KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

Mabadiliko ya mtalaa

Ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari umekuwa wa kuzingatia maudhui zaidi kuliko mchakato wa kuelewa dhana. Matokeo yake ni kwamba wanafunzi wamekuwa wakijifunza kwa juhudi za kumaliza mada za mihutasari kwa ajili ya kukabili mitihani.

Kwa hiyo wahitimu wa elimu ya sekondari wamekuwa wakizingatia ujifunzaji mkururo ambamo maarifa hupotea
baada ya kumaliza elimu yao. Wanafunzi waliomaliza wanajikuta hawajui stadi za lugha na ujuzi wa kuwawezesha kuunda na kuchanganua masuala mbalimbali ya kutekeleza shughuli zao katika maisha. Kwa msingu huo, mtalaa umebadilishwa na kuwa wenye mwelekeo wa ujenzi wa ujuzi. Mhamo huo wa ruwaza, ufundishaji na
ujifunzaji umejikita katika kumfanya mwanafunzi kuwa kitovu cha ujifunzaji na ufundishaji . Mwalimu ni mwezeshaji wakati mwanafunzi hujifunza maarifa, stadi, ujuzi wa kudumu. Mwalimu hujifunza kutokana na shughuli za mwanafunzi wake na mazingira yanayomzunguka.
Mfumo huo wa mwelekeo huhusisha mambo kadhaa:
a) Kumwezesha mwanafunzi kujenga ujuzi kutokana na mchakato ambao yeye mwenyewe ni mshiriki mkuu. Kwa mfano, katika lugha, mwanafunzi kuwasiliana kwa kushiriki kuigiza muktadha fulani ambapo anazungumza na kuwasiliana kama inavostahili. Hapo, kazi ya mwalimu ni kumwezesha kuunda muktadha na kuelekeza.
b) Katika kutekeleza muhamo wa ruwaza, uzingatiaji wa masuala ya mtambuko ni muhimu. Masuala kama ufundishaji unaozingatia usawa wa kijinsia, mazingira vutivu ya kujifunza na uzingatiaji wa haki za mtoto kunamfanya mwanafunzi awe tayari anashiriki kikamilifu katika kujifunza.
c) Mbinu zinazomshirikisha mwanafunzi ni nyenzo kuu na muhimu katika kufanikisha ujifunzaji fanisi, mchakato ambao mwanafunzi hupata fursa ya kutenda , kufikiri peke yake, kujadili na wenzake katika vikundi na katika darasa zima, kushiriki na wenzake katika kufikiri na kutenda, kubuni, kuchunguza na kufikia kukuza vipawa vya kila mmoja.
d) Unyumbufu wa mwalimu na mwanafunzi katika mahusiano yao wenyewe na mazingira ya kujifunzia na kufundishia hutiliwa mkazo. Njia zinazomshirikisha mwanafunzi, zana zinazomfikirisha mwanafunzi na kumpa fursa ya kudadisi, kujenga mantiki na kumfanya ajiamini na ajenge maana na ujuzi wa kudumu.
e) Kwa kuzingatia haya yote, muhutasari wa somo la Kiswahili katika shule za sekondari Kidato cha 1- IV wa mwaka 2005 umeandaliwa katika mwelekeo wa kumpatia mwanafunzi ujenzi wa ujuzi.
f) Maudhui yaliyo katika mwongozo huu ni muhimu kwa walimu wote na waandishi wa vitabu vya shule. Kwa mwalimu ni muhimu maudhui yawafikie pia wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Hii ina maana kwa taratibu zitakazowawezesha wasioona na viziwi wazisome zifanywe na Mamlaka husika za uendeshaji wa shule. Taratibu hizo
zinajumuisha kuweka maandishi hayo katika hati ya breili (maandishi yenye nukta nundu maalumu kwa wasioona)
na lugha ya viziwi kwa madhumuni hayo.

Inafaa mwalimu awapangewasioona na wenza wanaoona ili wanaoona wawasaidie kubaini yanayofundishwa na kujifunza. Uteuzi wa wanaoona ufanywe kwa uangalifu mkubwa ili wale wanaoona wawe ni wale wenye upendo na umakini wa kusaidia. Pia mwalimu anapofundisha darasa la walio viziwi ashauriwe kuzungumza akiwa unawatazama wanafunzi. Hii ni kwa sababu mara
nyingi viziwi hubaini maneno yako kwa kufasiri mtembeo wa midomo yako. Ukiwageuzia mgongo unakata
mawasiliano nao.

Leave a Reply