ya kuanzia darasa la kwanza hadi la nne. Darasa la tano hadi la nane na elimu ya sekondari na ya juu ilifundishwa kwa lugha ya Kiingereza. Baadaye Kiswahili kilifundishwa kama somo katika elimu ya sekondari katika madarasa ya chini yaani darasa la tisa hadi la 12.

Wakati huo pia kilitumika katika ofisi za Serikali pamoja na jeshi. Katika enzi hizo vitabu kadhaa vya kufundishia Kiswahili viliandikwa.
Pia vitabu vya taaluma mbalimbali viliandikwa kwa Kiwahili ambavyo miongoni mwake vilikuwa ni vya masomo ya sayansi na Kilimo kwa shule za msingi.
Baada ya uhuru, Kiswahili kiliingizwa na kufundishwa katika kidato cha nne, tano na sita na katika vyuo vikuu. Pia Kiswahili kilipewa hadhi ya kufundisha elimu yote ya
msingi. Mabadiliko ya hivi karibuni ya mwaka 1997 ambapo mihutasari yote ya sekondari na somo la Kiswahili ilibadilishwa.

Kuanzia wakati huo mabadiliko mengi yametokea ndani na nje ya nchi ambayo ni ya kisiasa, kiuchumi,
kijamii, kielimu na kiteknolojia.

Mabadiliko hayo yameathiri lugha na ufundishaji wake,
Kutokana na hali hiyo, mtalaa wa Kiswahili uliboreshwa mwaka 2005 baada ya kufanyiwa utafiti mwaka 2004. Utafiti huo ulibaini upungufu wa mtalaa wa mwaka 1997.

 

 

Leave a Reply